VIDEO:- KICHUPA CHA G-NAKO “MORALE”

  • Video ya wimbo wa G-Nako, ‘Morale’ iliyoongozwa na Hanscana.

Hii ni moja ya vichupa vya hivi karibuni kabisa vya G-Nako ambayo inakwenda kwa jina la Morale, mwonekano wake ni mzuri na imefanyika katika mazingira ya kitaa…

Labda jambo lililonifurahisha kwenye nyimbo hii hususan mashairi yake ni pale G anaosikika akisema anapingana na wale wanao sema “Nako2Nako is back”.

Hebu tazama kichupa hiki na ujiinjoi

 

Advertisements

WIMBO MPYA WA HAPPY BALICE “LIAR”

Happy Balice

Sikiliza wimbo wa mdada Happy Balice, wimbo huu unaitwa “LIAR”

Bofya hapa chini kusikiliza…

http://www.hulkshare.com/bongofive/liar-happy-balice

Advertisements

WIMBO WA AT “SITAKI KUSEMWA”

AT-MSANII-600x400

SITAKI KUSEMWA ni ngoma mpya ya mkali wa Muziki wa Mduara AT, ambaye aasema hii ni Style yake mpya inaitwa Taracha ngoma imefanyika katika Studio ya AT zinazo julikana Palace Music, nyimbo hii imefanywa na Producer Davidizo.

BOFYA HAPA KUSIKILIZA…

http://www.hulkshare.com/bongofive/at-sitaki-kusemwa

Advertisements

WIMBO MPYA WA SHO DADDY Ft BOB JOUNIO “MAPENZI LAWAMA”

MAPENZI YA LAWAMA SHODADY Ft BOB JUNIOR

Pata mwimbo mpya kutoka kwa msani mpya Sho Daddy ambaye amemshirikisha bob Jounio unaojulikana kama “Mapenzi Lawama”

BOFYA HAPA KUSIKILIZA

http://www.hulkshare.com/bongofive/sho-daddy-feat-bob-junior-mapenzi-ya-lawama

Advertisements

VIDEO MPYA YA FEZA KESSY “MY PAPA”

Cheki video mpya ya wimbo wa “MY PAPA” kutoka kwa Feza Kessy ambayo imefayika Afrika ya kusini.

Advertisements

WIMBO WA G RICO “DHARAU”

grico-1024x568

Huu ni wimbo mpya kutoka kwa G Rico Classic ngoma inaitwa “Dharau” imefanyika Kiri Records.

BOFYA HAPA KUSIKILIZA

http://www.hulkshare.com/bongofive/g-rico-classic-dharau-mkamanga-com

Advertisements

BEHIND THE SCENES: VIDEO ANACONDA YA NICKI MINAJ

NICKI MINAJ

Weekend iliyopita rapper wa Young Money, Nicki Minaj alishoot video ya wimbo wake mpya ‘Anaconda’ itakayopatikana kwenye album ya ‘The Pink Print’. Pata kilichojiri wakati wa utengenezaji wa video hiyo (behind the scenes ).

Advertisements

SIKILIZA SONGI JIPYA LA PIPI YA KIJITI KUTOKA KWA MENINAH

Menina-Pipi-Ya-Kijiti-Teaser-Cover-21

Mwanadada Meninah ameachia ngoma yake Mpya “Pipi ya Kijiti”. Hii ikiwa ni nyimbo yake baada ya ile video ya kacopy na ku-paste .

Nyimbo hii mpya imefanyika kwenye studio za A.M Records chini ya usimamizi wa producer Bob Manecky.

bofya hapa chini kusikiliza

http://www.hulkshare.com/bongofive/menina-pipi-ya-kijiti-1

//
Advertisements

“WAHENGA WALINENA UTAVUNA ULICHOPANDA, MAPENZI TELE KWA KILA MTU”, LADY JAYDEE

Lady Jaydee

Lady Jaydee  July 27 alitangazwa kuwa washindi katika tuzo za AFRIMMA 2014 nchini Marekani alipo shinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kike Afrika mashariki. Tuzo hizo ziliwashindanisha wanamuziki mbalimbali wakubwa wa Afrika.

Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Facebook aliwashukuru mashabiki wake, aliandika:

“Nashukuru wote mnaokubali kazi zangu, wote mnaosimama na kutetea JayDee bila kusita, nashukuru kwa Tuzo nyingine tena toka AFRIMMA . Wahenga walinena kuwa utavuna ulichopanda, mapenzi tele kwa kila mtu”

jide afrimma

Katika post nyingine Jide amepost picha ya tuzo yake na kuandika:

“Tuzo yangu ya 30. Asanteni kwa ushirikiano, nimeipokea na ninarudi nayo nyumbani. Shhhhhh! !!! Kimya Kimya”.

