UZINDUZI WA MSIMU WA PILI WA TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGI, CINEMAX OYSTERBAY

Uzinduzi wa siri ya mtungi season II ndani ya ukumbi wa Century Cinemax Oysterbay wafana hapa ni kati ya washiriki wakipata ukodak wa pamoja na wafadhili waliofanikisha Episode hii kukamilika na kuwa hewani. Wafadhili hawa ni kutoka Marekani na ndiyo chachu ya Episode hii kukamilika na kuiwezesha kuwa hewani hili watu wajifunze kilichopo ndani yake.

Vyombo vya habari pamoja na Camera ya Vijmambo vikiwajibika hili kuwajuza kilichokuwa kimefanyika ndani ya ukumbi huu wa Century Cinemax.

Juu na chini washiriki wa Episode hiyo wakibadirishana mawazo huku pia wakiendelea kuangalia walichokifanya ndani ya Episode hiyo.

Ni mambo ya ukodak tu mwanzo mwisho hili kutunza kumbukumbu kwa washiriki wa Episode hiyo

Starring wa Episode hiyo bwana Juma Rajabu aka Cheche akiongea mbele ya camera juu ya nini alichokifanya ndani ya Episode hii ya siri ya mtungi. Kwa picha zaidi jitiririshe kwa kubofya soma zaidi.

Advertisements

MOVIE REVEW: – PICHA YA SAVING PRIVATE RYAN (1998).

Saving_Private_Ryan_by_Narusargent

Leo wakati napitia order za movie nimekutana na order ya Saving Private Ryan, nikastuka siyo kwavile haipo kwenye maktaba yangu, la hasha bali mdau wangu amenikumbusha filamu ambayo Motion Picture Arts and Sciences waliipendekeza kuwania zaidi ya tuzo 11 mwaka 1998 huku ikijikusanyia mapato ya zaidi ya dola milioni 481.8 na director wake Steven Spielberg kufanikiwa kupata tuzo ya Second Academy Award ya director bora.

Movi ya Saving Private Ryan (1998) ni moja ya filamu za kivita za Marekani ambayo inaonyesha shambulio la Normandy kwenye vita kuu ya pili ya dunia. Ikiwa imeongozwa na director bingwa Steven Spielberg na kuandikwa na Robert Rodat, filamu hii inasifiwa kwa ubunifu wake hasa katika dakika 27 za mwanzo kwa nanamna walivyo weza kuonyesha uhalisia wa shambulio la Omaha Beach la Juni 6, 1944 na harakati za kapteni wa jeshi la marekani John H. Miller (Tom Hanks) ambaye aliongoza kikosi cha watu 8 kumtafuta James Francis Ryan (Matt damon) mwenye cheo cha Private First Class , huyu akiwa ni miongoni mwa ndugu wanne ambao kaka zake wote walipoteza maisha vitani.

Rodat aliandika filamu script 1994 baada ya kuudhulia kumbukumbu ya mazishi ya ndugu 8 waliokufa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani. Rodat akafikilia kitu kama hicho na kutengenezea story kwenye vita vya pili vya dunia. Script ilikabidhiwa kwa Mark Gordon ambaye alimkabidhi Hanks na baadae kumfikia Spielberg.

Actors                   :               Tom Hanks, Tom Sizemore, Edward Burns, Barry Pepper, Adam Goldberg, Vin Diesel, Giovanni Ribisi, Jeremy Davies, Matt Damon, Ted Danson, Paul Giamatti, Dennis Farina, Joerg Stadler, Max Martini, Dylan Bruno

Directors              :               Steven Spielberg

Countries             :               USA

Release                 :               July 24, 1998

Categories            :               Drama, War, Action

Duration              :               169 Dk.

Budget                   :               70,000,000 usd

Hili ni bonge la movi ambalo si la kukosa.

