VIDEO:- KICHUPA CHA G-NAKO “MORALE”

  • Video ya wimbo wa G-Nako, ‘Morale’ iliyoongozwa na Hanscana.

Hii ni moja ya vichupa vya hivi karibuni kabisa vya G-Nako ambayo inakwenda kwa jina la Morale, mwonekano wake ni mzuri na imefanyika katika mazingira ya kitaa…

Labda jambo lililonifurahisha kwenye nyimbo hii hususan mashairi yake ni pale G anaosikika akisema anapingana na wale wanao sema “Nako2Nako is back”.

Hebu tazama kichupa hiki na ujiinjoi

 

Advertisements

TAZAMA KICHUPA KIMPYA CHA 2FACE IDIBIA; “LET SOMEBODY LOVE YOU”

2Face Idibia ameachia kichupa kipya {Official Video} ya wimbo wake “Let Somebody Love You” ambae amemshirikisha msanii maarufu Bridget Kelly. Nyimbo hii ni moja ya vibao vyake sita ambavyo vinapatikana kwenye santuri (Album) yake inayo julikana kama Ascension. Kichupa hiki kimeongozwa na Luke Biggins na kimeshutiwa kwenye sehemu mbalimbali ya jiji la Lagos.

Source:- MTV Base.

TAMASHA LA PASAKA LAIPAMBA SHEREHE HIYO NDANI YA JIJI LA DAR

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka lililofanyika jana kwenye u8wanja wa Taifa akizungumza na mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika tamasha hilo na kuwaomba kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa katiba mpya akisema uamuzi mtautoa nyini ni serikali gani mnaiihitaji iwe moja, Tatu au Mbili nyinyi ndiyo mtaamua na sisi tutakipitisha kile mlichokiamua, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Angela Kairuki.

Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.

Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani jana.

Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na kwa mbwembwe wakati alipokuwa akifanya vitu vyake  kwenye uwanja wa Taifa jana.

  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete akiongozwa kuelekea jukwaani na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.

Mwimbaji wa ijini kutoka nchini Uingereza Dayo Bello akiimba na mkewe Ruth Tobi wakati wa tamasha la pakasa kwenye uwanja wa Taifa jana.

Mwimbaji Jesca BM naye alipagawisha mashabiki.

Mchungaji mtarajiwa Masanja Mkandamizaji akifanya vitu vyake jukwaani.

Umati uliojitokeza  katika tamasha hilo.

 

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernald Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka akirejea kuketi huku akizungumza na Richard Kasesela na Alex Msama katikati.

 Upendo Kilahiro akiimba jukwaani na kundi la Victoria Singers.
 
Untitled
 

Mashabiki mbalimbali wakimshuhudia mwanamuziki Kekeletse Phoofolo hayupo ichani wakati alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani.

Ikafika zamu ya Upendo Nkone

Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo kazi moja tu burudani .

Rose Muhando na kundi lake wakipagawisha kwenye tamasha la Pasaka jana katika uwanja wa Taifa.

HALA HALA ARUSHA! CHADEMA WASUSIA UPATANISHI

CHADEMA
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesusia upatanisho wa Serikali ya CCM kuwaingiza kwenye maridhiano ya amani yasiyo na tija kwa umma na taifa.

Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi aliandika barua kuhusu maridhiano ya amani kati ya vyama vya siasa, polisi, na taasisi za kidini pamoja na wananchi wa Arusha.

Taharifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema Chadema kama chama cha siasa na kama taasisi inayoitumikia jamii kinatambua nia njema kabisa ya Jaji Mutungi, na inamuunga mkono kufanya maridhiano haya yanayogusa jamii.
Hata hivyo nia hii njema ya jaji Mutungi imetiwa doa tena mbaya kabisa na serikali ya ccm na jeshi la polisi. Tukianzia na Jeshi la polisi ambalo ni sehemu ya maridhiano ya amani, december 4 walifanya uchunguzi wa tukio la kuchomwa moto ofisi yaa chadema mkoa wa Arusha, habari za uhakika zinadai kabla hata hawajamaliza uchunguzi wakaitisha mkutano na waandishi wa habari, wakatoa taarifa za uchunguzi ambayo ilionekana kutokamilika, taarifa iliyoonyesha udaifu na kuidhalilisha jeshi la polisi. Kwa taarifa ambayo jeshi la polisi imetoa  inaonyesha chadema wameichoma ofisi yao wenyewe, yaani mchezo ule ule wa kusema chadema walijilipua wenyewe Soweto, Kijana Ally Zona(RIP) aliuawa na kitu chenye ncha kali, Daudi Mwangosi (RIP) alirushiwa kitu chenye ncha kali …………
Serikali ya ccm kwa upande wake ilitegemea maridhiano/mapatano ya Jumamosi yawe sehemu ya chadema kumtambua meya Gaudence Lyimo, meya ambaye alichaguliwa kwa njia ya hila, meya ambaye ndiye chanzo cha mauaji ya January 5 2011, meya ambaye ni chanzo cha kufukuzwa kwa madiwani wetu Arusha, meya ambaye ni chanzo cha mlipuko wa bomu soweto, eti chadema tukae meza moja na ccm!!!!

Nia na dhamira ya CHADEMA ni kila mtanzania kuwa na amani, lakini amani haiji bila kuwa na haki, kwani CHADEMA inatambua kuwa Amani ni tunda la haki, na kwamba CHADEMA itaendelea kupigania haki ya watanzania wote wakati wote ili wawe na amani.

Hata hivyo kwa taarifa nilizopata ni kwamba chadema itaandika barua kwa taasisi zote za dini na za kiraia kuelezea sababu za msingi za kususia mkutano wa Msajili unaohusu upatanishi baada ya kutiwa doa na serikali ya ccm.

CHADEMA inatamka kwamba kabla ya wao kukutanishwa na ccm mambo yafuatayo yafanywe:
1. Meya feki ajiuzulu ili uchaguzi wa haki ufanyike,
2. Serikali iwawajibishe wale wote waliolipua bomu na kupiga risasi za moto soweto Arusha,
3. Serikali itueleze mabomu yaliyotumika soweto yalitoka wapi na yaliingia vipi nchini, na kwa makusudi gani, nani aliingiza, na hatua gani anatakiwa kuchukuliwa.
4. Serikali iwachukulie hatua polisi wote waliowaua raia kwenye mauaji ya Jan 5 2011
5. Serikali iwashushe vyeo polisi wote waliopandoishwa vyeo baada ya kutekeleza mauaji ya raia ya january 5, mauaji ya Daudi Mwangosi na mauaji ya kijana Ally Zona aliyeuawa Morogoro na maeneo mengine ambayo polisi wametekeleza mauaji ya raia wasio na hatia, halafu wapelekwe mahakamani.

Baada ya hapo CHADEMA watakuwa tayari kukaa meza moja na ccm.

Kwa habari zaidi CHADEMA Arusha watazungumza na waandishi wa habari kuelezea zaidi

TCRA YAPELEKA ELIMU YA FUTA DELETE KABISA KWA MABLOGGERS

 

 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma, akifungua semina ya siku mbili ya kuwaongezea umahiri Waendeshaji wa Blogu na mitandao mingine ya Kijamii, leo Makao Makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasilino wa TCRA Innocent Mugy na Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Google Kusini mwa Jangwa la Sahara, Joe Mucheru na wapili ni Mtaalamu wa masuala la Blog na mitandao ya kijamii kutoka kampuni ya Tech Walk Technology, Kenya, Liz Wachuka

 

 

 Washiriki kutoka Chama cha Ma-blogger wa Arusha. 

 

Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo

KABLA YA KUAMUA KUOLEWA AU KUOA SOMA HAPA

people-wedding
Kuna athari kubwa kama ni kweli unayeoana naye ni mtu wa kwanza au wa mwisho kuzaliwa ingawa kuna exceptions.
Kama una mchumba ambaye kwao ni mtoto wa mwisho kuzaliwa jambo la msingi ambalo naweza kukushauri ni wewe kuwa tayari for adventures, na kama ni mtoto wa kwanza kuzaliwa basi jiandae kuwa audited kila kitu au kukaliwa au kuongozwa bila kujali ni mwanaume au mwanamke period.

