BARUA YA MUME WA FLORA MBASHA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA

MUME WA FLORA MBASHA

Hii barua ya Mume wa Mwimbaji wa Nyimbo za injili nchini – Flora Mbasha kwenda kwa mchungaji maarufu nchini, Mchungaji Gwajima inakuhusu….

“Mchungaji …yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’ wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!

Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!! Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana! Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!! Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..”

Kwako – Mchungaji Gwajima

SOURCE:- mwanahalisiforum.com

Advertisements

MFANYABIASHARA DAMAS (CHUSA) AFUTIWA MASHITAKA CHINI YA KIFUNGU CHA 91 CHA SHERIA YA MWENENDO WA MASHAURI YA JINAI

Erasto

 • NI KATIKA KESI YA MAUJI YA ERASTO MSUYA

 • SHAIDI WA KWANZA NA WAPILI WAMTAJA KUWA NI MUHUSIKA MKUU.

MFANYABIASHARA anayemiliki vitalu vya kuchimba madini ya Tanzanite huko Mirerani mkoani Manyara, Joseph Damas, maarufu kwa jina la ‘Chusa’, ndiye anayedaiwa kupanga mauaji ya mfanyabiashara mwenzake wa madini.

Aprili 16 mwaka huu Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Elieza Feleshi, alimfutia mashitaka ya mauaji Joseph Damas kwa kufuata kifungu cha 91 cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai.

Msuya aliuawa kwa mtutu wa bunduki Agosti 7 mwaka jana saa 6 mchana barabara ya Moshi-Arusha eneo la Mjohoroni, Wilaya ya Hai, Kilimanjaro baada ya kumiminiwa risasi zaidi ya 20.

Kwa mujibu wa maelezo ya mashahidi 57 yaliyosomwa Juni 10, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi, Munga Sabuni, tajiri huyo anadaiwa kufanikisha mipango ya kumuua Msuya ikiwemo kutoa pesa zilizofanikisha wauaji kutekeleza uasi huo.

Akisoma maelezo hayo ambayo yatatumiwa na upande wa mashitaka kujenga msingi wa kesi hiyo, wakili wa serikali, Stella Majaliwa, aliieleza mahakama kuwa mfanyabiashara huyo alipanga mauaji akilipiza kisasi kwa Msuya.

Akinukuu maelezo ya mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Shariff Mohamed, wakili huyo akisaidiwa na mwenzake Florentina Sumari, alibainisha kwamba mfanyabiashara huyo alitoa maelekezo ya kuuawa kwa Msuya akiwa mjini Babati, Manyara.

Huko inadaiwa mfanyabiashara huyo alikuwa akipatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza kutokana na kutuhumiwa katika mauaji ya mfanyabiashara mwingine wa madini, William Mushi anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi.

Katika maelezo ya kukiri kuhusika kwenye mauaji hayo, mshitakiwa huyo alidai kisa cha kutekeleza mauaji hayo ni madai kwamba Msuya alitoa fedha ili mfanyabiashara huyo asiachiliwe huru katika mauaji ya Mushi.

“Chusa aliniambia mateso yote ninayoyapata hapa ni kwa sababu ya Erasto maana ametoa pesa nyingi ili niunganishwe kwenye hii kesi, aliniomba nifanye kazi ya kumtoa roho Erasto na atagharamia kila kitu,” alidai Shariff katika maelezo yake ya maungamo.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, mshitakiwa huyo baada ya kutoka Babati alirudi siku nyingine na kukutana na mfanyabiashara huyo akishikiliwa na akamtaka kwa mara nyingine afanye hiyo kazi na kama atashindwa, mfanyabiashara huyo aliahidi kuifanya mwenyewe.

Mshitakiwa huyo aliendelea kueleza, mfanyabiashara huyo aliomba atafutwe mtu aitwaye Mredii ili amuue Erasto na alitekeleza jukumu hilo. Alikutana na Mredii ambaye katika kesi hiyo anatajwa kwa jina la Jumanne Mvungi akiwa mshitakiwa wa pili.

Wawili hao wanadaiwa kukutana ambapo Mredii alidai kazi hiyo itafanywa na watu wanne ambapo namba mpya sita za simu zilitengenezwa na kununua simu mpya nne zilizofanikisha mauaji hayo.

Naye Jumanne Mvungi ‘Mredii’ katika maelezo yake alidai Julai 26 mwaka jana alifuatwa na mshitakiwa wa kwanza na kumweleza kuwa kuna kazi ya kumuua Erasto na kwamba Chusa analalamika kuwa anamfuatilia kwenye biashara zake.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo anadai katika maelezo yake kuwa alimweleza Shariff hatoweza kuifanya kazi hiyo japo yupo tayari kumtafutia vijana wa kuifanya.

Akadai baada ya maelezo hayo alipewa sh 300,000 na mshitakiwa wa kwanza na kujaziwa mafuta kwenye gari lake kisha kusafiri hadi Babati alikokutana na mtu mwingine aitwaye Ally Msuya na kumweleza juu ya mpango wa kumuua Erasto.

Siku ya mauaji ilipofika mshitakiwa wa kwanza alikiri kuwa ndiye aliyebeba silaha aina ya SMG iliyotumika katika mauaji hayo hadi eneo la King’ori mkoani Arusha na kuikabidhi kwa Karim Kihundwa ambaye ni mshitakiwa wa tano.

Alidai baada ya kuikabidhi kwa Kihundwa, alirejea Arusha huku akisihi wasichukue kitu chochote kutoka kwa marehemu pindi watakapotekeleza mauaji hayo ikiwa ni maelekezo kutoka kwa Chusa.

Kwa mujibu wa maelezo ya mshitakiwa huyo, baada ya mauaji hayo mshitakiwa wa pili na wa sita, Sadik Jabir ‘Msudani’ walimfuata hadi Arusha na aliwapa sh milioni 10 huku sh milioni sita nyingine akiahidi kuwalipa baada ya kukutana na Chusa.

Mshitakiwa huyo akahitimisha maelezo yake kuwa baada ya mauaji hayo alimfuata Chusa mjini Babati hospitali alipokuwa anashikiliwa na askari magereza na baada ya kumweleza kuwa kazi imefanyika, alifurahi sana.

BAADA YA UTATA KULIKUMBA BUNGE LA KATIBA, ZANZIBAR WATAFUTA MSIMAMO WA PAMOJA KWA KUJADILI KATIBA MPYA NJE.

 Mwenyekiti wa Kongamano la Kitaifa la Kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh. Khamis Yussuf, akizungumza katika Kongamano hilo na kutowa maelezo juu ya Kongamano hilo linalojadili Rasimu hiyo, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar SUZA 
 Mtoa Mada Shekh. Muhidin.akitowa mada katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa SUZA, likizungumzia mustakabali wa Rasimu ya Katiba Mpya ya Tanzania.
 Mwanasia wa Chama cha Upinzani Zanzibar Rashid Joe, akichangia katika Kongamano hilo, lililoandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) akichangia mada iliowasilishwa na watoa Mada wawili Ndg. Ali Saleh na Shiekh. Muhidin.
          Picha juu na chini   Mwananchi akichangia Mada katika Kongamano hilo la Kitaifa la kujadili Rasimu ya Pili.ya Katiba.
  Mshiriki wa Kongamano la Kitaifa lililoandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) akichangia katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha SUZA Vuga.na kuwashirikisha Wananchi na Maimamu.
   Mmmoja wa Mshiriki katika Kongamano la Kitaifa kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, akichangika katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa SUZA Vuga.

SAUTI ZA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI ZASIKIKA KUTOKEA ZANZIBAR

 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Mhe. Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutoka kwa Wajumbe wa UKAWA kutoka Vyama vya Upinzani Wanaohudhuria Bunge Maalum la Katiba
 Viongozi wa UKAWA wakiwa katika mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Mzsons Shangani Zanzibar baada ya mkutano wao kuahirishwa na jeshi la Polisi Zanzibar kwa sababu za kiusalama .
 Mwenyekiti wa  CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari sababu za kutoka katika bunge maalum la katiba Tanzania.akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Zanzibar.
 
 Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.
 
  
Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.

MAWIO BADO MATATANI, BAHADA YA KIBONZO SASA NI HATI YA MUUNGANO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Assah Mwambene akitolea ufafanuzi juu ya Taarifa iliyotolewa na Gazeti la Mawio mapema jana jijini Dar es Salaam,kushoto ni Afisa habari wa Idara ya Habari -MAELEZO Fatma Salum

Serikali imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na kukejeli nia njema ya serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano.

Akizungumza jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu.

Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi Aprili 23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23, mwaka huu lenye kichwa cha habari ‘Hati za Muungano utata’, taarifa husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili.

Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20 waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

“Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazona imeandikwa pasipo shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua,”alisema.

Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.

ILIVYOKUWA MKUTANO WA CHADEMA NA WANAHABARI JUU YA KUWAVUA WANACHAMA BAADHI YA VIONGOZI WAKE

Baada ya mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  kuwasili alianza kwa kusema kuwa kamati kuu imemteua kamanda Tundu Lissu kuwa mwanasheria mkuu wa chama na pia kamati kuu imefikia maamuzi ya kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa baadhi ya viongozi.

Mwenyekiti akamkaribisha Tundu Lissu kwa ajili  ya kutoa taarifa ya maazimio ya kamati kuu kwa niaba yake.

Tundu Lissu alianza kwa kusema kuwa kamati kuu imefanikiwa kupata waraka wa siri wenye mpango wa kukipasua chama chini ya uratibu wa Zitto Kabwe,  Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye bado awajafanikiwa kumpata.

Lissu anaendelea kueleza waraka huo uliopewa jina la waraka wa ushindi inavunja  katiba ya chama na wala wahusika awajawahii kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama.

Lissu alieleza kuwa wahusika waliomba kujiuzulu baada ya waraka huo kukamata lakini uongozi wa chama ulikataa kwa vile awakuona sababu ya watu hao kupata nafasi ya kuondoka kwa heshima ambayo awastahili.

Haidha chama hicho kimeagizwa kuwaandikia barua wahusika kuwataka wajieleze kwanini wasivuliwe uanachama kwa kosa kubwa waliofanya.

Mwisho alimaliza kwa kusema waraka huo utasambazwa nchi nzima ili wananchi wausome.

MAHAKAMA YA MOROGORO YAZIZIMA, BAADA YA PONDA KUFIKISWA CHINI YA ULINZI MKALI.


 
Sheikh Ponda Akishuka kwenye basi la Magereza tayari kuingia Mahakamani Kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.Sheikh Ponda alishatikiwa katika Mahakama Hiyo akikabiliwa na Mashtaka Matatu Ambayo inadaiwa aliyatenda Mkoani Morogoro katika Mkutano Hadhara mwezi uliopita.Kesi hiyo imearishwa tena Mpaka Tarehe 01.10.2013.Mshitakiwa Amenyimwa Dhamana na Amerudishwa Rumande.

