BBC SASA KUNGURUMA KUTOKEA DAR ES SALAAM

19Idhaa ya kiswahili ya BBC imezindua rasmi studio zake za jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ni matokeo ya mkakati na uwekezaji wa miaka mingi wa shirika la BBC duniani kuhakikisha kuwa matangazo yake yanawafikia wasikilizaji katika hali ya ubora wa hali ya juu na ya kisasa zaidi.

2

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika ofisi hizo hizo mpya zilizoko eneo la Mikocheni, mkuu wa kitengo cha uandishi wa habari katika BBC, Nicki Clarke, ameshukuru serikali ya Tanzania, kwa kuwaruhusu kujenga studio hizo za kisasa zitakazoinua tasnia ya habari nchini humo na uhuru wa habari kwa ujumla.

7

Naye mkuu wa ofisi ya Dar es Salaam, Hassan Mhelela mbali na kuwataka wafanyakazi wa BBC Tanzania, kuzidi kuonyesha ushirikiano pamoja na utendaji kazi wa pamoja, pia ametangaza kuanishwa rasmi kwa ushirikiano kati ya BBC na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari.

11

Ushirikiano huo amesema kuwa unalenga kusaidia kutoa mafunzo kwa wandishi wa habari chipukizi walioko mafunzoni katika chuo hicho, ambao kwa nyakati tofauti, watakuwa wakijiunga na BBC ili kupata mafunzo katika uandaaji vipindi vya redio na televisheni pamoja na utangazaji.

22

Kwa upande wa BBC, kuanzishwa kwa ofisi hii, yenye studio za kisasa kabisa za redio na televisheni mbali na kuongeza ubora wa vipindi lakini pia kutawezesha matangazo ya redio na televisheni kufanyika moja kwa moja kutokea Dar es Salaam.

Na kuanzia sasa matangazo ya Amka na BBC yatakuwa yakiandaliwa Dar es Salaam.

Itakumbukwa kuwa Tanzania mbali na kuwa na wasikilizaji wengi wa idhaa ya kiswahili ya BBC, lakini pia ndiko kunakozungumzwa zaidi lugha ya kiswahili.

Tanzania pia ina rekodi ambapo mtangazaji wa kwanza au sauti ya kwanza iliyosikika mwaka 1957, ilikuwa ya mtanzania Oscar Kambona ambapo alikuwa mwanafunzi mjini London.

26

12

13

14

16

17

18

22

25
Chanzo: BBC Swahili

Advertisements

WAKAZI MTO WA MBU NA WAFANYAKAZI WA HIFADHI YA ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA

DSC_0281

DSC_0285

DSC_0286

DSC_0290

DSC_0292

DSC_0296

DSC_0301
Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani

WAKAZI HAO WA KATA YA MTO WA MBU waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko

Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbal;i wanaokuja kutembelea mbuga hizo

Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu.

SOURCE:- MAHMOUD AHMAD

TACAIDS WAONGEA NA WANAHABARI KWENYE VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa

 

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva Matemu)

STENDI KUU YA MABASI YAFUNGULIWA JIJINI MBEYA

Wakazi wa jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi katika stendi kuu mpya iliopo eneo la nane nane RRM kwaajili ya kuomba maeneo ya kufanyia biashara zao katika eneo hilo.Wageni kutoka mikoani mnataarifiwa kua stendi kuu ya jiji la Mbeya kwa sasa ipo eneo la nanenane (karibu na Uyole) na si mjini soko matola tena kama iliyokuwa hapo awali,lakini si wa mikoani tu bali hata baadhi ya wilaya za jiji la Mbeya.Hivyo ukifik jijini Mbeya usishangae kuambia kuwa basi linaishia hapo eneo la Nane nane,kwani ndipo ilipo Stendi Kuu mpya kwa sasa na siku zote.

 

Muonekano wa eneo la Stendi kuu hiyo.
Abiria wakisubiria Usafiri kwenye stendi kuu hiyo.
Sehemu ya kuingilia Mabasi.
Mabasi madogo yanayofanya safari zake katika baadhi ya Wilaya za Jiji hilo la Mbeya.
Sehemu ya Wakazi wa Jiji la Mbeya waliojitokeza kwa ajili ya kuomba maeneo ya kufanyia biashara zao kwenye Stendi kuu Mpya ya jiji la Mbeya.Picha zote na Fadhil Atick

SERIKALI YALEGEZA MSIMAMO, SASA KUFUTA MISAMAHA YOTE YA KODI

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.PICHA KUTOKA MAKTABA

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.PICHA|MAKTABA

Dodoma. Waziri ya Fedha, Saada Salum Mkuya jana aliwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014, ambao umefuta misamaha ya kodi katika maeneo yaliyokuwa yakilalamikiwa na watu wa kada mbalimbali nchini.

