SASA NI ZAMU YA HAPPINESS MISS WORD… GO TEAM TZ GO

10614252_800789863300579_6044778737800766960_n

NEW TOP 10 on the Miss World People’s Choice!

AUSTRALIA
BARBADOS
HAITI
INDIA
NEPAL
NETHERLANDS
PHILIPPINES
SOUTH AFRICA
TANZANIA – NEW ENTRY!
THAILAND

TANZANIA jumps up into the top 10 today, with Russia dropping out!

Voting closes 15:30 on Sunday 14th December, so there is only 96 to go!

Download the Miss World App for free to register your vote now!

http://www.missworld.com/TheCompetition/TheMissWorldMobileApp/

10846445_10152970401239974_5092824672817370692_n

Advertisements

{PICHA} TUZO ZA WATU ZILIZOFANYIKA JUNE 27 SERENA HOTEL, JIJINI DAR

Picha za Tuzo za watu zilizo fanyika Usiku wa June 27 Jiji Dar Es Salaam katika Hotel ya Serena

Jakobo Steven aka Jb

Jacob Stephen aka JB

B12 Mtangazaji wa Clouds Fm

Mtangazaji wa Clouds FM, B12

Batuli akiwa na Bond

Waigizaji wa filamu, Batuli na Bond

Faraja Nyarandu

Faraja-Nyalandu

Fezza kessi

Feza Kessy

Joshi Murunga na Salama Jabir

Josh Murunga na Salama Jabir

Madam Rita

Madam Rita

Mameneja BabuTale na Mkubwa Fella

Mameneja, Babu Tale na Mkubwa Fela

Mariam Kitosi akiwa na Mmewake Criford Ndimbo

Maryam Kitosi wa Times FM akiwa na mume wake Clifford Ndimbo

Mariam Kitosi Kutoka Time Fm

Maryam Kitosi wa Times FM

Martini Kadinda

Martin Kadinda

Meck Kaloka Muongozaji wa Video

MeckY Kaloka Muongozaji wa Video

Mh.Jerry Slaa

Mh.Jerry Slaa Meya wa Ilala

Millard Ayo wa Clouds Fm

Millard Ayo wa Clouds FM

Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 Media Nancy Sumari

Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 Media Group Nancy Sumari

Msanii Asia

Msanii Asia

Mzee King Majuto akiingia

Mzee King Majuto akiingia

Salim Kikeke kutoka BBC Swahili

Salim Kikeke kutoka BBC Swahili

Sammi Misago wa EA Radio

Sam Misago wa EA Radio

Wastara Juma

Wastara Juma

Young Killer akiwa Rafiki yake

Young Killer akiwa rafiki yake

1

2

5

7

8

9

12

13

18

19

20

27

30

31

CEO Wa Bongo5 Media Luca Neghest

33

35

36

37

38

39

40

42

43

45

46

47

49

50

52

53

54

55

56

57

58

59

//

WEMA IBUKA TENA NA TUZO NYINGINE

 • WEUSI, WANAUME FAMILY NI SHIDA ….. ILIKUWA NDANI YA PASAKA DAR LIVE

Mrembo Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa na tuzo yake baada ya kuibuka Ijumaa Sexiest Girl 2013/14 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Wema akiwashukuru mashabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi.

…Akiwapa tano mashabiki waliofurika Dar Live katika Sikukuu ya Pasaka.

Wema, Wema, Wema… mashabiki wakimshangilia ‘Beautiful Onyinye’ baada ya kutangazwa mshindi.

DSC_0116001

 

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa lililokuwa likiendesha shindano la Ijumaa Sexiest Girl, Amran Kaima (kulia) akipozi na mshindi Wema Sepetu. Kushoto ni shabiki wa Wema.

Amran Kaima akielezea mchakato uliotumika kumpata mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl.

Mashabiki wakiwa wamepagawa na shangwe za Dar Live.

Mratibu Mkuu wa kampuni ya Global Publishers, Luqman Maloto akiwakaribisha Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho na msanii Nikki wa Pili kukabidhi tuzo kwa mshindi.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiongea machache kabla ya zoezi la utoaji tuzo.

 

Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili akimtaja mshindi.

Wema Sepetu akiwa stejini baada ya kutangazwa mshindi.