MOVIE REVEW:- PICHA MPYA “MY MAN IS A LOSER” (2014).

my_man_is_a_loser_2014 two

My man is a loser ni filamu ambayo ni ya ucheshi (comedy) kwa mara ya kwanza ilionyeshwa kwenye big screen Julai 25, 2014. Stori line ya filamu hii ni wanandoa wawili ambao walimwajiri rafiki yao kapera (single playboy) ili awasaidie kuokoa ndoa zao, lakini mambo haya kwenda kama yalivyo tarajiwa …. haikuchukua muda wake zao wakabaki wakijiuliza kama matendo ya waumezao ya sasa ni bora kuliko yale ya awali?

Runtime               :               95 mins

Release Date       :               25th July 2014

Genres                  :               Comedy

Actors              :               John Stamos, Tika Sumpter, Sean Young, Michael Rapaport, Diane Guerrero, Bryan Callen, Carly Brooke Pearlstein, Emilie Kuznicki, Ronnie Mund, Courtney Cooper, Wass Stevens, Heidi Armbruster, Stephanie Domini Ehlert, Dasha Kittredge, Lisa Ferreira, Megan Reinking, Kathy Searle, Takara Sewitt, Maria Bartiromo, Katelynn Bailey, Ava Paloma, Mo Mandel, Libby Winters, Alexandra Stebbins, Tina Marie Connell, Jessica Press, Chella Ferrow, Hyejin J., Stevie Steel, Nicole Neuman.

MOVIE REVEW:- PICHA MPYA YA EXPENDABLES 3 (2014).

the-expendables-3
Picha ambalo lilikuwa linasubiliwa la Expendables 3 ambayo inatoka rasmi Agosti 24 2014 tayari imeingia mitaani. Hii ni bonge la picha na naweza sema ni kali zaidi ya zile zote Expendables zilizo tangulia.

Ndani ya Expendables 3 Barney (Stallone), Krismasi (Statham) na timu nzima ikiwausisha wakali kama Jet Li, ya Expendables wanakutana uso kwa uso na Conrad Stonebanks (Gibson), ambaye miaka iliyopita alishiriki kuanzisha Expendables yeye pamoja na Stallone. Stonebanks hatimaye akawa mfanyabiashara katili jambo ambalo lilimlazimu Stallone kumuua … au yeye Rambo kuamini hivyo.. Stonebanks, ambaye alifanikiwa kukwepa kifo mikononi mwa Stallone anafanya mkakati wa kulifutilia mbali kundi la Expendables – bila kufahamu Stallone ana mipango mingine. Stallone anaamua kupambanisha damu ya zamani na damu mpya, na huleta enzi mpya ya Expendables yenye wanachama wapya kwa kuajiri watu ambao ni mdogo, wenye kasi na tech-savvy zaidi.

Unahitaji muda wa dakika 103 kuweza kuwa mmoja wa shuhuda wa hii mission ya Expendables katika vita ya kibinafsi.

Runtime               :               103 mins

Release Date        :               15th August 2014

Genres                   :               Action, Thriller, Adventure, HQ-Link

Actors                :               Sylvester Stallone, Jason Statham, Jet Li, Antonio Banderas, Wesley Snipes, Dolph Lundgren, Mel Gibson, Harrison Ford, Arnold Schwarzenegger, Ronda Rousey, Kellan Lutz, Terry Crews, Kelsey Grammer, Natalie Burn, Sarai Givaty, Robert Davi, Victor Ortiz, Randy Couture, Glen Powell, Bashar Rahal, Lisbeth Olofsson, Thomas Canestraro, Velizar Binev, Ivan Kostadinov, Tzvetislav Samardjiev, Harry Anichkin, Mason Brett, Slavi Slavov, Anton Poriazov

kama unaitaji kitu hiki  tuwasiliane….

MOVIE REVEW;- KITU CHA COVERT AFFAIRS SEASONAL 1

Covert-Affairs-USA-Network-poster-season-1-2010

Kitu cha Covert Affairs mpaka sasa kinaendelea kuonyeshwa kwenye TV network za marekani ambapo imefikia Seasonal 5. Kwa maana hiyo unaweza kujipatia mpaka Seasonal 4.

