BAADHI YA PICHA AMBAZO ZIMO KWENYE KICHUPA CHA MWANA FA KIBOKO YANGU

10838631_330848257125108_963639433_n

Ali Kiba, akiwa amezungukwa na warembo huku Binamu akionekana kwa nyuma kwenye moja ya scene ya video itakayo julikana ‘Kiboko Yangu’ ambayo Binamu aka The Choir Master, amemshirikisha Ali Kiba, video hiyo imefanyika jijini Nairobi.

 

10831918_502390816567545_505425812_n

Ali Kiba, akiwa amezungukwa na warembo kwenye moja ya scene ya video itakayo julikana ‘Kiboko Yangu’ ambayo Binamu aka The Choir Master, amemshirikisha Ali Kiba, video hiyo imefanyika jijini Nairobi.

 

ka

Ali Kiba, akiwa na  Binamu aka The Choir Master, kwenye moja ya scene ya video itakayo julikana ‘Kiboko Yangu’, video hiyo imefanyika jijini Nairobi.

 

as

a

Ali Kiba, akiwa na Binamu aka The Choir Master, kwenye moja ya scene ya video itakayo julikana ‘Kiboko Yangu’, video hiyo imefanyika jijini Nairobi.

 

Advertisements

MOVIE REVEW: – PICHA YA SAVING PRIVATE RYAN (1998).

Saving_Private_Ryan_by_Narusargent

Leo wakati napitia order za movie nimekutana na order ya Saving Private Ryan, nikastuka siyo kwavile haipo kwenye maktaba yangu, la hasha bali mdau wangu amenikumbusha filamu ambayo Motion Picture Arts and Sciences waliipendekeza kuwania zaidi ya tuzo 11 mwaka 1998 huku ikijikusanyia mapato ya zaidi ya dola milioni 481.8 na director wake Steven Spielberg kufanikiwa kupata tuzo ya Second Academy Award ya director bora.

Movi ya Saving Private Ryan (1998) ni moja ya filamu za kivita za Marekani ambayo inaonyesha shambulio la Normandy kwenye vita kuu ya pili ya dunia. Ikiwa imeongozwa na director bingwa Steven Spielberg na kuandikwa na Robert Rodat, filamu hii inasifiwa kwa ubunifu wake hasa katika dakika 27 za mwanzo kwa nanamna walivyo weza kuonyesha uhalisia wa shambulio la Omaha Beach la Juni 6, 1944 na harakati za kapteni wa jeshi la marekani John H. Miller (Tom Hanks) ambaye aliongoza kikosi cha watu 8 kumtafuta James Francis Ryan (Matt damon) mwenye cheo cha Private First Class , huyu akiwa ni miongoni mwa ndugu wanne ambao kaka zake wote walipoteza maisha vitani.

Rodat aliandika filamu script 1994 baada ya kuudhulia kumbukumbu ya mazishi ya ndugu 8 waliokufa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani. Rodat akafikilia kitu kama hicho na kutengenezea story kwenye vita vya pili vya dunia. Script ilikabidhiwa kwa Mark Gordon ambaye alimkabidhi Hanks na baadae kumfikia Spielberg.

Actors                   :               Tom Hanks, Tom Sizemore, Edward Burns, Barry Pepper, Adam Goldberg, Vin Diesel, Giovanni Ribisi, Jeremy Davies, Matt Damon, Ted Danson, Paul Giamatti, Dennis Farina, Joerg Stadler, Max Martini, Dylan Bruno

Directors              :               Steven Spielberg

Countries             :               USA

Release                 :               July 24, 1998

Categories            :               Drama, War, Action

Duration              :               169 Dk.

Budget                   :               70,000,000 usd

Hili ni bonge la movi ambalo si la kukosa.

MOVIE REVEW:- PICHA MPYA “MY MAN IS A LOSER” (2014).

my_man_is_a_loser_2014 two

My man is a loser ni filamu ambayo ni ya ucheshi (comedy) kwa mara ya kwanza ilionyeshwa kwenye big screen Julai 25, 2014. Stori line ya filamu hii ni wanandoa wawili ambao walimwajiri rafiki yao kapera (single playboy) ili awasaidie kuokoa ndoa zao, lakini mambo haya kwenda kama yalivyo tarajiwa …. haikuchukua muda wake zao wakabaki wakijiuliza kama matendo ya waumezao ya sasa ni bora kuliko yale ya awali?

Runtime               :               95 mins

Release Date       :               25th July 2014

Genres                  :               Comedy

Actors              :               John Stamos, Tika Sumpter, Sean Young, Michael Rapaport, Diane Guerrero, Bryan Callen, Carly Brooke Pearlstein, Emilie Kuznicki, Ronnie Mund, Courtney Cooper, Wass Stevens, Heidi Armbruster, Stephanie Domini Ehlert, Dasha Kittredge, Lisa Ferreira, Megan Reinking, Kathy Searle, Takara Sewitt, Maria Bartiromo, Katelynn Bailey, Ava Paloma, Mo Mandel, Libby Winters, Alexandra Stebbins, Tina Marie Connell, Jessica Press, Chella Ferrow, Hyejin J., Stevie Steel, Nicole Neuman.

BARUA YA MUME WA FLORA MBASHA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA

MUME WA FLORA MBASHA

Hii barua ya Mume wa Mwimbaji wa Nyimbo za injili nchini – Flora Mbasha kwenda kwa mchungaji maarufu nchini, Mchungaji Gwajima inakuhusu….

“Mchungaji …yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri’ wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!!

Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??

Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!

Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!

Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!

Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!

Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!! Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!

Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako… na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!! Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??

Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana! Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!! Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!

Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!

Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!

Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!

Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..”

Kwako – Mchungaji Gwajima

SOURCE:- mwanahalisiforum.com

KAZI YA UKAGUZI NA URASIMISHAJI WA KAZI ZA MUZIKI NA FILAMU LAANZA; TRA

Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’ imetoa tangazo kwa tasnia za sanaa ya filamu,muziki, kwa kuanza zoezi la urasimishaji wa kazi za wasanii kwa kuanza kukagua bidhaa za wasanii na kuziwekea stika.

10431899_340541062760789_1672094960_n

Taasisi za Serikali zilizokabidhiwa jukumu la kushughulikia urasimishaji wa tasnia za sanaa ya muziki na filamu, zimeanza rasmi zoezi la kukagua na kukamata bidhaa zote za muziki na filamu ambazo hazina sifa ya kuuzwa na kusambazwa katika soko la ndani na kupelekwa nje ya nchi.