Nikki wa Pili akimkabidhi tuzo ya Ijumaa Sexiest Girl, mrembo Wema Sepetu.

Wema akipozi na tuzo yake.

Wema akicheza wimbo wa Number One ulioimbwa na mpenzi wake Diamond Platnumz baada ya kutwaa tuzo.

Washereheshaji katika usiku wa Pasaka, Pamela Daffa na Benjamin Mwanambuu wakifanya yao stejini.

Said Fella (wa pili kushoto) akiwa na crew ya Madj ndani ya Dar Live.

Dogo Aslay akiwapagawisha mashabiki wa burudani waliofurika ndani ya Dar Live.

…Aslay akijiachia na shabiki wake aliyepanda stejini kumpa sapoti.

…Akimchombeza shabiki mwingine aliyepanda stejini.

Kundi la TMK Wanaume Family likifanya vitu vyao stejini.

Mhe. Temba akiwarusha mashabiki wa Dar Live.

Chegge Chigunda ‘Mtoto wa Mama Said’ akizikonga nyoyo za wana Dar Live.

TMK Wanaume Family wakizidi kulishambulia jukwaa la Dar Live la kupanda na kushuka.

Wana Hip hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini (kulia) na G-Nako wakiwapa raha mashabiki.

Mashabiki wakifuatilia shoo ya Weusi.

Joh Makini kazini.

G-Nako akiwadatisha wapenzi wa Hip hop.

UTAJUAJE KUWA UNAANGALIA FILAMU YA BONGO MOVIE….

 • Walinzi wengi huwa ni comedians.

 • Tajiri anakuja kumpenda masikini.

 • Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara na koti refu jeusi.

 • Wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani.

 • Mtu yupo village,life gumu ana wave kichwani.

 • Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha.

 • Nusu saa mtu anatembea, anakimbizwa, ananunua vitu.

 • Wakifika hotelini imezoeleka ni juice au wine isiyofunguliwa.

 • Madem wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa.

 • Part 2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part 1 ilikuwaje.

 • Jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke..!

Source jamiiforums.com

SIMU ZILIZO NUNULIWA SANA (ULIMWENGUNI) MWEZI MACHI

1. Sony Xperia Z:

Orodha ya simu kumi bora kwa mauzo katika mwezi wa Machi imeongozwa na Sony Xperia Z. Orodha hii huchukua mauzo ya simu kutoka nchi 70 za mabari sita Duniani na kuchapishwa kila mwezi. Ubora na vielelezo utatolewa kwa simu tano za mwanzo tu.

Sony Xperia Z: Imepanda kutoka nafasi ya pili ambayo simu hii ilishikilia katika mwezi wa Februari. Sifa kuu za simu hii ni:

 • Vielelezo vya hali ya juu
 • Haiathiriki na maji (water proof)
 • Nyembamba na kubwa
 • Kamera ya megapiksel 13 nayo ni kivutio
 • Timescape UI
 • Sony Mobile BRAVIA Engine 2

2. Samsung I9500 Galaxy S4Haikuwemo katika orodha ya mwezi ulioita. Sifa zinazofanya simu hii kupata mauzo mazuri ni:

 • Mafanikio ya Samsung Galaxy SII na SIII.

 • Ni simu yenye prosesa yenye core nane (baadhi yake tu)

 • Umbile lenye kuvutia

 • Imevuma sana kufuatia uzinduzi wa aina yake.

 • Koti la TouchWiz na sifa mbali mbali mpya hasa za kamera na hata simu yenyewe kiujumla.


3. Apple iPhone 5

Imeshuka kutoka namba moja mwezi uliopita, iPhone 5 iliongoza orodha hii kwa miezi 6 mfululizo. Hakuna simu iliyofanya hivyo ambayo si iPhone. Sifa zinazovutia mauzo:

 • Ina jina (brand name) kubwa, yaani Apple

 • Inatumia iOS, ni OS ya kipekee ambayo haipatikani kwenye simu yoyote isiyo iPhone.

 • Inaongozakwa ubora na idadi ya apps ambazo zinapatika kwenye AppStore.

 • Inaongoza kwa vifaa (accessories), na hasa vifaa vinavyotumia apps kama vile kipima msukumo wa damu (BP), vifaa vya mazoezi kama Jawbone wristbandna Nike Fuelband, Drone, Mizani na kadhalika.

