UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NI KWELI CCM IMEONGOZA LAKINI IMEPOTEZA SANA

baadhi ya wananchi walio wakishiriki  kwenye uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa mwaka 2014

baadhi ya wananchi walio wakishiriki kwenye uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa mwaka 2014

Mwanamichezo Lance Armstrong anayeshikilia rekodi ya kushinda mara nyingi katika mchezo wa baiskeli aliwahi kunukuliwa akisema “Kama uko tayari kuchunguza kushindwa kwako, kwa kuangalia sababu za kushindwa za ndani na nje ikiwemo utendaji wako, basi kushindwa kunaweza kuwa na thamani zaidi ya kujitangazia ushindi”.

Wengi wanaweza kuhoji kwa nini nimemkumbuka Bw. Amstrong leo, ila sababu za msingi ni chaguzi za nafasi za wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na nafasi za wajumbe wa serikali za vijiji na kamati za mitaa ambao umemalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika chaguzi hizo matokeo ya awali ya jumla yanaonyesha CCM kushinda kwa ushindi mnono, lakini kimantiki chama hicho kinazidi kupoteza udhibiti wake katika siasa za Tanzania  karibia sehemu zote, vilevile ikumbukwe katika mapambano unapopima mafanikio huwa tunaangalia ulichopoteza sio ulichonacho, ni kweli CCM imeongoza lakini imepoteza sana.

Swali kwa wana CCM, imesikia sauti za wananchi kupitia sanduku la kura ambao wamepiga kura kwa pande zote? mwananchi anayepiga kura ya hapana anakuwa na maana nyingi katika kura yake, je tumejipa muda wa kufikiri na kunyambua mantiki ya maana ya kura za hapana kwa faida ya chama na taifa kwa ujumla badala ya kutuchagiza kuingia mitaani kucheza mdundiko kwa sababu  ya kutuaminisha tumeshinda?

Lazima nikiri wazi kuwa kinasaba, kijana mpambanaji Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye hunivutia sana kama alivyokuwa Muhammad Saeed al-sahhaf, waziri wa habari wa Iraq wakati wa vita na marekani chini ya Sadamu Husein. hususan pale anapojitokeza kujenga hoja juu ya anguko la chama chake.

hatahivyo, Kwa ufahamu wangu kitengo cha uenezi na itikadi siyo kitengo kidogo, na tunakishushia hadhi hasa pale tunapo jipambanua kwa hoja nyepesi nyepesi tena zisizo na uchunguzi. Kitengo hiki ndiyo roho ya chama, kama akieleweki basi bila ya shaka chama kitaenda mrama.

utafiti niliofanya unaonyesha wana CCM wengi hawana haja ya kujuwa wameshinda kwa asilimia ngapi? Hila wangependa kujuwa wamepotezaje nafasi zaidi ya  2,636 za uenyeviti wa vijiji na mitaa ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2009 ilipopata jumla ya viti 12,042.

Wana CCM wengi wanaona hakukuwa na haja ya tamko hilo la Nape kwa sasa, la kujinasibu kupata ushindi mkubwa kwa sababu alikuonyesha kwa kina tatizo la CCM ni nini.

Wengi wa wanachama wa chama hicho kikongwe wangependa ufanyike uchunguzi na tathmini ya kina ili kubaini kama sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow nalo ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kupoteza baadhi ya mitaa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Jumanne, Desemba 16 2014, katibu wa NEC mwenye dhamana ya Itikadi na Uenezi alisema kuwa chama chake kimefanya kazi kubwa tena katika sehemu ngumu akitolea mfano jimbo la Arusha mjini.

Kila mtu anajua kuwa kabla ya uchaguzi huu jimbo la Arusha mjini, Maskani ya Mbunge wa chadema Godbless Lema lilikuwa na wenyeviti 6 tu. Na baada ya uchaguzi wa mwaka huu wamepata wenyeviti 75, je huu bado ni ushindi wa  kishindo kwa Nape?

Ikumbukwe kuwa jimbo la Arusha mjini lilikuwa na jumla ya mitaa 154, ukitoa nafasi ya wenyeviti ambayo CCM imepata viti 78 mbele ya 75  vya Chadema, hali ni mbaya sana kwa matokeo ya jumla kwenye nafasi za wajumbe wa serikali za vijiji na kamati za mitaa ambapo chadema wanaongoza mitaa 104 kati ya 154.

Inapofikia hapo, ni vyema kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi kuamka kutoka ulevini, kusikia sauti za wapiga kura na kutuambia ukweli wapenzi na wadau wa chama cha mapinduzi cha CCM nini cha kufanya turudishe heshima ya chama chetu, baadhi ya watu wameanza kuoji Je kwa matokeo hayo ni kweli Nape ana uchungu na chama cha CCM? wengine wamekwenda mbali na kujiuliza kama kijana huyo mpambanaji anafahamu kuwa amepoteza viti zaidi ya 2,636.

Aliyekuwa Rais wa Marekani, John Fitzergerald Kennedy aliwahi kunukuliwa enzi za uhai wake kwa kusema, “Kwa kuungwa na umma kwa dhati, naweza kufanya jambo lolote salama; lakini kwa kuungwa mkono na wenye dhamira isiyoshabihiana na matakwa ya umma, lazima nitaona giza mbele”. 

Tafakuli hii ndiyo nawachia wapenzi wa chama hiki kikongwe kuliko vyama vyote nchini Tanzania, Je? Chama chetu kwa sasa kinaungwa mkono na watu wa namna gani?

kwa mazingira yetu leo, kijana wetu mpambanaji Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye haoni dalili ya giza mbele. 

