VIDEO INTERVIEW: JIMMY KABWE AELEZA MATARAJIO YAKE KAMA MTANGAZAJI MPYA WA KIPINDI CHA THE BIG EASY CHA CHOICE FM

Mtangazaji mkongwe wa redio nchini na mmoja wa watangazaji wa kwanza kabisa wa Clouds FM, Jimmy Kabwe, amechukua nafasi ya Chris Lugoe aka ML Chris kwenye kipindi cha The Big Easy cha Choice FM ambapo atakuwa akishirikiana na Abby.

“Kwakweli Choice FM is my choice,” Kabwe ameiambia Bongo5 kwenye mahojiano maalum. “Muda ulipofika wa mimi kurudi kwenye media napoangalia sasa radio stations ambazo zipo ni ipi inayoweza kunicompliment zaidi na Choice ilikuwa number one kwasababu Choice ni bilingual, mimi ni mtangazaji ambaye napenda kuwa free with languages na napenda niwe huru kutumia lugha zote mbili,” ameongeza.

Jimmy amesema kipindi cha Big Easy sio kigeni kwake kwakuwa hata wakati ML Chris anakianzisha kuna masuala alikuwa akimuomba ushauri kwakuwa ni marafiki wazuri.

“Nina excitement mara mbili, kipindi chenyewe nakipenda sana, nilikuwa msikilizaji mkubwa, nilikuwa mchangiaji mkubwa na sio kipindi ambacho utaenda kukichezea tu, nipo committed, dedicated to make sure kinaenda another level,” amesema Kabwe.

Kabwe ataanza kusikika kwenye kipindi hicho kuanzia Jumatatu ijayo.

Advertisements

SIKILIZA WIMBO MPYA WA JOSE CHAMELEONE UITWAO “WALE WALE”

Muimbaji wa Uganda, Jose Chameleone ameachia single yake mpya iitwayo Wale Wale.

“To all my fans worldwide Brand new!!!!! “WALE WALE” as i Activate invasion 2015,” hayo ndiyo maneno aliyoandika kwenye ukuta wake wa kitabu (Facebook).

//

MILIPUKO (UGAIDI) UNATUPITISHA ARUSHA KATIKA KIPINDI KIGUMU SANA; LEMA

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote

  • “Arusha tunapita katika kipindi kigumu sana. Kwanza tulishuhudia mlipuko wa bomu kanisani, ikafuatiwa na lile la mkutano wa hadhara wa Chadema, kabla ya mwingine kulipuka kwenye baa na sasa nyumbani kwa Sheikh,” Lema.

Arusha. Sheikh wa Msikiti wa Qiblatan,Sood Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini hapa amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku nyumbani usiku wa kuamkia jana.

Pamoja na Sheikh Sood, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu.

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.

Akizungumza hospitalini hapo, Sheikh, Sood alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la Majengo ya chini, usiku wa kuamkia jana saa 5:00 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni.

“Nikiwa sijui hili wala lile nilishtushwa na mlipuko ulioambatana na vyuma mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumba tulichokuwamo,” alisema Sheikh Sood.

Alidai anawajua waliotekeleza shambulio hilo kwa sababu amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu anaowafahamu na tayari alikuwa ametoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Alisema kuwa siku tatu kabla ya tukio hilo alikoswakoswa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na akatoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha kuhusu tukio hilo. Sood anasema kuna baadhi ya vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.

Sheikh huyo ambaye ni Kiongozi wa dhehebu la Answar sun Kanda ya Kaskazini amekuwa akitofautiana na waumini wenzake kutokana na msimamo wake wa kutokukubaliana na baadhi ya waumini wenye msimamo mkali wa msikiti huo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alikemea matukio ya mabomu yanayolitikisa Jiji la Arusha katika siku za karibuni na kuviagiza vyombo dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wote ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha tukio hili limetekelezwa na watu walio karibu na Sheikh. Polisi wanaendelea na uchunguzi kwa sababu baadhi ya watu wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili pia ni miongoni mwa watuhumiwa kwenye matukio mengine ya milipuko ya bomu Arusha,” alisema Mulongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabasi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea vyema huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alielezea kusikitishwa na matukio ya milipuko ya mabomu Arusha na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwakamata wahusika bila kujali vyeo, nyadhifa, dini, itikadi wala rangi zao.

“Arusha tunapita katika kipindi kigumu sana. Kwanza tulishuhudia mlipuko wa bomu kanisani, ikafuatiwa na lile la mkutano wa hadhara wa Chadema, kabla ya mwingine kulipuka kwenye baa na sasa nyumbani kwa Sheikh,” alisema Lema.