Sheikh Ponda akiwa Chini ya Ulinzi Mkali wakati akiingia Mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.
_MG_1506
_MG_1509
_MG_1511
_MG_1515
_MG_1520
_MG_1521
_MG_1522
_MG_1526 _MG_1529
_MG_1532

HOJA JUU YA HOJA KUTOLEWA LEO HILI RAIS ASITIES SAINI SHERIA YA MABADIRIKO YA KATIBA

JUKWA LA KATIBA NA VYAMA VYA UPINZANI

SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) pamoja na Mtandao wa TGNP , kwa kushirikiana na Wanaharakati wengine wakiwemo, Haki Elimu, LHRC, Jukwaa la Katiba, TAMWA na Mtandao wa Wanawake na Katiba, wameandaa mjadala wa wazi:

KWA NINI RAIS ASITIE SAINI MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2013.

JOPO LA WAZUNGUMZAJI: Prof Issa Shivji (Chuo Kikuu cha Dar es salaam), Prof Ruth Meena (TGNP Mtandao), Dr Azaveri Lwaitama (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Anna Henga(LHRC), Jenerali Ulimwengu( Mwanaharakati wa kijamii) na Deus Kibamba(Jukwaa La Katiba).

Lini: Jumatano Tarehe 18 Septemba 2013

Muda: saa 03:00 asubuhi – 07:00 mchana

MAHALI: Viwanja vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo Sokoni
Tafadhali sambaza ujumbe huu wa muhimu kwa watu wengi iwezekanavyo ili kufanikisha mjadala huu wa wazi,ratiba itafuata baadae.

KESI YA LISSU LIVE; DODOMA …

Lissu, waheshimiwa majaji wa rufaa, tarehe 4
septemba nilileta taarifa mahakamani ya
kuleta wakili na nilitaarifu Mahakama kuwa
nitakuwa na wakili Method Kimomogoro wa
Arusha, Leo Kimomogoro hayupo kwa kuwa
alininiletea taarifa ya kufiwa na mjomba wake
Karagwe, hivyo hatahudhuria mahakamani leo,
kwa hiyo alishauri nijiwakilishe mwenyewe.
Kuhusu na kesi, kwa vile tuna taarifa ya
kuondoa kesi hii nafikiri itakuwa sawasawa
tujadili, mahakama iangalie kama taarifa hii
ipo sawasawa kisheria, ili suala la kufanya
maamuzi au kusikiliza hoja za pingamizi
zitakuwa hazina sababu. Tusikilize hoja ya
kuondoa kesi hii
JAJI NATALIA KIMARO: Wakili wa serikali
WAKILI WA SERIKALI: Nnaunga mkono hoja ya
Lissu ili tuweze kujua sababu hasa za kuondoa
kesi hii mahakamani
Wasonga: wakati ambapo mnasubiri kujadili
kuhusu kuondoa hoja mahakamani, mimi
nilikuwa na wateja niliokuwa nawawakilisha,
na sasa mkianza kuendelea kujadili wakati
waliokuwa wateja wamejiondoa, sasa
mkiendelea kujadili mimi nitakuwa
ninamwakilisha nani?
a nani?
Majaji wanajadiliana kwa umakini
JAJI MASATi, Wewe unaweza kuondoa rufaa?
WASONGA: Wateja wamenikana kabisa
hawataki kuendelea nitakuwa namwakilisha
nani? Mimi sijaja kuielekeza mahakama,
mahama ndio iamue
LISSU:SWali analouliza Wasonga ni Muhimu
sana, anauliza anamwakilisha nani? Aiambie
mahakama lini alijua kuwa hana wateja wa
kuwakilisha katika mahakama hii? Barua yake
inasema Selema ameleta hati ya kiapo
mahakamani ili kumruhusu Wasonga kufungua
Rufaa. Ililetwa mahakamani 24 Mei mwaka
huu, miezi mitatu iliyopita, na ilipelekwa kwa
Wasonga na sisi tarehe hiyo hiyo. Hivyo
alikuwa na taarifa kwa muda mrefu, alikuwa
na muda wa kutosha wa kuleta taarifa
mahakamani kabla shauri halijapangwa
kusikilizwa, na kanuni za mahakama hii Majaji
zinalazimu muomba rufaa anayetaka kuondoa
kesi alete taarifa kabla rufaa haijapangwa
kusikilizwa. Wasonga alikuwa na taarifa miezi
mine hakuchukua hatua zozote kuitaarifu
mahakama, au sisi. Amesubiri hadi kesi
imepangwa kusubiri mpaka imepangwa,
akasubiri nikaweka wakili, akasubiri hadi
serikali ikaleta hoja za kupinga rufaa na kuleta
mawakili wake, akasubiri ibaki siku mbili, lengo
pekee tunaloona hapa ni kuzuia hoja za
pingamizi zisisikilizwe, kuzuia haki isitendeke
kwa kuondoa rufaa ili mahakama isitende haki,
taarifa hii imeletwa kwa nia mbaya,
(maliciously), anasema wateja wake ni akina
nani, gharama atalipa nani? Wakati kuna kiapo
mahakamani kinachosema kuwa hakuwahi
kuelekezwa kukata rufaa tangu mwezi mei. Sisi
tumeacha shughuli zetu tumekuja
mahakamani na wakati yeye alikuwa na
taarifa, sisi tutalipwa na nani? Naomba ombi
la kuondoa kesi lisikubaliwe, limeletwa kwa nia
mbaya. Kama itawapendeza mkimruhusu
aondoe kesi, gharama za rufaa hii azibebe
wakili aliyeleta rufaa bila kuambiwa na wateja
wake. Haitakuwa haki kuwalipisha watu ambao
wanasema sisi hatujamwambia wakili akate
rufaa.
WAKILI WA SERIKALI TANGO, Taarifa ya
kuondoa rufaa hii haipo sahihi kisheria. Hata
sheria iliyotumika kuondoa rufaa hii sio sahihi,
kanuni ya 102 ya mahakama za rufaa ndiyo
iliyotumiwa na wakili huyu kuleta taarifa,
niliyopewa ilikuwa haina hata muhuri wa
mahakama, Kanuni hii hutumika kumwomba
msajili kuondoa kesi kabla haijapangwa
kusikilizwa. Kuhusu maombi haya kuyaondoa
au la, naiomba mahakama itambue kuwa
haijapewa mamlaka kwa mujibu wa kanuni hii,
maana hata maombi yenyewe yapo
incompetent. Hili analosema Wasonga kuwa
atamwakilisha nani, yeye alipaswa awaite
wateja wake kuwaambia kuwa kukishakuwa na
hoja za pingamizi uwezekano wa kuondoa kesi
haupo, sasa yeye anakuja mahakamani
utadhani hajui sheria, yeye akiambiwa tu
nenda kaondoe kwa kanuni ambazo hata
hazikubaliki kisheria itakuwa sio sahihi. Mimi
ninaunga mkono hoja za Lissu kwa kuwa
maombi haya hayana nia nzuri
JAJI

CHANZO CHA TAHARUKI BUNGENI NI MAONI YA KAMBI YA UPINZANI

MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU

MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIAYA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013

(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)

Mtunza nidhamu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu akichangia Bungeni leo Dodoma

Msemaji wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni Wizara ya Sheria na Katiba Tundu Lissu alipokuwa akiwakilisha  mchango wa kambi yake Bungeni Dodoma

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.

Muswada huu wa sasa unalenga kufanya marekebisho katika Sehemu ya Tano ya Sheria inayohusu ‘Kuitisha Bunge Maalum.’ Sambamba na mapendekezo haya, kuna mapendekezo ya kufanya marekebisho katika Sehemu ya Sita kwa kufuta vifungu vya 32 hadi 36 vya Sheria vinavyohusu utaratibu wa kura ya maoni kwa ajili ya kuhalalisha ‘Katiba Inayopendekezwa.’ Marekebisho haya yamewekwa katika aya ya 57 ya Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013. Mapendekezo ya Muswada huu ni muhimu lakini yana utata mkubwa.

Mheshimiwa Spika,

Katika kutekeleza majukumu yake ya kuuchambua Muswada huu, Kamati ya Bunge lako tukufu ya Katiba, Sheria na Utawala ilikutana na wadau wengi mbali mbali. Hivyo, kwa mfano, Kamati ilipata maoni ya taasisi za kidini na za kiraia; taasisi za elimu ya juu na za kitaaluma; vyama vya siasa na asasi nyingine. Kwa sababu ambazo Kamati haikuelezwa vizuri na uongozi wa Bunge hili tukufu, mapendekezo ya Kamati kwenda Zanzibar kwa lengo la kukusanya maoni ya wadau wa Zanzibar juu ya Muswada huu muhimu kwa mustakbala wa Jamhuri ya Muungano yalikataliwa.

Kwa maana hiyo, ni muhimu Bunge lako tukufu lifahamu ukweli huu kwamba wadau pekee walioshirikishwa kutoa maoni yao juu ya Muswada ni Watanzania Bara tu. Wazanzibari hawakupatiwa fursa hiyo na hawakushirikishwa kabisa, licha ya Sheria yenyewe kuwa na mambo mengi yanayoihusu Zanzibar. Kwa vile wadau wa Zanzibar walishirikishwa kikamilifu kutoa maoni yao kuhusu Muswada uliopelekea Sheria hii kutungwa mwaka 2011, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua ni kwa nini uongozi wa Bunge na wa Serikali umeona si busara na sahihi kuwapatia Wazanzibari fursa ya kutoa maoni yao kuhusu Muswada huu wa kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inawahusu pia Wazanzibari na nchi yao.

URAIS WA KIFALME KWA MARA NYINGINE TENA!!!!

Mheshimiwa Spika,

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepigia kelele jitihada za serikali hii ya CCM kudhibiti mchakato wa Katiba Mpya kwa kuendeleza kile tulichokiita miaka miwili iliyopita, “… kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.[i] Hapo tulikuwa tunazungumzia mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wajumbe na watendaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, na tulisema kwamba mamlaka hayo yalikuwa na lengo moja tu: “kuhakikisha kwamba matokeo ya kazi ya Tume hiyo ni yale tu yanayotakiwa na Rais na Serikali yake na chama chake cha CCM.

 

Mheshimiwa Spika,

Katika Maoni yetu wakati wa kutungwa kwa Sheria hii mwezi Novemba mwaka 2011, Kambi Rasmi ya Upinzani ilipinga vikali mapendekezo ya kumwezesha Rais kuteua Wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na Bunge lako tukufu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Tulisema yafuatayo kuhusiana na jambo hili: “… wajumbe … wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais.

Kwa sababu ya upinzani huo, mapendekezo ya kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiokuwa wabunge na Wawakilishi yaliondolewa katika Muswada huo wa Sheria hii. Badala yake, kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria iliyotungwa na Bunge lako tukufu kiliweka wazi kwamba “wajumbe mia moja sitini na sita [watateuliwa] kutoka …” taasisi zilizotajwa katika kifungu hicho.