4. HTC One SV

Imepanda kutoka nafasi ya tisa kwenye orodha ya mwezi Februari. Sifa zinazovutia mauzo katika simu hii ni:

 • Umbile linalovutia

 • Bei nafuu mno

 • Sauti safi na bora ikiwa na Beats By Dre

 • HTC Sense

5. Sony Xperia ZL

Imeingia kwenye orodha hii kwa mara ya kwanza mwezi huu.

 • Simu hii ina sifa zote za Xperia Z inayoshika namba moja, tofauti kubwa ni kwamba hii haihimili maji (not water proof), na ni fupi na pana kulinganisha na Xperia Z, ingawa zote zina skrini zenye ukubwa sawa, hivyo tofauti ipo kwenye fremu.


6. Samsung Galaxy i9300 SIII: imepanda kutoka nafasi ya saba.

7. Sony Xperia E / E Dual: Imeingia kwenye orodha kwa mara ya kwanza.

8. Apple iPhone 4/4S: imeporomoka kutoka nafasi ya 3.

9. Samsung I8190 Galaxy S III Mini: Imeporomoka kutoka nafasi ya nne.

10. Blackberry Z10: Ni ingizo jipya katika simu 10 bora.

iPhone 5, iPhone 4S na Samsung Galaxy SIII ndo simu zilizoporomoka sana mwezi huu, huku Galaxy SIII Mini imeporomoka hadi kutolewa kabisa katika kumi bora hizi. Hata hivyo iPhone 5 imemuda kubaki kwenye nafasi ya tatu nalo si jambo dogo tukizingatia kuwa ni simu yenye miezi sita sokoni kwa sasa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba simu mpya zilizozinduliwa kwenye maonyesho ya WMC Barcelona na maonyesho ya CES, Las Vegas baina ya mwezi Januari na Februari ndio zimeanza kufikia idadi kubwa ya mauzo.

Wakati Sony Xperia Z haishangazi kuongoza kwa vile ina sifa ya kipekee muhimu yaani kutoathiriwa na maji, simu unayoshangaza kwa kukosekana kwake kwenye kumi Bora hii ni HTC One, ambayo sio tu ilitarajiwa iwemo kwenye 10 bora bali ilitarajiwa kuchuana na Xperia Z katika kugombania namba moja. Hata hivyo inawezekana sana uzalishaji hafifu ndio sababu ya msingi ya kukosekana kwa simu hiyo.

Hoja nyingine ya muhimu ni kwamba katika orodha hii ya simu kumi bora kwa mauzo haina hata simu moja inayotumia OS ya Windows Phone 8. Kwa upande wa OS, orodha hii imetawaliwa na simu saba zinatumia Android, hii inadhihirisha jinsi OS hii inavyotawala mauzo ya simu Ulimwenguni.

Kwa mwaka huu simu mbili tu ambazo hazikutoka bado ndizo zinazotarajiwa kuleta mabadiliko ya kimauzo katika orodha hii, simu hizo ni iPhone 6, iwapo itatolewa na Samsung Galaxy Note 3. Kwa utaratibu wa kawaida Apple mwaka huu walitarajiwa kutoa iPhone 5S, baada ya kutoa iPhone 5 mwaka jana, na iPhone 5S katika ratiba ya kawaida hutoka mwezi wa Septemba.

Hata hivyo katika hali ambayo si ya kawaida mwaka jana Apple walitoa iPad tatu tofauti, yaani iPad 3, iPad Mini na iPad With Retina Display. Miaka ya nyuma yote tangu kuzinduliwa kwa iPad ya kwanza Apple hutoa iPad moja kila mwaka. Hivyo huenda mwaka huu Apple wakatoa simu zaidi ya moja, kinyume na kawaida yao. Ikiwa ni hivyo basi moja kati ya simu hizo huenda ikazinduliwa kwenye mkutano wa WWDC 2013 ambao utatangazwa wakati wowote kuanzia mwezi huu.

Makala inayohusiana: Xperia Yaongoza Kwenye Kumi Bora

Chanzo: http://www.gajetek.com/

SABABU ZA KISAYANSI KWA WANAWAKE KUVAA NGUO ZA KUONYESHA MAUMBO YAO.

