FURSA YA WADAU KATIKA SEKTA YA TAMTHILIA NA FILAMU

TSCM tangazo

Hii ni fursa ya wadau katika sekta ya tamthilia na filamu, wakiwemo watayarishaji chipukizi na wakongwe kuongeza ujuzi wao.
Mafunzo hayo ni ya muda mfupi. Baadhi ya vitu vitakavyo fundishwa ni pamoja naSCRIPT WRITING – WIKI 4
Uandishi wa filamu, Screenplay au script ni kazi inayoandikwa na screenwriters kwa ajili ya filamu, video game, au vipindi vya televisheni.

VIDEO EDITING – WIKI 4
ni mchakato wa kuhariri picha tofauti za video ili kukamilisha simulizi. Pia uweka special effects na kurekebisha sauti wakati wa post-production

CAMERA OPERATIONS – WIKI 4
Katika filamu, anaitwa cinematographer, kwenye uzalishaji wa video anajulikana televisheni kamera operator, mtu huyu kulingana na mazingira na teknolojia ni wataalamu wa kamera

FILM DIRECTING – WIKI 4
Ni mtu ambaye anaongoza maamuzi ya filamu. Ni mdhibiti wa filamu na wasanii kwa kuhakiki script inafuatwa kwa kuwaelekeza technical crew na watendaji katika kutimiza maono hayo.

Chuo kinapatikana maeneo ya Mikocheni B, karibu na kituo cha Polisi au wasiliana nasi; +255714 421188, +255777919918 E-mail:- tanzaniaschoolofcreativemedia@gmail.com

 

Advertisements

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM HANDENI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
Wananchi wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana  wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83 vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vumba vya maabara za shule ya sekondari Kwaluguru.
Mbunge wa Jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara vya sekondari ya Kwaluguru.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma ya asili ya wazigua  .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika ambapo aliwaambia wajifunze kupima mambo ya viongozi wa siasa wasije wakaingizwa kwenye matatizo bila kutarajia kwani wapo zaidi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si ya wananchi ndio maana wanadiriki kutangaza maandamano wakati wao wenyewe hawapo wameenda nje ya nchi kupumzika.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakazi wa Handeni kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Handeni ambapo aliwaambia watu wanatakiwa kupewa fursa na kurahisishiwa maisha yao hivyo kodi ndogo zinatakiwa ziangaliwe upya kwani zimekuwa kero kwa wafanyabiashara ndogo ndogo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na madereva wa boda boda wa Chanika Handeni Watu wakiwa wamemzunguka Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kumaliza mkutano wake Soko la zamani Chanika wilayani Handeni.

WAZANZIBARI WAHADHIMISHA MIAKA 50 YA ELIMU BILA MALIPO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Msaidizi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Maulid Nafasi Juma wakati wa Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi waliopita mbele ya jukwaa la viongozi katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

KINANA HUYO…. AMALIZA WIKEND YAKE ORKESUMET LEO MERERANI

Wananchi wa Kijiji cha Kitwai A wakiwa wamenyoosha mikono juu,kwenye mkutano wa hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono jambo Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka,katika suala zima la Utekelezaji wa Ilani ya CCM .
Baadhi ya Wanahabari pichani kati Kulia ni Mwinshehe kutoka gazeti la Jamboleo na Mary kutoka Gazeti la Nipashe wakiwa sambamba na wafuasi wa chama cha CCM,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kitwai A,wilayani Simanjiro mkoani Manyara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao 30,mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka wakati akiangalia josho la ng’ombe la Orkirung’rung ambapo  kuna mradi wa ufugaji wa ng’ombe chotara ambao ni ufugaji wenye tija na unasaidia sana kuongeza thamani mifugo.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.Ole Sendeka akifafanua jambo Kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani),kuhuasiana na Mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa (Nyama na Maziwa),wakati akiangalia josho la ng’ombe la Orkirung’rung ambapo  kuna mradi wa ufugaji wa ng’ombe chotara,ufugaji wenye tija na unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
Pichani mbele ye bango kulia ni jengo la Mama na Mtoto la kituo cha Afya Orkesument,Wilayani Simanjiro,ambalo pia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikagua.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimsikiliza Dkt.Juma Nahonyo wakati wa ukaguzi wa jengo litakalokuwa bohari ya Dawa katika kituo cha Afya cha Orkesument,kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka 

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa Kikundi cha Mazingira kilichopo mjini Orkesument,Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.Kikundi hicho kitatumika kueleimisha wananchi wa mji huo katika masuala ya usafi na kulinda mazingira,kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mambo ya maambukizi ya UKIMWI,masuala ya Rushwa na mengineyo. 

