Rapper wa Necessary Noize, Nazizi wa Kenya amethibitisha kuwa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na producer Mtanzania aitwaye Herry Sappy ambaye ni mtayarishaji wa muziki katika studio ya Homeboyz Productions ya nchini Kenya, baada ya wawili hao kukanusha habari hizo miezi kadhaa iliyopita.

nazizi-1

“Yeah tuna date, unajua ni miezi michache sasa”, alisema Nazizi kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.”Sijamwona mwezi mmoja sasa ameenda Mwanza kufanya project kadhaa lakini unajua tunawasiliana, unajua hatujui mambo ya Mungu tunaangalia itakavyoenda.”

Nazizi ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyempata akiwa kwenye ndoa na aliyekuwa mume wake waliyeachana, hakusita kumsifia boyfriend wake wa sasa Sappy ambaye ni mwenyeji wa Mwanza.

“He is a nice guy he is a really nice guy he is also really hard working he is doing very well out there”.

nazizi-2

Nazizi amesema yeye na Sappy walikutana studio zaidi ya mwaka mmoja uliopita kama msanii na producer wake na baadae mapenzi yakazaliwa.

“Tulikutana studio, dats how we met. Ilichukua muda baada ya kukutana kabla ya kuanza kuzungumza kabisa, nilikutana naye nadhani zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Tulikuwa tukiongea mara moja moja, alinipa beats nilizokuwa natakiwa kufanyia kazi then nikawa bize. Amenitengenezea single mbili kwa EP yangu.”

Sappy aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa mapenzi yao yalianza rasmi iku ya Valentine’s (Feb 14, 2014) na kuwa wapo serious na wanapendana kwa dhati.

//
Advertisements