40

14476-1

african women romantic wear

Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nguo za kuonyesha maubile yao kwa kiasi kikubwa huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.

Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.

Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.

Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.

Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao

……NATOA HOJA KWA WALE WAKOSOAJI NAFASI NI YENU….

KWA WANAWAKE TU…..AINA KUMI ZA WANAUME WA KUWAOGOPA

1. Mwanaume Kicheche:
Hakuna mwanamke anayependa kuchezewa na wanaume, labda tu kama anafanya hivyo katika juhudi zake za kujikwamua kiuchumi, lakini pale mwanamke anapokuwa katika harakati za kutafuta mwanaume ambaye kama mambo yakiwa mazuri wafunge ndoa, ni vyema akajiepusha na wanaume vicheche wanaotongoza wanawake kwa lengo la kustarehe na kumaliza matamanio yao ya ngono. wakati mwingine mwanaume mwenye tabia ya kuchezea wanawake anaweza kumfuata mwanamke ambaye ametamani mwili wake na kujifanya eti amebadilika na kuwa mtakatifu. Anaweza kujiweka katika mazingira yanayoonyesha kwamba amebadilika ili kumvuta mwanamke. Shituka mwanamke, jasiri haachi asili atakutumia kama condom na kisha kukutupilia mbali. Wanaume wenye tabia hizo ni vigumu kubadilika. Inahitaji subira ya hali ya juu kujiridhisha kama kweli amebadilika au anazuga ili apate anachokitaka.

2. Mwanaume asiye na kazi na asiyejishughulisha:
Mwaume asiye na kazi na asiyejishughulisha ni mzigo usio na mwenyewe. Mwanaume asiyejishughulisha eti kwa sababu hajapata kazi huyo hana malengo. Kukubali kuwa na uhusiano na mwnaaume wa aina hiyo ni sawa na kuishi na mtu mfu anayetembea (dead alive), labda tu kama atakupa sababu inayoingia akilini kuhusu kutokuwa kwake na kazi na kutojishughulisha kwake. Kama atakuwa ni mtu wa kulalamika tu kwamba hakuna ajira na haonyeshi dalili zozote za kuhangaika kutafuta hata vibarua ili kujikimu eti kwa sababu ni msomi na badala yake anageuka kuwa ombaomba kwa ndugu zake na marafiki zake Nawashauri wanawake muwaepuke wanaume wa aina hii kwani hawafai wanataka kulelewa. Kama amekuona unafanya kazi au una vibishara vyako vinavyokuingizia shilingi mbili tatu zinazokufanya uishi vizuri hapa mjini jua kwamba hicho ndicho kilichomvuta kwako, ukikubali umekwisha maana atakukamua hadi tone la mwisho kisha ahamie kwa mwingine, si kilichomleta kwako hakipo, sasa awe na wewe kwa lipi….

3. Mwanaume asiyejiamini:
Kukubali kuwa na mahusiano na mwanaume asiyejiamini ni sawa na kuishi na bomu ndani ya nyumba. Mwanaume asiyejihisi kuwa yuko salama na mwenye mashaka muda mwingi kuhusu uhusiano wenu, hutawaliwa na wivu wa ajabu ambao licha ya kukuletea fedheha kwa ndugu, jamaa na marafiki zako, lakini pia anaweza kukudhuru au hata kukutoa roho siku moja. Wanaume wasiojiamini mara nyingi ni watu wa kujitilia mashaka kuhusu hali zao za kipato na uwezo wao katika tendo. Kuwa na mahusiano na mwanaume asiejiamini inabidi uishi kwa akili na uchague maneno ya kuzungumza kila uwapo naye, kwani kila neno utakalotamka litatafutiwa tafsiri na kitakachofuata ni tafrani, sasa tabu yote ya nini….. Tupa kule hafai kwa mchuzi wala kwa kulumangia…