Mheshimiwa Spika,

Ni kweli kwamba kifungu cha 22(1)(c) kama kilivyotungwa kilileta giza badala ya mwanga katika suala la uteuzi wa wajumbe hao. Kama tulivyoieleza timu ya wataalamu wa Serikali kufuatia mkutano wetu na Rais Jakaya Kikwete uliofanyika Ikulu tarehe 26 Novemba, 2011: “Toleo la Kiswahili la Sheria linasema kwamba wawakilishi wa makundi mengine ‘watakaoteuliwa kutoka’ kwenye makundi yaliyoorodheshwa. Toleo la Kiingereza linasema wajumbe hao watakuwa ‘drawn from’ (kwa tafsiri ya Kiswahili ‘watachukuliwa kutoka’). Maana za maneno haya hazifanani na wala hayako wazi kuhusu nani ‘atakayewateua’ au ‘kuwachukua’ wajumbe hao kutoka kwenye taasisi zao.[ii]

Kwingineko katika mkutano wetu na Rais Kikwete tulimweleza kwamba: “Wajumbe 166 wengine wanaowakilisha taasisi nje ya Wabunge na Wawakilishi hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala na taasisi zao kwani Sheria haisemi ni nani atakayewateua na/au kuwachagua.” Kwa sababu hiyo, tulipendekeza kwamba “Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa na’ taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi.[iii]

Mheshimiwa Spika,

Mapendekezo ya marekebisho yaliyoko kwenye Muswada huu yanaonyesha wazi kwamba ushauri wetu kwa Rais Kikwete na kwa timu yake ya watalaamu umepuuzwa. Badala yake, serikali hii sikivu ya CCM imeamua kuturudisha nyuma kwa zaidi ya miaka miwili kwa kuibua tena pendekezo la kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na Wabunge au Wawakilishi wa Zanzibar. Hii ni kwa sababu aya ya 3 ya Muswada inapendekeza kwamba wajumbe hao sasa wateuliwe Rais. Hiyo ni sawa na kusema kwamba kilichokuwa hakifai miaka miwili iliyopita sasa kinafaa; na kilichokataliwa wakati ule sasa kinakubalika!

Ili kuficha ukweli kwamba mwenye mamlaka ya uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi ni Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Muswada unapendekeza kuongezwa kwa vifungu vidogo vipya viwili katika kifungu cha 22. Kwanza, inapendekezwa kuwe na kifungu kidogo cha (2A) ambacho kitamruhusu Rais kualika kila kundi lilioainishwa katika kifungu kidogo cha 1(c) “kuwasilisha kwake orodha ya majina ya watu wasiozidi watatu ili kuteuliwa kuwa wajumbe.” Pili, inapendekezwa kuwe na kifungu kidogo cha (2B) kitakachomlazimu Rais kuzingatia sifa na uzoefu wa watu waliopendekezwa, na usawa wa jinsia wakati wa kufanya uteuzi wa wajumbe hao.

Mheshimiwa Spika,

Mapendekezo ya kumpa Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum hayakubaliki na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaliomba Bunge lako tukufu lisiyapitishe kuwa Sheria. Kwanza, mapendekezo haya yanarudisha dhana kwamba wajumbe hawa watakuwa watu wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM. Rais Kikwete na chama anachokiongoza ni wadau wakubwa wa mchakato wa Katiba Mpya na wana maslahi halisi na makubwa ya kuhakikisha kwamba matakwa ya chama chao ndio yanakuwa Katiba Mpya ya nchi yetu.

Ushahidi wa maslahi haya ya CCM ni kile kinachoitwa Ufafanuzi Kuhusu Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wanachama na Viongozi wa CCM uliotolewa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM tarehe 10 Juni, 2013. Katika Ufafanuzi huo, CCM imekataa mapendekezo yote muhimu yaliyoko kwenye Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume. Needless to say, Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa vikao vyote vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM. Kumpa Rais, na Mwenyekiti wa CCM Taifa, mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum litakaloijadili – na kuikubali au kuikataa – Rasimu ya Katiba ambayo chama chake kimekwishaikataa ni sawa na kuipa CCM fursa nyingine ya kujaza Bunge hilo na makada wake kwa lengo la kutekeleza matakwa ya chama hicho.

Pili, hata bila wajumbe hawa kuteuliwa kwa namna inayopendekezwa, tayari CCM peke yake ina zaidi ya 72% ya wajumbe wote wa Bunge Maalum wanaotokana na Wabunge na Wawakilishi. Kumpa Mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kuteua wajumbe wengine zaidi, kama inavyopendekezwa katika Muswada huu, ni kutoa mwanya kwa CCM kutumia kivuli cha makundi ya kiraia, taasisi za kidini na makundi mengine ili kujiongezea wajumbe wengine zaidi, na hivyo kuhakikisha kwamba Bunge Maalum litatekekeleza matakwa ya kuendeleza status quo.

Kwa maneno mengine, Serikali hii ya CCM na Wabunge wake inataka Mwenyekiti wao wa Taifa ayachagulie makanisa na awachagulie Wakristo wawakilishi wao katika Bunge Maalum; awachagulie Waislamu wa BAKWATA, Baraza Kuu, JUMAZA na taasisi nyingine za Kiislamu wawakilishi wao katika Bunge hilo; avichagulie vyama vya siasa vinavyoipinga CCM wawakilishi wao; awachagulie wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wahadhiri, wanafunzi, wafanyabiashara, walemavu na makundi mengine ya kijamii wawakilishi wao katika Bunge Maalum! Kama ni hivyo, hilo halitakuwa Bunge Maalum la Watanzania, bali litakuwa Bunge Maalum la CCM na Mwenyekiti wao. Hili halikubaliki kwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na, tunaamini, halitakubalika kwa wananchi wa Tanzania katika ujumla wao.

Tatu, kwa jinsi yalivyo kwa sasa, mapendekezo haya hayawezi kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria kinachotaka wajumbe wa Bunge Maalum wasiotokana na wabunge au wawakilishi kuwa mia moja sitini na sita. Hii ni kwa sababu, hata kama watu wote waliopendekezwa na makundi yaliyoainishwa na kifungu hicho watateuliwa kuwa wajumbe, bado idadi yao itakuwa wajumbe ishirini na saba kwa kuwa makundi yenyewe yako tisa tu! Muswada uko kimya juu ya wajumbe wengine mia moja thelathini na tisa watatoka wapi na watateuliwa na nani na kwa utaratibu upi.

Kuna hoja kwamba utaratibu wa uteuzi wa wajumbe unaopendekezwa na Muswada unafanana na uteuzi wa wajumbe wa Tume ulioko kwenye kifungu cha 6(6) cha Sheria ambapo Rais alialika vyama vya siasa, jumuiya za kidini, asasi za kiraia, n.k., kuwasilisha orodha ya majina ya watu ili kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume. Hoja hii sio sahihi. Kwanza, Tume ya Katiba sio sawa na Bunge Maalum. Tume ni chombo cha kitaalamu chenye majukumu ya kitaalamu ya kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti pamoja na Rasimu ya Katiba. Uhalali wa Tume unatokana na utaalamu wa wajumbe wake na weledi katika kutekeleza majukumu yao ya kitaalamu.

Kwa upande mwingine, Bunge Maalum ni chombo cha uwakilishi ambacho wajumbe wake wana majukumu ya kisiasa ya kuwakilisha wananchi wa makundi mbali mbali kwenye kazi ya kisiasa ya kuandika Katiba Mpya. Uhalali wa Bunge Maalum unatokana na upana na ubora wa uwakilishi wake wa makundi mbali mbali ya kisiasa na kijamii. Chombo cha uwakilishi cha aina hii lazima kitokane na wananchi na/au makundi ya kijamii kinachoyawakilisha ili kiwe na uhalali wa kisiasa. Dhana ya Rais – na Mwenyekiti wa CCM – kuteua Wajumbe wa Bunge Maalum inavuruga au kuondoa kabisa dhana ya uwakilishi wa wananchi na uhalali wa kisiasa katika mchakato wa Katiba Mpya.

Pili, kumpa Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi wa Zanzibar kunaleta dhana ya ubaguzi. Hii ni kwa sababu, Rais hana mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalum watakaotoka kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Hawa wataingia katika Bunge Maalum kwa mujibu wa nafasi zao Bungeni au katika Baraza na sio kwa fadhila ya Rais. Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini Rais awe na mamlaka ya kuteua wajumbe wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi wakati hana mamlaka hayo kuhusu Wabunge na Wawakilishi? Needless to say, ubaguzi huu unaenda kinyume na matakwa ya ibara ya 13(2) ya Katiba ya sasa na, kwa hiyo, haukubaliki.

Tatu, uteuzi wa wajumbe wa Tume uliofanywa na Rais na ambao unatumiwa kama mfano wenyewe ulikuwa na walakini kubwa. Katika hili, kuna ushahidi wa wawakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na asasi mbali mbali za kiraia zikiwemo za walemavu waliowasilisha maoni ya taasisi zao kwa Kamati juu ya Muswada huu. Wawakilishi hao waliiambia Kamati kwamba ijapokuwa waliandikiwa na Rais kuwasilisha majina ya wajumbe wao kwa ajili ya kuteuliwa kwenye Tume, na walifanya hivyo, hakuna hata moja ya majina waliyopendekeza aliyeteuliwa na Rais kuwa wajumbe wa Tume.

Badala yake, Rais aliteua watu aliowaona yeye na washauri wake wanafaa. Kama taarifa za wadau hawa ni za kweli maana yake ni kwamba Rais na Mwenyekiti huyu wa CCM Taifa hawezi kuaminika tena kuteua wajumbe halisi wa taasisi hizi katika Bunge Maalum ambalo ndilo litakalojadili na kuipitisha – au kuikataa – Rasimu ya Katiba Mpya ambayo tayari CCM na wapambe wao wametamka wazi kwamba wanaikataa!

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM WAONGEZWE

Mheshimiwa Spika,

Ili kutatua mkanganyiko huu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza Bunge lako tukufu lirejee na kukubali mapendekezo yetu kwa Timu ya Wataalamu wa Serikali ya Januari mwaka jana:

 • Ø “Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa na’ taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi;
 • Ø “Sheria itaje kwamba idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum watakaotokana na kila taasisi iliyoorodheshwa katika kifungu cha 22(1)(c) itakuwa 354 kama walivyoorodheshwa hapa chini:

(a)           “Asasi zisizokuwa za kiserikali zilizotajwa katika aya (i) zifafanuliwe kuwa ni makundi yanayounganisha asasi hizo, yaani, ANGOZA, TANGO, TACOSODE na Jukwaa la Katiba na kila moja ya makundi hayo itakuwa na wajumbe watano kwa jumla ya wajumbe 20;

(b)           “Asasi za kidini zilizotajwa katika aya (ii) zifafanuliwe kuwa ni makundi yanayounganisha asasi hizo, yaani, BAKWATA, Baraza Kuu, JUMAZA, TEC, CCT na PCT na kila moja ya makundi hayo itakuwa na wajumbe watano kwa jumla ya wajumbe 30. Aidha, Waadventista wa Sabato (SDA), Hindu, Shia Ithnaasheri na Sikh watakuwa na mjumbe mmoja mmoja, kwa jumla ya wawakilishi 35 wa taasisi za kidini;

(c)           “Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vilivyotajwa katika aya (iii) vitakuwa na wajumbe 72 watakaogawanywa katika makundi mawili: 1) vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu vitakuwa na wajumbe 42 ikiwa ni wajumbe wawili kwa kila chama; 2) vyama vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni vitakuwa na wajumbe 30 ikiwa ni CCM 18, CHADEMA 7, CUF 3 na NCCR-Mageuzi, TLP na UDP 3 kwa ujumla wao. Hii ni kufuatana na uwiano wa kura zote za Wabunge ambazo vyama hivyo vilizipata kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010;

