MOVIE REVEW:- PICHA MPYA YA EXPENDABLES 3 (2014).

the-expendables-3
Picha ambalo lilikuwa linasubiliwa la Expendables 3 ambayo inatoka rasmi Agosti 24 2014 tayari imeingia mitaani. Hii ni bonge la picha na naweza sema ni kali zaidi ya zile zote Expendables zilizo tangulia.

Ndani ya Expendables 3 Barney (Stallone), Krismasi (Statham) na timu nzima ikiwausisha wakali kama Jet Li, ya Expendables wanakutana uso kwa uso na Conrad Stonebanks (Gibson), ambaye miaka iliyopita alishiriki kuanzisha Expendables yeye pamoja na Stallone. Stonebanks hatimaye akawa mfanyabiashara katili jambo ambalo lilimlazimu Stallone kumuua … au yeye Rambo kuamini hivyo.. Stonebanks, ambaye alifanikiwa kukwepa kifo mikononi mwa Stallone anafanya mkakati wa kulifutilia mbali kundi la Expendables – bila kufahamu Stallone ana mipango mingine. Stallone anaamua kupambanisha damu ya zamani na damu mpya, na huleta enzi mpya ya Expendables yenye wanachama wapya kwa kuajiri watu ambao ni mdogo, wenye kasi na tech-savvy zaidi.

Unahitaji muda wa dakika 103 kuweza kuwa mmoja wa shuhuda wa hii mission ya Expendables katika vita ya kibinafsi.

Runtime               :               103 mins

Release Date        :               15th August 2014

Genres                   :               Action, Thriller, Adventure, HQ-Link

Actors                :               Sylvester Stallone, Jason Statham, Jet Li, Antonio Banderas, Wesley Snipes, Dolph Lundgren, Mel Gibson, Harrison Ford, Arnold Schwarzenegger, Ronda Rousey, Kellan Lutz, Terry Crews, Kelsey Grammer, Natalie Burn, Sarai Givaty, Robert Davi, Victor Ortiz, Randy Couture, Glen Powell, Bashar Rahal, Lisbeth Olofsson, Thomas Canestraro, Velizar Binev, Ivan Kostadinov, Tzvetislav Samardjiev, Harry Anichkin, Mason Brett, Slavi Slavov, Anton Poriazov

kama unaitaji kitu hiki  tuwasiliane….

Advertisements

SIKILIZA SONGI JIPYA LA PIPI YA KIJITI KUTOKA KWA MENINAH

Menina-Pipi-Ya-Kijiti-Teaser-Cover-21

Mwanadada Meninah ameachia ngoma yake Mpya “Pipi ya Kijiti”. Hii ikiwa ni nyimbo yake baada ya ile video ya kacopy na ku-paste .

Nyimbo hii mpya imefanyika kwenye studio za A.M Records chini ya usimamizi wa producer Bob Manecky.

bofya hapa chini kusikiliza

http://www.hulkshare.com/bongofive/menina-pipi-ya-kijiti-1

//

NAZIZI ATHIBITISHA KUWA NA UHUSIANO NA MTANZANIA HERRY SAPPY.

Rapper wa Necessary Noize, Nazizi wa Kenya amethibitisha kuwa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na producer Mtanzania aitwaye Herry Sappy ambaye ni mtayarishaji wa muziki katika studio ya Homeboyz Productions ya nchini Kenya, baada ya wawili hao kukanusha habari hizo miezi kadhaa iliyopita.

nazizi-1

“Yeah tuna date, unajua ni miezi michache sasa”, alisema Nazizi kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.”Sijamwona mwezi mmoja sasa ameenda Mwanza kufanya project kadhaa lakini unajua tunawasiliana, unajua hatujui mambo ya Mungu tunaangalia itakavyoenda.”

Nazizi ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyempata akiwa kwenye ndoa na aliyekuwa mume wake waliyeachana, hakusita kumsifia boyfriend wake wa sasa Sappy ambaye ni mwenyeji wa Mwanza.

“He is a nice guy he is a really nice guy he is also really hard working he is doing very well out there”.

nazizi-2

Nazizi amesema yeye na Sappy walikutana studio zaidi ya mwaka mmoja uliopita kama msanii na producer wake na baadae mapenzi yakazaliwa.

“Tulikutana studio, dats how we met. Ilichukua muda baada ya kukutana kabla ya kuanza kuzungumza kabisa, nilikutana naye nadhani zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Tulikuwa tukiongea mara moja moja, alinipa beats nilizokuwa natakiwa kufanyia kazi then nikawa bize. Amenitengenezea single mbili kwa EP yangu.”

Sappy aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa mapenzi yao yalianza rasmi iku ya Valentine’s (Feb 14, 2014) na kuwa wapo serious na wanapendana kwa dhati.

//