Mtoto wa kwanza kuzaliwa kawaida hujikuta ni kiongozi mahali popote na hupenda kuongoza, kupenda kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri na kama kilivyopangwa maana ndivyo alikuwa anaagizwa na wazazi kwake kuhakikisha wadogo zake wanatii kile ameagizwa;
“Hakikisha wadogo zako wamekula, wametandika kitanda, waosha vyombo, wamefagia uwanja, wamelala mapema nk”.
Mtoto wa mwisho kuzaliwa hujikuta ni mtoto hata akiwa mtu mzima kwa kuwa kwao bado ni mtoto na huwa hana shida na kitu chochote kwani kwake kila kitu ni rahisi na anapenda raha, sherehe na life is easy.

Kila kitu nyumbani kilikuwa ni kwa ajili yake kwa kuwa yeye ndiye mtoto hata baada ya kuwa mtu mzima bado anajiona ni mtoto Ndiyo maana huchelewa hata kuongea, kufanyia vitu mwenyewe kama vile kujua muda wa kula, sehemu ya kuweka nguo, kutandika kitanda, kuoga nk, yeye hujiona ni special kid, ni mtoto wa baba na mama na amekua wakati wazazi wamezoea maisha.
Kwa ujumla tabia za watoto wa kwanza kuzaliwa huwa ni kukaliwa wenzao (controlling, bossy, leading, perfectionist, auditors, no fun, firm and rigid) wengi ni viongozi na watoto wa mwisho kuzaliwa hujiona ni special kid, hujiona mtoto miaka yote, watu wa sherehe, don’t care, easy wengi ni comedians.

Je, inakuwaje wakioana mtoto wa kwanza na mtoto wa mwisho kuzaliwa?
Kama mmoja ni wa kwanza kuzaliwa na mwingine ni wa mwisho kuzaliwa (au mmoja ana tabia ya mtoto wa kwanza kuzaliwa na mwingine tabia ya mtoto wa mwisho kuzaliwa basi ndoa itakuwa nzuri kwani tabia zitawafanya wa-balance.
Uzembe wa mtoto wa mwisho utakomeshwa na mtoto wa kwanza kuzaliwa ambaye hupenda kuongoza na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa haijalishi ni mke au mume.
Hujasikia mwanamke analalamika kwamba mume wake hakustahili kuoa au kuishi na mke, maana yake ni mtoto wa mwisho na haijalishi amesoma au hajasoma watoto wa mwisho tabia hufanana.

Je, inakuwaje wakioana wote ni watoto wa mwisho au wote watoto wa kwanza kuzaliwa?
Ukweli ni kwamba match ya ndoa ya aina hii huwa inakera sana kwani kama wote ni watoto wa kwanza kuzaliwa kila mmoja atapenda kuwa kiongozi na sidhani kama hiyo meli haitazama. Na wakikutana wote watoto wa mwisho basi ni balaa kwani ndoa itakuwa haina kiongozi na itakuwa ni adventures.
Watoto wengi wa kwanza Ndiyo marais, wachungaji na viongozi mbalimbali na watoto wengi wa mwisho ni ma-MC na comedians.

Watoto wa kwanza kuzaliwa likija suala la sex wanachagua sana na kuwa na utaratibu ambao huchosha (routine sex), pia hufanya sex kama wakaguzi kama vile lazima kuoga kabla ya sex, taa zizimwe, kusiwe na mtu hajalala usingizi within 100m, piga mswaki, usiku tu tena baada ya saa tatu na si baada ya saa nne nk, ni usumbufu.

Bila watoto wa mwisho sherehe huwa hazinogi ingawa wao tatizo lao si kawaida yao kuwahi na kufika on time kwenye sherehe, ingawa watoto wa kwanza kwao ratiba ni muhimu.

Likija suala la siasa first born wengi ni wagombea na wanapenda kuwa viongozi wakati last born ni viongozi wa kuwasemea au kushabikia first born.
Watoto wengi wa kwanza kuzaliwa ni selfish, wachoyo, hawatoi vitu kirahisi bila maelezo ya kutosha, wakati wale wa mwisho ni easy, ni rahisi, hugawa ovyo si wachoyo ni watu wa to have fun.