(d)           “Taasisi za elimu ya juu zilizotajwa katika aya (iv) zifafanuliwe kuwa ni vyuo vikuu 28 vinavyotambuliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na vyuo vya elimu ya juu 16 vinavyotambuliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE). Taasisi hizi zitakuwa na mjumbe mmoja kwa kila moja kwa jumla ya wajumbe 44;

(e)           “Taasisi za elimu ya juu zinahusisha pia vyama vya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambavyo vitakuwa na mjumbe mmoja mmoja kwa chama cha wanafunzi kwa jumla ya wajumbe 44;

(f)  Taasisi za elimu ya juu zinahusisha pia vyama wahadhiri/wakufunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambavyo vitakuwa na mjumbe mmoja mmoja kwa kila chama kwa jumla ya wajumbe 44;

(g)           “Makundi yenye mahitaji maalum yaliyotajwa katika aya (v) yafafanuliwe kuwa ni mashirika yanayowakilisha wenye ulemavu wa macho, ngozi, viziwi/bubu, viwete na walemavu wa aina nyingine ambayo yatakuwa na wajumbe 10 kwa ujumla wao;

(h)           “Vyama vya wafanyakazi vilivyotajwa katika aya (vi) vifafanuliwe kuwa ni vile vilivyosajiliwa na vitakuwa na wajumbe 40 ikiwa ni wajumbe wawili kutoka kila chama cha wafanyakazi kilichosajiliwa;

(i)   “Jumuiya ya wakulima iliyotajwa katika aya (vii) itakuwa na wajumbe 10 watakaotokana na vyama vya wakulima wa mazao kama vile pamba, kahawa, korosho, chai, katani, karafuu, miwa na wavuvi;

(j)   “Jumuiya ya wafugaji iliyotajwa katika aya (viii) itakuwa na wajumbe 10 watakaotoka Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Wafugaji na Wawindaji/wakusanya matunda ya porini (PINGOS Forum);

(k)“Vikundi vingine vya watu wenye malengo yanayofanana vilivyotajwa katika aya (ix) vifafanuliwe kumaanisha Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Chama cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC); Chama cha Wafanyabiashara ya Madini na Nishati (TCME); vyama/mashirika ya wachimbaji madini wadogo wadogo; Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOWAT), Chama cha Waandishi Habari/Jukwaa la Wahariri Tanzania, Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Chama cha Mawakili Zanzibar (ZLS), Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) na Chama cha Wakandarasi Tanzania (CATA). Makundi haya yatakuwa na wajumbe wawili kwa kila moja kwa jumla ya wajumbe 26.”

 

Mheshimiwa Spika,

Kwa mujibu wa kifungu cha 22(1) cha Sheria kama ilivyo sasa, Bunge Maalum litakuwa na jumla ya wajumbe 604, yaani Wabunge 357, Wawakilishi 81 na wajumbe 166 wanaowakilisha makundi mbali mbali. Mapendekezo haya ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni yatafanya uwakilishi katika Bunge Maalum kupanuka hadi wajumbe 792 kwa Tanzania yenye idadi ya watu milioni 45 kwa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.

Hili, kwa vyovyote vile, ni ongezeko kubwa la wajumbe wa Bunge Maalum. Hata hivyo, ukubwa huu unaopendekezwa hauna tofauti kubwa sana na Mabunge Maalum ya nchi nyingine ambazo zimekamilisha utungaji wa Katiba Mpya kwa kutumia utaratibu huu. Kwa mfano, Bunge Maalum la Jamhuri ya Nepal la mwaka 2011 lilikuwa na wajumbe 601 kwa nchi yenye idadi ya watu milioni 26; Bolivia (2009) lilikuwa na wajumbe 255 katika nchi yenye watu milioni 9; Kenya (2005) lilikuwa na wajumbe 629 kwa idadi ya watu milioni 31; Eritrea (1997) lilikuwa na wajumbe 527 kwa idadi ya watu milioni 3.2, wakati Bunge Maalum la Ufaransa ya Mapinduzi ya 1789 lilikuwa na wajumbe 1145 katika nchi iliyokuwa na idadi ya watu milioni 28.[iv]

Kikubwa na muhimu zaidi, kwa mapendekezo haya, ni kwamba Bunge Maalum la Katiba litakuwa na sura ya Kitanzania zaidi badala ya utaratibu wa sasa unaolifanya Bunge Maalum kuonekana la kiCCM zaidi. Kwa kuongezea tu, Mheshimiwa Spika, wadau karibu wote waliotoa maoni yao kwenye Kamati walipendekeza kuongezwa kwa idadi ya wajumbe wa Bunge Maalum. Kwa kigezo chochote kile, kwa hiyo, mapendekezo haya ni ya kidemokrasia na tunaliomba Bunge lako tukufu liyaunge mkono ili kuiwezesha nchi yetu kujipatia Katiba Mpya yenye sura halisi ya kitaifa kuliko inavyopendekezwa sasa.

UWAKILISHI WA ZANZIBAR KATIKA BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Spika,

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekwishatoa Rasimu ya Katiba kwa mujibu wa kifungu cha 19(1)(d) cha Sheria. Rasimu hiyo imepndekeza mabadiliko makubwa katika muundo wa Jamhuri ya Muungano kwa kupendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu. Baada ya kukamilika kwa mchakato wa kutoa maoni juu ya Rasimu hii kwa mujibu wa kifungu cha 18, Tume itawasilisha ripoti kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa kifungu cha 20(1). Baada ya hapo, Rais, “… atachapisha Rasimu ya Katiba katika Gazeti la Serikali na kwenye magazeti mengine pamoja na maelezo kwamba Rasimu ya Katiba itawasilishwa kwenye Bunge Maalum kwa ajili ya kupitishwa Katiba inayopendekezwa.”[v]

Mheshimiwa Spika,

Ili kutimiza matakwa haya ya Sheria na kwa kuzingatia mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume, Bunge lako tukufu linahitaji kuangalia upya suala la uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar katika Bunge Maalum watakaotokana na makundi yaliyoainishwa katika kifungu cha 22(1)(c) “… haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao.” Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55.

Rasimu ya Katiba itakayojadiliwa na Bunge Maalum inahusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano peke yake. Rasimu hiyo imependekeza kwamba masuala yote yasiyo ya Muungano ya Washirika wa Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar, yashughulikiwe na Katiba za Washirika hao.[vi]

Kwa sasa Wabunge wanaotoka Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ni 83, wakati Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina wajumbe 76. Kwa ujumla, kwa hiyo, ili kutekeleza matakwa ya kifungu cha 22(1) na (2) cha Sheria, Zanzibar itakuwa na wajumbe 219 katika Bunge Maalum lenye wajumbe 604, sawa na takriban 36% ya wajumbe wote. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kujua: kama ilikuwa busara na sahihi kwa nusu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Zanzibar, kwa nini isiwe busara na sahihi vile vile kwa nusu ya wajumbe wa Bunge Maalum litakaloijadili na kuipitisha Katiba Mpya hiyo kutoka Zanzibar? Au ndio kusema kwamba hoja za usawa kati ya nchi Washirika wa Muungano huu ni kelele za majukwaani tu?

Mheshimiwa Spika,

Profesa Palamagamba J.A.M. Kabudi wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa Tume aliwahi kusema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika hapa Dodoma tarehe 12 Novemba 2011 kwamba: “Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.” Kwa sababu hiyo, na kwa kuzingatia mapendekezo ya ‘hadhi na haki sawa’ baina ya Washirika wa Muungano yaliyoko katika Rasimu ya Katiba,[vii] Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba idadi ya wawakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalum iongezwe hadi kufikia nusu ya wajumbe wote wa Bunge Maalum.

Hili linawezekana kwa namna mbili. Kwanza, kwa kuongeza idadi ya wajumbe waliotajwa katika kifungu cha 22(1)(c) hadi 354 kama tulivyopendekeza katika Maoni haya. Na pili, kwa kurekebisha kifungu cha 22(2) ili kisomeke kwamba idadi ya wajumbe kutoka Zanzibar ‘haitapungua asilimia hamsini na tano ya wajumbe hao.’ Kama pendekezo hili litakubaliwa na Bunge lako tukufu, wajumbe wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar wataongezeka kutoka 214 kwa mujibu wa Sheria ilivyo sasa, hadi 323. Muhimu zaidi, Bunge Maalum litakuwa limetimiza matakwa ya usawa wa Washirika wa Muungano kwa kuwa na idadi sawa ya wajumbe katika Bunge hilo. Hili litaondoa manung’uniko yanayoweza kujitokeza baadae kwamba Wazanzibari hawakutendewa haki sawa katika Bunge la Katiba.

WATUMISHI WA BUNGE MAALUM

Mheshimiwa Spika,

Muswada unapendekeza marekebisho mengine katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hivyo basi, aya ya 4 inapendekeza marekebisho ya kifungu cha 24(4) kama ifuatavyo: “Katibu wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Naibu wake na taasisi husika, atateua kutoka katika Bunge, Baraza la Wawakilishi na taasisi husika idadi ya watumishi kama itakavyoonekana inafaa kwa utekelezaji wa majukumu na mamlaka ya Bunge Maalum.” Kama kilivyo hivi sasa, kifungu hicho kinasomeka kama ifuatavyo: “Katibu wa Bunge Maalum baada ya kushauriana na Naibu Katibu wa Bunge Maalum watateua watumishi kutoka kwenye Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa idadi watakayoona inafaa kwa ajili ya kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya Bunge Maalum.”

Mheshimiwa Spika,

Kama inavyoonekana wazi, mabadiliko pekee yanayopendekezwa na Muswada ni maneno ‘taasisi husika.’ Maneno haya hayajatafsiriwa mahali popote katika Sheria, na Muswada uko kimya juu ya maana yake. Hata Maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria mbele ya Kamati yako kimya juu ya maneno hayo.[viii]

Ukimya huu una mwangwi mkubwa. Kama pendekezo hili litakubaliwa, kutakuwa na uwezekano wa watumishi wa Bunge Maalum la Katiba kuteuliwa kutoka katika taasisi na idara mbali mbali za serikali, au hata taasisi zisizokuwa za kiserikali. Kwa sababu Bunge Maalum litatekeleza majukumu yake kwa muda maalum unaopendekezwa katika aya ya 6 ya Muswada huu, ni wazi watumishi hao watatumikia Bunge Maalum on secondment kutoka kwenye taasisi zao za mwanzo. Kwa maana hiyo, watumishi hao watawajibika kwa taasisi zao na wanaweza kutumiwa na taasisi zao kutoa taarifa au siri muhimu juu ya shughuli za Bunge Maalum kwa taasisi zao.

Kwa upande mwingine, watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamepewa kinga ya kikatiba inayowakataza kupokea maelekezo kutoka taasisi nyingine nje ya Bunge. Kama kifungu cha 4(3) cha Sheria ya Uendeshaji Bunge, Na. 14 ya 2008, inavyoweka wazi, katika utekelezaji wa majukumu yao, watumishi wa Bunge “… hawatapokea maelekezo kutoka mahali popote nje ya Utumishi (wa Bunge).” Katika mazingira haya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mapendekezo ya kurekebisha kifungu cha 24(4) hayakidhi matakwa ya uhuru wa Bunge Maalum na, kwa sababu hiyo, yasikubaliwe na Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika,

Kuna hoja kubwa zaidi juu ya pendekezo hili. Hoja hii inahusu mamlaka ya Katibu wa Bunge Maalum na Naibu wake kuteua watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Mapinduzi Zanzibar kuwa watumishi wa Bunge Maalum chini ya kifungu cha 24(4) cha Sheria, na pendekezo la Muswada la kukifanyia marekebisho.

