NAMNA NYANI WALIVYOWAOKOA SAMAKI.

monkeyandfish

Msimu wa masika mwaka ule ulikuwa wa mvua nyingi kupita kiasi, mito karibu yote ilifurika huku ikiacha kingo zake zikivunjika. Hali hii ilisababisha mafuriko yasiyotarajiwa na kuwalazimu wanyama wote wakimbilie vilimani ili kunusuru maisha yao.

Hali hii iliwakumba wanyama wengi, waliyokuwa na bahati waliweza kuyanusuru maisha yao ila wengi wao waliangamia.

kwa upande wao Nyani wenyewe walitumia uhodari wao wa kuparamia miti hili kujinusuru, hali ilikuwa tofauti sana kwa samaki ambao muda wote walionekana (kuchupa nje ya maji) kwa kuruka ruka kwa furaha wakifurahia hali hii.

Nyani mmoja aliwaona wale samaki akapaza sauti na kumwambia mwenzake, “Loo! Angalia chini, rafiki yangu! Waone viumbe maskini wale. Huenda watazama. Unawaona jinsi wanavyohangaika majini?”

“Ndiyo,” baada ya kuangalia kwa muda nyuni mwingine alijibu, na kuongeza kwa sauti ilioonyesha huruma na upendo mkubwa. “Nawahurumia sana! Labda walichelewa kukimbia vilimani kwa sababu hawana miguu. Tunawezaje kuwaokoa?”

Baada ya mabishano ya muda fulani, walikubaliana waende kwenye ukingo wa mto ambako maji yana kina kifupi ili wawaopoe. Kazi hiyo ilikuwa ngumu ila Nyani hao waliitekeleza kwa umakini na uangalifu mkubwa na kufanikiwa kuwatoa samaki kwenye maji na kuwaweka sehemu kavu.

Haikuchukua muda, kukawa na lundo la samaki nje ya maji waliyo lala kimya bila kutikisika kwenye nyasi.

Kutokana na uchovu Nyani mmoja akasema kwa kunong’ona,  “Unaona? Walikuwa wamechoka, na sasa wanalala na kupumzika. Kama tusingewasaidia,  viumbe hawa wasio na miguu wangezama na kuangamia.”

Nyani mwingine ambaye alionekana kama kiongozi wao baada ya kuwaangalia wale samaki walivyolala kwenye nyasi kavu akasema, “Walikuwa wanajaribu kutukwepa kwa sababu hawakuweza kuelewa nia yetu njema. Lakini watakapoamka watatushukuru sana kwani tumewaokoa.”

yajiongeza  kwa kupanua wigo, safari hii waja na mradi mpya wa mafunzo kwa wanahabari tanzania

Ngano ya tanzania iliyosimuliwa na Padri Laurenti Magesa katika kitabu cha “towards African Narrative Theology” Paulines Publications Africa, 1996. Uk 136-137

  Source www.community.co.tz

Advertisements