Source :- TAZAMA

Advertisements

ARUSHA; CCM YAONGOZA MITAA 78 KATI YA HIYO 6 KWA PINGAMIZI HUKU UKAWA WAKIPATA MITAA 75, MTAA MMOJA KURUDIWA .

Baadhi ya wapiga kura wakipiga kura kwenye mojawapo ya kituo jijini Arusha.

baadhi ya wanachi wa mkoa wa Arusha wakisubili kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya jumapili.

Chama cha mapinduzi (CCM) kimeendelea kuongoza katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwabwaga mahasimu wao wakubwa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa ushindi kiduchu, ambapo imefanikiwa kunyakua mitaa 78 na chadema kuambulia 75 katika matokeo ya awali.

Pamoja na dosari za hapa na pale katika uchaguzi huo uliyopelekea kuailishwa kwa kituo kimoja nafasi ya mwenyekiti na vingine viwili nafasi za wajumbe hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi Juma.

Katika uchaguzi wa mwaka huu jumla ya wananchi  1,139,090 walijiandikisha kupiga kura huku vyama sita vikisimamisha wagombea ambavyo ni pamoja na ACT, CCM, NCCR, CUF pamoja na TLP.

Bw. Juma akitaja matokeo ya uwenyekiti wa mitaa alisema kuwa CCM inaongoza kwa kupata mitaa 78 ambapo kati ya kura hizo kura sita ni za kupita bila kupigwa, ikifuatiwa na CHADEMA mitaa 75.

Aidha alibainisha kuwa kulikuwa na jumla ya vituo 154 vya kupigia kura “mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umemalizika ila tumelazimika kurudia uchaguzi katika vituo vitatu,  ambapo kituo kimoja ambacho ni cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa kwa nafasi zote huku katika kituo cha AICC -Sekei uchaguzi utarudiwa kwa wajumbe watatu wa viti maalumu ambapo hii inatokana na kura za kufungana kwani wote walipata 31 kwa 31  na katika kituo cha Oldpolisi line napo wajumbe wawili walifungana kwa kura 64 kwa 64.

WARIOBA ATILIA SHAKA MAAMUZI YA BUNGE JUU YA ESCROW

Makamu wa kwanza wa rais na waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.
Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.
“Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015.”
Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.
“Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu,” alisema.
Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.
“Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?”
Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo… “Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?”

Waliopata mgawo

Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.

“Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata ukichukua fedha katika gunia lazima benki itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua. Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni dalili za kulindana.

Msingi wa uamuzi

“Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo walisema fedha za escrow ni za umma na wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma. Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda haki,” alisema.
Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo utakapomalizika… “IPTL imeendelea kutoa huduma na umma umepata umeme kutoka katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo. Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote katika kipindi kile ambacho walikuwa hawajakubaliana.
“Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.
“Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani.”
Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni kodi ambayo haikuwekwa wazi.“Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji. Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara wanayoisema na haihusiani na escrow kwa sababu hata kama escrow isingekuwa na matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu wa kawaida,” alisema.

Source:- Gazeti la Mwananchi

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA.

Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana.

LOWASSA, SITTA NA WASSIRA HAWANA SIFA ZA KUWANIA URAIS; WARIOBA

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” Jaji Joseph Warioba

  • Asema anatakiwa awe kijana mwenye maadili, mwajibikaji

  • Asema hatagombea urais, aachwe alee wajukuu

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ametoa dira ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kutaja sifa za rais anayefaa kuiongoza Tanzania.

Warioba alisema kwamba taifa la Tanzania linastahili kuongozwa na vijana wenye nguvu ya mwili na akili. “Mimi nafikiri tuangalie kati ya vijana tulionao, nani anatufaa kuiongoza nchi, tusirudi kuangalia wazee,” alisema Jaji Warioba.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Uchaguzi huo mkuu ambao ni wa tano wa vyama vingi nchini, unatarajiwa kulipatia taifa rais mpya, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake wa utawala wa awamu ya nne.

“Uongozi mzuri unatengenezwa na haiba, wajihi, dhamira, uwezo, maadili, uhodari, hekima na maarifa. Sifa hizi hazipatikani kutokana na uzoefu wa miaka mingi kwenye siasa hata baadhi ya vijana wanazo,” alisema Makamba.

Alitolea mifano mingi duniani ambapo vijana ambao hawakuwa na uzoefu kabisa katika nafasi za siasa wameshinda na kubadilisha nchi kama Tony Blair wakati anakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza aliongoza nchi hiyo kubwa wakati alikuwa hajawahi kuwa hata Naibu Waziri.

“Barack Obama (Rais wa Marekani) alikuwa Seneta miaka mitatu tu, Julius Nyerere alikuwa Mwalimu akaingia siasa akaja kupewa uongozi wa nchi akiwa na miaka 39 tu.”

Katika maelezo yake Jaji Warioba alisema kwamba tangu uhuru, walioshika madaraka ya kuliongoza taifa walikuwa ni vijana.

Wazee kugombea urais

Akijibu swali kama atakuwa tayari wananchi wakimtaka kuwania urais baada ya kazi kubwa ya kukamilisha Rasimu ya Katiba nchini, Jaji Warioba alisema:

“Hili nilikwishalijibu, tusahau mawazo kwamba sisi (wazee) tutarudi madarakani. Nadhani mara ya mwisho tulipozungumza niliwaambia inafika wakati kiongozi unang’atuka. Unawaachia vijana ambao wana nguvu ya kimwili na akili ndiyo watumikie taifa hili, waongoze nchi.

