VIDEO:- KICHUPA CHA G-NAKO “MORALE”

  • Video ya wimbo wa G-Nako, ‘Morale’ iliyoongozwa na Hanscana.

Hii ni moja ya vichupa vya hivi karibuni kabisa vya G-Nako ambayo inakwenda kwa jina la Morale, mwonekano wake ni mzuri na imefanyika katika mazingira ya kitaa…

Labda jambo lililonifurahisha kwenye nyimbo hii hususan mashairi yake ni pale G anaosikika akisema anapingana na wale wanao sema “Nako2Nako is back”.

Hebu tazama kichupa hiki na ujiinjoi

 

Advertisements

SAFARI HII NI ZAMU YA YAMOTO BAND; SAID FELA

Said Fela ndiye aliye nyuma ya kuanzishwa kwa kundi la vijana wanne waitwao ‘Mkubwa na Wanawe’ au Yamoto Band ambao kwa sasa wametokea kupendwa. Hadi sasa vijana hao wana nyimbo mbili, Yamoto na Nitajuta iliyotoka wiki iliyopita.

Akiongea na Bongo5 Fela amesema aliitengeneza bendi hiyo kuwa na muziki tofauti. “Mimi niliangalia kwamba kuna watu wanaimba, akina Diamond wanaimba, akina Ali Kiba wanaimba,” amesema.

“Sasa nikasema nikiwatoa kwa mitindo ya akina Ali Kiba, akina Diamond, watoto watakosoa tobo la kutoboa. Kwahiyo nakasema ngoja nianzishe kitu, kwa kuanzisha kitu ndio nikaona wachukue muziki wa Kitanzania kidogo na hii kisasa kidogo halafu tupenye pale. Ndo maana unaona Yamoto wamekuja na muziki wao.”

 

TIWA SAVAGE, ICE PRINCE, SARKODIE NA MAFIKIZOLO KUTUMBUIZA TUZO ZA BET

 

tiwa

Katika kuwapa pia nafasi wasanii wa Afrika, waandaaji BET Awards 2014 wamewatangaza wasanii hao kuwepo pia kwenye orodha ya watumbuizaji. Hii ni mara ya kwanza wasanii nje ya Marekani kutumbuiza kwenye tuzo hizo zitakazofanyika jijini Los Angeles tangu kuanzishwa kwa vipengele vya ‘Best International Act: Africa’ na ‘Best International Act: UK’ mwaka 2010.

Wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na K. Michelle, Mack Wilds, Mary J. Blige, Trey Songz na Jennifer Hudson. Chris Rock atakuwa host wa show hiyo.

DIAMOND PLATNUMZ NATAKA KULEWA (PITIO LA WIMBO NA VIDEO)

COVER LA NYIMBO YA DIAMOND NATAKA KULEWA

COVER LA NYIMBO YA DIAMOND NATAKA KULEWA

Ujio mpya wa msanii maarufu zaidi wa kizazi Kipya kwa sasa hapa Tanzania Nasibu Abdul AKA Diamond Platnumz wa nyimbo na video ya NATAKA KULEWA, ikiwa ni kazi yake ya kwanza baada ya kufanya mabadiliko makubwa kwa uongozi unao simamia kazi zake, kwa sasa yuko chini ya Meneja anayejulikana kwa jina la Ragey Mohamed.

Siku za hivi karibuni kupiti mitandao ya kijamii yamesemwa mengi kuhusu nyimbo hii pamoja na video yake. Wengi wakidai kuwa Kijana amefikia mwisho lakini M2S Songs & VIDEO Review Unit  wanakuhakikishia kuwa kijana bado yuko vizuri kwa kukuletea moja kwa moja kupitia blog hii nyimbo, Video na mashairi ya nyimbo yenyewe. Lazima nikiri kuwa tokea nianze kusikiliza sijachoka kuisikia na video yake inayodaiwa kuongoza kwa kugharimu pesa nyingi mpaka sasa hapa Tanzania.