Sheria ya Ushuru wa Bidhaa iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012, na kupitishwa kwa kanuni zake mwaka 2013 inamtaka kila mfanyabiashara wa bidhaa za muziki na filamu kuhakikisha kuwa bidhaa zote za muziki na filamu zinawekewa stempu za Ushuru wa Bidhaa zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kabla ya kusambazwa.

Taasisi za Serikali zinazohusika katika zoezi hili ni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania (TFCB), Chama cha Hakimiliki na Hakishirikishi Tanzania (COSOTA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Taasisi hizo kwa pamoja zimekuwa zikitoa elimu kwa wadau wote wanaojihusisha na utengenezaji, uaigizaji, usambazaji na uuzaji wa bidhaa zinazohusika na muziki na filamu pia kuhakikisha kuwa wanakamilisha mchakato wote wa uwekaji stempu za Ushuru wa bidhaa kwa kazi zinazoingizwa katika soko la ndani na zinazosafirishwa nje ya nchi.

Kwa mujibu wa sheria wahusika wote wa uzalishaji, uagizaji toka nje ya nchi na usambazaji wa bidhaa hizo wanatakiwa kufika kwa taasisi hizo ili kusajiliwa na kukamilisha utaratibu wa kusajili na kukaguliwa kwa kazi husika kabla hazijapatiwa stempu za Ushuru wa bidhaa kwa ajili ya kubandikwa kwenye kazi husika.

Utaratibu unawataka wale wote wanaokusudia kushughulika na kazi za muziki kuanzia BASATA na baada ya hapo kufika COSOTA ambapo huko hupewa vibali kabla ya kwenda TRA ili kununua stempu. Kwa kazi za filamu wahusika wanatakiwa kwenda Bodi ya Ukaguzi wa Filamu kabla hawajapeleka kazi husika COSOTA na baadaye TRA kwa ajili ya ununuzi wa stempu.

Stempu hizi zinapatikana ofisi za Idara ya fedha, Makao Makuu ya TRA. Kila kazi, yaani CD, DVD au kanda zinatolewa stempu mbili zenye namba moja katika mtiririko maalum wa namba (serial number). Stempu moja hubandikwa katika kasha na nyingine kwenye CD, DVD au kanda. Utaratibu unamtaka mhusika anayehitaji stempu kuwasilisha maombi tofauti kwa kila kazi husika. Hairuhusiwi kuweka stempu zilizoombwa kwa ajili ya kazi moja kwenye kazi nyingine hata kama kazi hizo zimetolewa na mzalishaji au msambazaji mmoja.

Aina za stempu na matumizi yake ni kama ifuatavyo:

 • Filamu toka nje ya nchi – rangi ya kijani (green).

 • Muziki toka nje ya nchi – rangi bluu (blue).

 • Filamu zilizotengenezwa ndani ya nchi – zambarau (violet)

 • Muziki wa ndani ya nchi – rangi ya pinki (pink)

MWILI WA MAREHEMU BI SHIDA SALUMU MAMA MZAZI WA ZITTO WASAFIRISHWA

MAMA1

Zitto Kabwe akiwa na Prof  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi.

mama4

Ndege ikiandaliwa ili kuweza kuingiza mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe.

MAMA2

Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi.

MAMA3

Prof. Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwezie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea Kigoma kwenye maziko.

mama5

Rais wa TASWA Juma Pinto akiwa VIP ya Terminal 1 JKN Airport alipokutana na Cardinal Pengo wakati wa kuaga mwili wa Mama yake Zitto Kabwe.

WEMA IBUKA TENA NA TUZO NYINGINE

 • WEUSI, WANAUME FAMILY NI SHIDA ….. ILIKUWA NDANI YA PASAKA DAR LIVE

Mrembo Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa na tuzo yake baada ya kuibuka Ijumaa Sexiest Girl 2013/14 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Wema akiwashukuru mashabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi.

…Akiwapa tano mashabiki waliofurika Dar Live katika Sikukuu ya Pasaka.

Wema, Wema, Wema… mashabiki wakimshangilia ‘Beautiful Onyinye’ baada ya kutangazwa mshindi.

DSC_0116001

 

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa lililokuwa likiendesha shindano la Ijumaa Sexiest Girl, Amran Kaima (kulia) akipozi na mshindi Wema Sepetu. Kushoto ni shabiki wa Wema.

Amran Kaima akielezea mchakato uliotumika kumpata mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl.

Mashabiki wakiwa wamepagawa na shangwe za Dar Live.

Mratibu Mkuu wa kampuni ya Global Publishers, Luqman Maloto akiwakaribisha Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho na msanii Nikki wa Pili kukabidhi tuzo kwa mshindi.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiongea machache kabla ya zoezi la utoaji tuzo.

 

Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili akimtaja mshindi.

Wema Sepetu akiwa stejini baada ya kutangazwa mshindi.

Nikki wa Pili akimkabidhi tuzo ya Ijumaa Sexiest Girl, mrembo Wema Sepetu.

Wema akipozi na tuzo yake.

Wema akicheza wimbo wa Number One ulioimbwa na mpenzi wake Diamond Platnumz baada ya kutwaa tuzo.

Washereheshaji katika usiku wa Pasaka, Pamela Daffa na Benjamin Mwanambuu wakifanya yao stejini.

Said Fella (wa pili kushoto) akiwa na crew ya Madj ndani ya Dar Live.

Dogo Aslay akiwapagawisha mashabiki wa burudani waliofurika ndani ya Dar Live.

…Aslay akijiachia na shabiki wake aliyepanda stejini kumpa sapoti.

…Akimchombeza shabiki mwingine aliyepanda stejini.

Kundi la TMK Wanaume Family likifanya vitu vyao stejini.

Mhe. Temba akiwarusha mashabiki wa Dar Live.

Chegge Chigunda ‘Mtoto wa Mama Said’ akizikonga nyoyo za wana Dar Live.

TMK Wanaume Family wakizidi kulishambulia jukwaa la Dar Live la kupanda na kushuka.

Wana Hip hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini (kulia) na G-Nako wakiwapa raha mashabiki.

Mashabiki wakifuatilia shoo ya Weusi.

Joh Makini kazini.

G-Nako akiwadatisha wapenzi wa Hip hop.

UTPC YAWASHANGAZA WENGI KWA KUPINGA DAUDI MWANGOSI KUJENGEWA MNALA WA KUMBUKUMBU

 • WENYEWE WADAI KAMA UTAJENGWA NA CHADEMA UTAWAPA UMAARUFU CHAMA HICHO.