Seasonal 1 ina jumla ya Episodes 11, Story hii inaanza pale mwanadada mwenye umri wa miaka 28 Annie Walker, anapoitwa ghafla kutoka mafunzoni ya upelelezi na shirika la kijasusi la CIA nchini Marekani ili kufanya kazi maalum. Ofisi ya CIA ilieleza kuwa walimchagua kutoka miongoni mwa wanafunzi wenzake kutokana na umakini katika mafunzo maalum, Sifa nyingine ya ziada ni uwezo wake wa kuzungumza kwa ufasaha lugha za Kirusi, kitaliano, Kihispania, Kijerumani, Kifaransa, Kiajemi, Kireno na lugha nyingine kadhaa.

Alipo wasili CIA alikabidhiwa kwa Jasusi Agosti Anderson, jina la utani “Auggie” ambaye amepoteza uwezo wake wa kuona alipokuwa kwenye operation nchini Iraq, Idara hiyo ikiongozwa na jasusi Joan Campbell, ambapo yeye alikuwa na wajibu wa kumpa msaada wa kiufundi.

Original Title: Covert Affairs
Country, Channel: USA, USA Network
Release Date: June 13, 2010
Genres: Action, Crime, Drama, Mystery, Thriller
Creators: Chris Ord, Matt Corman
Cast: Piper Perabo as Anne Catherine “Annie” Walker, Christopher Gorham as August “Auggie” Anderson, Kari Matchett as Joan Campbell, Anne Dudek as Danielle Brooks, Sendhil Ramamurthy as Jai Wilcox, Peter Gallagher as Arthur Campbell, Emmanuelle Vaugier as Liza Hearn, Gregory Itzin as Henry Wilcox, Eion Bailey as Ben Mercer, Noam Jenkins as Vincent Rossabi, Oded Fehr as Eyal Lavin

Runtime: 60 min
Language: English

Kama unaitaji movie hii au nyingine zozote wasiliana nasi kwa simu +255 732 981 189

FILAMU YA I LOVE MWANZA YAZINDULIWA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akisadiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, kukata utepe kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone YouthEmpowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akionyesha CD ya  filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wa watatu kushoto), Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akinunua CD ya filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, baada ya kuizindua katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza Jumamosi usiku. Waziri Membe aliwezesha filamu hiyo kununuliwa na wadau kwa zaidi ya Milioni 50/- katika hafla hiyo. Kulia ni Msanii wa Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.

SHIKAMOO MZEE NA SHADA NI MOJA YA FILAMU ZILIZOSHINDA TUZO ZA ZIFF

Filamu ya JB, King Majuto na Shamsa Ford, ‘Shikamoo Mzee’ na ‘Shahada’ aliyoigiza Claud zimeibuka kidedea kwenye tuzo za ZIFF zilizotolewa jana visiwani Zanzibar.

14475455931_a95bcd8186_z
Mtitu akipokea tuzo ya ZIFF kwa niaba ya Claud

Katika tamasha hilo la filamu la kimataifa, Zanzibar limehusisha zaidi ya waongozaji na watengeneza filamu 30 kutoka nchi mbalimbali.

14478825905_28d3da931d_z

14477600954_cb15c60968_z

Filamu za Bongo Movie zilizo tuzwa  zimetuzwa kwenye na ZIFF kupitia ZUKU people Choice.

ZUKU PEOPLE CHOICE:- Shikamoo Mzee

BEST ACTOR:- Jackson Kabirigi for Kisate and Nguvu ya Imani

BEST ACTRESS:- Esha Buheti for Mimi na Mungu wangu

BEST DIRECTOR:- Issa Musa Cloud for Shahada

BEST FEATURE FILM:- Shahada Issa Musa

FAMILIA YA BONGO MUVI YAMPOTEZA MUONGOZAJI NA MWIGIZAJI ADAM KUAMBIANA

http://api.ning.com/files/ul6fByF3mQflPAkDymTC6l7oSIe5Z-7ttjPkRqMZ5Ap7e*eCA8BS7VPT0qilab3hk2YvlMI2178ZBXtAi7ag1PSLIQkl*wIU/Kuambiana1.jpg

Adam Kuambiana enzi za uhai wake.