Kumbuka kama unaoana na mtoto wa mwisho kuzaliwa hakikisha huweki matarajio makubwa sana kwani kwake ndoa ni jambo la kawaida tu naamini wale ambao tayari mpo kwenye ndoa mnafahamu hili kwani mmmeshakutana na maajabu ya kutosha.
Pia mimi ni mmoja ya watoto wa katikati (middle) hivyo sisi ni waasi (rebels) hatutaki tabia zenu ninyi watoto wa mwisho (don’t care) na ninyi watoto wa kwanza kuzaliwa (controlling) Ndiyo maana tunajua kuboko cha mtoto wa mwisho kuzaliwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa ingawa mkioana na sisi watoto wa mwisho hatuna shida ndoa inaenda tu maana tunawajua sana.

Anyway ninyi watoto wa kwanza kuzaliwa ni muhimu sana kwetu maana bia ninyi ndoa zingekuwa za kizembe sana, na ninyi watoto wa mwisho ni muhimu sana maana bia nyingi ndo haziwi na sherehe wala “to have fun”, ila mmezidi yaani hata kumaliza kupaka nyumba rangi unalilia sherehe?

Source: Mbilinyi Blog

KINANA, NAPE ZIARANI KILOMBERO.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akivishwa skafu na chipukizi alipowasili  eneo la kivuko cha Kilombero tayari kuanza ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro,Kinana alikuwa akitokea wilayani Ulanga.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

 Wanachama wa CCM wakiimba wimbo wa kumkaribisha wilaya ya Kilombero Katibu Mkuu wa CCM Andulrahman Kinana, akitokea wilaya ya Ulanga pamoja na vingozi wengine wa chama hicho.

 

Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipandisha bendera kuzindua rasmi Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

 

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa Shina la Wakereketwa  wa CCM la tawi la Manjechanga, Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 16, 2013.

 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na watoto waliokuwa sehemu ya watu walioshuhudia  uzinduzi wa Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipandisha bendera kuzindua rasmi Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero

Ranfred Majiji ambaye alikuwa mfuasi wa Chadema akikabidhiwa kadi ya CCM na Kinana

 Anna Mwakitosi aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Anna Mwakitosi akishangiliwa na wafuasi wa CCM baada ya kujiunga CCM

 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Ifarakara Mjini

 Sehemu ya umati wa wananchi uliofika kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wafuasi wa Chadema wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Stendi ya mabasi ya Ifakara mkoani Morogoro, Aprili 16, 2013.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Elias Masala (kulia), akijibu maswali mbele ya Kinana jinsi alivyopanga mikakati ya kuwaletea mandeleo wananchi wa wilaya hiyo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akimkabidhi ubani mtoto wa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero, marehemu Oswald Mkokochela, Edward wakati uongozi wa chama hicho ulipokwenda jana  kuifariji familia kwa msiba wa uliotokea juzi. Ifakara Mjini,

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocenti Kalogaries akimkabidhi ubani Edward.

RAILA ODINGA STILL FIGHTING TO THE END

Prime Minister Raila Odinga on Wednesday warned of an elaborate attempt to kill devolution even as governors from across the country demanded to meet President-elect Uhuru Kenyatta over the matter.

Mr Odinga urged governors and senators to unite in defence of devolution, warning that gains made in the Constitution that ushered in devolved governments could be lost.

The PM warned of attempts to undermine governors to dilute devolution, a system he said was being opposed by some government insiders.

He asked the government to allow governors to take over the offices currently occupied by provincial and county commissioners, saying that it was sad that some civil servants were humiliating governors.

“As a coalition, we stand strongly for the full and undiluted devolution of powers and resources to the counties,” said Mr Odinga. “That is why I want to call on all governors and county assembly members, regardless of party, to hold their ground, stand firm and demand to be given the full space and mandate to implement the devolution agenda for their voters”

He also urged senators to immediately initiate demands for full funding for devolved governments.