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Bunge, Katibu wa Bunge hana mamlaka ya kuteua watumishi wa Bunge peke yake. Hayo, kwa mujibu wa Sheria hiyo, ni mamlaka ya pamoja kati ya Katibu na Tume ya Utumishi wa Bunge na utekelezaji wake unahitaji mashauriano kati ya vyombo hivyo viwili.[ix] Kwa sababu hiyo, na kwa kuzingatia utaratibu wa Sheria hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza watumishi wa Bunge Maalum wateuliwe kutoka miongoni mwa watumishi wa Bunge na Baraza la Wawakilishi baada ya mashauriano kati ya Katibu wa Bunge Maalum na Naibu wake pamoja na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Pendekezo hili lina faida kwamba watumishi wa Bunge Maalum watakuwa wameteuliwa na watawajibika kwa Bunge Maalum na siyo kwa taasisi nyingine nje ya Bunge Maalum. Kwa maana hiyo, pendekezo la Muswada juu ya uteuzi wa watumishi wa Bunge Maalum nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar halina umuhimu na linapaswa kukataliwa.

TAFSIRI YA RASIMU YA KATIBA

Mheshimiwa Spika,

Muswada unapendekeza marekebisho ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayohusu tafsiri ya maneno mbali mbali. Mapendekezo ya Muswada yanahusu tafsiri ya maneno ‘Rasimu ya Katiba’ na ‘Kanuni.’ Pendekezo la kutafsiri neno ‘Kanuni’ halina utatanishi wowote na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaliunga mkono. Kwa upande mwingine, Kambi Rasmi Upinzani Bungeni inapinga tafsiri inayopendekezwa ya maneno ‘Rasimu ya Katiba.’ Kwa mujibu wa aya ya 2 ya Muswada, maneno ‘Rasimu ya Katiba’ yatakuwa na maana ya “… Rasimu ya Katiba ambayo imetayarishwa na Tume kutokana na maoni na mapendekezo ya wananchi chini ya Sheria.”

Pendekezo hili linapingana na maudhui ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwanza, pamoja na kwamba maoni ya wananchi ni chanzo muhimu cha ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba, maoni hayo sio chanzo pekee cha ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba. Kwa mujibu wa kifungu cha 17(4) cha Sheria, Tume inatakiwa kupitia “na kuchambua michango, mawazo, maoni, taarifa na mapendekezo yaliyokusanywa na kufanyiwa tathmini siku za nyuma….” Kifungu hicho kimeorodhesha nyaraka nyingi muhimu na za kihistoria ambazo zimejenga taswira ya kikatiba ya nchi yetu tangu uhuru wa Tanganyika mwaka 1961. Tume inawajibika kuzipitia na kuzichambua nyaraka zote hizo “katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria hii….”

Pili, Tume pia inawajibika kutumia “tafiti za kiuchambuzi na kitaalam zitakazofanywa na Tume”,[x] na “nyaraka nyingine zozote ambazo Tume itaona ni muhimu.”[xi] Vyanzo vyote hivi vinatakiwa kutumika katika matayarisho ya Rasimu ya Katiba. Kwa maana hiyo, madhara ya mapendekezo ya Muswada juu ya tafsiri ya maneno ‘Rasimu ya Katiba’ ni ya wazi na mabaya. Kama yatakubaliwa na kuwa Sheria, vyanzo vyote hivi vya ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba vitakuwa redundant.

Aidha, mapendekezo ya Tume na Rasimu ya Katiba yanayotokana na vyanzo hivyo yatakuwa kinyume cha Sheria na yatabidi yaondolewe kwenye ripoti na Rasimu ya Katiba. Kwa sababu hizi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba maneno ‘Rasimu ya Katiba’ yatafsiriwe kumaanisha “… Rasimu ya Katiba ambayo imetayarishwa na Tume kwa mujibu wa Sheria hii.” Tafsiri hii inayopendekezwa inajumuisha maoni ya wananchi pamoja na vyanzo vingine vyote vya ripoti ya Tume na Rasimu ya Katiba vilivyoainishwa kwenye Sheria.

UHALALISHAJI WA KATIBA MPYA

Mheshimiwa Spika,

Muswada unapendekeza marekebisho katika kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinachohusu ‘uendeshaji wa kura ya maoni.’ Inapendekezwa kwamba kifungu hicho kifutwe na badala yake kiwekwe kifungu kipya kitakachosema kwamba “masharti yote yanayohusu uendeshaji wa kura ya maoni utawekwa na Sheria ya Kura ya Maoni.” Kwa vile tayari kuna Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni, 2013, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakubaliana na pendekezo hili.

Hata hivyo, kifungu cha 31 sio kifungu pekee katika Sheria hii chenye masharti ya uendeshaji wa kura ya maoni. Kuna vifungu vingine vinavyotaja au kuweka utaratibu wa kura ya maoni. Ukweli ni kwamba Sehemu ya Sita yote inayohusu ‘uhalalishaji wa Katiba Inayopendekezwa’ inahusika na masuala mbali mbali ya kura ya maoni. Vile vile, kifungu cha 4(1)(n) na (2) navyo pia vinataja kura ya maoni. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, vifungu hivi pamoja na Sehemu ya Sita yote vinahitaji kurekebishwa kwa kufutwa.

Mheshimiwa Spika,

Muswada unapendekeza kufanya marekebisho katika kifungu cha 27(2) cha Sheria kinachohifadhi ‘uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge Maalum’ kwa kuweka kinga ya mashtaka dhidi ya wajumbe wa Bunge Maalum. Zaidi ya hayo, Muswada unapendekeza muda usiozidi siku sabini kwa Bunge Maalum kujadili Rasimu ya Katiba. Muda huo unaweza kuongezwa kwa siku nyingine zisizozidi ishirini kwa ridhaa ya Rais “baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar….” Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakubaliana na mapendekezo yote haya ya Muswada kwa caveat kwamba pendekezo la muda wa nyongeza lisiwekewe muda mahsusi. Hii ni kwa lengo la kuwezesha muda kuongezwa kulingana na hali halisi ya majadiliano ndani ya Bunge Maalum.

JEDWALI LA MAREKEBISHO LA SERIKALI

Mheshimiwa Spika,

Serikali iliwasilisha Jedwali la Marekebisho ya Muswada huu mbele ya Kamati ikipendekeza marekebisho kadhaa katika Muswada na katika Sheria mama. Mapendekezo haya ni ya aina mbili. Kwanza, ni mapendekezo ya marekebisho ya Muswada uliosomwa mbele ya Bunge lako tukufu katika Bunge la Kumi na Moja, na ambayo yalijadiliwa na Kamati na wadau mbali mbali. Haya ni marekebisho yanayopendekezwa katika sehemu A, B na D ya Jedwali la Marekebisho ya Serikali. Marekebisho haya yanaenda sambamba na matakwa ya kanuni ya 84(3) na (4) ya Kanuni za Kudumu na kwa hiyo yanakubalika kikanuni.

Kwa upande mwingine, marekebisho yanayopendekezwa katika sehemu C na E za Jedwali la Marekebisho ya Serikali ni mambo mapya ambayo hayakuwepo kwenye Muswada uliosomwa kwa Mara ya Kwanza katika Bunge lililopita. Marekebisho haya hayakujadiliwa na wadau wan je ya Bunge, na hayajulikani kwa Wabunge wasiokuwa wajumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala. Kwa sababu hiyo, marekebisho haya yanakiuka masharti ya kanuni ya 86(7) ya Kanuni za Kudumu inayoelekeza kwamba “mjadala wakati wa Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Pili utahusu ubora na misingi ya Muswada huo tu.” Ili kulinda heshima ya Bunge lako tukufu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inakuomba, Mheshimiwa Spika, utekeleze wajibu wako chini ya kanuni ya 5(2) ya Kanuni za Kudumu kwa kufutilia mbali sehemu C na E za Jedwali la Marekebisho ya Serikali kwa sababu zinakiuka matakwa ya kanuni tajwa ya Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika,

Sehemu C ya Jedwali la Marekebisho ya Serikali tunaokuomba uifutilie mbali inapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 22A katika Sheria. Katika pendekezo la awali kuhusu kifungu hicho, ilikuwa inapendekezwa kumfanya Spika wa Bunge hili tukufu kuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum kwa ajili ya kutengeneza Kanuni za Kudumu za Bunge Maalum, na kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Baada ya Kamati kuhoji na kuelezwa kwamba Spika/Mwenyekiti wa Muda atakuwa pia na haki ya kugombea kuwa Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum na hivyo kutengeneza mgongano wa wazi wa maslahi, Kamati ilielekeza kwamba Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum watasimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda ambaye hatakuwa na haki ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum. Hata hivyo, hoja ya msingi kwamba hili ni pendekezo jipya ambalo halikuwepo kwenye Muswada uliosomwa Mara ya Kwanza inabaki pale pale.

Kuhusu sehemu E ya Jedwali la Marekebisho ya Serikali, sehemu hiyo inapendekeza kufifisha matakwa ya kifungu cha 26(2) cha Sheria inayoweka masharti ya kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa theluthi mbili ya wajumbe wote wa Bunge Maalum wanaotoka Tanzania Bara na idadi hiyo hiyo ya wajumbe wanaotoka Zanzibar. Pendekezo jipya ni kupunguza idadi ya uungwaji mkono hadi wingi wa kawaida (simple majority) ya wajumbe wote wanaotoka Tanzania Bara na idadi hiyo hiyo ya wajumbe wanaotoka Zanzibar endapo Bunge Maalum litashindwa kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa theluthi mbili baada ya kupiga kura mara mbili. Pendekezo hili nalo linakiuka matakwa ya kanuni ya 86(7) na linapaswa kuondolewa katika mjadala wa Muswada huu.

MENGINEYO

KUITISHWA TENA BUNGE MAALUM?

Mheshimiwa Spika,

Kuna maeneo mengine ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo, kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha utekelezaji bora wa Sheria hii. Eneo mojawapo ni masharti ya kifungu cha 28(2) yanayoruhusu Bunge Maalum kuitishwa tena baada ya kukamilisha majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kuvunjwa chini ya kifungu cha 28(1) cha Sheria hii.

Kifungu cha 28(1) kinasema: “Baada ya kutunga Katiba Inayopendekezwa, masharti yatokanayo na mashrti ya mpito, Bunge Maalum litavunjwa na mamlaka ya kutunga masharti ya Katiba inayopendekezwa, masharti yatokanayo na masharti ya mpito yatakoma.” Kwa upande mwingine, kifungu cha 28(2) kinatengua masharti ya kifungu cha 28(1) kwa maneno yafuatayo: “Kuvunjwa na kukoma kwa mamlaka ya Bunge Maalum hakutachukuliwa kuwa kunaondoa mamlaka ya Rais kuliitisha tena Bunge hilo kwa lengo la kuboresha masharti yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa.”