MWIGIZAJI na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo. Marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar. Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Marehemu Kuambiana katika muonekano wake wa siku zake za mwisho za uhai wake

…katika pozi na msanii Irene Uwoya

…(kushoto) akiwa na wasanii wenzake JB (kutoka kulia), Tino na Mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi

BAADHI YA KAZI ALIZOCHEZA/KUONGOZA MAREHEMU KUAMBIANA:

R.I.P Adamu Kuambia.

{KICHUPA} EPIC STORY ABOUT “NANI ANAFAIDIKA NA MADINI YA MERELANI

A survey conducted by the Institute for Information Media2solution in Simanjiro for about three months to determine the benefits that communities of these areas benefit from the Tanzanite mining. This project was funded by Tanzania Media Fund.
 
Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya kihabari ya Media2solution katika wilaya ya Simanjiro kwa takribani miezi mitatu kwa lengo la kubaini faida ambazo jamii ya maeneo hayo ufaidika kutoka kwenye madini ya Tanzanite. Uchunguzi huu ulidhaminiwa na Tanzania Media Fund.

MASHINDANO YA KUMSAKA MWAKILISHI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KATIKA FILAMU YAFANA

 Mshiriki wa Tanzania Movie Talents akihojiwa mara baada ya kumaliza usaili katika Shindano la Tanzania Movie Talents katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya
 
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwaajili ya kuhudhuria usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa usaili.
 
 Washiriki waliojitokeza kwaajili ya kushiriki mashindano yya Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya usaili wa shindano la Tanzania Movie Talents  Mkoani Mbeya ikiwa unawakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
 Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya wakisubiri shindano la Tanzania Movie Talents kuanza.

Kundi la Kwanza La vijana waliojitokeza kwaajili ya usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents mkoani Mbeya.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited – Mbeya

Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi Juzi katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo usaili huo unafanyika Mkoani Mbeya Katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa uliopo Soko Matola Mkoani Mbeya.

Washiriki wapatao 150 wamejitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili la Tanzania Movie Talents ambapo washindi watatu kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini watazawadiwa kitita cha Shilingi laki tano za Kitanzania na Baadae kupewa Tiketi ya Kuelekea Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kushiriki fainali itakayowakutanisha Washindi waliopatikana katika Kanda ya Ziwa, Kati na kanda zilizobakia za Pwani na Kaskazini na mshindi katika fainali hiyo atajinyakulia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania pamoja na Mikataba minono kutoka Kampuni ya Proin Promotions Limited na washindi kumi katika fainali hizo watakuwa chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited na kuweza kutengeneza filamu ya Pamoja ambapo watanufaika na Mauzo ya filamu yao.

Mashindano ya Tanzania Movie Talents yataendelea Mkoani Mbeya kwa Siku nne ambapo siku ya jumanne washindi wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watapatikana na kupewa Zawadi zao.

{VIDEO} TANZANIA BADO KUNUFAIKA NA TANZANITE

Hiki ni Kichupa kipya kabisa, ambacho ni matokeo ya uchunguzi wa zaidi ya miezi mitatu merelani simanjiro. Pata undani wa matukio ambayo uwezi kuyaona sehemu nyingine yoyote na kwa uwazi.

Fwatilia bila kukosa kupitia matinya yako ya hapa nyumbani, mfululizo wa makala Nne zenye maelezo, uchambuzi, utafiti na ufafanuzi wa kina kuhusiana na madini hayo meusi ambayo yanapatikana sehemu moja tu duniani.

VIDEO:- MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA 29112013 BAADA YA MAAMUZI YA KAMATI KUU

Kichupa hiki si cha kukosa, ni mkutano mzima ambao wananchi wa Arusha wameweka msimamo wao huku wakibainisha yafuatayo.

 • Wasema wenyewe ni wazoefu wa kushugulikiana.