In Naivasha, where all the 47 heads of county governments were attending a workshop, they demanded an urgent meeting with the President-elect Kenyatta and his deputy, Mr William Ruto, get their commitment on devolved governments.

They have also expressed alarm at the manner in which the Treasury allocated Sh9.8 billion and then dictated how the money that the counties will spend over the next three months will be used.

Speaking on the sidelines of their first meeting, which is going on at the Great Rift Valley Lodge, the governors said they had sent messages to Mr Kenyatta asking for the meeting.

“We would like to know from him what he intends to do to ensure that there is immediate implementation of the procedures of devolution,” said Mr Isaac Ruto, the governor for Bomet.

He said the main agenda at the first meeting of the governors was to ensure success of the system that took effect with the election of governors and county assembly representatives on March 4.

He (Mr Kenyatta) committed himself to implementation, it is very clear in the manifesto and I think it is very important and incumbent on him to assure the governors that we intend to travel this road together,” Mr Ruto said.

Mr Kinuthia Wamwangi, who heads the Transition Authority, on Tuesday said that a meeting between Mr Kenyatta and the governors would be convened immediately he is sworn in.

Mr Ruto said statements from President Kibaki on Tuesday, when he officially opened the conference, were “disastrous” and suggested the lack of political goodwill to ensure devolution works.

On Tuesday, the governors were angry at the President’s insistence that despite the devolution of political power to the counties, Kenya remains a unitary state.

There is no unitary government in Kenya. We are simply in one republic called Kenya and the territory of Kenya is divided into 47 counties, and Kenya is a multi-party state and a sovereign state. That sovereignty is exercised at the national and county governments,” said Mr Ruto.

Wednesday was the meeting’s second working day and the governors embarked on a series of workshops to guide them on how to run the governments they now head.

In another tent nearby, the county speakers, their deputies, county clerks and interim clerks gathered for training on how the county assemblies ought to be run.

odinga

VIDEO YA LONDON FASHION WEEK YAINGIA MITAANI

Wabunifu  mitindo watatu walishiriki maonyesho ya mavazi London Fashion Week yaliyotayarishwa na shirika la British Council na kudhaminiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wetu Uingereza.

Tanzania na Nigeria ndiyo nchi pekee za Kiafrika zilizong’arisha “jua” lake kati ya mataifa zaidi ya 25.

Filamu hii fupi iliyotayarishwa na Urban Pulse wakishirikiana na Freddy Macha inakupa taswira ya mambo yalivyokua.

SOUTH AFRICAN ACTRESS MBOYA, TO CLIMB KILIMANJARO TO HIGHLIGHT WOMEN’S RIGHTS

 

Hlubi Mboya AKA Nandipa.

With the support of the United Nations and partners, an all-female team will climb Mount Kilimanjaro in Tanzania to highlight the importance of women’s rights and in particular, education for girls.

The team, which will commence their climb tomorrow, is made up of seven Nepalese women who have previously climbed Mount Everest, and three African women, including South African actress and World Food Programme (WFP) National Ambassador Against Hunger, Hlubi Mboya. Many of the women in the team have faced serious challenges to their education and development, and with the climb, they hope to inspire other young women.

“In Africa and Asia, young women and girls face barriers to education – early marriage and pregnancy, household duties, shortage of money for school fees and a preference for sending boys to school instead of girls,” <”http://www.wfp.org/news/news-release/all-female-team-climbs-africas-highest-peak-help-un-world-food-programme”>said WFP Country Representative Richard Ragan.

“All the team members have had to climb their own personal mountains, overcoming challenges to attend school and get where they are today. We hope their determination will be an example to youth everywhere.”

One of the Nepali climbers, Nimdoma Sherpa, was a recipient of WFP school meals before becoming the youngest ever female to climb Mount Everest at the age of 16 – a record she held until last year.

“At first my parents sent me to school just to get the meals,” said Ms. Nimdoma. “While there, I was encouraged to focus on my studies and this opened so many doors for me. I’ve learned that education and hard work can really take you places and I’m excited to be continuing my journey by climbing Mt. Kilimanjaro.” 