Mheshimiwa Spika,

Misingi mikuu ya tafsiri za kisheria inaelekeza kwamba chombo chenye mamlaka au majukumu ya kisheria ya kufanya jambo fulani kikishakamilisha kutekeleza mamlaka au majukumu yake hayo kinakuwa functus officio katika jambo hilo, yaani kinakuwa hakina mamlaka tena kisheria juu ya jambo hilo.[xii] Huu ndio msingi wa kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Athari ya kifungu cha 28(2) ni kulifufua kutoka katika wafu Bunge Maalum ambalo, kwa mujibu wa kifungu cha 28(1), linakuwa limekuwa functus officio baada ya kupitisha Katiba Mpya na masharti ya mpito. Na hii inafanywa na Rais ambaye – na chama cha siasa anachokiongoza – ni mdau mkubwa wa mchakato wa Katiba Mpya.

Katika Maoni yetu wakati wa mjadala wa kupitishwa kwa Sheria hii mwezi Novemba 2011, tulisema yafuatayo juu ya kifungu hiki: “Maana halisi ya maneno haya ni kwamba Rais atakuwa na mamlaka ya kuita tena Bunge la Katiba ili lifanye marekebisho ya mambo ambayo yeye au serikali yake au chama chake hawayapendi katika Katiba Mpya kabla haijapigiwa kura ya maoni na wananchi! Kama chombo huru cha wananchi, Rais hawezi kujipa madaraka ya kupingana na kauli ya wananchi kupitia Bunge la Katiba.”

Katika mapendekezo yake kwa timu ya Wataalam wa Serikali iliyoundwa kufuatia mkutano wa tarehe 26 Novemba, 2011 kati ya CHADEMA na Rais Jakaya Kikwete, CHADEMA ilipendekeza kwamba kifungu cha 28(2) kifutwe kabisa.[xiii] Huu ni wakati muafaka kukiangalia upya kifungu hiki ambacho kinaweza kuleta mgogoro usiokuwa na sababu endapo Rais ataamua kuliitisha tena Bunge Maalum kwa sababu Serikali au chama chake hakikubaliani na Katiba Mpya iliyopitishwa na Bunge Maalum.

MCHAKATO WA KATIBA YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Mheshimiwa Spika,

Tarehe 3 Juni, 2013 Tume ilichapisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2013. Kwa kufanya hivyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 18(5) cha Sheria, Tume imekamilisha jukumu lake la kwanza baada ya kukamilisha zoezi la kukusanya maoni ya Watanzania juu ya Katiba Mpya. Rasimu hii inapendekeza mambo mengi na muhimu kwa mustakbala mzima wa nchi yetu na tayari imezua mjadala mkali wa kitaifa. Mwanazuoni mmoja maarufu nchini ameyaita mapendekezo ya Rasimu ‘Mapinduzi ya Kimya Kimya’[xiv]; wakati mwingine amehoji kama Rasimu hii ni ‘Mwarobaini au Sanduku la Pandora?’[xv] Aidha, Profesa Issa G. Shivji ambaye pengine ni msomi maarufu wa masuala ya kikatiba katika sehemu hii ya Afrika, ameonyesha kile ambacho amekiita ‘Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu ya Katiba Mpya.[xvi]

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kama ilivyo kwa wadau wengine ambao wamezungumzia Rasimu hiyo ya Katiba, eneo muhimu pengine kuliko yote ni muundo wa Jamhuri ya Muungano kama shirikisho lenye serikali tatu. Kwa sababu hiyo, Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume imejikita katika masuala ya Muungano tu. Na kwa mujibu wa Mwenyekiti wake, Tume haikushughulikia masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar kwa sababu mambo hayo yanatakiwa kushughulikiwa na Katiba za Washirika wa Muungano.

Kwa maana hiyo, masuala haya sasa itabidi yashughulikiwe kwa utaratibu mwingine wa kisheria Zanzibar na Tanganyika vile vile, ambao utakuwa tofauti na utaratibu uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kutokana na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba, mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano hautakamilika bila ya kuwepo, na kukamilika, kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika na ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika,

Kuanza na kukamilika kwa mchakato wa Katiba Mpya kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar ni suala muhimu kwa muundo wowote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au hata bila Muungano kuwepo, kwa sababu zifuatazo. Kwanza, hata kama muundo wa Muungano utakuwa wa serikali moja, au mbili za sasa, au tatu zinazopendekezwa na Rasimu, ni lazima masuala yote yanayoihusu Tanganyika yaingizwe kwenye mchakato wa Katiba Mpya. Hii ni kwa sababu Rasimu inahusu masuala saba ya Muungano tu, na Zanzibar ina Katiba yake tayari. Pili, hata kama wananchi wa Tanzania watakataa kuendelea na Muungano wa aina yoyote na kudai uhuru kamili wa Washirika wa Muungano, bado masuala ya Katiba Mpya ya Tanganyika na Zanzibar yatahitajika kufanyiwa kazi. Tatu, bila masuala ya Tanganyika kuamuliwa katika Katiba Mpya, mchakato mzima hautakamilika, na kwa maana hiyo, hakuwezi kukawa na uchaguzi wowote wa Jamhuri ya Muungano kwa upande wa Tanganyika.

Kwa vyovyote vile, constitutional gridlock hii lazima ipatiwe suluhisho. Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mchakato wa Katiba Mpya ya Tanganyika na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar, 1984 uanze mara moja ili uendane sambamba na mchakato wa Katiba Mpya ya Jambhuri ya Muungano. Kwa vyovyote vile, kwa maoni yetu, Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kama ilivyo sasa haiwezi kutumika kwa ajili ya mchakato huo kwa sababu sheria hiyo ilitungwa kwa ajili ya mchakato wa Katiba ya Muungano tu.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa ajili ya mchakato wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na Tume yenyewe imekiri kwamba haikujishughulisha na masuala yasiyokuwa ya Muungano kwa sababu hayakuwa sehemu ya majukumu iliyokabidhiwa kisheria. Kwa muundo wake, Tume hiyo haiwezi kujibadilisha na kuwa Tume ya Katiba ya Tanganyika. Kwa maana hiyo, mchakato wa Katiba ya Tanganyika unatakiwa kuwekewa utaratibu mpya na tofauti kabisa wa kisheria na wa kitaasisi. Hii itahitaji kutungwa kwa sheria mpya kwa ajili ya mchakato huo.

Sambamba na mchakato wa Katiba ya Tanganyika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kuanzishwa kwa mjadala juu ya masuala ya mpito kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kwamba Katiba Mpya, ya Muungano peke yake au ya Muungano na za Washirika wake, yaani Tanganyika na Zanzibar, zisiwe tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Au hata kama zitakuwa tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu, kuna uwezekano mabadiliko makubwa ya kisheria na ya kitaasisi yatakayohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa Katiba Mpya, yasiwe tayari kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao. Kwa kuangalia mfano wa Kenya, Katiba Mpya ya nchi hiyo ilikamilika mwezi Agosti, 2010. Hata hivyo, mabadiliko mbali mbali ya kisheria na kitaasisi kwa ajili ya utekelezaji wa Katiba hiyo yalichukua zaidi ya miaka miwili na nusu hadi Uchaguzi Mkuu wa mwezi Machi, 2013.

Ikumbukwe kuwa Kenya haikuwa na suala la Muungano kama Tanzania. Sisi tuna Muungano wa muundo ambao upande mmoja wa Muungano huo una dola yenye Katiba na taasisi kamili za dola, wakati upande mwingine hauna dola wala Katiba na taasisi kamili za dola. Hii ina maana kwamba maandalizi yetu ya kisheria na kitaasisi yanaweza kuhitaji muda mrefu zaidi kuliko ilivyokuwa kwa Kenya. Hatuna budi kuanza kuyafikiria na kuyajadili mambo haya muhimu sasa.

 

—————————————

TUNDU A.M. LISSU

WAZIRI KIVULI & MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA


[i] Angalia Maoni ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria, Mheshimiwa Tundu A.M. Lissu, Kuhusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011, Novemba, 2011.

[ii] Angalia Mapendekezo ya CHADEMA Juu ya Awamu ya Pili ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011, Januari, 2012.

[iii] Angalia Waraka wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Juu ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba, 2011, Novemba, 2011.

[iv] Angalia InterPeace, Constitution-Making for Peace: The Constitution-Making Handbook, www.interpeace.org/publications/doc_download/196-part-3-institutions-groups-and-procedures-english, 2011.

[v] Kifungu cha 20(2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

[vi] Aya za 57(3) na 61 za Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2013.

[vii] Aya za 61(5), 62(1).

[viii] Maelezo ya Mheshimiwa Mathias M. Chikawe, Waziri wa Katiba na Sheria Akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 (T.L. 2012) Kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, 29 Julai, 2013.

[ix] Angalia vifungu vya 9(1), 12(2) na 13(b).

[x] Kifungu cha 17(4)(m).

[xi] Kifungu cha 17(4)(n).

[xii] Angalia uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi ya Bibi Kisoko Medard vrs. Minister for Lands, Housing and Urban Development & Another [1983] TLR 250, kuhusu tafsiri ya functus officio.

[xiii] CHADEMA, Mapendekezo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) juu ya Awamu ya Pili ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadilikoy ya Katiba, 2011, Dodoma, Januari, 2012.

[xiv] Chris M. Peter, The Draft Constitution 2013: A Silent Revolution, Geneva, Juni, 2013.

[xv] Khoti C. Kamanga, The Tanzania Draft Constitution of 2013: Panacea or Pandora’s Box?, Dar es Salaam, Juni, 2013.

[xvi] Issa G. Shivji, Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu ya Katiba Mpya: Mhadhara wa Kuaga Kigoda cha Mwalimu, Dar es Salaam, Juni, 2013.

SADLY KAGAME IS ONLY GOING HALF WAY TOWARDS OUR TRAP.

Kagame General Troops

For the past few weeks Tanzanians lead by media have been discussing non other than Kagame while speculating the coming war. so Rwandies media have call Tanzania citizens the war mongers.

May be I should make it clear to you that Tanzanians, though quite, polite and peaceful, they are like puff adders who strike only after being trampled upon, unlike black mambas who are always looking for something to strike.. It shouldn’t therefore, come to surprise that we spend a significant chunk of our precisious time to discuss about war with Kagame. We always wish someone could provoke us to fight. Sadly Kagame is only going half way towards our trap. We love to fight where there is reason for that. The presence of our soldiers in different parts of the world is point in case.

KWANINI SI MUUMINI WA SERIKALI TATU: MWANAKIJIJI

MWANAKIJIJI

Aprili 30, 1992 aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais John Samwel Malecela alitoa hotuba ndefu Bungeni ambapo alipinga hoja ya serikali tatu. Kwanza alipinga kwa sababu tume ya Nyalali ilipata asilimia 49 tu ya watu 36299 waliotoa maoni walitaka serikali tatu. Kwamba watu karibu 17,000 ndio walitaka serikali tatu na kwa hilo tu tume ikapendekeza serikali tatu. Hata sasa suala la serikali tatu hatujaambiwa ni watu wangapi wanataka hilo kwenye tume ya Warioba hadi Tume iliingize kwenye rasimu ya Katiba. Na idadi hiyo inaendana vipi na wale wengine waliotaka mifumo mingine ya serikali.