 • BAADHI YA WANAHABARI WAOJI UTAWAJENGA VIPI CHADEMA WAKATI MNALA HUO UTAKUWA WA MWANGOSI.


Makamu mwenyekiti wa UTPC Bi Jane Mihanji akitoa tamko la UTPC dhidi ya Chadema kutaka kutumia kifo cha Mwangosi kisiasa

Rais wa UTPC Bw Keneth Simbaya kushoto akimpongeza makamu wake Bi Jane Mihanjo kwa tamko zuri alilolitoa

Wajumbe wa bodi ya UTPC wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa juu wa UTPC baada ya kutolewa tamko la kupinga uamuzi wa Chadema kutaka kushirikiana na IPC katika ujenzi wa mnala wa marehemu Daudi Mwangosi ,kutoka kushoto ni makamu mwenyekiti Jane Mihanjo ,Rais wa UTPC Keneth Simbaya na mkurugenzi wa UTPC Bw.Abubakar Karsan
………………………… ………………………… ………………………… …………….
BAADA ya chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema) jimbo la Mufindi kusini kuandika barua ya maombi ya fedha na kutaka ushirikiano na klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) katika ujenzi wa mnala wa kumbukumbu ya kifo cha Daudi Mwangosi ,Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC) imetoa tamko la kupinga hatua ya Chadema kutaka kujitafua umaarufu kupitia kifo hicho.


Akitoa tamko kwa niaba ya bodi ya UTPC jana , Makamu wa Rais Jane Mihanji wakati mkutano mkuu maalumu wa kupitisha marekebisho ya Katiba ya UTPC uliyofanyika Mjini Dodoma kwa muda wa siku mbili.

Alisema kuwa Chama hicho kisitumie kifo cha mwandishi wa habari huyo kujinufaisha katika maslahi binafsi ya kisiasa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutumia vifo kama mtaji wa kisiasa.


“..Sisi kama UTPC tunatoa tamko hilo kwa uchungu na pia chama hicho kisitumie kifo cha Daudi Mwangosi katika maslahi ya kisiasa kwani hatuko tayari na swala hilo au zoezi hilo la kujenga mnara kwenye sehemu hiyo kwani tunapinga vikali ujenzi huo unaotarajiwa kufanywa na chama hicho’Alisema Mihanji.


Alisema ujenzi wa mnara huo ambao inatarijiwa kufanywa na chama sio kazi yao kwa ili wanatafuta umaharufu wa kwenye majukwaa na kuwataka waache wakawaachia wahusika wenyewe jumuhia za waandishi wa habari ambao ndiyo wenye mamlaka na si vinginevyo.


Mihanji alisema kuwa, Mwangosi hakuwa mwanasiasa bali alikuwa ni mwana taalumu katika tasnia ya habari “Kwani yeye kufuatia mauaji yake hakuwa katika harakati za kisiasa bali alikuwa kikazi ambayo ni ya kitaaluma kwahiyo wenye mamlaka ya ujenzi au kufanyiwa jambo fulani la kihistoria ni wahusika ambao ni wanataaluma wenyewe na siyo chama cha kisiasa.


“UTPC ndiyo wenye mamlaka ya kufanya suala au zoezi hilo na siyo chama hicho kwahiyo ni vema swala hilo waakaliacha kama lilivyo kwani sisi ndiyo wahusika kwahiyo tunajua nini tunataka kufanya juu ya Mwangosi kwahiyo tamko letu ndiyo hilo kwa chama hicho swala hilo liachwe na tuachiwe wenyewe”Alisema makamu wa rais huyo.


Mwangosi alikuwa mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Chanel ten Mkoani Iringa ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani humo (Iringa Press Club) ambapo ameuawa mikononi mwa jeshi la polisi mnamo 2012.

Hata hivyo hadi sasa bado suala la kifo cha Mwangosi limeendelea kupigwa dana dana kutokana na kesi yake kutosikilizwa na hakuna mwandishi aliyeitwa kutoa ushahidi wake juu ya mauwaji hayo .

Mwangosi hakuuwawa kama mwanachama wa Chadema bali aliuwawa akiwa kazini kutimiza wajibu wake wa kitaalum ya uandishi hivyo kwa kitendo cha Chadema kutaka kushirikiana na IPC katika ujenzi huo itakuwa ni kuvuruga mwenendo wa kesi na kupingana na msimamo wa awali ya IPC ,UTPC na vyombo vingine kuhusu taarifa za awali ambazo jeshi la polisi lilianza kutaka kupotosha kuwa eti alikuwa ni mwanachama wa Chadema jambo ambalo si kweli.

TAMKO LA UTPC – YOUTUBE

CCM BUKOBA YAWATIMUA MADIWANI WAKE WA NANE KWA MADAI YA UKOROFI

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amenukuliwa wakati alipokutana na wanahabari kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa wa Kagera kimeamua kuwafukuza uwanachama madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba pamoja na kuwafutia nyadhifa za udiwani huku akitaja sababu kuwa ni mgogoro uliokuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo

1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)
XXXXXXXXXXXXX

Kujua historia ya chanzo cha yote hapa fungua hapa chini.

Mangula kazima moto kwa petrol Bukoba

Ufisadi wa Meya wa Bukoba Anatory Aman

Jeuri ya Kagasheki: Madiwani walipwa posho kususia bajeti ya Manispaa ya Bukoba!

Vita ya Kagasheki na Dk Aman ngoma nzito,madiwani waburuzwa Takukuru

Mgogoro wa Umeya Bukoba: Mangula ageuka mbogo; awataka wasiomtaka Amani kurudisha kadi

KAULI YA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KWA WAZIRI WILLIAM LUKUVI NA HALI YA USALAMA MKOANI ARUSHA TAREHE 19 JUNI 2013

Tanzania

Mtandao wa Wateteziwa Hakiza Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea haki za binadamu zaidi ya mia moja, pamoja na mashirika wananchama Mkoani Arusha, tumesikitishwa na kushtushwa sana na kauli iliyotolewana Waziriwa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu (Sera, Uratibuna Bunge) William Lukuvi dhidi ya asasi zakiraia.

Katika kauli yake Bungeni tarehe 17 mwezi Juni, akizungumzia tukio la bomu dhidi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), Lukuvi ameendeleza kile ambacho kwa muda mrefu serikalii liyopomadarakani imekuwa ikikifanya yaani kutumia lugha mbaya za kuwachonganisha wateteziwa hakizabinadamu na asasiza kiraia kwa ujumla na kuwaita kwamba ni wachochezi, vibaraka wa upinzani na lugha nyingine zenye dhihaka.