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa Orkesument kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo wilayani Simanjiro,Kinana aliwaeleza wananchi hao kuwa ahadi za Rais zilizoahidiwa 2010 zitatekelezwa kwa zilivyoahidiwa kwa wananchi wa Simanjiro,pia aliwasisitizia wananchi hao kutochagua viongozi wa vijiji wa hovyo ambao mwisho wa siku ndio wanaoleta mikorogo na migongano kwa wananchi kwa kuuza ardhi,hali inayoleta migogolo isiyokwisha kila siku.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakielekea kukagua jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,wilayani Simanjiro

 Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka akitetea jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Kitwai A,Simanjiro mkoani Manyara.

Mdau akifuatilia jambo

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM,wilayani ya Simanjiro,Ndugu Brown Ole Suya pamoja na  Mbunge wa jimbo la Simanjiro,Mh Christopher Ole Sendeka .

Jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A,wilayani Simanjiro lililozinduliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana

TIMU YA WABUNGE YAJICHIMBIA ARUSHA KWAAJILI YA MAZOEZI

IMG_0890Timu ya WABUNGE mpira wa miguu wakifanya mazoezi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
IMG_0879Mwenyekiti wa timu Idd Azan akijiweka sawa kwaajili ya mazoezi
IMG_0885
IMG_0891
IMG_0894Halima Mdee ndani ya pushup
IMG_0892Timu ya wabunge mpira wa pete wakifanya mazoezi
IMG_0902TIMU YA WABUNGE  ya mpira wa miguu  imeahidi kurudi na kombe katika michuano ya kombe la mabunge la Jumuiya ya Afrika mashariki yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Disemba 8 huko kampala nchini Uganda.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ambapo timu hizo za mpira wa miguu na mpira wa pete zimeweka kambi mwenyekiti wa timu Idd Azan alisema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wabu nge karibu wote ambao wanaunda timu hizo wameshafika kambini tayari.
 
Kikosi hicho kilichopo chini ya kocha Kassimu Mjaliwa ambaye ni naibu waziri wa tamisemi kinaundwa na wachezaji kumi na tano ambao ni wabunge na wachezaji sita ambao ni watumishi wa bunge.
 
Azan alisema kuwa kilichopelekea kwa timu hiyo kushindwa kuchukua ubingwa ni timu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweka idadi kubwa ya Watumishi huku ikichezesha  wabunge sita tu ambapo kwa mwaka huu utaratibu huo umefutwa.
 
“Mwaka jana tulishindwa kuchukua ubingwa kutokana na timu uliyocheza nayo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchezesha watumishi wengi na idadi ya wabunge ni sita tu lakini kama wangechezesha wabunge tu ushindi ulikuwa uwe wa kwetu”alisema Azan
 
Kwa upande wake katibu wa timu hiyo Waziri Kizingiti alisema kuwa wamefurahia maandalizi na na jumla ya wanamichezo 45 lakini baada ya mazoezi wachezaji 35 wanaounda timu zote mbili wataondoka kuelekea nchini Uganda.
 
Kizingiti alisema kuwa changamoto kubwa ni muda mdogo wa mazoezi kutokana na ratiba za Wabunge lakini kutokana na mazoezi mazuri na mafundisho ya Kocha wana imanoi kuwa Kombe hilo litarudi nyumbani Tanzania.
 
Aidha aliongeza kuwa katika mechi ya Ufunguzi ambayo itachezwa tarehe 9 bunge la Tanzania itacheza na timu ya Wabunge kutoka Nchini Kenya.
 