Katika muswada huo Serikali imefuta misamaha ya kodi ya mapato inayotokana na  michezo kubahatisha na ukodishaji wa ndege nje ya nchi.

“Muswada umependekeza  waziri husika kutotoa msamaha wa ushuru wa mafuta kwenye mafuta isipokuwa mafuta ya petroli yanayotumika kwenye miradi mbalimbali inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo,” alisema Mkuya.

Mkuya alisema kuwa katika muswada huo, Serikali imeondoa saruji, nondo na mabati katika orodha ya bidhaa zinazochukuliwa kuwa ni bidhaa za mtaji ambazo kwa sasa hupata msamaha wa kodi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Lengo ni kuhamasisha uzalishaji wa saruji, nondo na mabati pamoja na kulinda viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini dhidi ya ushindani wa bidhaa za aina hiyo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi,”alisema Mkuya.

Alisema kuwa Serikali imefuta msamaha wa kodi ya mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya nchi ili kupunguza misamaha isiyokuwa na tija.

“Marekebisho haya yanalenga kutoza mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya nchi, badala ya kusamehe kodi ya mlipakodi asiye mkazi, ambaye hatimaye hulazimika kulipa kodi itokanayo na mapato hayo nchini kwake,”alisema Mkuya.

Marekebisho hayo yanapendekeza kufuta misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni ya simu isipokuwa vifaa vya ujenzi wa minara ya simu.

Pamoja na marekebisho hayo muswada huo unapendekeza kuongeza kifungu cha 3(d) ili mtu yoyote asiruhusiwe kutoa misamaha ya kodi kwa miradi nayohusu upanuzi na ukarabati wa miradi inayofanywa na wawekezaji.

Aidha ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi (soda) pamoja na kwenye maji ya matunda (juice), iliyotengezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini utabaki kama ulivyo sasa ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Mkuya alisema vinywaji baridi vimefanyiwa marekebisho ambapo ushuru kwenye vinywaji hivyo utapunguzwa kutoka Sh 91 kwa lita hadi Sh 55 kwa lita.

VIINGILIO VYA SABASABA MWAKA HUU KULIPWA KWA M-PESA.

001 SABAZMeneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna Bulando.

003 SABAZKaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa na usalama katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kulia ni Meneja  bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom.

Ni kupitia huduma ya M pesa

-Watu wazima kulipa 2500/- kwa siku na watoto 500/-

-Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/-  maroli ni 40000/-

Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayoanza tarehe 28 ya mwezi juni hadi tarehe 8 mwezi julai.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Anna Florence Bulondo amesema viingilio vya mwaka huu havina tofauti na vya mwaka jana lakini sasa yamefanyika maboresho ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kielectroniki na kwa njia ya M -pesa.

“Viingilio vya mwaka huu ni Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000.” Alisema Bulondo.

“Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.”

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa, katika maonesho ya Mwaka huu, Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na kutakuwa na Ulinzi wa Uhakika pamoja na Camera maalum zitakazo wekwa katika mageti na sehemu mbalimbali kuzunguka maeneo yote ya maonesho.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema kwa mwaka wa pili sasa wameendelea kuwawezesha watu, kufanya malipo ya tiketi kwa njia ya M pesa.

“M pesa inaendelea kurahisisha maisha ya Watanzania na mwaka huu, watu wote watakao kuja katika maonesho haya tumewawezesha kulipa viingilio kupitia M pesa na pia kufanya manunuzi na kulipa kwa M pesa katika banda letu la Vodacom.” Alisema Twissa.

Malipo ya ada binafsi.

1. Kwa siku – watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-

2. Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-

3. Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-

4. kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-

5. malipo kwa kipindi chote cha maonyesho – Beji kwa wahusika wa maonyesho   – 20,000/-

6. Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/- 

Tiketi za uegeshaji magari.

1. Kwa siku (magari madogo)  – 4,000/-

2. kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-

3. Malipo kwa pamoja – 200,000/-

4. Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-

5. Maroli na magari makubwa – 500,000/-

6. Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-

Maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kununua vitu mbalimbali kwa gharama nafuu na kupata fursa ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.