Malecela alisema kwa uthabiti hivi:

Sisi hatuoni kuwa kuna hoja ya kisheria na ya kisiasa ya kubadili mfumo wa sasa wa Serikali mbili na kuanzisha mfumo wa Serikali tatu. Tunaamini kuwa mfumo wa Serikali tatu, utadhoofisha Muungano wetu kisiasa na kiuchumi.
Nyerere akielezea hili kwenye kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (UWHT) anasema hivi:

Waziri Mkuu aliisahau hotuba hii; na wabunge waheshimiwa walisahau shangwe zao na
makofi yao. Wakapitisha Bungeni, “kwa kauli moja”, Azimio la kutaka Serikali ya Tanzania ilete
muswada wa kubadili Katiba ya Nchi yetu ili kuwa na Serikali ya Tanganyika “ndani ya Muungano”,
kwa madai ya kwamba hayo ndiyo ” matakwa ya wananchi wa Tanzania.
Lakini ukweli wa suala hili unabaki pale pale: Wananchi wa Tanzania hawadai Serikali ya Tanganyika;
na mimi nasema, ukifufua Tanganyika, utaua Tanzania. Fahari wawili hawakai zizi moja: “Yeltsin”
wa Tanganyika’ ataua Muungano. Lakini pia sababu zile zile za ukabiIa na udini na tamaa za
uongozi zitakazoua Tanzania hatimaye zitaiua Tanganyika nayo.

Nyerere aliona – na mimi nakubaliana naye – suala la kudai Tanganyika wakati ule kama ilivyo leo ni suala la tamaa ya uongozi na matokeo yatakuwa ni yale yale.

Nyerere aliona kuwa watu wa Tanzania wanachotaka ni kuwadhibiti viongozi wao. Yeye aliona kwa usahihi kabisa kuwa kuleta Tanganyika haitatatua tatizo la viongozi wahalifu kwani sasa utakuwa na viongozi wabovu kwenye Muungano na wengine kwenye Tanganyika na Zanzibar. Alisema suala basi ni kuweka utaratibu wa kuwawajibisha viongozi sawasawa.

Nyerere akaelezea vizuri kwanini wakati wa Muungano hatukwenda kwenye serikali moja au kwenda serikali tatu. Alisema hivi:

Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa
mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya udogo wa Zanzibar na
ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi
na mbili (12,000,000). Muungano wa Serikali Moja ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza
Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tutuhumiwe hata kwa makosa,
kwamba tunaanzisha ubeberu mpya!

Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama
kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha
Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa
Tanganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali
yake ya watu 12, 000, 000 na pia ndiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la
watu 12,300,000.

Ni Watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo
ingekuwa ndogo. Gharama ya Serikali ya Tanganyika isingekuwa ndogo, (waulizeni Wazanzibari), na
wala ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo. Hata bila ya gharama za mambo yasiyo ya
Shirikisho. Na gharama zote hizo kwa kweli zingebebwa na Tanganyika.

Ni vizuri kuangalia hizo namba leo hii; Zanzibar ina watu kama milioni 1.3 na Bara kuna zaidi ya watu milioni 45. Hivyo serikali tatu kwa mantiki ya Nyerere bado Tanganyika itabeba mzigo mkubwa zaidi – kuwa na serikail ya kuhudumia watu milioni 45 na pia kuchangia mchango mkubwa kwa serikali ya watu milioni 46.3.

Nyerere alikutana na viongozi wa chama na wabunge wa CCM na kuwashawishi kuipinga hoja ya serikali tatu na serikali nayo. Lakini alipoondoka kwenye Asia akiwa kwenye ziara ya Nchi za Kusini (alikuwa Mwenyekiti) huku nyuma serikali na viongozi wakashindwa kupinga kwa hoja maridhawa kabisa serikali tatu (kama tunavyoona sasa). Nyerere aliandika kwa ukali na uwazi hili tena kwa mshangao. Alisema:

Nilipouliza kwa nini hawakupinga hoja ya Serikali tatu kama tulivyokuwa tumekubaliana majibu ya viongozi wetu wakuu yalikuwa ni ya ajabu kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa wakali kama mbogo! Tena walikuwa wakiwatukana wenzao (yaani wabunge wa Zanzibar) kwa kuwataja majina.

Hizi ni sababu za ajabu sana za kuwafanya viongozi watu wazima watelekeze msimamo mzima wa Chama chao na makubaliano ya watu makini kuutetea msimamo huo na waamue kuikumbatia hoja ya mbogo wakali! Huu ni uongozi wa ajabu kabisa!

Nyerere alifikia hitimisho ambalo hata leo tunaliona. Watu wanataka serikali ya Tanganyika kwa sababu wamechoka na Wazanzibari. Nyerere anasema hivi:

Ndivyo viongozi wetu waheshimiwa wanavyojaribu kufanya hata katika suala hili la Muungano.
Wanataka kuvunja Tanzania maana “wamechoka na Wazanzibari”; lakini hawataki kusema hivyo wazi wazi. Wanachosema ni kwamba wanataka Serikali ya Tanganyika “ndani ya Muungano”, ingawa wanafahamu, maana si watu wapumbavu, kwamba ukifufua Tanganyika utaua Tanzania.

Muundo wa Muungano unabadilika na si lazima uwe serikali tatu
Mimi siamini katika serikali tatu kwa kiasi kikubwa kwa sababu zile zile za Nyerere. Lakini pia ninaamini kuwa wananchi ndio wana haki ya kuamua mfumo wa Muungano na hata uwepo wa Muungano wenyewe. Sasa hivi watu wanajadili serikali tatu kwa sababu wamekatazwa kujadili kuuvunja Muungano! Watu wamekubali kuwa ni lazima tuungane hivyo tutafute namna ya MUungano. Mimi naamini wananchi ndio wanapaswa kuamua kwanza kama Muungano uwepo na wakishaamua hivyo uwe wa namna gani.

Nyerere anasema hivi:

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala
la sera, si amri ya Mungu. Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalinbali kuhusu
muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio
utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. Muundo wa Serikali mbili unakubaliwa na wananchi,
lakini unatokana na sera ya TANU na ASP, na kwa sasa CCM. Chama Cha Mapinduzi kikipenda
kinaweza kubadili sera hiyo ya muundo wa Serikali mbili bila kuuliza wananchi kwanza. Kinaweza
kufunya hivyo kwa kuhisi kuwa hivyo ndivyo wananchi wengi watakavyo; lakini pia kinaweza kufanya
hivyo kwa sababu kinaamini kuwa inafaa kufanya hivyo, hata kama wananchi wengi hawakudai au
hawapendi mabadiliko.

Na Hapa chini ndio msimamo wangu vile vile: Kwanini tunalazimishwa kujadili serikali tatu. Kwanini tumesalimu amri na kufikiria serikali tatu? Kwanini CCM wameamua tujadili serikali tatu na sisi tunajadili serikali tatu. Hivi kweli watu wanafikiria hili wazo la serikali tatu limetokana na wananchi kwenye maoni ya tume ya Warioba au ni carryover ya mjadala wa 1992?

Nyerere anasema:

Nasema, niliamini kuwa ni kosa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kukubali chama kiulize wananchi
kama inafaa tuwe na Serikali Tatu. Kwanza, kwa sababu hiyo niliyoeleza; na pili, hata kama CCM
ingependa kubadili sera yake, kwa nini turukie Serikali Tatu? Kwa nini tusitake maoni ya wananchi
kuhusu Serikali Moja! Au hata kuhusu SerikaIi za Majimbo? Tumejadili katika vikao gani
tukakubaliana kuwa miundo mingine yote haifai ila muundo unaofaa ni ule wa Serikali Tatu? Au hata
Bunge lenyewe, limejadili miundo mbali mbali ya Muungano katika kikao gani hata wabunge
waheshimiwa pamoja na waheshimiwa mawaziri wetu wakafikia uamuzi baada ya mjadala kwamba
muundo peke yake unaofaa ni huu wanaopendekeza, wa kuwa na Serikali Tatu?

Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!

Hizi zote ni mbinu za viongozi wetu waheshimiwa kutaka kukiingiza Chama katika njia moja tu
nyembamba, na kutuburura kama vipofu tuitumbukize nchi yetu shimoni. Ni jitihada za kukifanya
chama na sisi wengine wote tukubali msimamo wao wa kutaka kuigawa nchi yetu.

Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu. Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu – hili ni jambo dogo zaidi lakini tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!

Mimi napinga serikali tatu – naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.

mwanakijiji@jamiiforums.com
The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging – http://www.mwanakijiji.com

SOUTH AFRICA IS NOW PLANNING TO SCRAP FIRST-COME, FIRST SERVED PRINCIPLE IN MINING, OIL & GAS SECTOR

The new draft law before South Africa Parliament appears to scrap the first-come, first-served mineral right award principle and replace it with a public auctioning process.

Moreover, the mineral beneficiation provisions of the 2013 Minerals and Petroleum Resources Development Act (MPRDA) Amendment Bill are wide-ranging, Fasken Martineau mining law partner Matthew van der Want said on Friday.

Van der Want and Fasken Martineau environmental law specialist Matthew Burnell were speaking at a mining seminar on the most important of the many changes to South Africa’s mining and environmental legislation.

“Many of the amendments the Bill proposes are fairly complex and far-reaching,” Van der Want told Mining Weekly Online in a video interview (see attached).

The complexities arise not only from the introduction of the 2013 Act but as a result of amending legislation coming into force and then being partly withdrawn at the eleventh hour, Fasken Martineau Africa mining head Andrew Mitchell explained.

Burnell drew attention to a section of environmental legislation being inadvertently repealed and the potential confusion arising from two different amendment Acts for mining-related activities failing to dovetail.

“Certain provisions of the MPRDA have been deleted, which leaves portions of the environmental legislation unregulated for the next 18 months,” Burnell told Mining Weekly Online.

Meanwhile, the 2013 Bill is providing insight into the new direction in which the Department of Mineral Resources (DMR) intends taking the transferring of rights, beneficiation and mine-dump processing rights.

“One of the most important changes by far is the scrapping of Section 9 and the ordering of applications and to replace it with a kind of public auction idea, it seems to me.

“Essentially, what’s happening is they’re planning on scrapping the first-come, first-served principle, which has always applied,” Van der Walt said.

Currently, the first mineral right application submitted is the first to be considered and if two applicants put their applications in on the same day, there is a match off of the black economic-empowerment (BEE) credentials and the applicant with the better BEE credentials is awarded the right.

The 2013 Bill proposes that the first-come, first-served procedure be scrapped entirely and replaced with what appears to be a public auction of available or lapsed rights.

It is proposed that the Mineral Resources Minister can invite applications for rights in any area, prescribe when the applications may be lodged and lay down the terms and conditions on which rights will be granted.

The new proposal is also that no awards can be made in areas where rights have been relinquished, abandoned or have lapsed until the Minister gives the go-ahead.

“It’s not entirely clear how this will work,” Van der Want added.

MINERAL BENEFICIATION

Under the 2013 Bill, the Minister must promote beneficiation and is entitled lay down the percentage of a mineral output that must be reserved for local value addition.

Also determined is the developmental price at which the designated output must be sold to facilitate local beneficiation.

Should shale gas be exploited, producers will be obliged to offer a percentage of the raw gas for local processing at a prescribed price.

The Minister can thus decide the percentage of production that must be processed locally and the price at which it may be sold after processing.