 • Watoa haadi ya kupambana na wapinzani kama Fukwe.
 • Lema asema kaingia madarakani kwa maandamano na ndivyo nchi hii itakavyo kombolewa.
 • Wana wa Arusha watoa maamuzi yao kuhusiana na Zitto

 

NJIA NYEUPE KWA WATENGENEZAJI WA FILAMU WA KITANZANIA KUUZA KAZI ZAO KWENYE MITANDAO

IMG_7030

MKurugenzi wa Kampuni ya Blue Sky, Richard Signeski (kulia), akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ukumbi Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam  kuhusu ushirkiano walioingia na  Kampuni ya Status Communications ya nchini kuwawezesha waandaaji filamu nchini kuuza filamu zao  kwenye mitandao ya kijamii. Kushoto ni Mwakilishi wa Status Communication, Monalisa Shayo.

IMG_7022

Omar Salisbury akizungumza na waandishi wa habari.

Kampuni ya Status Communications imetangaza ushirikiano na kampuni ya usambazaji wa filamu ya Kimarekani Blue Sky Media ili kuwawezesha kuuza filamu kwenye mitandao ya ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao mingine ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski alisema ushirikiano huu utawafanya watengeneza filamu kutoka Afrika Mashaaiki na kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao mikubwa ya usambaji dunia nzima.

‘’Lengo la ushirikiano huu ni kuwapa watengeneza filamu kutoka Afrika mashariki na kati kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji dunia nzima’’ alisema Signeski.

Mwakilishi wa Status Communications, Monalisa Shayo alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya tu ya ushirikano na makampuni ya kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki.

 ‘’Mwaka 2013 umekuwa mwaka muhimu kwa Status Communications kwani tumeweza kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la Afrika Mashariki’’ alisema Monalisa.

‘’Mwanzoni mwa mwaka huu tumeingia mikataba na makampuni kama Media Zone Authority  ya Abu Dhabi (twofour54) pamoja na Qatar’s Media Group International pamoja na Visual Unity ya Abu Dhabi ili kuwawakilisha kwenye masoko yao kwenye miji kama ya Prague’ alisisitiza Monalisa wa Status Communications.

‘’Fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wa Afrika Mashariki kuuza filamu kwenye masoko tofauti duniani’’ alisema Monalisa.

Akielezea sababu za kuja nchini, Signeski alisema alichokigundua hapa nchini ni kuwa watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi kwenye utengenezaji wa filamu zao kwani wanahofia uchache wamasoko ya kuuza filamu zao.

‘’Hivyo nawaomba watengeneza filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa urahisi’’ alimaliza Signeski.

KI CHUPA KIPYA CHA JUMA KASSIM NATURE FT TUNDA MAN “HAIPOTEI”

Kichupa hiki cha mtunzi, muimbaji na kwasasa mtayalishaji Juma Kassim Mohamed Kiroboto ambacho amemshirikisha Tunda Man Rais wa manzese, kilitufikia Mei 28 2013.

Kichupa ni chakawaida sana ambacho kimenakshiwa na ufundi wa kugani wa wakongwe hao. Kilicho wazi ni kwamba kama kuna walio fikiri Sir Nature amepote au atapotezwa hivi karibuni… jibu liko wazi “HAIPOTEI”

Juma Nature au Sir Nature (amezaliwa mwaka 1980 Jina kamili akijulikana kama  Juma Kassim Mohamed Kiroboto jijini Dar es Salaam) ni mwanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flava kutoka nchi ya Tanzania. Pia ni muanzilishi wa kundi la Tmk Wanaume.

Nature ni msanii mbunifu katika wa Bongo Flava na Hip Hop ya kiTanzania. Sio mtunzi tu pia ana kipaji na kujaliwa sauti nzuri ya uimbaji. Sababu nyingine zipelekeazo muziki wa Juma Nature kupendwe Afrika Mashariki ni mashairi anayotunga.

Albamu Alizotoa

 • Nini Chanzo (2001)

 • Ugali (2003)

 • Ubinadamu-Kazi (2005)

 • Zote History (2006)

ZUKU YANOGESHA! WAZINDUA CHANELI YA SWAHILI MOVIES

??????????????????????