Advertisements

SIKILIZA WIMBO MPYA WA JOSE CHAMELEONE UITWAO “WALE WALE”

Muimbaji wa Uganda, Jose Chameleone ameachia single yake mpya iitwayo Wale Wale.

“To all my fans worldwide Brand new!!!!! “WALE WALE” as i Activate invasion 2015,” hayo ndiyo maneno aliyoandika kwenye ukuta wake wa kitabu (Facebook).

//
Advertisements

VIDEO: MR BLUE AKIWA NA VIJANA WA B.O.B MICHARAZO WAMEACHIA KICHUPA KIPYA KIITWACHO “SHUT UP” (KIMYA).

Vijana wa B.O.B Micharazo, wakiongozwa na front runners, Mr Blue na Nyandu Tozi, wameachia video ya ngoma yao mpya iitwayo ‘Shut Up’ (Kimya).

Kwenye ngoma hiyo iliyotayarishwa na Marco Chali, rappers hao wanafanya mtindo wa kubeto na hivyo kupeleka onyo kali kuwanyamazisha wapinzani wao. Katika verse ya Mr Blue ambaye amesima vizuri amefungua ngoma hiyo kwa panch “Helo Dar es Salaam mbona kimya jiji zima mbona limezizima/Hakuna cha Sharobaro wala ming’aro ya kuazima/ Mmebakiza uharo kumbe washenzi mlipima/Wabaya wetu mbona kimya, vipi wazima au nanyinyi mlipima,” anarap Kabayser.

Wengine waliochana kwenye ngoma hiyo ni Blood Gaza, Bobby MC, Cotton, Uswege na Beka Title aliyesimama kwenye chorus.

Advertisements

VIDEO MPYA KUTOKA KWA MKALI J. MARTINS FT DJ ARAFAT “FARO”

Mkali kutoka Nigeria J. Martins ameachia video mpya ya wimbo wake ‘Faro’ akiwa amemshirikisha Dj Arafat. J.Martins na Dj Arafat wanaonekana kuwa na mchanganyiko mzuri sana wanapoimba pamoja, wimbo mwingine ambao walishirikiana ni single iliyopita ya J.Martins ‘Touchin body’ iliyotoka mwaka jana. Itazame hapa video mpya.

Advertisements

SUBIRA NDIYO NYIMBO MPYA YA SHAA YENYE LADHA ZA KISWAZI; BONGE LA NGOMA JIINJOI HAPA…

SHAA SUBIRA GROUP

Shaa ameachia muendelezo mwingine wa ladha za kiswazi. Awamu hii amekuja na wimbo uitwao Subira uliotayarishwa na Shirko. bofya hapa kusikiliza ….


http://www.hulkshare.com/bongofive/shaa-subira

 

Advertisements

VIDEO: SNURA AMEACHIA KICHUPA KIPYA CHA WIMBO WAKE “USHAHARIBU”

Msanii wa muziki Snura Mushi, ameachia video ya wimbo wake ‘Ushaharibu’ chini ya director AJ. Itazame hapa.

Advertisements

WIMBO KWA AJILI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADAHAN; BOB HAISA

Bob-Haisa-ramadhan kareem

Msanii Bob Haisa kutoka Jiji Mwanza amechia wimbo Maluum kwa ajili ya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadahan wimbo unaitwa “Ramadhan Kareem” Bofya hapa kusikiliza …

http://www.hulkshare.com/bongofive/bob-haisa-ramadhan-kareem-hassbaby-blog

Advertisements

NYIMBO MPYA YA SAMMY; “WAIT FOR ME”

Sammy-wait 4 me

Sammy ni msanii Mpya, ametambulisha nyimbo yake mpya inaitwa “Wait For Me” ngoma imefanyika Bm Records Producer Jack Power. Bofya hapo kuisikiliza….

http://www.hulkshare.com/bongofive/sammy-wait-for-me

Advertisements

KAZI YA UKAGUZI NA URASIMISHAJI WA KAZI ZA MUZIKI NA FILAMU LAANZA; TRA

Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’ imetoa tangazo kwa tasnia za sanaa ya filamu,muziki, kwa kuanza zoezi la urasimishaji wa kazi za wasanii kwa kuanza kukagua bidhaa za wasanii na kuziwekea stika.