SERENGETI BREWERIES LIMITED (SBL) YAPATA MWENYEKITI MPYA WA BODI YA WAKURUGENZI

Kampuni ya Serengeti Breweries Limited ( SBL ) inatangaza utuezi wa Ndg. Nehemia Mchechu kama Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL. Uteuzi wa Ndg. Mchechu unafuata ukamilisho wa umiliki wa Mhe. Jaji (mstaafu) Mark Bomani . Katika nafasi yake mpya , Bw Mchechu pia atakukwa memba ya bodi ya kampuni ya bia ya East Africa.

Ndugu Nehemia Mchechu kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa( NHC) . Bw. Mchechu anauzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi. Hapo awali alishika nafasi muhimu katika sekta ya benki , hasa kama Mkuu wa Masoko Kimataifa na mkurugenzi msaidizi benki ya Standard Chartered, na kuwa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .

Ndugu Mchechu ana Shahada ya Biashara (Fedha) na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye pia ni Rais wa Umoja wa wanfunzi waliomaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na mwanachama wa ACI – Financial Market Association Tanzania.

Miongoni mwa nafasi nyingine muhimu, Ndugu Mchechu pia ni Mkurugenzi na mwanachama wa CEORT na pia ni Mkurugenzii wa TIC.

SBL inachukua fursa hii kumkaribisha na kumpongeza Mwenyekiti wake mpya wa bodi na kuwashukuru mwenyekiti wa bodi Mheshimiwa Bomani kwa mchango wake bora na wa kipekee wakati wa uongozi wake.

Mwenyekiti wa Bodi ya SBL aliemaliza muda wake,Mh. Mark Bomani akimpongeza mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo,Ndg. Nehemia Mchechu mara baada ya hafla ya kumpongeza.

Picha ya pamoja na Sehemu ya Wakurugeni wa SBL.

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya SBL,Ndg. Nehemia Mchechu akizungumza machache kwenye hafla hiyo.

 

WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA CHINA WAKUTANA LEO DAR

PIX 1.Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akihutubia viongozi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara maarufu wa ndani na nje ya nchi katika Jukwaa la Pili la biashara kati ya Tanzania na China lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 2.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akiwahutubia baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara maarufu wa ndani na nje ya nchi katika Jukwaa la Pili la biashara kati ya Tanzania na China lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 4.Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginard Mengi akitoa hotuba yake fupi kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara maarufu wa ndani na nje ya nchi katika Jukwaa la Pili la biashara kati ya Tanzania na China lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 5.Baadhi ya wajumbe wakiwemo wafanyabiashara maarufu wa ndani na nje ya nchi wakifatilia hotuba zitolewazo na viongozi kuhusiana na maendeleo makubwa ya kibiashara yafanywayo na Serikali ya Tanzania na ya Jamhuri ya Watu wa China leo katika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 6.Viongozi kutoka Serikali ya China na Tanzania wakitiliana saini mikataba ya makubaliano  inayohusu miradi ya maji yenye lengo ya kuisaidia Tanzania katika sekta ya maji wakati wa Jukwaa la Pili la biashara kati ya Tanzania na China lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 7.Viongozi kutoka Serikali ya China na Tanzania wakitiliana saini mikataba ya makubaliano  inayohusu miradi ya maji yenye lengo ya kuisaidia Tanzania katika sekta ya maji wakati wa Jukwaa la Pili la biashara kati ya Tanzania na China lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 8.Viongozi kutoka Serikali ya China na Tanzania wakibadilishana mikataba mara baada ya kutiliana saini leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam.

PIX 9.Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akimshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) mara baada ya kukabidhi pikipiki kwaajili ya Jeshi la Polisi Tanzania leo baada ya kukamilisha mkutano wa Jukwaa la Pili la biashara kati ya China Tanzania lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam. PIX 10.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (wa saba toka kushoto, mstari wa mbele waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda (katikati) walipokutana leo baada ya kukamilisha mkutano wa Jukwaa la Pili la biashara kati ya China Tanzania lililofanyika leo katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jijini Dar es Salaam.

KAMISHNA WA MAGEREZA NAMIBIA ATEMBELEA GEREZA LA KARANGA MOSHI

imageKamishna wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Magereza Mkoani Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014 Mkoani Kilimanjaro. image_1Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Rafael Tuhaferi(wa pili kushoto) akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Kiwanda cha viatu, Gereza Karanga Moshi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa. image_2Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakishona viatu vya ngozi katika Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Wafungwa hao wamepewa Mafunzo ya Ufundi wa kutengeneza viatu vya aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa ambapo kutokana na ujuzi huo pindi wamalizapo vifungo vyao watakuwa wamepata ujuzi ambao utawasaidia huko katika jamii zao. image_3Viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa Nchini vinavyotengenezwa na Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi. Kiwanda hicho pia hutengeneza viatu vya ngozi vya aina mbalimbali ambavyo hutumiwa pia hata na raia. photoKamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Tuhaferi(suti nyeusi) akiteta jambo na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(vazi la drafti) alipotembelea Kiwanda cha Viatu, Gereza Kuu Karanga Moshi, Juni 21, 2014. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro.