Nyimbo hii ya Nataka Kulewa imefanyika A.M Records chini ya Usimamizi wa Maneke (Producer), Mirindimo ya nyimbo hii ni ya Kiafrika inayorindima kwa kufuata staili ya Bondeni (South Afrika) huku Diamond akiwa anapita kwenye nyimbo hii kwa stail ya aina yake mashairi yakiwa yana zungumzia kwa nini anataka kulewa. Kwa ufupi anajaribu kuchukuwa taswira ya mwanaume ambaye ametatizwa au kutendwa kwenye mahusiano. Katika moja ya mistari analalama kuwa kusema “kumbe mjinga ni mimi ninaye tunza na wengine wanachukuwa, ho o mapenzi, yamenifanya ni lie kama mtoto, mie siwezi walionikuta waache ni seme jina.” Kwenye ubeti wa pili kwa hisia kubwa anabainisha “Ni kwa mapenzi mskini nikamvisha na pete kwa kutaka kumuoa, kukata vilimi limi vya wazushi wanawake wanamponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, siye tuko kama ishirini mabuzi vingasti wengine anawahonga”

Nyimbo hii ni tofauti na nyimbo za awali za msani huyu kama vile NALIA NA MENGI, KAMWAMBIE, MBAGALA na NITAREJEA. wimbo huu una tempo ya juu na hivyo kuufanya kutimiza malengo ya kuchezeka pamoja na kusikilizika. Tatizo kidogo ni kufanana kwa milindimo na merodi hasa mianguko na nyimbo yake iliyofanywa na Rama inayojulikana kwa jina la MOYO WANGU.

kwa Kwa kusikiliza bonyeza kitufe hapo chini ujipatie nyimbo pamoja na video huku ukifwatilia mashairi ya nyimbo hii. Kwa ujumla nakushauri usikilize nyimbo hii ambao M2S wameipa alama 4/5. Video yake nayo imepewa 4/5 ambayo imefanywa na an i-View Studios Director akiwa Ragey Mohamed.

UKITAKA AUDIO BOFYA HAPA

UKITAKA AUDIO BOFYA HAPA

 

DARAJA {Bridge}

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

UBETI WA KWANZA:

Usiniulize kwa nini? Sababu utazengua, ukitaka jiunge na mimi, kama ni pesa ww kunywa nitanunua, mie mwanzo sikuamini, nikajuaga vya kuzua, kumbe mjinga ni mimi, ninaye tunza  wenzangu wanachukuwa, ahi! oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, mie siwezi walionikuta waniache ni seme jina. oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, na nina mengi yamenikaa moyoni.

KIITIKIO:

Leo nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa, zikipanda nimwage radhi, nataka kulewa, lewa mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa, zikipanda nimwage ladhi

DARAJA {Bridge}

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

UBETI WA PILI:

Ni kwa mapenzi mskini, nikamvisha na pete kwa kumuoa, kukata vilimi limi vya wazushi wanawake wanamponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, sie tuko kama ishirini, mabuzi vingasti wengine anawaonga, oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, mie siwezi walionikuta waniache ni seme jina. oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, na nina mengi yamenikaa moyoni.

KIITIKIO:

Leo nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa zikipanda nimwage ladhi, tilalila nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa lewa, zikipanda nimwage ladhi

DARAJA {Bridge}:

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

Mashairi haya ni kama yalivyonukuliwa na M2S Songs Review Unit wakiwa wanausikiliza wimbo wenyewe. Sio mashairi rasmi, kwa maana kutoka kwa mtunzi na muimbaji mwenyewe.

TUNAWEZA BLOG ADVERT3

WIMBO WA MRISHO MPOTO “CHOCHEENI KUNI…” (PITIO LA WIMBO)

Leo ningependa tumwangazie Mtunzi na muimbaji nguli wa fasihi simulizi kwa njia ya nyimbo zenye mahadhi ya ushairi ambayo yanauganisha mapokeo ya zamani na ya sasa, Nguli Mrisho Mpoto hususan katika kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la Chochea Kuni uliotengenezwa  katika studio za DATISHAIZO RECORDS.

Nyimbo yenyewe imetengenezwa kwa kutumia vyombo vichache hili msikilizaji aweze kusikiliza mashairi kwa upesi zaidi. Maadhi ya mirindimo yake ni ya kiafrika ikiandamana na vijisauti vya ndege na hivyo kutoa tswila halisi ya mazingira ya watanzania wengi wa kule pembezoni.

