DIAMOND PLATNUMZ NATAKA KULEWA (PITIO LA WIMBO NA VIDEO)

COVER LA NYIMBO YA DIAMOND NATAKA KULEWA

COVER LA NYIMBO YA DIAMOND NATAKA KULEWA

Ujio mpya wa msanii maarufu zaidi wa kizazi Kipya kwa sasa hapa Tanzania Nasibu Abdul AKA Diamond Platnumz wa nyimbo na video ya NATAKA KULEWA, ikiwa ni kazi yake ya kwanza baada ya kufanya mabadiliko makubwa kwa uongozi unao simamia kazi zake, kwa sasa yuko chini ya Meneja anayejulikana kwa jina la Ragey Mohamed.

Siku za hivi karibuni kupiti mitandao ya kijamii yamesemwa mengi kuhusu nyimbo hii pamoja na video yake. Wengi wakidai kuwa Kijana amefikia mwisho lakini M2S Songs & VIDEO Review Unit  wanakuhakikishia kuwa kijana bado yuko vizuri kwa kukuletea moja kwa moja kupitia blog hii nyimbo, Video na mashairi ya nyimbo yenyewe. Lazima nikiri kuwa tokea nianze kusikiliza sijachoka kuisikia na video yake inayodaiwa kuongoza kwa kugharimu pesa nyingi mpaka sasa hapa Tanzania.

Nyimbo hii ya Nataka Kulewa imefanyika A.M Records chini ya Usimamizi wa Maneke (Producer), Mirindimo ya nyimbo hii ni ya Kiafrika inayorindima kwa kufuata staili ya Bondeni (South Afrika) huku Diamond akiwa anapita kwenye nyimbo hii kwa stail ya aina yake mashairi yakiwa yana zungumzia kwa nini anataka kulewa. Kwa ufupi anajaribu kuchukuwa taswira ya mwanaume ambaye ametatizwa au kutendwa kwenye mahusiano. Katika moja ya mistari analalama kuwa kusema “kumbe mjinga ni mimi ninaye tunza na wengine wanachukuwa, ho o mapenzi, yamenifanya ni lie kama mtoto, mie siwezi walionikuta waache ni seme jina.” Kwenye ubeti wa pili kwa hisia kubwa anabainisha “Ni kwa mapenzi mskini nikamvisha na pete kwa kutaka kumuoa, kukata vilimi limi vya wazushi wanawake wanamponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, siye tuko kama ishirini mabuzi vingasti wengine anawahonga”

Nyimbo hii ni tofauti na nyimbo za awali za msani huyu kama vile NALIA NA MENGI, KAMWAMBIE, MBAGALA na NITAREJEA. wimbo huu una tempo ya juu na hivyo kuufanya kutimiza malengo ya kuchezeka pamoja na kusikilizika. Tatizo kidogo ni kufanana kwa milindimo na merodi hasa mianguko na nyimbo yake iliyofanywa na Rama inayojulikana kwa jina la MOYO WANGU.

kwa Kwa kusikiliza bonyeza kitufe hapo chini ujipatie nyimbo pamoja na video huku ukifwatilia mashairi ya nyimbo hii. Kwa ujumla nakushauri usikilize nyimbo hii ambao M2S wameipa alama 4/5. Video yake nayo imepewa 4/5 ambayo imefanywa na an i-View Studios Director akiwa Ragey Mohamed.

UKITAKA AUDIO BOFYA HAPA

UKITAKA AUDIO BOFYA HAPA

 

DARAJA {Bridge}

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

UBETI WA KWANZA:

Usiniulize kwa nini? Sababu utazengua, ukitaka jiunge na mimi, kama ni pesa ww kunywa nitanunua, mie mwanzo sikuamini, nikajuaga vya kuzua, kumbe mjinga ni mimi, ninaye tunza  wenzangu wanachukuwa, ahi! oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, mie siwezi walionikuta waniache ni seme jina. oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, na nina mengi yamenikaa moyoni.

KIITIKIO:

Leo nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa, zikipanda nimwage radhi, nataka kulewa, lewa mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa, zikipanda nimwage ladhi

DARAJA {Bridge}

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

UBETI WA PILI:

Ni kwa mapenzi mskini, nikamvisha na pete kwa kumuoa, kukata vilimi limi vya wazushi wanawake wanamponda, kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua, sie tuko kama ishirini, mabuzi vingasti wengine anawaonga, oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, mie siwezi walionikuta waniache ni seme jina. oh mapenzi, mapenzi yalinifanya kama mtoto nilie vibaya, na nina mengi yamenikaa moyoni.

KIITIKIO:

Leo nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa, lewa zikipanda nimwage ladhi, tilalila nataka kulewa, lewa, mie nataka kulewa, lewa, nataka kulewa lewa, zikipanda nimwage ladhi

DARAJA {Bridge}:

Haya yayaya-ya,  ww niache niende ye niende ye, Haya yayaya-ya,  niache niende ye niende ye

Mashairi haya ni kama yalivyonukuliwa na M2S Songs Review Unit wakiwa wanausikiliza wimbo wenyewe. Sio mashairi rasmi, kwa maana kutoka kwa mtunzi na muimbaji mwenyewe.

TUNAWEZA BLOG ADVERT3

Advertisements