4.Mtoto wa mama:
Inawezekana mwanaume akalazimika kuishi nyumbani kwao kwa muda baada ya kumaliza masomo au amepoteza ajira na akawa bado hajapata ajira au hajapata shughuli ya maana itakayomwezesha kujitegemea, hii inakubalika. Hata hivyo kama mwanamke anakutana na mwanaume ambaye anaishi na wazazi wake na haonyeshi dalili za kutafuta kazi au shughuli yenye kipato itakayomwezesha kuondoka hapo kwao na kujitegemea, usije ukajiingiza katika uhusiano na mwanaume wa aina hiyo, itakula kwako, huyo ashakuwa kupe na tegemezi, utakuwa ni mzigo wako na atakuganda kama luba na kupoteza bahati ya kukutana na wanaume wenye mwelekeo wa maisha.5. Mwanaume anayependa kutukuzwa kama mfalme:

Unaweza kukutana na mwanaume aliyejipachika kibandiko ufalme ambaye anapenda sana kuhudumiwa kama mfalme. Yaani anataka afanyiwe kila kitu, na hajishughulishi kukusaidia kazi hata zile zinazotakiwa zifanywe na mwanaume, yeye kazi yake ni kukaa sebuleni na kuangalia TV au kusoma vitabu au magazeti huku akiagiza kila kitu asogezewe miguuni. Hawezi hata kunyanyuka kufuata kitu anachotaka na badala yake ni kuamrisha aletewe. Mwanaume wa aina hii ni wa kuepukwa kwani mwanamke kukubali kuwa na uhusiano na mwanaume mwenye tabia za kupenda kutukuzwa kama mfalme ni kutaka kuishi kwa msongo wa mawazo na jakamoyo na hivyo kufupisha umri wako wa kuishi hapa duniani. Kinga ni bora kuliko tiba, ukikutana na mwanaume wa aina hii chapa lapa hakufai..

6. Mwanaume mwenye utititri wa watoto kila kona:
Mwanaume kuwa na watoto nje ya ndoa si jambo la kushangaza siku hizi, lakini pale unapokutana na mvulana mwenye umri wa miaka 25 lakini ana watoto watatu kwa mama tofauti, mh! hapo sikushauri ujiingize kwenye uhusiano na mwanaume huyo. Hata hivyo si lazima awe na miaka 25 tu hata mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi ya huo halafu ana watoto watatu au hata wanne au zaidi kutoka kwa mama tofauti ni wa kuepuka. Hivi atakupa sababu gani zilizomfanya akawa na watoto kwa mama tofauti kila kona ya mtaa mpaka umuelewe! Kuwa na mahusiano na mwanaume aina hiyo ni kukaribisha shari nyumbani kwako maana kila siku utapata wageni wanaokuja kudai hela za matumizi kutoka kwa mumeo tena wengine watakuja kishari hasa na kukuharibia siku. Mh mh! sikushauri mwanamke, sepa zako, bado nafasi unayo ya kumpata mwanaume mwingine mwadilifu.

7. Mwanaume anayejipenda mwenyewe:
Mwanaume anayejipenda mwenyewe ni kizungumkuti kingine ambacho wanawake wanapaswa kujiepusha nacho. Utakuta mwanaume anajipenda mwenyewe hakuna anachojali kuhusu mwenzi wake zaidi ya kujijali yeye mwenyewe. Wanaume wenye tabia hii ya kujipenda wenyewe, huwa wana kawaida ya kujijali wao wenyewe. Wanataka wavae nguo nzuri za thamani ili wao wapendeze na si wenzi wao. Swala la kumjali mwenzi wake halipo katika vichwa vya wanaume wa aina hii kabisa. Mwanamke sikushauri uingie katika moto huu.

8.Mwanaume bahili:
Unakutana na mwanaume mtoko wa kwanza tu anakuchagulia aina ya chakula au kinywaji kwa kuangalia bei rahisi na wakati wa kulipa anahesabia hela yake mfukoni, huyo ni janga. Utakapoingia katika uhusiano na mwanaume wa aina hii atakusumbua sana na pia katika kupanga bajeti nyumbani usishangae akihesabu finyango za nyama au vipande vya samaki jikoni. Sikushauri mwanamke, we ingia mitini hakufai huyo……..