10431899_340541062760789_1672094960_n

Taasisi za Serikali zilizokabidhiwa jukumu la kushughulikia urasimishaji wa tasnia za sanaa ya muziki na filamu, zimeanza rasmi zoezi la kukagua na kukamata bidhaa zote za muziki na filamu ambazo hazina sifa ya kuuzwa na kusambazwa katika soko la ndani na kupelekwa nje ya nchi.

Sheria ya Ushuru wa Bidhaa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012, na kupitishwa kwa kanuni zake mwaka 2013 inamtaka kila mfanyabiashara wa bidhaa za muziki na filamu kuhakikisha kuwa bidhaa zote za muziki na filamu zinawekewa stempu za Ushuru wa Bidhaa zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kabla ya kusambazwa.

Taasisi za Serikali zinazohusika katika zoezi hili ni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania (TFCB), Chama cha Hakimiliki na Hakishirikishi Tanzania (COSOTA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Taasisi hizo kwa pamoja zimekuwa zikitoa elimu kwa wadau wote wanaojihusisha na utengenezaji, uaigizaji, usambazaji na uuzaji wa bidhaa zinazohusika na muziki na filamu pia kuhakikisha kuwa wanakamilisha mchakato wote wa uwekaji stempu za Ushuru wa bidhaa kwa kazi zinazoingizwa katika soko la ndani na zinazosafirishwa nje ya nchi.

Kwa mujibu wa sheria wahusika wote wa uzalishaji, uagizaji toka nje ya nchi na usambazaji wa bidhaa hizo wanatakiwa kufika kwa taasisi hizo ili kusajiliwa na kukamilisha utaratibu wa kusajili na kukaguliwa kwa kazi husika kabla hazijapatiwa stempu za Ushuru wa bidhaa kwa ajili ya kubandikwa kwenye kazi husika.

Utaratibu unawataka wale wote wanaokusudia kushughulika na kazi za muziki kuanzia BASATA na baada ya hapo kufika COSOTA ambapo huko hupewa vibali kabla ya kwenda TRA ili kununua stempu. Kwa kazi za filamu wahusika wanatakiwa kwenda Bodi ya Ukaguzi wa Filamu kabla hawajapeleka kazi husika COSOTA na baadaye TRA kwa ajili ya ununuzi wa stempu.

Stempu hizi zinapatikana ofisi za Idara ya fedha, Makao Makuu ya TRA. Kila kazi, yaani CD, DVD au kanda zinatolewa stempu mbili zenye namba moja katika mtiririko maalum wa namba (serial number). Stempu moja hubandikwa katika kasha na nyingine kwenye CD, DVD au kanda. Utaratibu unamtaka mhusika anayehitaji stempu kuwasilisha maombi tofauti kwa kila kazi husika. Hairuhusiwi kuweka stempu zilizoombwa kwa ajili ya kazi moja kwenye kazi nyingine hata kama kazi hizo zimetolewa na mzalishaji au msambazaji mmoja.

Aina za stempu na matumizi yake ni kama ifuatavyo:

  • Filamu toka nje ya nchi – rangi ya kijani (green).

  • Muziki toka nje ya nchi – rangi bluu (blue).

  • Filamu zilizotengenezwa ndani ya nchi – zambarau (violet)

  • Muziki wa ndani ya nchi – rangi ya pinki (pink)

Advertisements

LADY JAY DEE AFUNIKA SHOW YA MASAKU RUGBY 7S AFTER PARTY NAIROBI

Lady Jaydee alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Masaku Rugby 7s After Party lililofanyika Jumamosi jijini Nairobi. Takriban watu 40,000 walihudhuria kwenye show hiyo iliyodhaminiwa na Tusker Lager. Wasanii wengine walitumbuiza ni pamoja na Jua Cali, Radio n Weasel, Wyre, Kidum, Keni wa Maria.

Copy of image

Copy of image(7)

Copy of image(6)

Copy of image(5)

Copy of image(4)

Copy of image(3)

Copy of image(2)

Copy of image(1)

Advertisements

{VIDEO} KICHUPA KIPYA CHA KALA JEREMIAH Ft NAY WA MITEGO; “SIMU YA MWISHO”

simu ya mwisho

Video Mpya kutoka Kala Jeremiah akiwashirikisha Nay Wamitego na Mo Music ngoma initwa “Simu ya Mwisho” Video imeongozwa na Director Pablo

Advertisements