Katika siku za karibuni, zimekuwepo jitihada za makusudi za baadhi ya vyama vya siasa, makundi ya kijamii na watu binafsi kupandikiza chuki kwa raia dhidi ya vijana wetu wa Jeshi la Polisi, kuwafanya raia wawachukie askari, kuwafanya raia wasiwaamini askari, kuwafanya raia wasiwape ushirikiano askari na hatimaye kuwa na taifa ambalo halitawaliki,” alisema Lukuvi

Kauli kama hii kutolewa kiongozi mkubwa wa serikali tena katika Bunge la Tanzania ni kejeli kwa waliopoteza ndugu zao Mjini Arusha, na ni kauli ya vitisho dhidi ya asasi zisizo za kiserikali nchini. Nchi yetu imekumbwa na kasumba ya viongozi kuacha kutatua dalili zinazoashiria upotevu wa amani na kutaka kuonyesha kuwa asasi za kiraia na makundi mengine ndio chanzo cha matatizo hayo. Kauli kama za Mh Lukuvi zimeshatolewa ndani ya miezi sita iliyopita na mawaziri na viongozi wenginewasiopungua watano. Waziri Kagasheki alizishutumu wazi wazi asasi za kirahia zinazotetea haki za wafugaji Loliondo kuwa ni wachochezi wa mgogoro huo, wakati huo huo Naibu waziri wa Ardhi aliendeleza shutuma na vitisho hivyo dhidi ya Asasi zinazotetea rasimali ardhi nchini. Tunamsihi Lukuvi, atambue kuwa imani ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi nchini haijawahi kuondolewa na asasi za kiraia, bali huondolewa na matendo ya kidhalimu ya jeshi hilo dhidi ya wanachi na vyama vyao. Jeshi la polisi litaweza kurudisha imani kwa wananchi endapo tu litaacha kutumika na watawala kwa maslahi binafsi na kisiasa na sio kwa kauli za kubeza zitolewayo na viongozi wa serikali dhidi ya asasi za kiraia na makundi mengine. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni katika uchaguzi wandani wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. JakayaKikwete, aliwatahadhrisha wana –CCM wasiendelee kulitegemea Jeshi la Polisi kamanguzo yake kisiasa. Viongozi waache mzaha katika hali ya usalama wa Taifa kwa sasa kwani hakuna anaependa amani ya Taifa itoweke. Hadi sasa matukio ya kutishia amani ya Nchi yamekuwa yakishika kasi bila kuona jitihada za makusudi za kukomesha hali hiyo. Toka kushambuliwa kwa wahariri Saed Kubeneana Ndimara Tegambwage, kutekwa na kuteswa kwa Dk. Stephen Ulimboka, kuuwa kwa Mwangosi, Mwenyekitiwa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda, kuuwa kwa mapadre na mashekh, mlipuko wa Olasit dhidi ya waumini wa Kanisa katoliki, migogoro ya kidini na mengineyo, hakuna hata limoja lillilopatiwa ufumbuzi wa kudumu. USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI

Mtandao pia unalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwanyima uhuru waandishi wa habari, na kuwafukuza waandishi wa habari katika mikusanyiko ya mjini Arusha.Mtandao unalisihi jeshi la Polisi kumwachia mwandishi wa Chanel Ten Ashiraf Bakari, aliyekamatwa tarehe 18/6/2013 katika eneo la Soweto alipokuwa akichukua picha za matukio ya jeshi la polisi dhidi ya raia waliopiga kambi katika viwanja. Tunaalani kitendo cha jeshi la polisi kumkamata bwana Ashirafu aliekuwa na vitendea kazi pamoja na kitambulisho chake cha uandishi wa habari.

WITO WETU

 1. Tunamsihi Waziri Lukuvi aifute kauli yake dhidi ya asasi za kirai aambazo kimsingi kwamujibu wa utendaji kazi zao ni Watetezi wa Hakiza Binadamu katika fani mbalimbali na hawahusiki kwa namna yoyote ile katika hali ya sasa ya uvunjufu wa amani unaondelea nchini.

 2. Aidha tunaomba asasi kwa upande wao zisijihusishe naitikadi yoyote ya kisiasa baliwaendelee kuwatumikia Watanzania waitikadizote bilaubaguzi wowote.

 3. Jeshi la polisi mkoani Arusha limwachie mwandishi wa chanel Ten bwana Ashiraf Bakari, na kuwapa uhuru waandishi kureport habari yoyote.

 4. Viongozi wote wakiwemo wa madhebu mabalimbali walaani vikali hali inaoyoendelea Arusha kwa sasa.

 5. Balozi mbalimbali na Mashirika mbalimbali kukemea hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Mjini Arusha.

 6. Viongozi watambue kazi za asasi za kirai na kuzieshimu na kuacha kuwaita wachochezi

Tarehe, 19/06/2013

SAFARI YA MWISHO YA MANGWEA LEO MOROGORO, JANA MAELFU YAMSINDIKIZA DAR.

Mamia ya Wakazi wa jiji walijitokeza kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki Mei 28, mwaka huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za kimuziki. 

Mangwea alisafirishwa mchana wa June 5, 2013 kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika leo June 6.

 
 
 
 Wanafamilia wakipita kuaga mwili wa ndugu yao….
  Mbunge wa kinondoni  Idd Azzan anamuaga Ngwea
  P. Funky akipita kuaga na kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Mangwea
 Wasanii wa Bongo Movie wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu
Hata wanahabari nao kama Issa Mnali walitoa heshima za mwisho.

 Miraji Kikwete akizungumza machache na Ummy Wenselaus ‘Dokii’ viwanja vya Lidaz
  Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Mangwea
   Sehemu ya waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakionekana katika viwanja vya Leaders Club leo.
  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa Chadema (BAVICHA), John Heche wa tatu kutoka kushoto akijadiliana na viongozi wenzake waliokwenda kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea leo viwanja vya Leaders Club leo.
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.
Gari ya polisi ikiongoza msafara wa magari mengine kuelekea mkoani moogoro muda mfupi baaada ya mamia ya mashabiki na wananchi wa jiji la Dar es Salaam na Vitongoji vyake kutoa heshima za Mwisho kwa mwili wa msaniii mashukuri nchini albert Mangwe.Picha Zote na Mdau, Muhidini Sufiani, Mroki Mroki na Mdau Kambi Mbwana

CCM WALAANI VYOMBO VYA HABARI KUMNUKUU VIBAYA KIKWETE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM

KUTOKA KWA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI

Mei 19, 2013 Chama Cha Mapinduzi kilifanya kikao cha siku moja na wabunge wanaotokana na CCM, kikao hicho kilifanyika mjini Dodoma ambapo pamoja na viongozi wengine wa juu wa CCM kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la wabunge wa CCM na viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais na mtekelezaji mkuu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kubadilishana uzoefu wa namna ilani ilivyotekelezwa hasa kwenye majimbo kwa kipindi cha nusu ya muhula wa miaka mitano. Baada ya kubadilishana mawazo uliwekwa mwelekeo wa namna bora ya kutekeleza ilani na ahadi mbalimbali kwa kipindi kilichobaki.

Kwahiyo kwa kifupi lengo la kikao hicho ilikuwa ni kutathimini utekelezaji wa ilani majimboni na kuangalia namna bora ya kuweka msukumo mpya na mkubwa zaidi kwa kipindi kilichobaki cha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa 2010/2015, lengo likiwa kuhakikisha ilani na ahadi za CCM na wagombea wake zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo baada ya semina hiyo baadhi ya vyombo vya habari vimenukuu kauli inayodaiwa kutolewa na Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Kikwete kuwa ameruhusu wanaokusudia kuomba ridhaa ya CCM kugombea Urais wa 2015 kufanya kampeni.

CCM imesikitishwa na nukuu hiyo ya kupotosha ukweli wa kilichojadiliwa na hivyo tumelazimika kutoa ukweli wa kilichojiri na kujadiliwa. Ni kweli kuwa mjadala juu ya watu mbalimbali wanaotajwa au wanaojitaja kuwa na nia ya kugombea nafasi mbalimbali hasa udiwani, ubunge na Urais ulikuwepo na ulikuwa mkali.

Hata hivyo hitimisho la kikao na majumuisho ya Mwenyekiti wa CCM Taifa lilikuwa ni kukemea kwa nguvu zote pirika hizo na uvunjifu huu wa makusudi wa kanuni za Chama chetu ambazo kimsingi pirika hizi zinakigawa Chama na kuvuruga mshikamano na umoja ndani ya Chama.

Nasisitiza nukuu hiyo ya baadhi ya vyombo vya habari si sahihi na ni ya kupotosha ukweli. Inaelekea kuna kikundi cha watu wanamgombea wao wa kuchonga ambaye bila shaka anapungukiwa na sifa, hivyo wanajaribu kumuongezea sifa kwa kumlisha Mwenyekiti maneno na kuwaapa baadhi ya waandishi, uhuni huo haukubaliki.

CCM ina kanuni na taratibu zake zinazoisimamia na kuiongoza katika kufanya shughuli zake mbalimbali zikiwemo za mchakato wa kuwapata wagombea wake katika ngazi mbalimbali kuanzia shina hadi taifa.

Kanuni hizo ni pamoja na kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Februari, 2010 na Kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la 2012.

Katika Kanuni za Uchaguzi wa CCM Toleo la 2012 kanuni za jumla Ibara ya 33 inazungumzia Miiko ya kuzingatiwa wakati wa shughuli za uteuzi na uchaguzi. nanukuu“ Maadili na nidhamu ya chama katika kusimamia na kutekeleza shughuli za uchaguzi wa chama lazima kuzingatiwa na wale wote wanaohusika. Hivyo yawapasa kuelewa na kutambua kuwa;-

(1). “….wanachama wenye nia ya kugombea hawaruhusiwi kufanya kampeni ya aina yoyote kabla ya majina yao kuteuliwa na kikao kinachohusika”.

(4). “Ni mwiko kwa kiongozi au mwanachama yeyote wa CCM kuunda vikundi visivyo rasmi ndani ya chama, au kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chini chini kinyume na ratiba ya uchaguzi na taratibu rasmi zilizowekwa”.

Ibara hiyo ya 33 kifungu kidogo cha 1 na 4 vinaweka wazi msimamo wa kikanuni wa Chama. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Februari, 2010 na Kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la 2012 na kwa mujibu wa maagizo yaliyotolewa na kupokelewa kwenye kikao cha Mwenyekiti wa CCM Taifa na wabunge wa CCM mjini Dodoma tarehe 19/05/2013;

Ni marufuku kwa mwanachama yeyote wa CCM anayetaka kuomba CCM impe nafasi ya kugombea kwenye uchaguzi wa dola kujipitishapitisha na kuita wapiga kura na kukutana nao kinyume na kanuni za Chama. Hatua kali zitachukuliwa kwa mwana CCM yeyote atakaye kiuka agizo hili.

Lakini pia ni marufuku kwa viongozi na watendaji wa Chama kujihusisha na kuwakusanyia wapiga kura watu hao wenye nia ya kugombea kupitia CCM kwenye uchaguzi wa dola. Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi na watendaji wote watakao kiuka agizo hili la Chama.

Tunawataka wote wenye nia, viongozi na watendaji wa CCM kuzingatia agizo hili, ili tusije laumiana mbele ya safari.

Imetolewa na;-

Nape Moses Nnauye

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi

WADADA FAHAMU MBINU SAHIHI YA KUWASAIDIA WAPENZI WENU GOIGOI…

Safety_Pin

Kwa wale wadada wenye mausiano au mko kwenye ndoa na mwenzi wako anatatizo la kufika mapema ndani ya safari ya faragha basi uanweza kumsaidia kwa kufanya yafutayo.

UFUMBUZI.

Dadkika chache kabla hamjaanza majamboz, tafuta pini(exactly iwe dizaini kama hiyo pichani). Ibane kwenye nywele zako(za kichwani), hakikisha mwenzi wako haioni. Kisha anzeni majambozi.

Nakuhakikishia mtapiga gemu na jamaa hatofika ila ataendelea kuwa fit mpaka utakapoitoa ile pini ndipo ‘atamaliza’

So kazi itakuwa kwako mwanadada kwani pini yako ni kama remote control yako, ukitaka amalize unaitoa pini yako ukitaka aendelee hata kwa masaa matatu mfululizo unaicha tuu pini.

KUMBUKA.
Hii ni kwa akina dada wenye nywele ndefu ziwe natural au hata ‘wivingi’, rasta etc.

ZINGATIA:
Mwenzi wako hatakiwi kuiona hiyo pini wala hatakiwi kujua kama unatumia hii mbinu.

NB: huu sio uchawi na wala haihusiani na ushirikina bali ni urithi kutoka kwa bibi zetu.
Proudly African.