Kushoto ni Fadhili Mwasyeba, Meneja mkuu Zuku Tanzania katikati ni Mohammed jenneby Mkurugenzi Mtendaji Wananchi Satellite na aliye simama kulia ni Jackie Karanja Afisa Mausiano wa ZUKU, walipokuwa wakiongea na vyombo vya habari kabla ya uzinduzi wa ZUKU Kiswahili Channel.

??????????????????????

Baadhi ya wanahabari wakifwatilia kwa makini hotuba ya uzinduzi kutoka kwa viongozi wa ZUKU PAY TV

??????????????????????

Kushoto ni Fadhili Mwasyeba, Meneja mkuu Zuku Tanzania katikati ni Mohammed Jenneby Mkurugenzi Mtendaji Wananchi Satellite

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

??????????????????????

Jumamosi, Juni 8, 2013. Zuku Pay Tv imezindua Zuku Swahili Movies chaneli namba 210 ambayo ni watakua  wakionesha burudani za muziki na filamu za kiswahili .

Tukio hili la kifalme lilitekwa utamaduni wa kiswahili na kuthamini historia ya filamu nchini Tanzania na kuthamini mchango wa  waenzi pamoja na nyota mpya wa sekta ya filamu.

Waigizaji, wakuzaji wa filamu wa Arusha na Dar es Salaam walikaribishwa kwa kapeti nyekundu.
Akizungumza katika uzinduzi wa Zuku Kiswahili Channel, Mohammed Jenneby Mkurugenzi Mtendaji Wananchi Satellite alionyesha matumaini yake na kueleza mkakati wa biashara kwa zaidi ya  wateja million mia moja katika kanda ya Afrika Mashariki. “Kiswahili ni lugha ambayo inawaunganisha wakazi wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Lugha ya Kiswahili itaendeleza jukumu muhimu ya kuleta maendeleo ya kanda. Chaneli ya Zuku Swahili inasherekea maendeleo yetu na pia kukuza nje utamaduni wetu kupitia filamu duniani

Mtange wa Satelitie wa Zuku hupatikana kwa nchi 15 Afrika Mashariki na kampuni ya Wananchi inalengo la kupanua utaambazi wake kufikia nchi 40 hivi karibuni. Kampuni pia imeelezea  nia yake ya kuendelea kuwekeza katika kanda ya Afrika Mashariki

Zuku Swahili Channel 210 inajivunia filamu bora, sinema na burudani ya kiswaili kutoka Tanzania na inelenga  kujumuisha uzalishaji kutoka Uganda, Kenya, Rwanda na DRC katika miezi ijayo.

Zuku Kiswahili Channel 210 inaonyesha filmau, michezo ya kuigiza, majadiiano na muziki. Chaneli hii inapatikana katika vifurushi vya Zuku Poa, Zuku Classic, na Zuku Premium

Fadhili Mwasyeba, Meneja Mkuu Zuku Tanzania aliwashukuru wazalishaji na watunga filamu ambao wameshirikiana na Zuku kuzindua chaneli hii. “Kampuni inaendelea kutafuta filamu bora; nia yetu ni kununua haki za kuonyesha filamu hiii kwenye jukwaa letu la Zuku Pay TV. Tunawakaribisha watengenezaji wa filamu katika kanda ya Afrika Mashariki kutumia jukwaa letu na kufanya biashara na sisi, alisema.

“Ili kuhakikisha tunakutana na watunga filamu wote tutakuwa na msafara wa Zuku Caravan ambao utatembea kote nchini. Tunawahimiza wadau wote kukutana na kufanya biashara nasi” alisema Bw.  Mwasyeba.

Ziara ya kwanza ya msafara utaanza Arusha tarehe 15 Juni Arusha na baadaye kutembelea mikoa ya Moshi, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dodoma, Shinyanga, Bukoba na Dar es Salaam.

UTAJUAJE KUWA UNAANGALIA FILAMU YA BONGO MOVIE….

 • Walinzi wengi huwa ni comedians.

 • Tajiri anakuja kumpenda masikini.

 • Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi na mvuta sigara na koti refu jeusi.

 • Wote wanaouwawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni sio kichwani.

 • Mtu yupo village,life gumu ana wave kichwani.

 • Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha.