TIGO, DTBI NA COSTECH WAJA NA MBINU MPYA ZA AJIRA KWA VIJANA


4

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya utiliaji saini kati ya kampuni ya Tigo na kituo cha biashara ya teknohama DTBi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez na Afisa Mtendaji Mkuu wa DTBi Eng. George Mulamula.

Tigo Tanzania leo imeingia katika ushirikiano na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi)  ambayo itaona kampuni hiyo ya simu ikiwezesha washiriki wa teknohama kukuza vipaji vyao kupitia mpango maalum wa mafunzo na biashara ambayo itasaidia kukuza ajira nchini kupitia taaluma hii ya teknohama.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo katika makao makuu ya Tume ya Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Bw. Diego Gutierrez alisema kwamba ushirikiano huo na DTBi utawapatia watanzania ambao ni wanasayansi wa baadaye fursa ya kujifunza na kuendeleza vipaji vyao huku biashara inayotokana na teknohama ikizidi kukua na kuchangia suluhu za kidigitali katika jamii.

 “Hadi sasa teknohama inachangia asilimia 2.3 katika GDP ya nchi, Tigo ina dhamira ya dhati katika kuhakikisha kiwango hiki kinakua kupitia uwekezaji wa rasilimali watu. Ni kwa sababu hii kupitia Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Tigo pia tunatoa ahadi kuwasomesha watanzania 10 katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kila mwaka, pamoja na kutoa nafasi ya mafunzo na nafasi za ajira kwa wale ambao wamejikita katika masomo ya Teknohama,” Gutierrez alisema.

3

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kushoto) wakimsikiliza kwa makini mmoja wa washiriki wa mpango maalum wa Tigo na DTBi katika kukuza vipaji vya teknohama Bw. Godfrey Magila ambaye ameweza kubuni programu ya kuangalia vipindi vya Bunge kupitia simu za mkononi za kisasa. Tigo pia itatoa fursa za mafunzo kwa vitendo na nafasi za ajira kwa wale ambao wamejikita katika masomo ya Teknohama.

Gutierrez aliongeza, “Hii inaendana barabara na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ya mwaka 2015 na sera ya Tanzania ya Teknohama ya mwaka 2013 katika kuongeza upeo wa ufahamu wa masuala ya teknohama katika jamii ya watanzania. Kwahiyo tunafuraha ya kuungana na serikali ili kutoa mchango wetu katika kufanikisha hili.    

Utiaji saini wa ushirikiano huu ulishuhudiwa na Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia Professa Makame Mbarawa ambaye aliipongeza Tigo na DTBi kwa kuingia katika ushirikiano huo. Alisema, “Serikali inayo furaha kubwa sana kuwaunga mkono katika ushirikiano huu ambayo utaendelea kuwawezesha vijana na wajasiriliamali wa teknohama kupata maarifa na msaada katika kukuza ubunifu wao ili kuweza kushindana kikamilifu katika soko la biashara siku za usoni.”

“Tunaamini ya kwamba ushirikiano huu hautatoa fursa ya ajira tu kwa vijana wetu kuonyesha ubunifu wao  bali utawawezesha pia kuweza kujipatia kipato  na kupanua wigo wa aina za biashara zitakazoweza kufanyika hivyo kuwezesha ukuaji wa kasi wa maendeleo ya kiuchumi na kifedha katika jamii yetu. Napenda kuipongeza Tigo, DTBi na COSTECH kwa ushirikiano wao huu ambao utakuza  teknolojia na kutengeneza thamani kubwa ya biashara za aina yake kwa vijana,” alisema Mbarawa.

Akizungumza katika uzinduzi wa ushirikiano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa DTBi Engineer George Mulamula alisema kwamba ushirikiano huu utawapa washiriki fursa mbalimbali kuonyesha vipaji vyao kitaifa na kimataifa.

2

Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kulia) akitiliana saini na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Eng. George Mulamula kama ishara ya  ushirikiano kati ya Tigo na kituo hicho cha biashara ya teknohama DTBi. Wanaoshuhudia kutoka nyuma ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk. Hassan Mshinda. Tigo itatoa nafasi ya kuwasomesha watanzania 10 katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kila mwaka.