“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” alihoji Jaji Warioba.

Alisema kuwa tangu uhuru hadi sasa Tanzania imetayarisha vijana wengi wanaofaa kuliongoza taifa na kuongeza:

“Hatuna ombwe la uongozi, tunao vijana wengi sana, tena kwa bahati nzuri nchi kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikiongozwa na vijana.”

Huku akitaja mifano ya viongozi hao vijana walioongoza taifa, Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema:

Makundi ya urais

Warioba pia aliulizwa iwapo makundi yanayotajwa kusaka urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuwa huenda yanahusika na kusuasua kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Alisema kwamba, yeye na wenzake waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kutafakari mchakato huo unavyokwenda ukihusisha maeneo na makundi mbalimbali.

“Tulikwenda kutafakari, hatutaki kwenda kwenye matukio, wala kuzungumzia makundi, nasema wote wakae pamoja waone masilahi ya taifa, kwa sababu wasipokaa pamoja kuna hatari ya mchakato huu wa Katiba Mpya kukwama. Na kukwama siyo kwa masilahi ya taifa,”alisema.

Ikiwa Rasimu ya Katiba Mpya itapitishwa na mapendekezo yake ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, kutalazimika kuwapo kwa Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo nguvu na mfumo wa kisiasa kubadilika.

SOURCE: MWANANCHI

NINA WASIWASI KAMA MWAFAKA AU MARIDHIANO YATAPATIKANA AGOSTI WAKATI BUNGE MAALUMU LITAKAPOKUTANA; BOMANI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga

Dar es Salaam. Jaji mstaafu Mark Bomani amelishauri Bunge Maalumu la Katiba kuweka kando suala la muundo wa serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha mgawanyiko mkubwa baina ya wajumbe.

Pia amewashauri wajumbe wa Bunge hilo wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni ili mchakato huo uweze kuendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema suala la muundo wa Serikali licha ya kusababisha mgawanyiko limesababisha hoja nyingine muhimu kusahaulika. 

“Kwa bahati mbaya sana kwa maoni yangu, mjadala wa mapendekezo hayo umezua malumbano na ubishi mkali, kiasi cha kufanya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kujitoa,” alisema Jaji Bomani. 

Alisema amewahi kutoa maoni kwamba suala lote la muungano na idadi ya Serikali linatakiwa lijadiliwe kwanza ama na Serikali mbili zilizopo, yaani Zanzibar na ya Muungano au Wazanzibari waulizwe iwapo wanautaka muungano. 

“Hata hivyo nina wasiwasi kama mwafaka au maridhiano yatapatikana mwezi Agosti Bunge Maalumu litakapokutana, kwa kuwa zimejitokeza tofauti kubwa za kimtazamo au kiitikadi bila kusahau masilahi binafsi,” alisema Jaji Bomani. 

Alisema kwa uzoefu wake katiba nzuri kwa nchi yoyote ni ile ambayo imepatikana kwa wananchi wengi kuikubali na siyo vinginevyo.

“Katiba nzuri ni ya maridhiano. Katiba nzuri haiwezi kupatikana kwa wingi wa kura au hoja ya nguvu tu bali inatakiwa iwe inakubalika na walio wengi (consensus),” alisema.

Aliyataja mambo mengine muhimu ambayo yanapaswa kujadiliwa na wajumbe kuafikiana ni pamoja na suala la uwakilishi sawa wa jinsia yaani asilimia 50 kwa 50, kwenye ubunge na halmashauri za wilaya.

“Suala la mawaziri kutokuwa wabunge nalo pia nafikiri linaweza kujadiliwa na mwafaka ukapatikana, muundo wa tume huru ya uchaguzi na suala la mgombea binafsi nalo naamini linajadilika wanaoliogopa hawana msingi wa kufanya hivyo,” alisisitiza Jaji Bomani.

SOURCE:- Mwananchi

CHADEMA SASA WALIA NA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA

  • Mnyika asema Katiba ya Chadema ya 2006 haikurekebishwa, bali iliundwa upya.

  • Jaji Mutungi asema ofisi yake inafanya kazi kitaaluma na haiingizi siasa

Tunachomtaka Mutungi ni kuheshimu katiba ya chama na kuwaheshimu wanachama wa Chadema na ayapuuze madai ya wasaliti wachache. Asubiri uamuzi wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ubainishe kama katiba ilivunjwa Mnyika.

“Tunachomtaka Mutungi ni kuheshimu katiba ya chama na kuwaheshimu wanachama wa Chadema na ayapuuze madai ya wasaliti wachache. Asubiri uamuzi wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ubainishe kama katiba ilivunjwa” Mnyika.

 

Dar es Salaam. Mvutano mpya umeibuka baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumvaa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kikidai ofisi yake inatumiwa na wasaliti wa chama hicho.

Pia, chama hicho kimemtaka Jaji Mutungi ajitokeze hadharani kubainisha iwapo yeye ndiye aliyemtuma msaidizi wake, Sistyl Nyahoza kutangaza kuwa mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa ya kugombea uongozi ndani ya chama hicho kutokana na kuzuiwa na katiba ya Chadema.

Jana, Nyahoza alikaririwa na vyombo vya habari akisema Mbowe na Dk Slaa hawana sifa za kugombea uongozi wa chama hicho kutokana na katiba ya chama chao kuwabana.

Alibanisha kuwa kipengele cha ukomo wa mgombea katika katiba yao ya mwaka 2006 kiliondolewa kinyemela bila idhini ya mkutano mkuu.