 • Nusu saa mtu anatembea, anakimbizwa, ananunua vitu.

 • Wakifika hotelini imezoeleka ni juice au wine isiyofunguliwa.

 • Madem wanaamka wana makeups usoni na hereni kabisa.

 • Part 2 ya movie ukiiona mwanzo unajua part 1 ilikuwaje.

 • Jini akifika barabarani anaangalia pande zote ndo avuke..!

Source jamiiforums.com

KWA WALE WENYE VISIMBUSI TAMTHIRIA YA BUNGE YAREJEA TENA

 • BAADHI YA VIVUTIO KAMA REPOTI YA CAG VIMEONDOLEWA BAADA YA WAIGIZAJI KUANZA KUIGIZA UKWELI NA KUSABABISHA MADHARA KWA SERIKALI (KADHIA YA UKUSANYAJI WA KULA 70).

 • TAARIFA ZINASEMA UWASILISHAJI WA RIPOTI YA CAG BILA KUJADILIWA NI HATUA KUBWA AMBAYO AIWEZI KUBEZWA KUTOKANA NA KUWAEPUSHA WAIGIZAJI KUIGIZA KWA NJIA SALAMA BILA KUUMIZANA AU KULETA MADHARA KWA SERIKALI HILIYO MADARAKANI.

Episode ya 11 ya tamthiria ya watunga sheria za nchi hii unaanza leo mjini Dodoma, huku watayarishaji wake wakijigamba kufanya mabadiliko kadhaa ya taratibu za uendeshaji ambazo sitawezesha hata watoto kuangalia bila kuondoa radha na msisimko wake.

Taarifa iliyotolewa jana na Mratibu Msaidizi wa tamthiria kurugenzi ya (Habari), ilijinasibu kuwa bado wanapambana na  tishio la kutokuonyeshwa live kama baadhi ya wazandiki wa filamu hii walivyopendekeza. hata hivyo wazandiki hao wamefanikiwa kupunguza watazamaji kutokana na kuanzishwa kwa visimbusi (Vingamuzi) hali inayowapelekea watanzania wengi wasio kuwa na uwezo kujionea yanayojiri. Tamthiria hii itananza kurushwa tena leo live kupitia vituo pendwa vya TV na kukamilika Juni 28, mwaka huu huku ikilenga namna ya kuwakamua zaidi wananchi wake kwa kuwa neemesha wachache.

Kutokana na mabadiliko hayo, leo asubuhi wakati wa ufunguzi rasimi washiriki watapokea Azimio la Marekebisho ya Kanuni zake ambazo zinatarajiwa kuwasilishwa na Naibu Spika, Ndugu kazi.

Aliyataja mabadiliko hayo kuwa ni utaratibu mzima jinsi ya uwasilishaji bajeti za wizara, kwa mwaka huu itaanza Ofisi ya Waziri Mkubwa ambayo itajadiliwa kwa siku tano. “Siku zote tumezoea kuona Bajeti ya Sela-kali ndiyo inayotangulia kuanza kuwasilisha bajeti yake, utaratibu huo umeonekana siyo mzuri kutokana na mapendekezo ya wanazuoni wa kulinda maslahi yetu, hivyo tunaanza na wizara zingine ili Ngawila iwe ya mwisho,” ilisisitiza taharifa hiyo kutoka kurugenzi ya (Habari) ya filamu hiyo.

Hata hivyo, taarifa za zilizopatika kutoka ndani zinadai kanuni nyingi zinatarajia kubadilishwa na kwamba, iwapo zitapitishwa zitapunguza watazamaji wake kuichukia Sela-kali yao.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kesho itakuwa siku maalumu kwa Ofisi ya Waziri Mkubwa kuwasilisha bajeti yake, ambayo itajumuisha wizara zote zilizo chini yake na inatarajia kujadiliwa kwa muda wa siku tano.

Mabadiliko mengine ni kuwasilishwa mezani kwa taarifa ya CAG kwa mwaka 2011/12 bila kujadiliwa hili kuondoa madhingila ya kuumizana waingizaji na kuakikisha atuta lifumuo tena baraza letu.