9.Mwanaume chapombe mlevi kupindukia:
Hakuna ubaya mtu kunywa pombe, hasa kama unajua kiwango chako cha unywaji, lakini kuwa na uhusiano na mwanaume mlevi anayekunywa pombe kupindukia kila siku non stop 24/7 huyo hafai. Mwanaume wa aina hii ndio wale wanaosema kunywa pombe watoto wakitembea uchi atajua mama yao. Hata siku moja hawezi kuzungumzia maendeleo kwa ustawi wa familia, kwake utakuwa ni msamiati mgumu.10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :

Mwanaume mwenye kisirani ni ngumu sana kuishi naye. Mwanaume mwenye kisirani na anayependa kuweka vitu rohoni na asiyeweza kusamehe ni janga. kuishi na mwanaume wa aina hii ni sawa na kuishi na explosive material ambayo yakipata joto tu hulipuka. Mwanaume umetoka naye mtoko wa kwanza na kwa bahati mbaya mhudumu wa mghahawa akasau kitu katika vitu mlivyoagiza akagomba kupita kiasi na kuwakusanya mameneja wote wa mghahawa akiwemo mpishi mkuu akilalamika. Na kama hiyo haitoshi mtaondoka hapo mghahawani njia nzima kambeba kichwani mhudumu yule masikini aliyeghafilika mpaka mwisho wa safari yenu na huenda akalala naye kichwani. Mwanaume huyo hafai kama gome la mgomba lisilofaa kwa dawa ya miti shamba wala kuni, labda kwa kufungia ugoro. Huyo mpishe ajiendee zake hakufai……

source jamiifolum.

A CONCERT IS CUT SHORT AFTER RAPPER TONE LOC COLLAPSES ON STAGE.

TONE

Rapper Tone Loc has collapsed on stage during a performance in Iowa.

 Loc, whose real name is Anthony T Smith, collapsed after finishing a song during a night concert on a bridge in central Des Moines.

 According to the Des Moines Register newspaper, the concert ended abruptly and fans were asked to leave while the 47-year-old was treated.

 Police sergeant Steve Woody said paramedics responded after Loc collapsed, but the singer refused to be taken to hospital.

 The rapper’s condition was not immediately clear. He was not listed publicly as a patient at any Des Moines hospital.

 Loc’s representative did not immediately respond to phone and email messages.

In 2009, Tone Loc collapsed on stage after apparently overheating

 It is not the first time the rapper has collapsed on stage.

 Loc, who is best known for his 1980s hits Funky Cold Medina and Wild Thing, collapsed and had a seizure during a 2009 concert in Pensacola, Florida, after authorities said he had apparently overheated.

 He also collapsed in 1995 while attending a Los Angeles Lakers game with no reason provided.

 Loc has also appeared in a number of television shows and movies, including Ace Ventura: Pet Detective with Jim Carrey and Heat with Al Pacino.

 He has also been the voice of several animated characters.

MWANAMKE ANAANGALIA NINI KWA MWANAUME WANAPOKUTANA

mimi

 1. Kwanza hutazama tembea yako, kisela au kiheshima ili wajue kama una kazi au la.

 2. Kama nguo zako zimefubaa unatembea juani, kama hazijanyooshwa basi hata pasi kwako huna. 

 3. Kama viatu vina vumbi moja kwa moja gari huna. 

 4. Kama pesa hutoi kwenye waleti hujazoea kuwa na pesa tena yawezekana hata laki hujawahi kushika. 

 5. Kama hunukii vizuri basi wanawake huwajui vizuri, na hujui romance, hata hug hujawahi kupewa. 

 6. Kama hutunzi nywele zako hata zake hutazigharamia. 

 7. Ukiongea nae muda mrefu na maswali mengi, hata kama hujamtongoza, anajua umempenda. 

 8. Ukimshika au kumgusa popote kwenye maongezi basi unamtaka kimwili. 

 9. Kama mkanda wa suruali na viatu havimachi rangi, hujawa na mwanamke kwa muda mrefu. 

 10. Usipomtazama machoni, yawezekana muongo au hujiamini na unamuogopa.

KIHAYA

VIDEO YA LONDON FASHION WEEK YAINGIA MITAANI

Wabunifu  mitindo watatu walishiriki maonyesho ya mavazi London Fashion Week yaliyotayarishwa na shirika la British Council na kudhaminiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wetu Uingereza.

Tanzania na Nigeria ndiyo nchi pekee za Kiafrika zilizong’arisha “jua” lake kati ya mataifa zaidi ya 25.