Naye kaptein wa timu ya wanawake Grace Kiwelu alisema kuwa mazoezi yanaendelea vizuri na kila kitu kinakwenda sawa na kwamba kombe hilo bado litarudi nyumbani Tanzania.
Timu ya Bunge ya wanawake  ya mpira wa Pete ilichukua ubingwa katika mashindano yaliyopita na timu ya Wanaume ya mpira wa miguu ilichukua nafasi ya pili

THE CITIZEN BUREAU CHIEF ZEPHANIA UBWANI WON A TOP AWARD IN THE MEDIA

Ho.Amama Mbabazi The Prime Minister of Uganda(6th from right in the group pictures with winners of 6th East Africa Community and East Africa Bussiness Council at Munyonyo,Kampala,Uganda

Kampala. For the second year running, The Citizen Bureau Chief in Arusha Zephania Ubwani has won a top award in the media contest organized by the East African Community (EAC) and the East African Business Council (EABC).

Mr. Ubwani emerged the first in the Higher Education Reporting Award ahead of two other contestants from Burundi and Rwanda during the prize giving ceremony at a Kampala hotel on Thursday evening.

Eleven other journalists from all the five EAC partner states; Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi and Rwanda were feted and took home certificates, plaques, iPads as well as cash prizes.

The Citizen journalist was the only from Tanzania to enter the finals of the race this year. In all there were 12 finalists in the seven categories contested.

The National Media Group (NMG) scooped most of the awards through its popular titles; The East African, Daily Nation, Daily Monitor, The Citizen and NTV.

The overall winner was Ben Agina from NTV who won the EAC Secretary General’s Award for his exclusive coverage which saw him travelling across the region to expose a host trade cumbersome barriers.

Mr. Ubwani’s winning article was on an initiative taken by EABC and the Inter University Council on East Africa (IUCEA) to link the academic and research institutions and the industry in order to create jobs, enhance production and boost economy.

Last year, the Arusha-based journalist won an award in the Health Reporting Category. He is the only Tanzanian journalist so far to win the EAC Media Awards introduced some years ago.

Other top winners were Christabel Ligami of The East African ( Health Reporting and Business and Financial Reporting categories) and Daily Nation’s Joshua Masinde (Agriculture and Food Security)

NMG journalists who emerged runner-up were Dorothy Nakaweesa (Daily Monitor), Lydia Namono (Daily Monitor), Patrick Mayoyo (Daily Nation), Dicta Asiimwe (The East African). The latter was a runner’s up in two categories.

A young Rwandan journalist with The New Times Eric Kabeera was an impressive lot. He emerged first in two categories ( Environmental Reporting and Political Federation) and came third in Higher Education category which was won by The Citizen.

Other winners were Eric Nsengiyumva from a Burundi media outlet called IGIHE and Isaac Mwangi of the East African News Agency (Eana).

The Uganda prime minister Amama Mbambazi, EAC secretary general Dr. Richard Sezibera, EABC executive director Andrew Luzze graced the ceremony at the Munyonyo Commonwealth Resort.

Mr. Ubwani joined Mwananchi Communications Limited (MCL) which publishes The Citizen on September 1st, 2004 and was  posted to Arusha in the same capacity. He has consistently been reporting on EAC integration matters.

DIAMOND KUWASHA MOTO ARUSHA “USIKU WA WASAFI”

diamond.....
Msanii  maarufu wa muziki wa Kizazi kipya Diamond Platnum anatarajiwa kufanya  shoo ya aina yake jijini  Arusha  siku ya Jumamosi  ya  tarehe 30 katika viwanja vya Hoteli ya Mount Meru ijulikanayo kama “ usiku wa wasafi”
 
Muandaaji wa shoo hiyo,Mkurugenzi wa kampuni ya Mwandago Investment Faustine Mwandago akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Arusha jana alisema kuwa maandalizi  ya awali ya shoo hiyo yamekamilika kwa kiasi kikubwa 
 
Mwandago alisema kuwa  shoo hiyo itakuwa ya kukata na shoka  na itawapa burudani ya kutosha mashabiki wa msanii huyohivyo kuwataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi siku ya jumamosi
 