“It’s going to have some pretty severe implications,” Van der Want commented.

The export of designated minerals is also subject to Ministerial consent.

“These provisions are going to be a major sticking point in the Parliamentary consultation process,” Van der Want predicted.

MINE DUMPS

Mine dumps have been the subject of several court cases and there has for long been a degree of uncertainty around so-called historic mine dumps.

Lawyers contend that prospecting and mining rights are not required to process dump material that pre-dates the 2004 MPRDA.

However, from June 7 the 2008 Amendment Act extends the definition of dumps to include dumps under old-order rights, which places the MPRDA mantle over dumps created before 2004.

The terms that the MPRDA applies to dumps are residue stockpiles, which are dumps or tailings placed by a holder of a new-order right, and residue deposits, which are the deposits still remaining after the right to them has expired.

The DMR has attempted to assert jurisdiction over dumps, which has led to contestation.

Now the proposed changes give the DMR the power to take control of dump processing.

PROCLAIMED THEN UNPROCLAIMED

The 2010 changes to the 2008 MPRDA Amendment Act, which many assumed had been erased, were proclaimed “out of the blue” three years after the 2008 Amendment Act had been signed into law by President Jacob Zuma – only for parts of it to be unproclaimed six days later.

“The legal concept is new to me. I did not know you could proclaim an Act and then unproclaim parts of it, but there you go. So developments have been pretty confusing,” Van der Want commented.

Most of the amendments effected by the 2008 Amendment Act have been in force from June 7, except for certain environmental provisions.

ENVIRONMENTAL LIMBO

Burnell told Mining Weekly Online that confusion had been created as a result of the deletion of certain MPRDA provisions, which left portions of the environmental regulation unregulated for the next 18 months.

Despite the deletions, the provisions would continue as in the past.

“Everyone’s just going to turn a blind eye,” Burnell said.

But if a dispute arose relating to the deleted sections, problems could well arise.

New provisions were laying down indefinite periods of environmental liability.

If the provision in the 2013 Bill went ahead, the liability would enter the realm of the perpetual and place question marks over effective enforcement.

Once the Department of Environmental Affairs became the authority, Burnell believed confusion would abate.

SOURCE:- miningweekly.com

MUGABE TEAM CLAIM TO WIN ZIMBABWE ELECTION

Robert Mugabe team claims to win Zimbabwe election: Source at ruling party
A senior source in the ruling party of Zimbabwe, ZANU-PF, says President Robert Mugabe has defeated Prime Minster Morgan Tsvangirai in the presidential election. Claim
“We’ve taken this election. We’ve buried the Movement for Democratic Change (MDC). We never had any doubt that we were going to win,” said the source, who spoke on condition of anonymity, on Thursday.
In response to the claim, a high-ranking source in Tsvangirai’s MDC party issued a statement saying that “Zimbabweans have been taken for a ride by ZANU-PF and Mugabe, we do not accept it.”
On the same day, police said that “people who announce results of elections before the Zimbabwe Electoral Commission” would be arrested.
Vote counting began immediately after the presidential and parliamentary elections ended on Wednesday night.

Some 6.4 million people, or half of the Zimbabwean population, were eligible to cast their ballots at 9,670 polling stations across the country.

Five presidential candidates are competing in the race, including Mugabe and Tsvangirai.

The two rivals have been sharing power since 2009, following a deal brokered by a regional bloc to end the unrest that had sparked after the 2008 election.

In that election, violence broke out, forcing Tsvangirai out of the race despite a first round win after 200 of his supporters were killed in the turmoil.

Press Tv

PINDA KAWA WAZIRI MKUU WA KWANZA WA TANZANIA KUBURUZWA MAHAKAMANI.

PINDA

Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda

Kituo cha sheria na haki za binadam LHRC kimemfungulia mashitaka waziri mkuu Mizengo Peter Pinda kuhusiana na kauli yake aliyoisema bungeni kwamba wananchi watakaoshindwa kutii sheria wapigwe tu.Akizungumza na waandishi wa habari mahakama kuu mkurugenzi wa kituo hicho Hellen Kijo Bisimba alisema watashirikiana na chama cha mawakili wa Tanganyika ili kuhakikisha waziri mkuu anafuta kauli hiyo.

Eatv breaking news.

VIDEO:- HATUTAPIGWA, HATUTALIA WALA KULALAMIKA TENA; CHADEMA

 • Wasema Watashinda Kwa Kishindo na kutaja asilimia.

 • Wamshanga Mwigulu Nchemba kwa siasa ambazo zinamuhusisha Mwenyekiti wa chama chake.

 • Wataja vikosi vyao vya kujilinda na kusema ndiyo mwisho wa kuonewa.

JESHI LA POLISI NA SERIKALI WAJIULIZE WAMETUFIKISHA VIPI HAPA?
Badala ya kuipiga mikwara CHADEMA na kuwatishia viongozi wake uongozi wa jeshi la polisi na Ikulu inapaswa wawe na ujasiri wa kusimama mbele ya vioo na kujiuliza maswali ambayo majibu yake yagonge visogo vyao. Maswali hayo baadhi yake ni haya:

 1. Kwanini CHADEMA imefikia mahali pa kutaka kujilinda?

 2. Vyombo vya usalama vimepungukiwa nini kiasi kwamba chama kikuu cha upinzani nchini haiviamini?

 3. Je, uongozi wa vyombo vya usalama una mahusiano gani ya kikazi na viongozi wa CHADEMA?

 4. Je, ni kwanini matukio yaliyotokea na kugusa CHADEMA hayachunguzwi kwa kasi ile ile kama matukio mengine – mfano mauaji ya Padre Mushi kule Zanzibar yamepewa uzito wa uchunguzi (Hadi Rais kaingilia kati) kuliko mauaji ya wanawake na mtoto mdogo Arusha?

 5. Je vyombo vya usalama vinaweza kuchukua hatua gani kurudisha imani ya CHADEMA na wanachama wake kuwa vinafanya kazi kwa weledi na siyo kama sasa ambavyo vimebatizwa majina ya CCM kama PoliCCM (badala ya Polisi), na TICCM (Badala ya TISS) n.k?

 6. Rais Kikwete ajiulize kwanini wale aliowakabidhi dhamana ya kusimamia usalama nchini wameifikisha nchi hapa – kuwalaumu CHADEMA kwa kujilinda ni kukosa umakini na kuwa na usahaulifu unaobagua (selective amnesia).

BY:- Mwanakijiji….

Haki ya kujilinda ni miongoni mwa haki za msingi kabisa za binadamu ambazo zinatokana na mtu kuwa binadamu na haziwezi kuondolewa au kufutwa na chombo chochote. Ni haki ambayo mwanadamu anayo kwa kuzaliwa kwake. Haki hii kwa kadiri tunavyokua tunaiacha kwenye vyombo mbalimbali lakini mwisho wa siku bado ni haki yetu ya msingi kama binadamu. Mwanadamu anaposhambuliwa ana haki ya kujikinga kukinga maisha yake na mali yake; na kama ni familia yake inashambuliwa ana haki ya kulinda familia yake. Huwezi kumwambia mtu kuwa akipigwa ainame na kukubali kipigo bila kujilinda.

Haki hii ni tofauti na haki ya kujitetea au kulipiza kisasi – japo ni haki zinazoendana pamoja katika ile haki ya msingi ya kutokudhulumiwa. Haki ya kujilinda ni haki ambayo mtu si lazima alipe kisasi lakini ni haki ya kuzuia kutendewa vibaya. Hii ndiyo sababu watu wamejenga kuta kwenye nyumba zao, wameweka vyombo vya ulinzi na kuajiri walinzi. Wote hawa wanatumia haki yao ya kujilinda bila kulazimika kulipa kisasi. CHADEMA kama chama cha siasa ambacho tayari kimeshadhurika mara kadhaa sasa na kwa niaba ya wanachama wake kimeamua kutoa mafunzo ya ukakamavu na kujilinda; wanatumia haki hii ya msingi.

Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama na wale wote wanaobeza wanahitaji kutafakari upya kama wao wangekuwa upande wa pili kama wasingetafuta mbinu ya kujilinda. Kama wale watu waliowekwa kutoa ulinzi ndio hao hao wanaoharibu ulinzi utakuwa ni ujinga wa hali ya juu kuwategemea. Bila mabadiliko ya msingi ya mfumo na utendaji wa jeshi la polisi katika mazingira ya vyama vingi vya siasa ni vigumu kwa chama cha upinzani kama CHADEMA kuweka maisha yake na maisha ya viongozi wake mikononi mwa chombo hicho. Ni wajibu na ni haki kwa wao kufikiri namna ya kujilinda na kulinda maslahi yake. Hili halihitaji baraka kutoka CCM, Ikulu, au Polisi.

KILEWO NA WENZAKE KUSUBIRI MAHAKAMA KUU.

 • WASHITAKIWA WARUDISHWA GEREZANI.

 • WAKINAMAMA WAKIONGOZWA NA JOYCE KIRIA WAANGUA VILIO.

 • UPANDE WA MAWAKILI WA UTETEZI WAWASILISHA HATI YA DHARULA KUOMBA KESI IFUTWE.

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0001

Mawakili wa upande wa utetezi wakiongea na wanahabari jumatatu Julai 8 2013 mkoani Tabora.20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0002

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0003

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0004

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0005

20130708-M2S-CHADEMA MAHAKAMANI TABORA-0000

washitakiwa walipokuwa wanaelekea na kutoka vyumba vya mahakama mkoani Tabora jumatatu Julai 8, 2013. PICHA zote kwa hisani yaTumaini Makene; Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA

Jumatatu july 8, 2013 Ilishuhudia Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Tabora ikitumia dk. 7 tu kutolea maamuzi shauri lililofikishwa mbele yake linalo husiana na mashitaka dhidi ya Katibu wa Chadema Wilaya ya Kinondoni, Henry John Kilewo na wenzake wanne, kwa madai ya Ugaidi.

HAkitolea maamuzi Hakimu Mkuu Mkazi ilinukuliwa akisema kuwa hoja za upande wa utetezi na kesi yenyewe mahakama yake haina uwezo wa kuzisikiliza, na kudai kuwa ni Mahakamu Kuu Pekee ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza kesi za Ugaidi.

Maamuzi hayo yalipelekea washitakiwa hao kurejeshwa rumande katika gereza la Uyuwi, hatuo hiyo ilipelekea sintofahamu baina ya ndugu na wafuasi wengi wa CHADEMA walio kuwa wamejitokeza kwa wingi kusikiliza shauri hilo.

Huku hayo yakitokea zilisikika sauti za kina mama ambao waliongozwa na Mke wa Kilewo {Joyce Kiria} wakiangua kilio huku wakilaani watu wanaotumia sheria vibaya kwa lengo la kuwatesa na kuwanyanyasa wapinzani wao kisiasa.

Baadae Taarifa ilitolewa kupitia Jopo la Mawakili Nguli wa Chadema kuwa wamewasilisha maombi Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora kuiomba mahakama hiyo kupitia upya uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na Ikiwezekana kuifutilia mbali kesi hii.

Ombi hilo limewasilishwa kwa Hati ya Dharura na Wakili Peter Kibatala ambaye aliwasilisha ombi hilo kwa niaba ya Jopo hilo la mawakili Nguli.