Nyahoza alisema katiba ya Chadema ya mwaka 2004, ilikuwa na kipengele cha ukomo wa madaraka kuwa kiongozi aliyeongoza vipindi viwili vya miaka mitano mitano, hawezi kuwania tena nafasi hiyo.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema Jaji Mutungi hana mamlaka ya kubaini sifa za viongozi wa chama hicho, bali wenye mamlaka hayo ni wanachama wa chama hicho pekee.

Mnyika alisema mwaka 2006, katiba ya Chadema haikurekebishwa, bali iliundwa upya na kuridhiwa na mkutano mkuu wa chama na kwamba Agosti 13, 2006 ilizinduliwa na nyaraka zote alikabidhiwa Msajili wa Vyama wa wakati huo, John Tendwa.

Katika uzinduzi huo wa katiba pamoja na bendera mpya ya Chadema, Tendwa alikimwagia sifa chama hicho kwa kuonyesha mwelekeo na mwenendo mzuri na kuvishauri vyama vingine viungane nacho kuunda chama cha upinzani chenye nguvu nchini.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Mbowe alikaririwa na gazeti hili Agosti 15, 2013 akisema yalikuwa yanalenga kuimarisha mapambano ya kisiasa ya chama hicho.

Mnyika alisema: “Mkutano mkuu wa chama uliipitisha Katiba hiyo baada ya mchakato mrefu wa kukusanya maoni kutoka kwa mabaraza ya wilaya na majimbo. Hatukurekebisha katiba kama inavyoidaiwa. Ni makubaliano ya wanachama wote ambao waliafikiana na mambo yaliyotakiwa kuwamo.”

Alisema katika mchakato huo kulikuwa na makubaliano na mabishano katika baadhi ya masuala lakini suala la ukomo wa uongozi liliafikiwa na wanachama wote bila tatizo na kupitishwa kuingia katika katiba na Ofisi ya Msajili ilipelekewa fomu ya marekebisho pamoja na katiba mpya kama sheria inavyotaka… “Kama wameipoteza waseme tuwapatie katiba wairejee.”

“Tunachomtaka Mutungi ni kuheshimu katiba ya chama na kuwaheshimu wanachama wa Chadema na ayapuuze madai ya wasaliti wachache. Kama vipi asubiri aone uamuzi wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu ubainishe kama katiba ilivunjwa,” alisema Mnyika.

Mnyika alisema wameshtushwa na kauli ya ofisi hiyo na kuituhumu kwamba imeanza kutumika kisiasa na wasaliti.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo jana, Jaji Mtungi alisema: “Hili suala lisimamiwe na chama husika kwa kuwasiliana na Ofisi ya Msajili… hakuna haja ya kulikuza katika vyombo vya habari. Wanachama wa Chadema watapata taarifa kutoka kwa viongozi wao ni nini kinaendelea.”

Kuhusu madai kwamba ofisi yake inatumika kisiasa alisema:  “Kama nilivyosema, hayo tuyaache hii ofisi yetu ipo more technical (kitaalamu zaidi) hatuingizi siasa. Wao (Chadema) waje kwenye ofisi yetu tuongee kama taasisi, iwapo tunataka kuwasilisha jambo katika vyombo vya habari, basi tutaitisha mkutano na waandishi wa habari,” alisema Mutungi.

Mamlaka ya msajili

Mnyika aligusia pia mamlaka ya msajili huyo akisema… “Hana mamlaka ya kutangaza sifa za mgombea wa Chadema. Sifa na uamuzi vimetajwa katika katiba na kanuni za chama. Kifungu cha 6.3.2 cha katiba ya 2006 kinabainisha wazi kuwa kiongozi aliyemaliza muda wake na mwenye sifa ya kugombea anaruhusiwa kugombea…?” Alisema hata katika uchaguzi wa ndani wa mwaka 2009 viongozi wengi walichaguliwa na wakiwa wameshamaliza ukomo wa uongozi na msajili wa vyama hakuzungumza chochote.

Alisema hawababaishwi wala kuguswa na uamuzi uliotolewa na Ofisi ya Msajili wa kwa kuwa mkutano mkuu wa Chadema unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, ndiyo utakaoamua hatima wa kiongozi yeyote wa chama hicho.

SOURCE:- Gazeti la Mwananchi.

CHADEMA WAJIBU MAPIGO, SASA WAMTAKA CAG KUWEKA WAZI RIPOTI ZA HESABU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA VYAMA VYA SIASA

CHADEMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuweka wazi ripoti za hesabu za mapato na matumizi ya vyama vyote vya siasa nchini, kwa ajili ya kusimamia misingi ya uwajibikaji.

Kimesema siku zote kimekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi ndani na nje ya chama, hivyo kwa upande wake hakina hofu yoyote ya ripoti za ukaguzi wa hesabu hizo kuwekwa wazi.

Pia kimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kujiandaa kupokea maandamano ya wanachama na viongozi halali wa CHADEMA watakaofika ofisini kwake kumpatia ukweli na kukitetea chama chao dhidi ya propaganda ambazo zimefikishwa kwake na watu kiliodai ni mamluki na masalia ya wasaliti, baada ya viongozi wao kufukuzwa uanachama mapema mwaka huu.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa chama hicho, John Mnyika, alisema kama Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ameamua kuwa ‘mpokeaji’ wa maandamano, basi ajiandae kwa maandamano makubwa ambayo yatabeba ujumbe wenye hadhi ya CHADEMA badala ya hoja za kipuuzi alizopelekewa hivi karibuni.