 “kwa hapa Arusha Diamond tumezoea kumuona  kwenye shoo za Mamiss kama Miss Arusha na nyinginezo lakini kwa sasa hivi anakuja kwa ajili ya kutoa burudani tu kwa mashabiki wake hivyo naamini kuwa shoo hiyo itakata kiu kwa watakaohudhuria.”alisema mwandago
 
Mbali na burudani kutoka kwa msanii huyo wasanii chipukizi kutoka jijini hapa watapata nafasi ya kumiliki jukwaa hali itakayopelekea vipaji vyao kutambulika
Wasanii hao chipukizi ni Marry,Kandisi,Roggerz na madansa wa boda 2 boda waliopo chini ya Mwandago Investment watapamba shoo hiyo.
 
Katika kunogesha shoo ya Diamond  dress code itakuwa vazi jeupe kuendana na jina la shoo la Usiku wa Wasafi

P SQUARE NDANI YA DAR

 Wanamuziki wanaotajwa kuwa na mvuto zaidi barani Afrika, P Square, wamewasili usiku huu katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere  kwa ajili ya onesho lao linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika viwanja va Leaders Club maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pichani juu ni Petter(wa pili kutoka kushoto na Paul).Kulia ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East africa Radio na TV
 Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao
Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea…
Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi

ARUSHA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA TAMSHA LA ARUSHA FESTIVAL

DSCF0769

Mshauri mkuu wa vipindi vya Radio 5 David Rwenyagira akiongea na vyombo vya habari jana  kuhusu Tamasha la Arusha Festival linalotarajiwa kuanza rasmi tarehe 14/10/2013 jijini hapa lenye lengo la kuenzi kazi za Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere

DSCF0766

Kulia niMkurugenzi wa kampuni ya Shining Stars LTD  Ibbrahim Thabit katikati Sarah Keiya Meneja masoko wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha na Lalit Sharma Meneja maoko PEPSI

DSCF0795

Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akiwaelezea  waandishi wa habari wasanii watakaopamba Tamasha hilo kuwa ni Jambo Squared,Watoto wa simba,Ngoma za Asili na wengine wingi.

DSCF0794

Katika Tamasha hilo pia watapiga vita ujangili pamoja na matumizi mabaya ya Maliasili na Rasilimali kwakuwa Baba wa Taifa enzi ya uhai wake  alikuwa Mstari wa mbele

DSCF0771

DSCF0775

David Rwenyagira akisisitizia jambo kuhusu Tamasha hilo ambapo alisema litaanza kwa maandamano katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid”Stadium”jijini Arusha kuelekea katika uwanja wa General Trye

DSCF0773

Baadhi ya waandishi wa habari wakifanya kazi yao

DSCF0799

Hapa wadhamini wa Tamasha hilo wakaamua kugonga cheers kuashiria tamasha hili litakuwa la kukata na soka

DSCF0796

DSCF0801

Wasanii wa  muziki wa kizazi kipya Jambo Squared wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Arusha Festival linalotarajiwa kufanyika October 14 katika viwanja vya General trye mkoani Arusha.
 
Akizungumza na vyombo vya habari moja kati ya waandaji wa tamasha hilo Devid Runyagira kutoka Tan Communication Media ambao ni wamiliki wa redio 5 Arusha alisema kuwa tamasha hilo ni maalum kwa ajili ya kumuenzi baba wa taifa pamoja na kazi alizokuwa akifanya hivyo kutumia fursa hiyo kukaa pamoja na wananchi ili kudumisha umoja na mshikamano.
 
“Mkoa wa arusha una watu wengi sana hivyo tunatumia siku hii maalum ambayo ni Nyerere Day kukutana pamoja na kushiriki michezo mbalimbali ili kudumisha umoja wetu ambao hayati Baba wa Taifa aliusisitiza”alisema devid
 
Alisema tamasha hilo litaanza kwa maandamano ya amani kutoka katika viwanja vya sheikh Amri Abeid Stadium majira ya saa mbili asubuhi hadi katika viwanja hivyo ambapo pia viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuwepo akiwemo Mkurugenzi wa shirika la hifadhi la Taifa (TANAPA) Allan Kijazi.
 