Mrisho Mpoto kama kawaida yake, anasafiri na msikilizaji wake na kumpa taswira halisi ya kile anacho analenga hadhira yake isikie (kuwasilisha). Mashairi yake yamepangika katika hali usika ya kukufanya utafakari kwa kina unapojaribu kuileta katika hali mahalia ya watanzania. Bonyeza kitufe cha kusikiliza wimbo wenyewe huku ukifuatisha mtiririko wa mashairi yake kama yalivyoandikwa hapo chini ya wimbo:

Mwisho kama unaswali au sehemu ambayo ujaelewa tujadili pamoja hili tujaribu kupata ujumbe sahihi wa huyu nguli wa mambo ya ushairi.

downloadbuttons150x40

BONYEZA HAPA UPATE WIMBO HUU

KIITIKIO:

Chocheeni kuni mbichi moto ukolee, Ugali uive mnachotaka kitokee, Alikeni mamluki, wakija wangojee, Mikeka waweke, wanachotaka kitokee, Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea, chochea , chochea oooo, Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea, chochea…

UBETI WA KWANZA:

Watanzania, mwenda kwao siku zote haogopi giza, Acheni nirudi nyumbani safari imenishinda, nauli zenu nitarudisha. Mtu anatapika nyongo yake, anailamba tena anaangaliwa? Ni sawa na tawi kavu linapoanguka watu wakapiga kelele, ayaaaa! Katika misimu minne kwa mwaka, tuongeze msimu mwingine wa tano wakujistusha, Raha ya jamvi siku zote ni viraka viraka, Na dungu, linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tu? Eti ooo, imenyesha juzi tu, maji sio mengi, nisubirini kule, Ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti, ndio mkawaambia watu wavuke? Mjomba, binaadamu ni kama ganda la kitabu, Mpaka umfungue maandishi, ndio uweze kumuelewa, Eti lilotokea mbali tufanye limepita, na haliwezi kumdhuru mwingine, Kweli! Inayotaka kunyesha huwa haisubiri mawingu, Mimi, sidhani kama kujiponya kwa mambo mazito, Tunahitaji cheti kilichogongwa muhuri wa moto, Au mtaalamu wa magonjwa ya akili, zaidi ya kutumia neno sahau tu, Unawaulizaje watu magongo ya nini, wakati umesema kuna nyoka? Mjomba, wewe si uliwapaka wanja, ngoja wao wakupake pilipili, Halafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga

KIITIKIO:

Chocheeni kuni mbichi moto ukolee, Ugali uive mnachotaka kitokee, Alikeni mamluki, wakija wangojee, Mikeka waweke, wanachotaka kitokee, Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea, chochea , chochea oooo Chochea, chochea , chochea , chochea , chochea , chochea , chochea, chochea…

UBETI WA PILI:

Mngekuwa mnajua anachokula nyuki, msingethubutu kusema asali ni tamu, Niwashukuru, kwa kufikiri mjini mimi nilifaha niende, Halikuwa wazo baya kwa wakati ule, Maana mlionyesha ukomavu kutoka kwenye shingo kwenda chini na sio juu, Mbona hamkumfikiria aliyekuwa ndani, kafungiwa kwa nje? Usingizi hapati anawaza jinsi ya kutoka, Nikisema uwezo wa watu kufikiri na mahitaji unatofautiana, mtaanza kusema nina dharau na matusi, Lakini kumbukeni ulimi unauma kuliko meno, Mnawezaje kumfikiria aliyekuwa ndani, kajifungia mwenyewe, funguo anazo mwenyewe, Kalala fo fo fo, asijue hata idadi ya misumari iliyoshikilia mlango wake, Kulipamba jeneza, hakumfanyi aliyekufa kufufuka nyinyi, Kama kusema nimeshasema sana, mwishowe nitakuwa kama mwanasiasa, Hawajitokezi mpaka kuwe na maafa, Natoa katoni ishirini za sabuni ya unga, aliyekwambia wale wachafu nani? Kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndio mrudi kwa wananchi, Ndugu zangu, tawi kavu, kuanguka wala sio ajabu, Wakati wao wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga, Ninyi chocheeni kuni zilizoloa, maji yapate moto ugali usongwe, wakiwauliza, waambieni huu ni utani hehehe, Hapa kwetu tuna makabila 120, tunataniana, Waliopo hatuwataki, wanaotaka hatuwaamini, Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukijua maana yake, Kwa mfano neno la kitoto, mtoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza, Neno la kitoto, mtoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakua, Mtoto akisema babaa, ile ndege yangu, Baba hata kama huna baiskeli, utamwambia ikitua nitakuletea, ndio utaratibu, Lakini maneno ya kitoto, mtu mzima kumwambia mtu mzima mwenzie, kuna walakini, Mimi safari imenishinda, na sitaki tena kuulizwa kwanini

KIITIKIO … hadi mwisho

Mashairi haya ni kama yalivyonukuliwa na M2S Songs Review Unit wakiwa wanausikiliza wimbo wenyewe. Sio mashairi rasmi, kwa maana kutoka kwa mtunzi na muimbaji mwenyewe.

TUNAWEZA BLOG ADVERT3