“DTBi inalenga katika kutengeneza utamaduni wa ujasiriamali wa teknohama pamoja na kuongeza ajira katika wigo wa ubunifu wa teknolojia. Tuligundua ya kwamba washiriki wetu walikuwa wanakosa uzoefu wa kutosha pamoja na uzoefu wa mazingira  ya kufanya biashara ambao ungewawezesha kuwafanya kuwa wajasiriamali bora zaidi. Kwahiyo tuna matumaini makubwa ya kwamba Tigo watatusaidia kutatua tatizo hili,” alisema Engineer Mulamula.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk. Hassan Mshinda pia alisema kwamba ushirikiano huu kati ya Tigo na DTBi unaenda sambamba na dira ya tume hiyo katika kuendeleza uchumi wa taifa kupitia ukuaji wa maarifa, utafiti na maendeleo ya teknolojia pamoja na ubunifu kwa ajili ya maendeleo nchini Tanzania. Aliongeza, “Tigo inawapa fursa ya kipekee washiriki wetu wa teknohama katika kutimiza ndoto zao.”

“Kupitia ushirikiano kama huu wa kidigitali tunaweza tukafanya kazi na sekta binafsi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi huku tukikuza kiwango cha teknohama na maarifa yake kwa wadau mbalimbali nchini,” alisema Dk. Mshinda. “Pia ni namna ya kuonyesha kwamba kupitia ubunifu unaotokana na sayansi na teknolojia tunaweza pia kuendeleza ufanyaji biashara ambao utatoa matokeo chanya katika uchumi wetu pamoja na kutuongezea  nafasi za ajira nchini. ”

1

Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (wa pili kulia) akipongezana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) Engineer George Mulamula mara baada ya kutiliana saini ya ushirikiano ambapo Tigo itawawezesha washiriki wa teknohama wa DTBi kuendeleza vipaji vyao kupitia mpango maalum wa mafunzo na biashara ambayo itasaidia kukuza ajira nchini kupitia taaluma ya teknohama. Kushoto ni Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Hassan Mshinda.

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA MABALOZI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo  na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya  mkutano aliowaandalia Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).Picha na IKULU

TMF YAJIONGEZA KWA KUPANUA WIGO, SAFARI HII WAJA NA MRADI MPYA WA MAFUNZO KWA WANAHABARI WA TANZANIA.

DSC_0540

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake  ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri  na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.

WAANDISHI WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna weka taaluma yao rehani.

Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na watayarishaji wa vipindi vya luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati wa kuripoti.

“kuendelea kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Kabaka

Amesema mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

DSC_0434

Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani.

Kabaka aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.

“kwa sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya kusambaza madawa hayo hatari,”

“kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626 walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,” alisisitiza Kabaka.

Amesema nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.

DSC_0515

Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA), Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

Kwa upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari hapa nchini.

“kwa kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri

Usiri aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye nchi.

DSC_0423

Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika sekta husika (Specialization).

DSC_0490

Wadau watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya Kudhibiti dawa za kulevya.

DSC_0458

Wadau mbalimbali na wageni waalikwa wakifuatilia yaliyojiri kwenye uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, viwanda, jinsia, madawa ya kulevya, kuzuia madawa ya kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.

DSC_0498

Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo amesema kwamba mradi huo umekuja katika muda mwafaka kwa taifa la Tanzania kwa sababu takwimu za matumizi ya dawa za kulevya zinatisha kwa vijana ni lazima taasisi za ndani na jamii za kimataifa kushirikiana kupambana na janga hili.

DSC_0405

Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali.

DSC_0406

DSC_0410

DSC_0395

DSC_0418

Afisa Habari kutoka kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari (UNIC), Stella Vuzo (kulia) pamoja na Bw. Phillip Musiba kutoka UNIC.

DSC_0432

Afisa mafunzo wa TMF, Bi. Raziah Mwawanga akinakili mambo muhimu yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi huo.

DSC_0414

 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya (kushoto) na Mwandishi wa Habari Mkongwe Mama Eda Sanga (katikati) ambaye ni miongoni mwa mentors kwenye mradi huo. Kulia Sawiche Wamunza kutoka UNFPA.

DSC_0416

DSC_0442

Mkurugenzi wa kampuni ya Branding Resources Limited, Abdul Razak Badru ambaye amesema kwamba kampuni yao inasadia kutoa mafunzo na ushauri jinsi ya kutengeneza kipato cha ziada bila ya kutegemea ufadhili wadhamini katika kuendesha taasisi mbalimbali nchini zikiwemo redio za jamii.

DSC_0479

Mwakilishi kutoka kampuni ya Life Media Cooperation, Lutundwa Kasese ambaye amesema kwamba watu wengi wanaoingia kwenye tasnia ya filamu na uatayarishaji wa vipindi vya luninga hawana uelewa wa kutosha kwa sababu ya kukosa mafunzo na kunachangia kudidimiza taaluma ya filamu kwa ujumla.

DSC_0469

Mwakilishi wa Tamwa, Zanzibar, Mzuri Issa Ali amesema mradi huo ni muhimu kwa waandishi wa habari ili waweze kuandika habari za kina kuhusu unyanyasaji wa kijinsia jinsi unavyoathiri jamii ya Zanzibar.

DSC_0558

Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura akionyesha zawadi ya kitabu atakachomkabidhi mgeni rasmi chenye jina la “TIME WELL SPENT”  ikiwa kama ni shukrani ya kushiriki uzinduzi wa mradi huo.

DSC_0564

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akipokea zawadi ya kitabu hicho toka kwa Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura.

DSC_0567

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akionyesha zawadi hiyo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

DSC_0577

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akitoa neno la shukrani  kwa zawadi hiyo na kusema hajajutia kuhudhuria uzinduzi huo.

DSC_0422

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.

DSC_0436

DSC_0584

Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kuzindua mradi huo.

DSC_0609

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka katika picha ya pamoja na wadau wa moja ya maeneo ya  mradi huo  wa kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya.

DSC_0598

 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa TMF nchini, Ernest Sungura mara baada ya tukio la picha ya pamoja.

source:-Na Damas Makangale, MOblog Tanzania

{KICHUPA} EPIC STORY ABOUT “NANI ANAFAIDIKA NA MADINI YA MERELANI

A survey conducted by the Institute for Information Media2solution in Simanjiro for about three months to determine the benefits that communities of these areas benefit from the Tanzanite mining. This project was funded by Tanzania Media Fund.
 
Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya kihabari ya Media2solution katika wilaya ya Simanjiro kwa takribani miezi mitatu kwa lengo la kubaini faida ambazo jamii ya maeneo hayo ufaidika kutoka kwenye madini ya Tanzanite. Uchunguzi huu ulidhaminiwa na Tanzania Media Fund.

{VIDEO} TANZANIA BADO KUNUFAIKA NA TANZANITE

Hiki ni Kichupa kipya kabisa, ambacho ni matokeo ya uchunguzi wa zaidi ya miezi mitatu merelani simanjiro. Pata undani wa matukio ambayo uwezi kuyaona sehemu nyingine yoyote na kwa uwazi.

Fwatilia bila kukosa kupitia matinya yako ya hapa nyumbani, mfululizo wa makala Nne zenye maelezo, uchambuzi, utafiti na ufafanuzi wa kina kuhusiana na madini hayo meusi ambayo yanapatikana sehemu moja tu duniani.

MINISTER NYALANDU LIVE ON BBC HARDTALK WITH STEPHEN SACKUR

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (third left) listens to Richard Porter, Controller of BBC Global News before the BBC HARDtalk interview in London UK.  Others in the picture from left are Imani Nkuwi, PA to the Minister, Paul Sarakikya, Assistant Director of Wildlife Division, David Tarsh, UK Media Consultant, Katie Waxman from BBC.

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (right) heading to the BBC HARDtalk Studio ready for the interview

BBC HARDtalk Presenter Stephen Sackur welcomes Hon. Lazaro Nyalandu in the studio ready for the interview.

Hon. Lazaro Nyalandu before the starts of the interview.Interview takes off between Stephen Sackur, BBC HARDtalk Presenter and Hon. Lazaro Nyalandu, Minister for Natural Resources and Tourism.

The inside view of the BBC HARDtalk Studio in London, UKHon. Lazaro Nyalandu smiles as a psychological means to control the interview while Stephen Sackur is seen taking note of the responses from Hon. Lazaro Nyalandu.

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu in a discussion with Carey Clark, Editor of the HARDtalk and News Features Programmes soon after the interview.

Hon. Lazaro Nyalandu, Minister for Natural Resources and Tourism (second right) shaking hands with Stephen Sackur, Presenter of the BBC HARDtalk soon after the interview. Others from left are Paul Sarakikya, Assistant Director of Wildlife Division, Imani Nkuwi, PA to the Minister and Pascal Shelutete, PR Manager Tanzania National Parks.

CHADEMA KIVUTIO ZIARA YA KIKWETE MWANZA

  • GARI LA MOVEMENT FOR CHANGE (M4C) LAONEKANA KWENYE MSAFARA  WA RAIS.

  • MAAFISA USALAMA WATAKA KULIZUIA WASHINDWA.

  • WAZIRI WA UJENZI, MAGUFULI AZOMEWA BAADA YA KUMTAJA MATATA.

  • WANANCHI WAPAZA SAUTI WAKITAKA MBUNGE WAO ATAMBULISHWE KAMA KIONGOZI KWENYE ZAIRA HIYO.

  • MBUNGE WA NYAMAGANA AWASALIMIA WANANCHI MBELE YA RAIS KWA KIBWAGIZO CHA PIPOZ….. WENYEWE WALIPUKA  POWER!!!!

Ziara ya RAIS Jakaya Kikwete jana ilishuudia nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza baada ya viongozi na matukio yanayo usisha cha hicho kuonekana kuwavutia zaidi wananchi wa jiji hilo.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA. hatua ambayo iliwakwaza maofisa wa usalama ambao walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.
Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika. Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza kupaza sauti wakitaka mbunge wao naye atambulishwe.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje baada ya kusimama alimshukuru Rais Kikwete kwa kumpa nafasi hiyo lakini akamwomba amvumilie kidogo atoe salamu maalumu ya wana Mwanza. Kama kawaida ya CHADEMA kwenye salamu yao, Wenje aliwaomba wananchi wakunje ngumi kisha akawasalimu kwa kibwagizo cha peoples… nao wakamwitikia power!
Akiwa katika viwanja vya Furahisha ambapo Rais Kikwete alichelewa kuanza mkutano wake, Wenje alifika hapo na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi huku polisi wakiwazuia bila mafanikio. Ilipofika saa 12 jioni kabla Rais hajaingia uwanjani, wananchi hao walimtaka Wenje awahutubie huku wakidai bendera ya taifa ishushwe kwani muda wake ulikuwa umefika.
Kikwete aliingia uwanjani hapo saa 12:10 akiongozana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali lakini wananchi hawakuonyesha kumshangilia badala yake walikuwa wakimwonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA wakiimba ‘peoples…power’. Viongozi wa CCM walionyesha kushangazwa na wananchi wa mwanza baada ya kumshangilia kwa nguvu mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliyekuwa ameongozana na Rais kwenye mkutano huo.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, alikumbana na jinamizi la kuzomewa mbele ya Rais baada ya kusimama jukwaani na kutaja jina la Matata (ambaye ni Meya wa jiji la Mwanza mwenye mgogoro na CHADEMA) , ambapo wananchi wengi walimzomea kwa miluzi huku wakimnyooshea vidole viwili.
Wananchi walizidi kuzomea pale Magufuli aliposema wabunge wa Ilemela na Nyamagana jijini hapa ni wana CHADEMA lakini ndani ya roho zao ni wana CCM. wananchi hao walizidi kukeleka pale waziri huyo aliposema kuwa iwapo Rais angehitaji kupokea kadi za CHADEMA zilizorudishwa angepokea nyingi.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alimpongeza mbunge wa Nyamagana kwa uchapakazi mzuri hasa kusimamia sekta ya elimu na kwamba wabunge wa namna hiyo wanastahili kuigwa.
Hata hivyo, alisema serikali yake imejipanga vizuri kuhakikisha usafiri wa reli, ndege, majini na barabara za lami vinaboreshwa maradufu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Serikali yangu imeweka nguvu kubwa katika kuboresha sekta ya uchukuzi, ujenzi na nyinginezo. Hii ni kutaka kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kisekta,” alisema.
Baadhi ya mawaziri walioongozana na Rais mbali na Magufuli ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Kitwanga, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri wa Ujenzi na Dk. Charles Tizeba.

WHY ADVERTISERS DON’T GET THEIR MONEY’S WORTH ON WORTHLESS BLOG ADS:

I have been going around blogs in Tanzania, especially these niche blogs that are all about reporting current events, I sincerely don’t like these blogs personally, but they have caught my attention these few days. When I say catch my attention, I’m not talking in a good way, but a way that annoys me because all these blogs do the same thing, most of them recycle the same news very few have original content, Tanzania bloggers do not understand the full meaning of blogging, if they did, with the time they spend publishing all those posts they would have been making a whole lot more money.

With so many blogs out there emerging on a daily basis, I’m going to have to focus on a few blogs, especially few of the most known blogs in Tanzania, blogs such as “issamichuzi.blogspot.com”, “djchoka.blogspot.com”,FULL SHANGWE BLOG , just to mention a few.

One thing you will notice in all of those above mentioned blogs, is how far down the content is. I mean really, I don’t know if these are blogs or ad management services. “issamichuzi.blogspot.com” is considered the best blog by most people, on my part its one of the worst blogs in Tanzania. It has, take or less 20 adverts at the top of the page, another 15 ads at the sidebar, I know advertisers think they are getting exposure due to the popularity if IssaMichuzi, but i’m going to disappoint them by saying how worthless all these ads are, and how worthless they are making the blog look.

To me stacking all those ads looks as if the blog is worthless, meaning putting an advert on these blogs is so cheap that a blog has 35 adverts on 1 page, seriously. If a blog really has that much traffic it should have a very high advertising rate that 1 advert can be worth all those 35 plus adverts, people that want to advertise should align and wait for the current advertiser’s contract to run out, I don’t even think they have contracts.

Why advertising on these blogs is a waste of time you ask?
I. First of all, it’s in Tanzania, loading that blog on a normal Computer, with a normal modem is hell.

It takes minutes to load a blog, I mean its hosted on Google’s servers for crying out loud, it shouldn’t take that long. It took me almost 2minutes for the whole website to load, and I have a very fast internet, trust me it’s really fast. I’m sure, the blogs loose overall traffic after putting all these ads, for people who can’t wait that long don’t wait, they just browse away from that blog.

II. Content is really far down,

I’m now asking myself if they blog for advertisers or do they actually blog for readers to get to read their content, it’s a mystery for me. People or readers, yes those people advertisers target, get into these blog for content the ads should be an added or extra for them.

III. The ads are just very huge

These blogs probably have Google Adsense ads too. For those who know these ads Look at those ad sizes(if not you can google ‘adsense sizes’ photos), those are standard ad sizes ,I don’t think if even one of them is that huge. None of them are 980 pixels width by 360 pixels high, I mean that’s half a website page. And having 20 of them is just absurd.
Adsense AD sizes
A
IV. Nobody Probably click your ads

For some, just the view is probably enough but most have links on those ads and want people to click them to get the full message of the advert, I mean an image puts across a message but people need convincing to get what you are selling. I’m sure very few people click those ads because people just scroll down looking for content, if the ads were carefully placed the readers would click them after seeing the content they were looking for, or after realizing the content isn’t actually what they were looking for.
V. These blogs are not mobile compatible

Imagine on an tablet or phone, having to go down 20 ads, 980 pixels wide by 360 pixels high. A standard mobile phone is 320 pixels wide, a standard tablet is 600-700 pixels wide, scrolling through those adverts is just impossibly frustrating, so there goes the mobile users ever seeing your adverts.

VI. Nobody is going to notice your advert

Simple and clear, 35 adverts, I don’t have time to waste looking at all of them. The teen you probably want to come to your event would rather be on facebook, the adult you want to get to know your product well has life to deal with.

I wouldn’t advise anybody to waste their time advertising on these blogs or website that have these type of ad formats or services. Don’t advertise on any website with already more than 3-5 adverts, if it has a lot of traffic it won’t be there after a while, and people probably won’t notice your ad with those stacks of adverts.

If you want your money’s worth, you better off signing up for Google adwords, finding a channel of that blog you want to advertise on and paying Google to advertise your product on those blogs. Google lets you pay after somebody has clicked your advert if not it stays their services till your budget runs out.
Or you can ask for a report on click throughs, meaning if you insist advertising on these blogs, let them give you a report of how many outbound links have been clicked, then you will see how many times somebody has noticed your advert.
For the blogger
Your blog has traffic, its worth a lot more than all those adverts put together are paying, don’t just take whatever to put up there. Find the highest bidder and put up
I also would advise them to have a featured post section at the top of the blog, find someone who can put that up a sliding featured post section at the top of your blog, and charge for those featured posts. A sliding featured post section will also get you paid if you want to make more money.

n.b : If I have misjudged a website feel free to let me know, if there is a website I am supposed to include please tell me media2solution@gmail.com it to be reviewed on a later date. There are many websites in this category but I have chosen these few to review for this post more will come out soon, and to the websites, this is merely creative criticism to help us grow our online experience as a whole. Please feel free to comment.

Miss Lou Acquiring Lore

Gallery of Life...

MAISHAZONE

ITS ALL ABOUT LIFE......For over 75 years, Jubilee Insurance has built a rich heritage of enriching lives by offering insurance solutions that make life carefree and rewarding.

this is... The Neighborhood

the Story within the Story

JAMIIBLOG

PAMELA MOLLEL

MEDIA 2 SOLUTION

- TRUTH SEEKERS -

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.