Mbali na wasanii hao burudani nyingine ni pamoja na ngoma za asili kutoka kwa Watoto wa Simba na African Culture na michezo mingine mingi ikiwemo ya watoto.
 
Kwa upande wake Vicky Mwakoyo alisema kuwa wasanii wachanga ambao hawajapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao  watapata fursa ya kufanya hivyo siku hiyo na zawadi mbalimbali zitatolewa kwawashindi ambao watatangazwa katika michezo mbalimbali.
 
Mwakoyo alisema kuwa kiingilio ni bure kwa watakaoingia mapema kwa maandamnao baada ya hapo watoto watalipa shilingi 500 na watu wazima shilingi 1000 ambayo itatumika kufanya usafi uwanjani hapo.
 
Wadhamini wa tamasha hilo ni Kibo Palace Hotel,Pepsi,KK security,Radio 5,Shed and Sons,Shining Stars,DSTV na Trinity.

MAJANGILI MWISHO WAO UMEFIKA….ASEMA BALOZI KAGASHEKI

Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)Bw.Allan Kijazi(T shirt nyeupe)akisalimiana na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro leo kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wakati wakimsubiri Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki kuongoza maandamano ua kupiga vita ujangili wa Tembo nchini
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki(wa pili kushoto)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators(TATO) jana kwenye uwanja wa ndege Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki(kushoto)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo na viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators(TATO) jana kwenye uwanja wa ndege Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki(wa pili kulia)akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(kulia) na viongozi wa Tanzania Association of Tour Operators(TATO) kwenye maandamo ya kupinga ujangili wa Tembo nchini.
Wadau wakiwa wa Mali Hai Arusha wakiwa katika picha ya pamoja

 


Na Mwandishi Wetu,Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki amesema serikali ya Rais Jakaya Kikwete haitakubali utalii ufie mikononi mwake kwa kuwaacha majangili kutamba kwa kuwaua hovyo wanyama mbalimbali hasa Tembo kwenye Hifadhi za taifa nchini.

Balozi Kagasheki leo ameongoza maandamano makubwa ya wadau wanaopinga vitendo nya ujangili vinavyohatarisha uwepo wa Tembo  kwa mika 15 ijayo kama hatua mahususi hazitachukuliawa.


“Sasa hakutakuwa na suala la wanaharakati kutaka kesi ziharakishwe mahakamani kwasababu maafisa wetu wakikutana na majangili huko porini mambo yatakua yanaishia huko huko,”alisema Kagasheki


Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya AICC Kijenge ,Mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa maandamano hayo ya Tanzania Association of Tour Operetors(TATO)Willy Chambuso alisema kuna kila sababu ya serikali ya Tanzania kuzungumza na serikali ya China ambako kumeonakana ni soko la pembe za Ndovu.Picha na Habari na http://www.rweyemamuinfo.blogspot.com

community-herder.gif

MKUTANO WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA WAKWAMA.

m2s breaking news

Habari zilizo tufikia hivi punde zinasema mkutano ambao ulikuwa ufanyike leo wa Halmashauri ya jiji la Arusha umeshindwa kufanyika baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Gaudience Lyimo kuugomea kwa madai kuwa akuwa na taarifa nao.

Duru za kisiasa zinadai kuwa mkutano huo ndiyo ulikuwa uweke wazi mbivu na mbichi kuhusiana na SAKATA la Mgogoro wa mradi wa taa za barababani kati ya Kampuni ya Skytel ya Arusha na Halmashauri  ya Jiji la Arusha.

WARSHA YA UELIMISHAJI JUU YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA SEKTA YA UZIDUAJI YAFANYIKA MWANZA

DSCF0557

Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Hakimadini Bw.Amani Mhinda akitoa mada katika warsha ya siku 3 kuhusu Utekelezaji wa EITI inayofanyika jijini Mwanza septemba 30 hadi Oktoba 2 ,2013 ,washiriki 41 kutoka maeneo ya madini kanda ya ziwa walihudhuria

DSCF0579

Bw,Silas Olan’g mchumi wa Taasisi ya Revenue Watch akitoa mada kwenye warsha ya siku tatu iliyowashirikisha wachimbaji wadogo,viongozi wa vyama vya wafanyakazi ndani ya migodi,viongozi wa dini,waandishi wa habari,AZAKI  na wawakilishi wa makampuni.