Among the African climbers is Ashura Kayupayupa, a youth activist advocating against early marriage, and teacher Anna Philipo Indaya from north central Tanzania’s nearly extinct Hadzabe hunter-gatherer people.

One of the climbers from Nepal ran away at the age of 14 to escape a forced marriage and another was a domestic worker in her teens.

“By staying in school and getting an education, girls can grow up to lead fulfilling lives and really contribute to their families and communities,” says Hlubi Mboya. “Providing them with a daily school meal helps them grow strong and concentrate on their studies. I like to think each step we take up Kili will bring girls in Africa a bit closer to reaching their potential.”

Their 5,895-metres climb will begin from the northern Tanzanian town of Moshi on Wednesday and if all goes according to plan, they will arrive at the summit on 4 March. A welcoming ceremony is scheduled to take place in Moshi the next day and will be followed by a news conference in Dar es Salaam on 7 March.

The climbers will record a special video message on Mount Kilimanjaro for International Women’s Day, observed on 8 March. They will also visit schools in Dar es Salaam and Arusha to tell their stories and highlight the importance of girls’ education.

The climb is being supported by the Tanzanian Government, WFP and Child Reach International, a non-governmental organization working with communities to improve children’s access to education and healthcare.

SOURCE UNITED NATIONS

DAR LIVE N’GOMA NZITO KHADIJA vs ISHA

Malkia wa mipasho, Khadija Kopa, akionesha umahiri wake wa kutikisa nyonga.

Mashabiki wanaomfagilia Isha Mashauzi wakiwa wamevamia steji baada ya kuwadatisha.

Aziza Abul ‘Bonge’ wa TOT Taarab akikamua.

Malkia wa mipasho akiserebuka na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani kumtunza.

Wakali Dancers wakiwajibika jukwaani.

Shabiki akimtunza Malkia wa mipasho baada ya kukunwa na mipasho.

Isha Mashauzi akikamua.

Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.

WAKALI wa miondoko ya muziki wa mwambao nchini, Malkia wa miondoko hiyo, Khadija Kopa akiwa na Kundi la TOT Taarab na Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ jana waliugeuza Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live kuwa uwanja wa mapambano baada ya kushindana kutoa burudani kwa kuonesha makali yao na kuwafanya mashabiki kila mmoja kumtaja mshindi wake.

Kabla ya wakali hao kuanza kuhenyeshana jukwaani burudani hizo zilianza kwa kunogeshwa na shoo kali ya washiriki wa shindano la Mic King linaloendeshwa ukumbini hapo kila Jumapili. Baada ya washiriki hao wanaowania gari, kundi la Wakali Dancers lilivamia jukwaa na kufanya vitu vyake pia.

(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

CAG AWAKAANGA VIGOGO WA TANESCO

The Controller and Auditor General (CAG), Mr Ludovick Utouh

The Controller and Auditor General (CAG), Mr Ludovick Utouh

  • Ripoti imekamilika na kubaini madudu.

  • Yaonyesha kuna kasoro katika ununuzi kwa kutofuata utaratibu na ubadilishaji wa fedha za kigeni(Dola) katka benki ambazo shirika halina akauti.

  • Pamoja na ripoti ya CAG kubaini makosa ya William Mhando hawawezi kumshtaki mahakamani

HITIMISHO la sakata la vigogo wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), litajulikana mwishoni mwa mwezi huu baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kukamilika na kuonyesha tuhuma nzito dhidi ya maofisa watatu wa shirika hilo.

Maofisa hao ambao kwasasa wanasubiri uamuzi wa bodi ya TANESCO ni pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi Harun Mattambo.

Maofisa hao walisimamishwa kazi julai 14 mwaka 2012 sambamba na aliyekuwa mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando, ambaye baadaye alifukuzwa kazi.

Akizungumza na gazeti moja la kila siku Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO Jenerali Mstaafu Robert Mboma alisema kazi ya kuwachunguza maofisa hao iliyokuwa ikifanywa na CAG imekamilika na wamepewa ripoti inayoonyesha kasoro kadha.