Mnyika alikuwa akijibu maswali ya gazeti hili, lililotaka ufafanuzi zaidi kutokana na kauli zake alizotoa mbele ya waandishi wa habari juzi mjini Dodoma alipokuwa akitoa msimamo wa CHADEMA kuhusu madai ya kundi la watu waliofika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na CAG, wakidai wao ni wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa chama hicho.

Kabla ya kwenda ofisi hizo mbili, watu hao walifanya mkutano na waandishi wa habari Juni 23, mwaka huu ambapo pia, bila kuonyesha vielelezo, walidai kuwa wao ni wajumbe wa vikao vya CHADEMA.

Katika hali ambayo inatia shaka uhalali wa ujumbe wao, siku moja baada ya mkutano huo, baadhi ya watu ambao majina yao yalionekana kuandikwa kwenye orodha, walianza kukanusha kuwa hawahusiki na kundi hilo, na kwamba wao ni wanachama watiifu kwa CHADEMA, na kwamba hawajui majina yao na saini zao viliwekwa kwenye orodha hiyo kwa nia gani.

“CHADEMA kama taasisi, si chama cha ufisadi wala ubadhirifu. Ni chama kinachoshirikiana na vyama vingine kuongoza Watanzania kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na ubadhirifu. Chama hiki hakiwezi kuvumilia ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote, iwe nje au ndani ya chama, ndiyo maana sisi ndio tuliotaka sheria ibadilishwe, utaratibu ubadilishwe, ili CAG akague mahesabu ya vyama vya siasa.

“Baada ya sheria kutungwa, udhaifu wa Ofisi ya Msajili, Ofisi ya CAG na Serikali ya CCM, umefanya kwa miaka mingi mahesabu yasikaguliwe. Zilipozuka hoja za ukaguzi wa hesabu, mzigo ukitaka kuhamishiwa kwa vyama, kama vile vyama havitaki, tukalielezea suala hili. Hatimaye CAG akafanya ukaguzi.

“Sasa hawa wamemuandikia mkaguzi wakitaka ripoti ya CHADEMA, mimi kama msemaji wa chama, nitoe mwito kwa CAG kuweka wazi ripoti za vyama vyote alivyovikagua.

“Aweke wazi kwa haraka kadiri inavyowezekana. Kwa sababu Bunge limeshaarifiwa kuwa mkaguzi amemaliza kufanya ukaguzi kwa baadhi ya vyama na vingine havijakaguliwa. Vile ambavyo havijakaguliwa vitajwe kwa majina na vikaguliwe. Halafu sasa tuone  hayo madai ya mara Mbowe hivi, mara Slaa hivi,” alisema Mnyika.

SERIKALI YALEGEZA MSIMAMO, SASA KUFUTA MISAMAHA YOTE YA KODI

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.PICHA KUTOKA MAKTABA

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.PICHA|MAKTABA

Dodoma. Waziri ya Fedha, Saada Salum Mkuya jana aliwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014, ambao umefuta misamaha ya kodi katika maeneo yaliyokuwa yakilalamikiwa na watu wa kada mbalimbali nchini.

Katika muswada huo Serikali imefuta misamaha ya kodi ya mapato inayotokana na  michezo kubahatisha na ukodishaji wa ndege nje ya nchi.

“Muswada umependekeza  waziri husika kutotoa msamaha wa ushuru wa mafuta kwenye mafuta isipokuwa mafuta ya petroli yanayotumika kwenye miradi mbalimbali inayofadhiliwa na washirika wa maendeleo,” alisema Mkuya.

Mkuya alisema kuwa katika muswada huo, Serikali imeondoa saruji, nondo na mabati katika orodha ya bidhaa zinazochukuliwa kuwa ni bidhaa za mtaji ambazo kwa sasa hupata msamaha wa kodi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

“Lengo ni kuhamasisha uzalishaji wa saruji, nondo na mabati pamoja na kulinda viwanda vya uzalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini dhidi ya ushindani wa bidhaa za aina hiyo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi,”alisema Mkuya.

Alisema kuwa Serikali imefuta msamaha wa kodi ya mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya nchi ili kupunguza misamaha isiyokuwa na tija.

“Marekebisho haya yanalenga kutoza mapato yanayotokana na ukodishaji wa ndege nje ya nchi, badala ya kusamehe kodi ya mlipakodi asiye mkazi, ambaye hatimaye hulazimika kulipa kodi itokanayo na mapato hayo nchini kwake,”alisema Mkuya.

Marekebisho hayo yanapendekeza kufuta misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni ya simu isipokuwa vifaa vya ujenzi wa minara ya simu.

Pamoja na marekebisho hayo muswada huo unapendekeza kuongeza kifungu cha 3(d) ili mtu yoyote asiruhusiwe kutoa misamaha ya kodi kwa miradi nayohusu upanuzi na ukarabati wa miradi inayofanywa na wawekezaji.

Aidha ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji baridi (soda) pamoja na kwenye maji ya matunda (juice), iliyotengezwa kwa matunda yanayozalishwa hapa nchini utabaki kama ulivyo sasa ili kuimarisha viwanda vya ndani.

Mkuya alisema vinywaji baridi vimefanyiwa marekebisho ambapo ushuru kwenye vinywaji hivyo utapunguzwa kutoka Sh 91 kwa lita hadi Sh 55 kwa lita.

MTEMVU AWADHIAKI WAPINZANI…..

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo

 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.

“NITAMSHUGHULIKIA KAFULILA”, WEREMA

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akijaribu kuwasuluhisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila katika Viwanja vya Bunge Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu (kushoto) akijaribu kuwasuluhisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila katika Viwanja vya Bunge Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

Dodoma. Mvutano kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila umechukua sura mpya baada ya mwanasheria huyo kugoma kupatanishwa huku akitishia ‘kumshughulikia’ mbunge huyo.

Ugomvi baina yao uliendelea jana asubuhi nje ya Ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuahirisha kikao cha Bunge hadi leo.

Licha ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kumwita Jaji Werema na Kafulila akiwataka kupeana mikono kama ishara ya kuzika tofauti zao, Jaji Werema alikataa na nusura amvamie mbunge huyo.

Juzi asubuhi baada ya Zungu kuahirisha kikao cha Bunge, muda mfupi baada ya Jaji Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni, mwanasheria huyo alitaka kumtia adabu Kafulila kwa kumwita mwizi.

Kafulila alimwita Jaji Werema mwizi akijibu mapigo baada ya awali kuitwa tumbili na mwanasheria huyo.

Ilivyokuwa jana

Wakati akizungumza na gazeti hili mara baada ya Bunge kuahirishwa jana, Jaji Werema alikutana uso kwa uso na Kafulila katika Viwanja vya Bunge na kuanza kumlalamikia mbunge huyo kwa kitendo chake cha kumwita mwizi.

“Unamuona huyo jana (juzi), aliniita mimi mwizi. Yaani mtu mzima kama mimi naitwa mwizi, kwa kweli sikupendezwa kabisa na kauli yake,” alisema Jaji Werema huku akimfuata Kafulila ambaye alitembea harakaharaka kumkwepa mwanasheria huyo.

Jaji Werema alisema juzi alishikwa na jazba baada ya kuitwa mwizi lakini akasema hakuwa na nia ya kumpiga ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Wakati Jaji Werema akiendelea kumlalamikia Kafulila, alitokea Zungu na kumtaka mwanasheria huyo kumsamehe mbunge huyo… “Mheshimiwa naomba mpeane tu mikono kama ishara ya kusameheana, yale mambo ya jana (juzi) yamekwisha.”

Lakini badala ya kukubaliana na ombi la Zungu, Jaji Werema alihamaki huku akitaka tena kumvamia Kafulila… “Mimi nakwambia Kafulila nitakukata kichwa, we subiri tu labda ukiniomba msamaha.”

Kafulila naye alijibu mapigo… “Huwezi kunikata kichwa Werema, huwezi, yaani uniue, hapana huwezi tena nakwambia huwezi.”

Wakati wakiendelea kurushiana maneno, Zungu alikuwa katikati yao, huku akiwasihi wapeane mkono na kusameheana bila mafanikio… “Haya mambo yamekwisha jamani, malizeni tofauti hizi.”

Kama vile alijua kuwa kauli ya kuua ilimchanganya Kafulila, Jaji Werema huku akitembea kuelekea katika Jengo la Utawala la Bunge alisema: “Siwezi kukuua kwa maana hiyo unayodhani, maana kufa utakufa kwa mapenzi ya Mungu, ila tutapambana tu, nitakuonyesha.”

 Kauli ya Kafulila

Akizungumza baadaye, Kafulila alisema: “Kutokana na hali ilivyo sasa, nimeandika barua Ofisi ya Spika juu ya vitisho nilivyopewa na Jaji Werema, kwanza jana (juzi) alitaka kunivamia pale bungeni na kunipiga, leo (jana) asubuhi amenitishia kuwa atanikata kichwa.”

Kafulila alisema barua hiyo pia ataipeleka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa maelezo kuwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakitokea matukio ya watu kutekwa, kuteswa na kutupwa porini… “Kwa nafasi yake, Werema anaweza kufanya lolote, hivyo barua hizo zinalenga kueleza alichokusudia kunifanyia.”

Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alipoulizwa kuhusu mvutano uliotokea juzi bungeni na barua za Kafulila alisema Ofisi ya Bunge haijapata malalamiko yoyote.

“Jana sikuwapo bungeni lakini mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote yaliyoletwa katika Ofisi ya Bunge. Kama wangeshikana mashati ndani ya Bunge  hilo lingekuwa kosa la kufanya fujo bungeni na adhabu zake zipo wazi,” alisema Joel.

Juzi, baada ya kurushiana maneno, Jaji Werema alinyanyuka alipokuwa amekaa na kuanza kumfuata Kafulila kabla ya kuzuiwa na kundi la mawaziri.

Mbali na kumzuia, mawaziri hao walimsindikiza hadi nje ya Ukumbi wa Bunge ambako alipanda gari lake na kuondoka.

BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKURUGENZI WA RASILIMALI WATU SERIKALINI

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu serikalini katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma.

 Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutanomkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmKatibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungumkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu .

Katibu Mkuu Ofisi Rais, Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper  mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.

 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuwa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wizarani, Idara za serikali zinazojitegemea, taasisi za umma na zinazojitegemea.

ZITTO AWASHANGA TRA; ASEMA SIYO MAPUNGUFU YA SHERIA NI UZEMBE

MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI, NAIBU KATIBU MKUU (CHADEMA) ZITTO KABWE 2

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kujieleza kwa kushindwa kesi hadi kupoteza Sh340 bilioni za kodi ya ongezeko la mtaji katika uchimbaji urani.

 Juni 21, 2014 gazeti hili liliripoti hukumu ya kesi kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kampuni ya JSC Atomredmetzoloto (ARMZ) ikiituhumu kukwepa kodi ya zaidi ya Sh340 bilioni.

 Mahakama ya Rufani za kodi ilitupilia mbali madai hayo ikiipa ushindi ARMZ.

 Akizungumzia hukumu hiyo, Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema jana kuwa kukosa kodi hiyo siyo upungufu wa sheria bali ni uzembe wa Mamlaka ya Mapato na Wizara ya Nishati na Madini.

 “Habari ya Serikali kukosa Sh340 bilioni za kodi ya ongezeko la mtaji, imenigusa moja kwa moja kwa sababu mbili kubwa,” alisema na kuongeza:

 “Moja, Mwaka 2012 niliwasilisha muswada binafsi bungeni kurekebisha Muswada wa Fedha 2012 ambao ulikuwa unabadili Sheria ya Kodi ya Mapato 2004 kwa lengo la kuweka vipengele vitakavyowezesha nchi kupata kodi kutokana na mauzo ya kampuni za wawekezaji wanapouziana hisa au mali nje ya nchi.

 “Pili, mwaka 2013 niligombana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusu suala la kodi kutoka Kampuni ya Mantra Resources na Waziri alilihakikishia Bunge kuwa lazima kodi italipwa.  Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo wa TRA, Richard Kayombo alipoulizwa kwa simu jana alisema asingezungumzia suala hilo Jumapili na kwamba suala hilo bado lipo mahakamani.

MAKAMU WA RAIS WA CHINA APOKELEWA NA PINDA JIJINI ARUSHA

PG4A3067Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akiongozana na Makamu wa rais wa  Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni  21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. 

PG4A3097Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akiongozana na Makamu wa rais wa  Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni  21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya  Rais, Utawala Bora, Capt.George Mkuchika.

PG4A3170Waziri Mkuu, Mizego Pinda  akizungumza na Makamu wa Rais wa China , Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni 21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini.


PG4A3185Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akizungumza na Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao baada ya mgeni huyo kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha  Juni  21, 2014 kwa ziara ya kikazi nchini.  Kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Rais, Utawala Bora, Capt. George Mkuchika.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) (FS)

UCHAGUZI MKUU CHADEMA SASA NI SEPTEMBER 2014

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kufanya uchaguzi mkuu ngazi ya taifa Septemba, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema uchaguzi huo utafanyika baada ya kuijenga CHADEMA kuanzia ngazi ya msingi nchi nzima.

Dk. Slaa alisema ili kuhakikisha wanapata misingi mingi, uchaguzi huo ulifanyika kwa zaidi ya mwaka na kuendelea hata sasa kufikisha asilimia 75 ya misingi nchi nzima.

Alisema katika uchaguzi huo wamefanikiwa kupata zaidi ya misingi laki 1.9 na kwamba itaongezeka idadi watapokamilisha zoezi hilo Juni 30.

Sambamba na uchugazi wa misingi, Dk. Slaa alisema uchaguzi wa matawi nao unaendelea na kwamba kati ya matawi 18,000 waliyokuwa nayo nchi nzima, uchaguzi umeshafanyika katika matawi 16,000.

Alisema kuanzia Julai, uchaguzi kwa ngazi ya jimbo, wilaya na mkoa utaendelea hadi Agosti, ili kupisha uchaguzi wa ngazi ya kitaifa.

Dk. Slaa alisema kwa sasa timu ya viongozi kutoka makao makuu ya chama hicho, wanazunguka katika mikoa yote nchini kuhakiki chaguzi ambazo zimekwishafanyika kama zimefuata katiba ya chama hicho na hakuna malalamiko.

UCHAGUZI MKUU CUF NI JUNI 23 – 27 BLUE PEARL UBUNGO, DAR ES SALAAM

CUF

ZIKIWA zimebakia siku mbili ili Chama cha Wananchi (CUF) kifanye mkutano mkuu wa kuwachagua viongozi wa juu wa kitaifa, imebainika kuwa hali si shwari ndani ya chama hicho.

Tanzania Daima limedokezwa jana kuwa hali hiyo imesababishwa na kujiengua kwa Machano Khamis Machano aliyetaka kutetea nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti.

Habari za kuaminika kutoka CUF zinasema kwamba awali waliogombea nafasi hiyo ni Juma Duni Haji na Machano ambaye alijitoa kwa sababu ya afya yake kudorora.

Taarifa hizo zilisema baada ya kutangaza kujiengua katika kinyang’anyiro hicho mjini Zanzibar, ‘wapambe’ wake walionyesha kutoridhika.

“Ukweli kuhusu Machano kujitoa katika kinyang’anyiro ni huu… mwenyewe kwa kauli yake wakati anarejesha fomu alisema anajiengua kutokana na hali yake ya kiafya, hivyo hataweza kuhimili tena mikikimikiki ya uchaguzi na uongozi,” alisema mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la CUF.

Bila kumung’unya maneno, mjumbe huyo alisema kwa miaka kadhaa sasa Machano anasumbuliwa na maradhi ya sukari yanayomfanya ashindwe kufanya shughuli za Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

“Hivyo nataka niwataarifu wanaCUF wenzangu wanaosema mzee Machano ameshinikizwa kuachia nafasi hiyo na wapambe wa babu Duni si kweli… kila mtu alikuwa na nguvu yake katika kinyang’anyiro hicho,” alisema mjumbe huyo.

Habari za ndani zilieleza kwamba jana kilifanyika kikao cha kupitisha majina ya wagombea mbalimbali huku Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba akipata upinzani kutoka kwa wagombea wawili waliojitokeza.

Katika nafasi ya uenyekiti wa CUF taifa waliojitokeza ni Chief Lutayosa Yemba kutoka Shinyanga na Mbezi Adam Bakari wa Temeke, Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo, Maalim Seif Shariff Hamad hakupata mpinzani na hivyo kuiacha nafasi hiyo wazi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo, alithibitisha kuwa maandalizi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika na kwamba utafanyika kuanzia Juni 23 hadi 27 katika Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

RIDHIWANI AWABEZA WAANDISHI WA HABARI

 

35 36e8f

Katika toleo  la Gazeti la NIPASHE   Juni 18, 2014, kulikuwa na habari iliyoanzia ukurasa wa kwanza na kuendelea wa tano iliyobeba kichwa cha habari: Ridhiwani kijana asiyekuwa na shukurani.

Habari hiyo ilikuwa ikizungumzia matamshi ya Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, akiwaponda wanahabari nchini kuwa asilimia kubwa ni makanjanja na kwamba wanapoandika habari wanasukumwa na weledi wa jinsi wanavyofikiria vichwani na itikadi zao za kisiasa.

Ridhiwani alitoa kauli hiyo Juni 8, mwaka huu wakati wa mahafali ya wanafunzi ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika vyuo vikuu vya mjini Morogoro, yaliyofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Umwema, mjini humo.

Alisema waandishi wengi hapa nchini wanasukumwa sana na utashi wa siasa zao, jinsi wanavyofikiria vichwani mwao na itikadi ya siasa. Aliongeza kuwa wakati mwingine hata jambo zuri likifanyika haliwezi kusifiwa badala yake kazi yao kubwa ni kuandika mambo ya ovyo ovyo tu.

Mbunge huyo alidai kuwa, asilimia kubwa ya waandishi nchini ni makanjanja na wanapokaa kwenye meza zao wanaandika vitu tu, wanapikapika vitu, akimaanisha wanaandika vitu vya kutunga.

Sisi tumeshangazwa sana na kauli ya mbunge huyu kijana ambaye ni miezi michache tu iliyopita amechaguliwa kushika nafasi hiyo kuwakilisha wananchi wa Chalinze.

Tunasema tumeshangazwa na kauli hiyo, kwa sababu Ridhiwani akiwa mwanasiasa kijana, anapaswa kutambua umuhimu na mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika taifa hili ambalo linakabiliwa na changamaoto nyingi za umasikini, badala ya kuwabeza.

Tunafahamu kuwa ni ukweli usiopingika kuwa tasnia ya habari nchini inakabiliwa na changamoto nyingi, lakini hiyo siyo sababu ya mtu kama Ridhiwani ambaye ni mwanasiasa na tena Mbunge kutumia lugha ya kejeli na kudhalilisha tasnia hiyo, badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo.

Kama amesahau, labda tumkumbushe Ridhiwani kwamba, ni vyombo vya habari na waandishi wa habari ambao leo anawabeza, wametoa mchango mkubwa katika kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa Chalinze hivi karibuni tu.

Ridhiwani alikuwa akizunguka na waandishi wa habari huku na huko katika jimbo zima la Chalinze waweze kuandika habari zake.

Ni waandishi wa habari hawahawa anaowabeza wamemsaidia kwa kiasi kikubwa Mbunge huyu katika kampeni hizo, wakitangaza na kueneza sera za chama chake na ahadi zake ili kuwashawishi wananchi wamchague, na kweli alifanikiwa na sasa ni Mbunge.

Ni Ridhiwani huyu huyu ambaye siku anaenda kuapishwa bungeni mjini Dodoma baada ya kuchaguliwa, anadaiwa kubeba rundo la waandishi wa habari kwenda kushuhudia kuapishwa kwake.

Leo tunashangaa kuona akitoa lugha zinazotaka kuaminisha watu kuwa waandishi wa habari ni watu wa ovyoovyo, wasiopaswa kuaminiwa katika jamii.

Ridhiwani amebeba hulka ile ile ya baadhi ya wanasiasa ambao huwatumia waandishi wa habari kufanikisha mambo yao, lakini wanapofanikiwa huanza kuonyesha kiburi, dharau na kutoa kauli za kudhalilisha dhidi yao.

Kama kweli Ridhiwani ana nia njema na waandishi wa habari, angekuwa mstari wa mbele kutumia nafasi yake ya ubunge aliyoipata, kuibana na kuishinikiza serikali kupeleka haraka bungeni muswada wa sheria ya vyombo vya habari na sheria ya uhuru wa kupata habari viweze kusimamia sekta hii muhimu, badala ya kutumia lugha za kejeli na kudhalilisha.

Tunamshauri mwanasiasa huyu kinda atambue kwamba ndiyo kwanza ameanza kutembea katika ulimwengu wa siasa, ajifunze kutafakari kabla ya kusema. Daima kuweka akiba kwa kila jambo ni busara zaidi. Ridhiwani aache kuvimba kichwa kwani kitapasuka mapema.

CHANZO: NIPASHE

BUNGENI JUNE 20 2014 GODBLESS LEMA AIVURUGA SERIKALI INAVYOONGEZA USHURU WA POMBE NA SIGARA

Godbless Lema 2

June 20 2014 Mbunge wa Arusha mjini Kamanda Godbless Lema aliishambulia serikali ya CCM kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma kwa kusema…

‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’

‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh. Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same serikali imeweka vibao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’

‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali ingeweza kabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingizwa kwenye gridi ya taifa na mngeweza kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’

‘Hata kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na serikali ambayo haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado inakopesheka, bado tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda kukopa barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe, ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali yenu ihamie hapa Dodoma’

‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu watu watakuwa wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya mapumziko itakua ni Iringa, Mbeya na Singida’

‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri wote na makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili hii nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za Urais huko kote anakokwenda’