DSCF0575

Afisa Uratibu(TEITI) Athumani Kwariko akitoa akitoa ufafanuzi wa TEITI na namna inavyofanya kazi zake katika warsha ya Uelimishaji juu ya Utekelezaji wa EITI

DSCF0566

Viongozi wa dini wakifatilia warsha kwa ukaribu

DSCF0562

“Tunafatilia mada”Baadhi ya washiriki kutoka kanda ya ziwa wakifatilia warsha

DSCF0561

DSCF0570

Washiriki wa mafunzo

DSCF0574

DSCF0572

Meneja wa kodi na mahusiano, Godvictor Lyimo kutoka kampuni ya Geita Gold Mining LTD ambaye pia ni mwakilishi wa chama cha wachimbaji wakubwa Tanzania akifatilia mafunzo

DSCF0578

DSCF0581

DSCF0557

Warsha hiyo iliandaliwa na Mashirika manne,Hakimadini,TEITI,Revenue Watch,COWI

KIKAO CHA BUNGE LA AFRIKA MSHARIKI CHAVUNJIKA

Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya aliyewasilisha hoja binafsi kwenye bunge la EAC leo
Sakata la vikao vya Bunge la Afrika Mashariki kufanyika kwenye nchi wanachama kwa mzunguko limeingia katika sura mpya baada ya kikao  cha leo jioni kuvunjika kufuatia Spika wa Bunge hilo,Magreth Zziwa Nantongo kukataa hoja binafsi ya mbunge kutoka Kenya Peter Mathuki aliyetaka utaratibu wa zamani kufanya vikao kwenda nchi wanachama uendelee.
 
Mbunge alimama na kuomba kuwasilisha hoja hiyo ambayo Spika aliitupilia mbali kuwa haina mashiko na kusababisha wabunge kutoka Rwanda kutoka nje ukumbi wa bunge yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.
 
Spika alitoa mapumziko na mashauriano ya dakika 15 na aliporejea wabunge wapatao 14 tu ndio walikubali kuingia ukumbini huku wengine wakigomea uamuzi wa Spika kukataa hoja ya mbunge kuwasilishwa na kuamua kuahirisha bunge hadi kesho.
 
Wabunge wanaounga mkono vikao kufanyika Arusha wanadai kuwa ni jambo la busara kutokana na kuwa ndio makao makuu ya EAC na fedha nyingi zimetumika kujenga makao hayo na iwapo vikao vya bunge vitafanyika kwa kuzunguka nchi wanachama zitatumika fedha nyingi kulipia kumbi za kufanyia vikao hivyo fedha ambazo zingetumika kwa shughuli za maendeleo.
 
Kwa upande mwingine wanaotaka vikao vya bunge vifanyike kwa mzunguko wanajenga hoja kuwa itasaidia kujenga uelewela wa mtangamano kwa wananchi na taasisi za kiraia kufatilia mwenendo huo kwa karibu.
 
Mbunge wa Tanzania,Nderakindo Kessy alipotakiwa kutoa maoni yake alisema jambo hilo limechukua sura mbaya na anayeweza kulizungumzia ni Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Adam Kimbisa ambaye hakuwepo na alipotafutwa Katibu wake Shyrose Bhanji alikua kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi.

RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO YARUDI HEWANI

TCRA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO

1.0 Utangulizi:

Mnamo tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za Utangazaji.

Kamati ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-

a) Vituo vyote vilipewa onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;

b) Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za utangazaji.

2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo
na Mamlaka ya Mawasiliano:

Baada ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani “Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla ya kuvifungulia.

3.0 Kurejeshwa kwa Matangazo

Kamati ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.

Kamati ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji. Kamati ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia leseni zao.

Kamati ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na kudumisha amani nchini.