“Awali CAG alileta taarifa ambayo tuliikataa na kumtaka airekebishe. Hii ya sasa tumeikubali na kuielewa, kikubwa alichogundua ni manunuzi yasiyofuata utaratibu na suala la kubadilishwa kwa fedha za kigeni (Dola) katika benki ambazo Shirika halina akaunti,” alisema Mboma.

Aliongeza baada ya jopo la wakurugenzi kumaliza kuwahoji watuhumiwa hao, litawasilisha mapendekezo kwa bodi ambayo itatoa uamuzi wake.

Uchunguzi uliofanywa na M2S uligundua kuwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando hawezi kushtakiwa mahakamani kwa sababu makosa aliyoyafanya ya kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa kimaslahi ni makosa ya kiuadilifu na hayawezi kufunguliwa mashitaka.

hakimadini sera

SHEHENA YA NYARA YAKAMATWA ARUSHA, PETER LAURENCE ATIWA KOROKORONI.


Mtuhumiwa wa nyara za serekali Peter Laurence (mwenye kofia katikati) akiwa na maofisa wa Polisi, eneo la Kisongo mtaa wa Mateves nje kidogo ya jiji la Arusha baada ya kukamatwa na shehena ya nyara za serikali  nyumbani kwake.

Miongoni mwa nyara za serekali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu  nyumbani  kwa mtuhumiwa Peter Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.

Maofisa wa jeshi la polisi wakitoa mabox yenye nyara za serekali kwenye ghala la mtuhumiwa.

Ngozi ya Mamba ambayo ilikutwa kwenye ghala la mtuhumiwa ikiwemo meno ya tembo, vichwa vya simba, vichwa vya nyati, ngozi ya simba, ngozi ya tembo na nyara nyingine nyingi za wanyama mbali mbali.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA MAHMOUD AHMAD – ARUSHA).

Polisi mkoani Arusha, wamekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa eneo la Matevesi Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.

Nyara hizo ni pamoja na Ngozi za Simba, Chui na Mamba, meno ya Tembo, vichwa vya Nyani, Swala na Nyati na Pembe za kifaru.

Sambamba na hilo jeshi la Polisi mkoani Arusha wanamshikilia mtuhumiwa anayesadikiwa kumiliki nyara hizo aliyetambulika kwa jina la Peter Leurence (55) mkazi wa Ngaramtoni ambaye zilikutwa zikiwa zimehifadhiwa kwenye maboksi zaidi nyumba kwake.

Kamanda wa polisi mkoni Arusha, Liberatus Sabas alisema kuwa baada ya jeshi hilo kupata taarifa za siri majira ya saa 5 asubuhi walifika eneo la tukio majira ya saa 7 mchana na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa walinzi wa eneo hilo kwani waliwanyima kuwapa maelekezo ya kumpata mmiliki wa nyumba hiyo.

hakimadini 002

DIAMOND PLATNUMZ NATAKA KULEWA (PITIO LA WIMBO NA VIDEO)

COVER LA NYIMBO YA DIAMOND NATAKA KULEWA

COVER LA NYIMBO YA DIAMOND NATAKA KULEWA

Ujio mpya wa msanii maarufu zaidi wa kizazi Kipya kwa sasa hapa Tanzania Nasibu Abdul AKA Diamond Platnumz wa nyimbo na video ya NATAKA KULEWA, ikiwa ni kazi yake ya kwanza baada ya kufanya mabadiliko makubwa kwa uongozi unao simamia kazi zake, kwa sasa yuko chini ya Meneja anayejulikana kwa jina la Ragey Mohamed.

Siku za hivi karibuni kupiti mitandao ya kijamii yamesemwa mengi kuhusu nyimbo hii pamoja na video yake. Wengi wakidai kuwa Kijana amefikia mwisho lakini M2S Songs & VIDEO Review Unit  wanakuhakikishia kuwa kijana bado yuko vizuri kwa kukuletea moja kwa moja kupitia blog hii nyimbo, Video na mashairi ya nyimbo yenyewe. Lazima nikiri kuwa tokea nianze kusikiliza sijachoka kuisikia na video yake inayodaiwa kuongoza kwa kugharimu pesa nyingi mpaka sasa hapa Tanzania.