SOURCE:- jamiiforum.com

KINANA AWAITA WAPINZANI WAONGO, WAZUSHI…… DHIDI YA TUHUMA ZAKE

 

1 1d5be

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameibuka na kupinga vikali tuhuma zilizotolewa dhidi yake na kambi ya upinzani bungeni kuhusu shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa Vietnam mwaka 2009 kuwa ni za kupika na za uongo.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

“Tuhuma hizo hazina ukweli wowote, zina nia mbaya dhidi yangu na zemelenga kuniharibia taswira yangu na ya chama changu,” alisema Kinana.

Aliongeza kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote na kuwa hata kambi hiyo ya upinzani bungeni inatambua kuwa mamlaka zote za ulinzi na usalama za ndani na kimataifa zilimsafisha kuhusiana na sakata hilo.

Kinana alisema baada ya shehena hiyo kukamatwa, Mamlaka ya Kimataifa ya Kudhibiti Wanyama Walio Hatarini Kutoweka (CITES) na Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) walifuatilia na wakabaini kuwa hakuhusika kwa namana yoyote na shehena hiyo.

Kwa mujibu wa nyaraka za uchunguzi kuhusiana na shehena hiyo, watuhumiwa walikamatwa na kufikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu ambao ni Eladius Colonerio (Mkurugenzi wa Team Freight (T) Ltd) Gabriel Balua (Meneja wa TEA Freight (T) Ltd) na Shaban Yabula (Mkurugenzi Mtendaji wa Kigoma M.N Enterprises (T) Ltd).

Wengine waliofikishwa mahakamani ni Erick Morand (Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika Bandari ya Dar es Salaam) Issa Lweno, Norbert Kiwale na Abubakari Omar Hassan.

Nyaraka hizo ambazo gazeti hili lina nakala zake, zinaonyesha kuwa maofisa wa forodha huko Haiport and Hanoi, Vietnam waliokamata pembe za ndovu kilo 6,200 zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Pia, kati ya Machi na Juni, 2009, maofisa wa forodha wa bandari ya  South harbor mjini Manila, Philippines walikamata shehena nyingine ya kilo 4,861 zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Kutokana na taarifa za kukamatwa kwa shehena hiyo ya pembe za ndovu kutoka Vietnam, Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi kwa kushirikiana na Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii, ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), INTERPOL na Taasisi ya Kupambana na Ujangili Kusini na Mashariki mwa Afrika (LAFT)

Uchunguzi huo uliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Angelist Bonga ambaye kwa sasa ni marehemu.

“Timu hiyo ya wachunguzi ilifanya kazi yake kwa umakini na kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa watano ambao baadaye walifunguliwa mashitaka mahakamani,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Wakati kesi hiyo ikiendelea, serikali iliamua kupeleka timu ya wachunguzi nchini Vietnam, lakini nchi hiyo ilikataa kuwaruhusu kufanya uchunguzi nchini humo kutokana na Tanzania kutokuwa na makubaliano ya kubadilishana taarifa za masuala ya uhalifu. Hadi sasa mafaili ya kesi hiyo yapo Mahakama ya Kisutu.

“Tuhuma dhidi yangu hazina msingina ukweli wowote, hivyo hazina uzito wowote. Najua  hii ni sehemu ya siasa chafu na nilitarajia mambo kama haya baada ya kuhutubia nikiwa Morogoro wiki mbili zilizopita kuwa Watanzania wajiepushe na siasa zenye lengo la kuleta vurugu kwa taifa….Msigwa (Peter) na CHADEMA wanapaswa kutoa hoja,” alisema Kinana.

Akiwasilisha hoja wakati wa kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Kivuli wa wizara hiyo Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini – CHADEMA) aliilaumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili na kumtaja Kinana kuwa mmoja wa wanaomiliki meli iliyosafirisha pembe za ndovu.

Hata hivyo, Kinana hamiliki meli yoyote na hajawahi kujihusisha na usafirishaji wa nyara hizo za serikali, suala ambalo kwa sasa bado lipo mahakamani.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, alimtuhumu Msigwa kuwa ana agenda ya siri na kuwa ameamua kumtuhumu huku akijilinda kwa kinga za bunge na kuwa kufanya hivyo ni kutumia vibaya kinga hizo.

Alisema ahusiki na hana uhusiano wa aina yoyote na tuhuma hizo na kwamba hata kipofu anaweza kuona kuwa hausiani nazo na alituhumu kambi ya upinzani bungeni kwa kushindwa kujadili hoja za maana za maendeleo na badala yake kujihusisha na siasa za kuchafua heshima za watu wengine.

“Bado nina nguvu na sijayumba kwa namna yoyote. Nina jukumu la kuilinda CCM na kutekeleza ahadi tulizozitoa kwa wananchi kupitia ilani ya uchaguzi,” alisisitiza na kuhoji kuwa suala la shehena hizo ni la tangu mwaka 2009, kwa nini lijitokeze sasa?

“Jibu lake ni jepesi, lengo lao ni kumvunja moyo Katibu Mkuu wa CCM ambaye CHADEMA wanamuona kuwa ni tishio kwao,” alisema Kinana.

CHANZO: Mtandao wa Mabadiliko

THERE IS A SECRET WHICH SENATOR MUTULA KILONZO WILL TAKE TO HIS GRAVE.

Makueni Senator Mutula Kilonzo was found dead in his Maanzoni home on Saturday afternoon . Former Vice President Kalonzo Musyoka announced the shocking news during a burial in Tseikuru in Mwingi North Constituency on Saturday afternoon.

Makueni Senator Mutula Kilonzo was found dead in his Maanzoni home on Saturday afternoon .
Former Vice President Kalonzo Musyoka announced the shocking news during a burial in Tseikuru in Mwingi North Constituency on Saturday afternoon.

NAIROBI KENYA: There is a secret so big that Makueni Senator Mutula Kilonzo will take to his grave. It is a story he warned Standard reporter Roselyne Obala would shake Kenya.

Though he refused to give details, the late Senior Counsel insisted to Obala the story would not only surprise Kenyans, but could have major consequences.

That was on March 28 after Mutula was sworn in as Senator. A post-mortem scheduled to be carried out on his body Monday will seek to establish why he died suddenly, and without making even a single call to family or friends for help.

Sunday, as those close to him called for thorough probe into his death on Friday or Saturday night, a special team of detectives from Criminal Investigation Department (CID) headquarters in Nairobi began working to try and piece together what transpired in the former Education minister’s final hours at his ranch.

At the same time, three committees were formed to plan his burial, after a day’s meeting with the family. They are the Senate, National Assembly and Family committees.

“We’ve had a consultative meeting with the family and agreed to form the three committees, the Senate, the National Assembly where he was before going to the Senate and the family one. The committee will meet on tomorrow for other arrangements,” said Machakos Senator Johnstone Muthama at Mutula’s home in Gigiri, Nairobi.

According to the Family committee’s interim secretary Mr Musyoki Kivindyo, each committee will meet and come up with a progressive report on burial arrangements that befit the late Senior Counsel.

STAIGHT TALKING.

It also emerged from his friend and former Attorney General Amos Wako, who is also the Busia Senator and was among the last to speak with Mutula, that the former Justice minister was in robust health.

Mutula’s trainer at the Hilton Hotel gymnasium, who took the former Makueni Senator through his aerobic sessions on Friday morning, corroborated this statement.

Later in the afternoon, Mutula would leave for his Maanzoni Ranch in Machakos County, where he would be found dead the following day, with foam on his mouth.

Mutula, a straight-talking politician and astute lawyer, told Obala a month before he died that he would reveal to her the secret he bore ‘with time’, but sadly he died before they could meet again.

On that March 28, after being sworn-in as Senator for Makueni, he said, during a short interview, that he had information that if published in the media, would “cause panic and mayhem”.

Said Obala: “A jovial Kilonzo emerged from the Senate and we had a brief encounter at the Senator’s lounge. It was on Thursday afternoon on March 28, when I engaged him in an interview to get to understand the Senate’s role,’’ reports Obala.

“From the outset, he appeared happy, energetic and raring to go, dressed in a brown suit. We exchanged pleasantries, and I began by congratulating him on his election as Senator for Makueni.”

SUDDENLY DIVERTED

Obala goes on: “He began outlining the responsibilities of Senators and how they will take the National Government to task over devolution. He then said their role was to be a link between County Governments and National Government.”

Mutula was explaining how they intend to take on the National Government over the implementation of the Devolution, “when he suddenly diverted and stated that there is a lot going on that Kenyans need to know,’’ Obala went on.

Mutula told her that it is no secret that the National Government is trying to frustrate the implementation of Devolved Government. ”

It was at this juncture that his tone changed, he looked serious and stated; “I have information that if I disclose to you Monday, your papers will be burnt the next minute.”

The statement came as a surprise, but when Obala pressed him, because she was curious to know more, and even offered not to name him in the story, Kilonzo retorted: “No, No, No.”

She pleaded with him, saying, “Please Mheshimiwa (Honourable), I will use an anonymous source,” he declined.

When she insisted he reiterated as they walked down the stairs: “Save the company (Standard Group Limited) and yourself. I promise to give you the information at the right time.”

Those were Mutula’s last words to the journalist as he walked away and, unfortunately, that is where the big story that never came to life ended.

Sunday, the officers from the CID’s Homicide Unit based at Mazingira Building along Kiambu Road took over the probe from their colleagues in Machakos. The team, led by the unit’s head Mr John Kariuki, will work with those from Machakos and are expected to attend Monday’s planned post-mortem exercise.

Officials at CID headquarters revealed the Homicide Unit revisited the scene where the body was found and was set to take over all samples that had been collected. They also interviewed Mutula’s workers who prepared him supper on Friday.

“They will visit the place where the food was prepared as part of the investigations into the death. They have also taken away samples of the food for testing and analysis,” said a senior officer aware of the probe.

The cause of the death is yet to be established.

SITTING ALONE.

“I do not know why I was not alarmed by this odd attitude. He was not keen on participating in Senate sessions, but wanted to talk more about his family and his career fulfillment. I should have prodded him further,” said Senator Wako, remarking wistfully about his last meeting with a friend he had known for over 35 years.

Wako last met Mutula on Thursday in the Senate during the afternoon sessions. He remembers seeing his friend walking in and sitting alone on a secluded seat. Mutula appeared dull and engrossed in personal thoughts; or may be it was just mental fatigue, said Senator Wako.

“I quickly moved to where he was and sat next to him and asked where he had been all this time. I was concerned that he had missed out on the Coalition for Reforms and Democracy (CORD) retreat at Naivasha, and other party engagements,” Wako told The Standard.

However, the Busia Senator does not remember getting a clear answer to his question. Instead he asked his friend, whether he was prepared to make any contributions to the ongoing debate on the floor of the House.

But Mutula, indifferently, said there was no need.

“What is there to discuss about?” he asked, as if to suggest the issue at hand was not beyond his parliamentary colleagues to handle.

According to his fitness instructor of six years, who identified himself only as Tim, Mutula was at the gym at 6am in the morning, and went through his routine aerobic paces for 30 minutes before leaving.

“He was jovial as usual and quite physically fit as I took the aerobic class through the usual paces. Mheshimiwa was fit and went through the paces non-stop, without showing any signs of slowing down,” Tim told The Standard.

UTATA MWINGINE WAKIGUBIKA KITI CHA SPIKA, KIFUNGU GANI KIMETUMIKA KUWAADHIBU WABUNGE 6 WA CHADEMA?

WAKATI wabunge sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakianza kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge la Bajeti vinavyoendelea mjini hapa, utata mkubwa umeibuka juu ya kanuni alizotumia Naibu Spika, Job Ndugai, kutoa adhabu hiyo.

Utata huo ulibainika jana wakati Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe, alipoomba mwongozo wa Spika Anna Makinda, kutaka kujua kanuni aliyotumia Ndugai wakati hakuna kanuni iliyomruhusu kutoa adhabu hiyo.
Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili jana pia walihoji kifungu kilichotumika hata kama wabunge hao walikosea.
Miongoni mwa waliohoji adhabu hiyo, wapo baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakupenda kutaja majina yao, wakisema kuwa uamuzi wa Naibu Spika ulitawaliwa na jazba za kibinadamu badala ya kufuata kanuni zinazoliongoza Bunge.
Katika mwongozo wake jana kwa Spika Makinda, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani alihoji kifungu kilichotumika kuwaadhibu wabunge wake.
Mbowe alisema juzi wakati Bunge lilipokuwa katika kipindi chake cha jioni, wabunge sita wa CHADEMA waliotolewa nje kwa maelekezo ya Naibu Spika, Job Ndugai.
Aliwataja wabunge waliotolewa kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Haghness Kiwia (Ilemela), Ezekia Wenje (Nyamagana), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Pete Msingwa (Iringa Mjini).
“Na wabunge hawa walipotolewa, walipewa vile vile adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge, adhabu iliyotolewa papo kwa papo na Naibu Spika.
“Kwa mujibu wa kanuni zetu, kanuni inayompa Naibu Spika au Spika mamlaka ya kumtoa mbunge kwa siku tano ni kanuni ya 73 ya kanuni ndogo ya tatu ambayo inahusu mbunge ambaye atashindwa kutoa vielelezo vya aidha kusema uongo ambayo inasema hivi: “Endapo mbunge yeyote atatakiwa kuthibitisha maneno aliyoyasema na hadi kufikia mwisho wa muda aliopewa, ameshindwa kutoa uthibitisho huo, Spika anaweza kumsimamisha mbunge huyo asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi vitano,” alinukuu.
Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA, alisema yaliyotokea bungeni juzi ni sintofahamu kati ya wabunge na kiti cha Spika ambapo katika mambo ya msingi CHADEMA ilitegemea kifungu cha nne cha kanuni za Bunge, kifungu kidogo cha kwanza kingetumika.
Kifungu kinasema: “Spika anaweza kutaja jina la mbunge kwamba amedharau mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge.
“Ikiwa kwa maneno au vitendo, mbunge huyo anaonyesha dharau kwa Spika au atafanya kitendo chochote cha makusudi cha kudharau shughuli ya Bunge au mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.”
Kutokana na kanuni hiyo, Mbowe aliomba mwongozo wa Spika kutaka kujua wabunge hao walitolewa kwa kanuni gani na ni lini wataweza kurejeshewa haki yao ya kurejea ndani ya Bunge.

Vituko vya juzi
Baadhi ya askari walioamriwa kuingia ndani ya Bunge, walisema hawakuwa tayari kumtoa Lissu kwa nguvu ndio maana walitumia muda mrefu kutimiza agizo hilo.
Askari hao walisema hofu yao ilikuwa ni usalama wa Waziri Mkuu kwani endapo vurugu zingeibuka, angekuwa katika wakati mgumu kiusalama.
Baada ya Lissu na wabunge wenzake kutoka nje ya ukumbi chini ya ulinzi, askari hao walipata wakati mgumu kuwatoa nje ya eneo la Bunge.
“Tulipanda juu hadi kwenye ofisi ya Lissu, alipofika alikaa chini, akafungua kompyuta yake, baadaye akaizima wala hakuwa na haraka na sisi wakati huo tulibaki tumesimama tu.
“Baadaye aliizima, akachomoa waya na kuziingiza kwenye begi lake, kisha alisimama taratibu na kuondoka kama vile hakuna jambo lililotokea,” alisema askari huyo.

Wenyewe wanena
Lema alisema: “Nimepokea kwa furaha adhabu hii kwa sababu imetokana na kupigania haki na ukweli ndani ya Bunge. Kwa hiyo adhabu hii kwangu ni baraka.”
Alisema uonevu wa wazi uliofanywa na Naibu Spika, Job Ndugai, baada ya muda kidogo Tanzania itashangilia ushindi mkubwa. Kwamba Watanzania watafurahia vijana wao na watoto wao walioshinda hofu.
“Ushahidi nilioombwa kuhusu mwenyekiti wa CCM kuwa mwasisi wa udini ninao, tena wa uhakika wa nguvu na imara na niko tayari kuutoa mbele ya Bunge kwa kuwa nilitoa maneno hayo mbele ya Bunge.
“Sitapeleka tena ushahidi wangu vichochoroni kwa kuwa nilipeleka ushahidi wangu kwa Spika kuhusu uongo wa Waziri Mkuu, walipiga chenga hadi wakanivua ubunge,” alisema.
Lema alidai kuwa ametumiwa meseji za vitisho kwamba wangelimuonyesha tena mahakamani, lakini akasema wafanye wafanyavyo ila moyo wake una furaha kuwa amesema yale ambayo wengine wameogopa kuyasema.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, alisema: “Bunge letu lina matatizo, halina mwelekeo. Job Ndugai anajidai yeye ndiye kiongozi wa serikali.”
Alisema kama Ndugai ana sifa hizo na anajiandaa kuwa Spika wa Bunge lijalo, anamwomba Mungu asiwe mbunge katika Bunge hilo.
“Tusi lililotolewa na Peter Serukamba wa CCM, lilikuwa kubwa kuliko matusi yote yaliyowahi kutolewa ndani ya Bunge katika mabunge ya Jumuiya ya Madola.
“Hili lilihitaji adhabu, lakini kitendo cha Naibu Spika kumtimua Lissu ambaye alikuwa anafuata kanuni ni cha kusikitisha sana,” alisema.
Mbilinyi alisema wananchi wa Mbeya Mjini hawakumtuma kushangilia bungeni.
Kwa upande wake Mchungaji Msigwa alisema: “Adhabu hii ni ya hovyo kwa sababu haikufuata taratibu; wamegeuza Bunge kama sehemu ya serikali.”
Alifafanua kuwa kama angepata adhabu iliyofuata kanuni asingekuwa na shida, angeipokea kwa furaha.
“Naibu Spika ana jazba, anapaswa apate mafunzo ya jazba zake. Viongozi wa Bunge wamejaa u-CCM zaidi kuliko utaifa. Binafsi sitajali kufukuzwa, ninachotaka haki itendeke,” alisema.
Mbunge wa Ilemela, Kiwia, alisema adhabu waliyopewa ni kinyume cha kanuni.
“Adhabu hiyo anapaswa apewe mtu aliyesema uongo na kushindwa kuthibitishwa, pamoja na hayo kanuni zifanye kazi kwa wabunge kwa usawa,” alisema.
Kiwia aliongeza kuwa kanuni hazipaswi kuwaona wabunge wengine wana haki na wengine hawana; kwamba hoja za msingi zijibiwe, maamuzi bungeni yasifanyike kwa mabavu.
Naye Lissu ambaye ni mwanasheria kitaaaluma, alisema hajui ni kanuni gani iliyotumika na kumwadhibu na kwa kosa gani.

HABARI HII INAPATIKANA KATIKA GAZETI LA TANZANIA DAIMA – 19.04.2013
Miss Lou Acquiring Lore

Gallery of Life...

MAISHAZONE

ITS ALL ABOUT LIFE......For over 75 years, Jubilee Insurance has built a rich heritage of enriching lives by offering insurance solutions that make life carefree and rewarding.

this is... The Neighborhood

the Story within the Story

JAMIIBLOG

PAMELA MOLLEL

MEDIA 2 SOLUTION

- TRUTH SEEKERS -

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.