Eng. Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013

KUHUSU KAMATI YA MAUDHUI:

1.0 UTANGULIZI:

1.1. Kamati ya Maudhui ni kamati iliyoundwa kwa mujibu wa sehemu ya IV kifungu cha 26 (1) cha Sheria Namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, na marekebisho yake katika kifungu 173 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) Mwaka 2010

Kwa mujibu wa sheria, majukumu na kazi za Kamati ya Maudhui ni pamoja na:-

(a) Kumshauri Waziri wa Sekta kuhusiana na Sera ya Utangazaji nchini;
(b) Kushughulikia malalamiko kutoka kwa watangazaji na watumiaji wa huduma za utangazaji nchini;
(c) Kusimamia na kuhakikisha kuwa kanuni za utangazaji zinafuatwa.
(d) Kusimamia na kufuatilia maudhui ya vituo vya utangazaji.

1.2. Kamati hii ilianza kazi zake Oktoba 2012 baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (MB) tarehe 4 Desemba, 2012.

1.3. Kamati ya Maudhui inaundwa na wajumbe watano. Wanne ni wateuliwa wa Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Utangazaji na Mwenyekiti ambaye huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya TCRA. Muundo huo umetolewa na sehemu ya 26 (2) ya Sheria ya TCRA ya Mwaka 2003.

Majina ya wajumbe ni kama ifuatavyo:-

i. Mhandisi Margareth Munyagi -Mwenyekiti
ii. Bwana Walter Bgoya -Makamu Mwenyekiti
iii. Bwana Abdul Ngarawa -Mjumbe
iv. Bwana Joseph Mapunda -Mjumbe
v. Bwana Yusuf Nzowa -Mjumbe

Joyce_0246

POLISI WATOA TAMKO JUU YA PONDA

 Sehemu ya kodonda katika bega la Sheikh Ponda baada ya kushinwa nyuzi.
  Katibu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, akiwa katika Wodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akitibia jeraha alilopata jana akidaiwa kupigwa risasi mjini Morogoro.
 Sheikh Ponda akiwa hospitalini hapo na jeraha katika bega la mkono wa kulia.
Sheikh Ponda akiwa na msaidizi wake hospitalini hapo.
TAMKO LA JESHI LA POLISI KUHUSU SHEIKH PONDA ISSA PONDA
 
1.  MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO,  KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA  ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.
2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA  MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA  ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA  ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.
3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA  MAWE ASKARI.  KUFUATIA PURUKUSHANI  HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.
4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA  MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.
5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI  CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.
6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA  WITO KWA  WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi

RAIS WA VILABU TANZANIA ATEMBELEA APC

DSCF0208Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Arusha(APC) Claud Gwandu akimkaribisha Rais wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania kutoka (UTPC) Keneth Simbaya katika ofisi za chama hicho

DSCF0207Viongozi wa chama hicho wakimsikiliza Rais wa vilabu

DSCF0204Rais Keneth Simbaya akiongea na viongozi wa chama cha waandishi wa habari Arusha(APC)DSCF0215Hapa nikishow love na mwandishi mkongwe Edward Selasini katika ofisi za APC

DSCF0210Hapa Rais akipatiwa zawadi na mjumbe janeth Mushi

DSCF0211Hapa Rais akisoma zawadi ya T-sheti aliyozawadiwa na Arusha Press Club….alionekana kufurahia sana zawadi hiyo na kuhaidi ushirikiano kwa club hiyo

SUMMAYE AWASHUKIA WANASIASA,ASEMA WANAWATUMIA VIJANA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA

DSCF0217WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Summaye akisoma hotuba kwa vijana waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Tanzania Youth Development Center jijini hapa,

DSCF0218Vijana wakifatilia hotuba

DSCF0221Mama nice(aliyevalia kitenge)akisikiliza hotuba kwa makini

DSCF0219Waalikwa mbalimbali wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi

DSCF0229Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kikazi zaidi

DSCF0223

DSCF0227WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Summaye amekemea tabia ya wanasiasa
nchini  kuwachanganya vijana na viongozi wa serikali kwa kuwashawishi
vijana kwa rushwa na na kuwatumia katika kusafirisha madawa ya kulevya
katika maeneo mbalimbli nchini na nje ya nchi.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa taasisi ya Tanzania Youth Development Center jijini hapa, Sumaye alisema tatizo la rushwa limekuwa likikuwa kwa kasi kubwa nchini kwa wanasiasa na viongozi wenye nyadhifa serikalini,kwa kutumia fedha zaokuwatumia vijana ambao wamekuwa chambo ya kusafirisha madawa hayo huku wakilipwa fedha ndogo ambapo baada  ya mda wanakamatwa na wao kunufaika mabilionea kupitia njia hiyo.