Filamu hii fupi iliyotayarishwa na Urban Pulse wakishirikiana na Freddy Macha inakupa taswira ya mambo yalivyokua.

WABUNGE WOTE UGANDA KUJIPATIA IPADS MPYA

Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) kimepokea na kukubali mpango wa serikali ya Uganda wa kununua toleo jipya kabisa la iPads kwa ajili ya wabunge, lakini kimesema wabunge hao wakopeshwe na sio wapewe bure.

Msemaji wa Chama hicho Wafula Oguttu ambae pia ni mbunge, amesema pendekezo la kununua iPads halikataliwi lakini hakuna sababu ya kuwapa bure na badala yake wapewe kwa mkopo.

Serikali ya Uganda imepanga kununua iPads za kisasa na kuwapatia wabunge kwa lengo la kupunguza gharama ya steshenari.

Uamuzi huo ulichukuliwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge na unasubiri utekelezaji kwa Kamati ya Mikataba.

WATAKAO CHUANA TUZO ZA SWAHILI FASHION WEEK 2012 WATAJWA.

Wandaaji wa Tuzo kubwa za mitindo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wametangaza majina ya waliopendekezwa kushiriki katika kuwania tuzo mbalimbali za Swahili Fashion Week 2012 ikiwa pamoja na njia zitakazotumika kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo.

Kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika tuzo za mwaka jana, Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zinazoendana na kusherehekea miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa la mitindo Afrika Mashariki na kati mwaka huu, zimeongezwa tuzo nyengine tatu kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweza kutoa changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo hapa nchini na ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati. Hivyo kufanya jumla ya tuzo 15 kuwaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.

Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year, East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality, Stylish Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion TV Program of the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion Photographer of the Year, Fashion Journalist of the Year, Best East African Journalist (Mpya), Upcoming Designer.

Mchakato mzima wa kuchagua mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012 unasimamiwa na PUSH Mobile ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa Namba ya mshiriki (CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba 15678, huku mchakato mzima wa kuzihakiki kura hizo utafanywa na PKF. Lakini pia kura zinaweza kupigwa kupitia blogu maalum ya kupigia kura ya www.sfw2012awards.blogspot.com.

Washindi wote wa Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili Fashion Week, jumamosi ya tarehe 8, Desemba, 2012 katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es salaam, Tanzania.

Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka kati

Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na: Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security,  BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania),  Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.

Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka katika ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa sasa. Huu ni mwaka wa Tano sasa, ambapo Swahili Fashion Week imekuwa ni Jukwaa la wanamitindo na watengeneza vito vya urembo kutoka katika nchi zinazoongea Kiswahili na bara zima la Afrika kwa ujumla kuweza kuonesha vipaji, kutangaza ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara ndani na nje ya nchi kwa wadau wa mitindo. Hili limelenga  kuhamasisha ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati  kwamba ubunifu wa mavazi ni njia moja wapo ya kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa zinazotengenezwa Afrika ( Made in Africa concept)

Ikiwa imeanzisha uhai na jukwaa la matumaini kwa kilinge cha mitindo katika ukanda huu, Swahili Fashion Week Swahili Fashion week imelenga kuwa maonyesho ya ubunifu wa mavazi linaloonekana sana Afrika na hasa kwa ajili ya soko la kimataifa, lililoundwa, kutengenezwa na kujengwa mwaka 2008 na Mustafa Hassanali.

Ifikapo mwaka 2013, Swahili Fashion Week ina lengo la kuwa ni tukio litakalotokea mara mbili kwa mwaka, ambapo kwa kuanza tukio la kwanza litafanyika nchini Kenya kama sehemu ya kwanza kisha tukio lenyewe kabisa kufanyika baadae nchini Tanzania kama sehemu ya pili.

TUNAWEZA BLOG ADVERT3

Miss Lou Acquiring Lore

Gallery of Life...

MAISHAZONE

ITS ALL ABOUT LIFE......For over 75 years, Jubilee Insurance has built a rich heritage of enriching lives by offering insurance solutions that make life carefree and rewarding.

this is... The Neighborhood

the Story within the Story

JAMIIBLOG

PAMELA MOLLEL

MEDIA 2 SOLUTION

- TRUTH SEEKERS -

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.