Nyimbo hii ya Nataka Kulewa imefanyika A.M Records chini ya Usimamizi wa Maneke (Producer), Mirindimo ya nyimbo hii ni ya Kiafrika inayorindima kwa kufuata staili ya Bondeni (South Afrika) huku Diamond akiwa anapita kwenye nyimbo hii kwa stail ya aina yake mashairi yakiwa yana zungumzia kwa nini anataka kulewa. Kwa ufupi anajaribu kuchukuwa taswira ya mwanaume ambaye ametatizwa au kutendwa kwenye mahusiano. Katika moja ya mistari analalama kuwa kusema “kumbe mjinga ni mimi ninaye tunza na wengine wanachukuwa, ho o mapenzi, yamenifanya ni lie kama mtoto, mie siwezi walionikuta waache ni seme jina.” Kwenye ubeti wa pili kwa hisia kubwa anabainisha “Ni kwa mapenzi mskini nikamvisha na pete kwa kutaka kumuoa, kukata vilimi limi vya wazushi wanawake wanamponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, siye tuko kama ishirini mabuzi vingasti wengine anawahonga”

Nyimbo hii ni tofauti na nyimbo za awali za msani huyu kama vile NALIA NA MENGI, KAMWAMBIE, MBAGALA na NITAREJEA. wimbo huu una tempo ya juu na hivyo kuufanya kutimiza malengo ya kuchezeka pamoja na kusikilizika. Tatizo kidogo ni kufanana kwa milindimo na merodi hasa mianguko na nyimbo yake iliyofanywa na Rama inayojulikana kwa jina la MOYO WANGU.

kwa Kwa kusikiliza bonyeza kitufe hapo chini ujipatie nyimbo pamoja na video huku ukifwatilia mashairi ya nyimbo hii. Kwa ujumla nakushauri usikilize nyimbo hii ambao M2S wameipa alama 4/5. Video yake nayo imepewa 4/5 ambayo imefanywa na an i-View Studios Director akiwa Ragey Mohamed.

UKITAKA AUDIO BOFYA HAPA

UKITAKA AUDIO BOFYA HAPA

 

DARAJA {Bridge}

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

UBETI WA KWANZA:

Usiniulize kwa nini? Sababu utazengua, ukitaka jiunge na mimi, kama ni pesa ww kunywa nitanunua, mie mwanzo sikuamini, nikajuaga vya kuzua, kumbe mjinga ni mimi, ninaye tunza  wenzangu wanachukuwa, ahi! oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, mie siwezi walionikuta waniache ni seme jina. oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, na nina mengi yamenikaa moyoni.

KIITIKIO:

Leo nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa, zikipanda nimwage radhi, nataka kulewa, lewa mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa, zikipanda nimwage ladhi

DARAJA {Bridge}

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

UBETI WA PILI:

Ni kwa mapenzi mskini, nikamvisha na pete kwa kumuoa, kukata vilimi limi vya wazushi wanawake wanamponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, sie tuko kama ishirini, mabuzi vingasti wengine anawaonga, oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, mie siwezi walionikuta waniache ni seme jina. oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, na nina mengi yamenikaa moyoni.

KIITIKIO:

Leo nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa zikipanda nimwage ladhi, tilalila nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa lewa, zikipanda nimwage ladhi

DARAJA {Bridge}:

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

Mashairi haya ni kama yalivyonukuliwa na M2S Songs Review Unit wakiwa wanausikiliza wimbo wenyewe. Sio mashairi rasmi, kwa maana kutoka kwa mtunzi na muimbaji mwenyewe.

TUNAWEZA BLOG ADVERT3

Miss Lou Acquiring Lore

Gallery of Life...

MAISHAZONE

ITS ALL ABOUT LIFE......For over 75 years, Jubilee Insurance has built a rich heritage of enriching lives by offering insurance solutions that make life carefree and rewarding.

this is... The Neighborhood

the Story within the Story

JAMIIBLOG

PAMELA MOLLEL

MEDIA 2 SOLUTION

- TRUTH SEEKERS -

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.