SOURCE: MWANANCHI

LOWASSA, SITTA NA WASSIRA HAWANA SIFA ZA KUWANIA URAIS; WARIOBA

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba

  • Asema anatakiwa awe kijana mwenye maadili, mwajibikaji

  • Asema hatagombea urais, aachwe alee wajukuu

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ametoa dira ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kutaja sifa za rais anayefaa kuiongoza Tanzania.

Warioba alisema kwamba taifa la Tanzania linastahili kuongozwa na vijana wenye nguvu ya mwili na akili. “Mimi nafikiri tuangalie kati ya vijana tulionao, nani anatufaa kuiongoza nchi, tusirudi kuangalia wazee,” alisema Jaji Warioba.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi huo mkuu ambao ni wa tano wa vyama vingi nchini, unatarajiwa kulipatia taifa rais mpya, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa utawala wa awamu ya nne.

“Uongozi mzuri unatengenezwa na haiba, wajihi, dhamira, uwezo, maadili, uhodari, hekima na maarifa. Sifa hizi hazipatikani kutokana na uzoefu wa miaka mingi kwenye siasa hata baadhi ya vijana wanazo,” alisema Makamba.

Alitolea mifano mingi duniani ambapo vijana ambao hawakuwa na uzoefu kabisa katika nafasi za siasa wameshinda na kubadilisha nchi kama Tony Blair wakati anakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza aliongoza nchi hiyo kubwa wakati alikuwa hajawahi kuwa hata Naibu Waziri.

“Barack Obama (Rais wa Marekani) alikuwa Seneta miaka mitatu tu, Julius Nyerere alikuwa Mwalimu akaingia siasa akaja kupewa uongozi wa nchi akiwa na miaka 39 tu.”

Katika maelezo yake Jaji Warioba alisema kwamba tangu uhuru, walioshika madaraka ya kuliongoza taifa walikuwa ni vijana.

Wazee kugombea urais

Akijibu swali kama atakuwa tayari wananchi wakimtaka kuwania urais baada ya kazi kubwa ya kukamilisha Rasimu ya Katiba nchini, Jaji Warioba alisema:

“Hili nilikwishalijibu, tusahau mawazo kwamba sisi (wazee) tutarudi madarakani. Nadhani mara ya mwisho tulipozungumza niliwaambia inafika wakati kiongozi unang’atuka. Unawaachia vijana ambao wana nguvu ya kimwili na akili ndiyo watumikie taifa hili, waongoze nchi.

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” alihoji Jaji Warioba.

Alisema kuwa tangu uhuru hadi sasa Tanzania imetayarisha vijana wengi wanaofaa kuliongoza taifa na kuongeza:

“Hatuna ombwe la uongozi, tunao vijana wengi sana, tena kwa bahati nzuri nchi kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikiongozwa na vijana.”

Huku akitaja mifano ya viongozi hao vijana walioongoza taifa, Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema:

Makundi ya urais

Warioba pia aliulizwa iwapo makundi yanayotajwa kusaka urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuwa huenda yanahusika na kusuasua kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Alisema kwamba, yeye na wenzake waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kutafakari mchakato huo unavyokwenda ukihusisha maeneo na makundi mbalimbali.

“Tulikwenda kutafakari, hatutaki kwenda kwenye matukio, wala kuzungumzia makundi, nasema wote wakae pamoja waone masilahi ya taifa, kwa sababu wasipokaa pamoja kuna hatari ya mchakato huu wa Katiba Mpya kukwama. Na kukwama siyo kwa masilahi ya taifa,”alisema.

Ikiwa Rasimu ya Katiba Mpya itapitishwa na mapendekezo yake ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, kutalazimika kuwapo kwa Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo nguvu na mfumo wa kisiasa kubadilika.

SOURCE: MWANANCHI

VIDEO: MR BLUE AKIWA NA VIJANA WA B.O.B MICHARAZO WAMEACHIA KICHUPA KIPYA KIITWACHO “SHUT UP” (KIMYA).

Vijana wa B.O.B Micharazo, wakiongozwa na front runners, Mr Blue na Nyandu Tozi, wameachia video ya ngoma yao mpya iitwayo ‘Shut Up’ (Kimya).

Kwenye ngoma hiyo iliyotayarishwa na Marco Chali, rappers hao wanafanya mtindo wa kubeto na hivyo kupeleka onyo kali kuwanyamazisha wapinzani wao. Katika verse ya Mr Blue ambaye amesima vizuri amefungua ngoma hiyo kwa panch “Helo Dar es Salaam mbona kimya jiji zima mbona limezizima/Hakuna cha Sharobaro wala ming’aro ya kuazima/ Mmebakiza uharo kumbe washenzi mlipima/Wabaya wetu mbona kimya, vipi wazima au nanyinyi mlipima,” anarap Kabayser.

Wengine waliochana kwenye ngoma hiyo ni Blood Gaza, Bobby MC, Cotton, Uswege na Beka Title aliyesimama kwenye chorus.