“hili tatizodawa za kulevya limekuwa likiwaathiri kwa sehemu kubwa
vijana wa nchi hii ambao ndio nguvu kazi ya taifa letu,wanasiasa
tuache hii tabia ya kuhonga vijana na taasisi hii tukiwapa masharti
yenye malengo yetu ya siasa tutakuwa tunajaribu kuwaondoa katika
malengo ya msingi ya taasisi yenyewe”alisema Sumaye

Sumaye alisema rushwa ya madaraka ina athari kubwa kwa umma na nchi ni
ile inayotolewa katika kusaka madaraka ya kisiasa ambapo mara nyingi
anayefanya hivyo amekuwa na uchu na uroho wa madaraka na yuko tayari
kufanya lolote na chochote ili apate  madaraka anayoyahitaji.

“vijana msikubali kutumia miili yenu kubebea madawa ya kulevya kwani
yanawaathiri kwa asilimia kubwa na mara nyingi tumeshuhudia wengine
wakifanyiwa upasuaji na badala yake wamekuwa wakipoteza maisha”alisema
Summaye

Aidha alisema kuwa kitendo cha vijana kutumiwa kama chambo cha
kusafirisha madawa ya kulevya nje ya Nchi ni unyanyasaji
mkubwa,unyama,kwani mwisho wa siku wanaonufaika ni wengine na wao
kubaki kuwa masikini.

Pia alisema rushwa imekuwa ikitumika katika nyakati za uchaguzi na
wananchi wamekuwa wakinunuliwa kwa njia mblimbali na wengine kubaki
wakiwa maskini wakati wana siasa wanapohitaji kupandishwa vyeo.

“ lazima tujiulize unawanunua wapiga kura ili iweje? Kama unajiamini
kuwa wewe unafaa kwa nafasi hiyo kwanini usiwaache wapiga kura
wakaamua bila vishawishi vya rushwa? Dalili kubwa ni kuwa kama
unatumia vishawishi vya rushwa wewe hutoshi katika hiyo nafasi
vinginevyo ungewaacha wapiga kura waamue wapendavyo,”alisema.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Lengai
Sabaya, alisema taasisi hiyo imeshaanzisha matawi kote nchini ili
kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri wenyewe, kupambana na
magonjwa hatarisi ikiwemo ugonjwa wa Ukimwi.
“Vijana walioshiriki katika uzinduzi huu ndugu mgeni rasmi wanatoka
katika kanda ya kaskazini na ni wenye umri wa kuaznia mika
15-35”alisema Sabaya

Alisema pia malengo mengine ya taasisi hiyo ni pamoja na kupambana na
dawa za kulevya, uchafuzi wa mazingira, rushwa ufisadi na uovu
unaosababishwa na madhara ya dawa za kulevya na kwamba ndoto kubwa ya baadae ni kusaidia vikundi vidogo vya maendeleo na kutoa ushauri wa
kitaalum katika kunufaisha maendeleo kwa vijana.

RADIO 5 WANG’ARA MAONYESHO YA NANE NANE WASHIKA NAFASI YA KWANZA

 Wafanyakazi  wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 kushoto ni Semio Sonyo ,Sarah Keiya meneja masoko,katikati ni David Rwenyagira na Deo Gee wakifurahia  kikombe cha ushindi ambapo jana waliibuka washindi wa kwanza kwenye maonyesho ya 20 ya Nane nane kwa kanda ya kaskazini,yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha

Meneja masoko wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio5 Sarah Keiya pamoja na Dadiv Rwenyagira wakiwa wameshikilia kikombe mara baada ya kuibuka washindi wakwanza maonyesho ya 20,ya nane nane kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha