ARUSHA; CCM YAONGOZA MITAA 78 KATI YA HIYO 6 KWA PINGAMIZI HUKU UKAWA WAKIPATA MITAA 75, MTAA MMOJA KURUDIWA .

Baadhi ya wapiga kura wakipiga kura kwenye mojawapo ya kituo jijini Arusha.

baadhi ya wanachi wa mkoa wa Arusha wakisubili kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya jumapili.

Chama cha mapinduzi (CCM) kimeendelea kuongoza katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwabwaga mahasimu wao wakubwa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa ushindi kiduchu, ambapo imefanikiwa kunyakua mitaa 78 na chadema kuambulia 75 katika matokeo ya awali.

Pamoja na dosari za hapa na pale katika uchaguzi huo uliyopelekea kuailishwa kwa kituo kimoja nafasi ya mwenyekiti na vingine viwili nafasi za wajumbe hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi Juma.

Katika uchaguzi wa mwaka huu jumla ya wananchi  1,139,090 walijiandikisha kupiga kura huku vyama sita vikisimamisha wagombea ambavyo ni pamoja na ACT, CCM, NCCR, CUF pamoja na TLP.

Bw. Juma akitaja matokeo ya uwenyekiti wa mitaa alisema kuwa CCM inaongoza kwa kupata mitaa 78 ambapo kati ya kura hizo kura sita ni za kupita bila kupigwa, ikifuatiwa na CHADEMA mitaa 75.

Aidha alibainisha kuwa kulikuwa na jumla ya vituo 154 vya kupigia kura “mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umemalizika ila tumelazimika kurudia uchaguzi katika vituo vitatu,  ambapo kituo kimoja ambacho ni cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa kwa nafasi zote huku katika kituo cha AICC -Sekei uchaguzi utarudiwa kwa wajumbe watatu wa viti maalumu ambapo hii inatokana na kura za kufungana kwani wote walipata 31 kwa 31  na katika kituo cha Oldpolisi line napo wajumbe wawili walifungana kwa kura 64 kwa 64.

Advertisements

SASA NI ZAMU YA HAPPINESS MISS WORD… GO TEAM TZ GO

10614252_800789863300579_6044778737800766960_n

NEW TOP 10 on the Miss World People’s Choice!

AUSTRALIA
BARBADOS
HAITI
INDIA
NEPAL
NETHERLANDS
PHILIPPINES
SOUTH AFRICA
TANZANIA – NEW ENTRY!
THAILAND

TANZANIA jumps up into the top 10 today, with Russia dropping out!

Voting closes 15:30 on Sunday 14th December, so there is only 96 to go!

Download the Miss World App for free to register your vote now!

http://www.missworld.com/TheCompetition/TheMissWorldMobileApp/

10846445_10152970401239974_5092824672817370692_n

UZINDUZI WA MSIMU WA PILI WA TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGI, CINEMAX OYSTERBAY

Uzinduzi wa siri ya mtungi season II ndani ya ukumbi wa Century Cinemax Oysterbay wafana hapa ni kati ya washiriki wakipata ukodak wa pamoja na wafadhili waliofanikisha Episode hii kukamilika na kuwa hewani. Wafadhili hawa ni kutoka Marekani na ndiyo chachu ya Episode hii kukamilika na kuiwezesha kuwa hewani hili watu wajifunze kilichopo ndani yake.

Vyombo vya habari pamoja na Camera ya Vijmambo vikiwajibika hili kuwajuza kilichokuwa kimefanyika ndani ya ukumbi huu wa Century Cinemax.

Juu na chini washiriki wa Episode hiyo wakibadirishana mawazo huku pia wakiendelea kuangalia walichokifanya ndani ya Episode hiyo.

Ni mambo ya ukodak tu mwanzo mwisho hili kutunza kumbukumbu kwa washiriki wa Episode hiyo

Starring wa Episode hiyo bwana Juma Rajabu aka Cheche akiongea mbele ya camera juu ya nini alichokifanya ndani ya Episode hii ya siri ya mtungi. Kwa picha zaidi jitiririshe kwa kubofya soma zaidi.

NAZIZI ATHIBITISHA KUWA NA UHUSIANO NA MTANZANIA HERRY SAPPY.

Rapper wa Necessary Noize, Nazizi wa Kenya amethibitisha kuwa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na producer Mtanzania aitwaye Herry Sappy ambaye ni mtayarishaji wa muziki katika studio ya Homeboyz Productions ya nchini Kenya, baada ya wawili hao kukanusha habari hizo miezi kadhaa iliyopita.

nazizi-1

“Yeah tuna date, unajua ni miezi michache sasa”, alisema Nazizi kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.”Sijamwona mwezi mmoja sasa ameenda Mwanza kufanya project kadhaa lakini unajua tunawasiliana, unajua hatujui mambo ya Mungu tunaangalia itakavyoenda.”

Nazizi ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyempata akiwa kwenye ndoa na aliyekuwa mume wake waliyeachana, hakusita kumsifia boyfriend wake wa sasa Sappy ambaye ni mwenyeji wa Mwanza.

“He is a nice guy he is a really nice guy he is also really hard working he is doing very well out there”.

nazizi-2

Nazizi amesema yeye na Sappy walikutana studio zaidi ya mwaka mmoja uliopita kama msanii na producer wake na baadae mapenzi yakazaliwa.

“Tulikutana studio, dats how we met. Ilichukua muda baada ya kukutana kabla ya kuanza kuzungumza kabisa, nilikutana naye nadhani zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Tulikuwa tukiongea mara moja moja, alinipa beats nilizokuwa natakiwa kufanyia kazi then nikawa bize. Amenitengenezea single mbili kwa EP yangu.”

Sappy aliwahi kuiambia Bongo5 kuwa mapenzi yao yalianza rasmi iku ya Valentine’s (Feb 14, 2014) na kuwa wapo serious na wanapendana kwa dhati.

//

VIDEO: MR BLUE AKIWA NA VIJANA WA B.O.B MICHARAZO WAMEACHIA KICHUPA KIPYA KIITWACHO “SHUT UP” (KIMYA).

Vijana wa B.O.B Micharazo, wakiongozwa na front runners, Mr Blue na Nyandu Tozi, wameachia video ya ngoma yao mpya iitwayo ‘Shut Up’ (Kimya).

Kwenye ngoma hiyo iliyotayarishwa na Marco Chali, rappers hao wanafanya mtindo wa kubeto na hivyo kupeleka onyo kali kuwanyamazisha wapinzani wao. Katika verse ya Mr Blue ambaye amesima vizuri amefungua ngoma hiyo kwa panch “Helo Dar es Salaam mbona kimya jiji zima mbona limezizima/Hakuna cha Sharobaro wala ming’aro ya kuazima/ Mmebakiza uharo kumbe washenzi mlipima/Wabaya wetu mbona kimya, vipi wazima au nanyinyi mlipima,” anarap Kabayser.

Wengine waliochana kwenye ngoma hiyo ni Blood Gaza, Bobby MC, Cotton, Uswege na Beka Title aliyesimama kwenye chorus.

HATIMAYE KITUO CHA REDIO CHA BBC CHANASA SAUTI ADIMU YA BI. REGINA MWALEKWA

Wakiwa wenye Nyuso za Furaha.Watangazaji mahiri wa Radio na Televisheni,Bi.Regina Mwalekwa aliyekuwa mtangazaji wa Radio One na baadae akahamia Clouds FM/TV na sasa amejiunga na Shirika la Utangazaji la BBC akiwa na mtangazaji mwenzake kutoka kituo cha televisheni cha ITV/Radio One Bi.Fatma Almas Nyangasa,kama walivyonaswa na Camera yetu ndani ya viwanja vya maonyesho ya Saba saba yanayoendelea hivi sasa jijini Dar. Bi Regina Mwalekwa kwa sasa sauti yake itakuwa ikisikika rasmi kupitia kituo cha redio cha BBC. Tunamtakia kila lakheri katika kituo chake kipya cha kazi.

Bi.Regina Mwalekwa akifanya mahojiano na mmoja wa washiriki wa maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya Saba saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwal. Julius Nyerere jijini Dar.

SASA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUANZA KUONEKANA ITV KILA JUMAMOSI USIKU.

 Jukwaa likitengenezwa kwaajili ya Washiriki Wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kupanda jukwaani na kuanza kuonyesha vipaji vyao, Onyesho hili ni onyesho la kwanza la kuelekea Kwenye Mchujo wa kumpata mshiriki Mmoja atakayejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Mahost wa Show ya Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwa kwa Steji tayari kwa Show kuanza

Timu ya Tanzania Movie Talents (TMT) ikiwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya Show ya Tanzania Movie Talents katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa usiku huu
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliohudhuria kwaajili ya kutazama onyesho la washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Wadau waliojitokeza kwaajili ya Kushuhudia onyesho la Tanzania Movie Talents.Picha zote na Josephat Lukaza

Washiriki 20 wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washindi kutoka kanda 6 za Tanzania wamepanda kwa steji katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwaajili ya kuanza kuonyesha vipaji vyao vya kuigiza.  Sasa ni safari kwa washiriki kuelekea kwenye kinyanganyiro cha kuwania Milioni 50 za Kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane.

Katika Onyesho hili litakalorushwa katika Runinga ya ITV siku ya Jumamosi saa 4 usiku kitakuwa kipindi cha kwanza kwa watanzania kuanza kuangalia na kuwapigia kura washiriki ambao watakuwa wamewavutia na kukonga nyoyo zao na hatimaye kuwawezesha kushiriki katika fainali kubwa Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Watanzania wanatakiwa kuendelea kutazama muendelezo wa vipindi vya TMT kupitia Kituo cha Runinga cha ITV saa nne Usiku siku ya Jumamosi na hatimaye kuanza kuwapigia kura washiriki. Ili kuweza kupata Taarifa za TMT unaweza kutuma neno “TMT” kwenda namba 15678

Mchujo kwa washiriki sasa waanza rasmi ili kuweza kumpigia kura mshiriki umpendae unatakiwa kutuma neno “TMT ikifuatiwa na namba ya Mshiriki” kwenda namba 15678

KILI MUSIC TOUR YA MWANZA NI MOTO…

BEN POL (1)

Msanii wa Bongo flava, Ben Pol akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mwanza wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

CHRISTIAN BELLA (2)

Msani wa muziki wa dance, Christian Bella akikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

FID Q (2)

Msanii wa bongo flava, Fid Q akizungumza na wakazi wa Mwanza wakati akitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

IZZO B

Msanii wa Bongo Flava Izzo Biznez akifanya vitu vyake wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

NYOMI (1)

Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza  katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

OMMY DIMPOZ (6)

Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

RICH MAVOKO (8)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko akipagawisha wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

VANNES MDEE (1)

Vanessa Mdee na Fid Q wakishirikiana kutoa burudani wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

WEUSI  (7)

Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza  katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

YOUNG KILLER (4)

Msanii wa miondoko ya Bongo flava, Young Killer akimtambulisha mama yake mzazi wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

SAUTI ZA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI ZASIKIKA KUTOKEA ZANZIBAR

 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Mhe. Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutoka kwa Wajumbe wa UKAWA kutoka Vyama vya Upinzani Wanaohudhuria Bunge Maalum la Katiba
 Viongozi wa UKAWA wakiwa katika mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Mzsons Shangani Zanzibar baada ya mkutano wao kuahirishwa na jeshi la Polisi Zanzibar kwa sababu za kiusalama .
 Mwenyekiti wa  CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari sababu za kutoka katika bunge maalum la katiba Tanzania.akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Zanzibar.
 
 Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.
 
  
Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.

NJIA NYEUPE KWA WATENGENEZAJI WA FILAMU WA KITANZANIA KUUZA KAZI ZAO KWENYE MITANDAO

IMG_7030

MKurugenzi wa Kampuni ya Blue Sky, Richard Signeski (kulia), akizungumza  na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ukumbi Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam  kuhusu ushirkiano walioingia na  Kampuni ya Status Communications ya nchini kuwawezesha waandaaji filamu nchini kuuza filamu zao  kwenye mitandao ya kijamii. Kushoto ni Mwakilishi wa Status Communication, Monalisa Shayo.

IMG_7022

Omar Salisbury akizungumza na waandishi wa habari.

Kampuni ya Status Communications imetangaza ushirikiano na kampuni ya usambazaji wa filamu ya Kimarekani Blue Sky Media ili kuwawezesha kuuza filamu kwenye mitandao ya ITunes, Microsoft, You Tube, RAIN na mitandao mingine ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski alisema ushirikiano huu utawafanya watengeneza filamu kutoka Afrika Mashaaiki na kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao mikubwa ya usambaji dunia nzima.

‘’Lengo la ushirikiano huu ni kuwapa watengeneza filamu kutoka Afrika mashariki na kati kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watazamaji dunia nzima’’ alisema Signeski.

Mwakilishi wa Status Communications, Monalisa Shayo alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya tu ya ushirikano na makampuni ya kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki.

 ‘’Mwaka 2013 umekuwa mwaka muhimu kwa Status Communications kwani tumeweza kuingia mikataba na makampuni mbalimbali ili kuweza kuingia soko la Afrika Mashariki’’ alisema Monalisa.

‘’Mwanzoni mwa mwaka huu tumeingia mikataba na makampuni kama Media Zone Authority  ya Abu Dhabi (twofour54) pamoja na Qatar’s Media Group International pamoja na Visual Unity ya Abu Dhabi ili kuwawakilisha kwenye masoko yao kwenye miji kama ya Prague’ alisisitiza Monalisa wa Status Communications.

‘’Fursa hii ni muhimu kwa watengeneza filamu wa Afrika Mashariki kuuza filamu kwenye masoko tofauti duniani’’ alisema Monalisa.

Akielezea sababu za kuja nchini, Signeski alisema alichokigundua hapa nchini ni kuwa watengeneza filamu wengi wanahofia kuwekeza fedha nyingi kwenye utengenezaji wa filamu zao kwani wanahofia uchache wamasoko ya kuuza filamu zao.

‘’Hivyo nawaomba watengeneza filamu mjitokeze kwa wingi ili muweze kuuza filamu dunia nzima kwa urahisi’’ alimaliza Signeski.

HOJA JUU YA HOJA KUTOLEWA LEO HILI RAIS ASITIES SAINI SHERIA YA MABADIRIKO YA KATIBA

JUKWA LA KATIBA NA VYAMA VYA UPINZANI

SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) pamoja na Mtandao wa TGNP , kwa kushirikiana na Wanaharakati wengine wakiwemo, Haki Elimu, LHRC, Jukwaa la Katiba, TAMWA na Mtandao wa Wanawake na Katiba, wameandaa mjadala wa wazi:

KWA NINI RAIS ASITIE SAINI MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA MWAKA 2013.

JOPO LA WAZUNGUMZAJI: Prof Issa Shivji (Chuo Kikuu cha Dar es salaam), Prof Ruth Meena (TGNP Mtandao), Dr Azaveri Lwaitama (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Anna Henga(LHRC), Jenerali Ulimwengu( Mwanaharakati wa kijamii) na Deus Kibamba(Jukwaa La Katiba).

Lini: Jumatano Tarehe 18 Septemba 2013

Muda: saa 03:00 asubuhi – 07:00 mchana

MAHALI: Viwanja vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo Sokoni
Tafadhali sambaza ujumbe huu wa muhimu kwa watu wengi iwezekanavyo ili kufanikisha mjadala huu wa wazi,ratiba itafuata baadae.

IS TANZANIA SOUTH AFRICA’S TROJAN HORSE?

THE TWISTS AND TURNS in the story of how Rwanda, Tanzania and Uganda have tangled and untangled over the last 35 years to create both the current face-off between Kigali and Dar es Salaam, and the crisis in eastern Democratic Republic of Congo today as reported in CRISIS IN THE GREAT LAKES 1: For Rwanda Its Back To 1996…And For Tanzania Its Back To Uganda 1982 were only beginning.

We need to look south for a moment.In 1994 Nelson Mandela became president of a free and democratic South Africa, and the African National Congress (ANC) took power. In the many years before Mozambique gained independence from the Portuguese in 1974 after a long liberation war, the armed wing of ANC, Umkhonto we Sizwe (“Spear of the Nation”), like several other Southern African resistance movements, was based in Tanzania. Tanzania paid a dear price in endless raids by the apartheid airforce, which was far superior to anything any African country then could throw at it.

The apartheid South African raids, many of them in Tanzania’s fertile south, combined with Nyerere’s socialist policies, to keep the country poor. That though, did not diminish Tanzania’s generosity or commitment to southern African liberation. That long sacrifice forged a blood link with southern Africa (expressed today in Tanzania’s membership of the Southern Africa Development Community [SADC]).

That is why the accusation that Tanzania is more committed to SADC than the five-member East African Community (EAC) is a little naïve and ignores history. Asking it to choose between the two is to demand that it walk away from itself.

Indeed the EAC could be said to a greater source of pain and betrayal to Tanzania than SADC. To appreciate this, it requires that we go back to 1974. At that time, Uganda’s Milton Obote, a close friend of Nyerere, was living in exile in Dar es Salaam. Uganda military dictator Idi Amin’s quarrels with Nyerere was reaching ridiculous levels. Not only did Amin, a former boxing champion, demand that he and Nyerere should enter a ring and fight to sort out their differences, but he also said if Nyerere were a woman, he would have married him!

In addition to Tanzania’s ideological – socialism vs. capitalism – difference with Jomo Kenyatta’s Kenya then, the EAC was facing the kind of stresses of the type we are seeing today. Eventually in 1977 it collapsed. Kenya had and kept the lion’s share of the EAC infrastructure, including its chunk of its shared telecommunications and airlines. Uganda got the next largest slice, and Tanzania was left with little else beside the Dar es Salaam port.

Already having to contend with the scarcities of a socialist economy of that period, the break up of the EAC plunged Tanzania into a Dark Age. For a considerable period it had no international telephone connection, and struggled with airline traffic – the East African Airways was already becoming Kenya Airways. To raise money to build a new phone system, Nyerere slashed public services pay by 25 percent, and sent a struggling middle class into the abyss. The difficulties that followed wired resentment of the EAC into the DNA of a generation of Tanzanians – including people like Kikwete. Only time, and their passing, will truly heal it.

Poor, isolated, trying to rebuild its infrastructure after the collapse of the first EAC, and trying to take advantage reduced South African attacks after the independence of Mozambique, Tanzania fell down another economic hole again. It had to send its army into Uganda to kick out Amin in 1979 after his troops invaded and trashed the Akagera Salient. And President Jakaya Kikwete, who was head of Tanzania’s post-war intelligence operation in Uganda, had to see that mission end in bitterness in 1982—and ingratitude in 1986 when Museveni swept to power.

As we’ve already remarked, perhaps it is because unlike soldiers who take the blows and get more personally touched by war, Tanzania’s president Julius Nyerere, his successors Hassan Mwinyi and Ben Mkapa were able to be pragmatic about relations with Uganda – though perhaps less so with Kenya.

And Museveni did redeem himself considerably with South Africa and Tanzania soon after he came to power. That redemption started with events in 1984, two years before Museveni became president with the signing of the Nkomati Accord, a non-aggression pact, between Mozambique and apartheid South Africa. Under the accord Mozambique agreed to expel the ANC and to dismantle the camps and infrastructure of its armed wing, Umkhonto we Sizwe (“Spear of the Nation”), while South Africa agreed to stop attacks on Mozambique and end its backing of the Mozambican National Resistance, Portuguese, Resistencia Nacional Mocambina, better known by its abbreviation RENAMO. Mozambique kept up its part of the deal, and two years down the road started shipping the ANC out of Mozambique. Mandela, and later Mbeki, had a lot of time for Kagame – not so Zuma

But where would Umkhonto go, given that it could not relocate to a southern African country? Museveni, then still a revolutionary firebrand, had just become the Big Man in Uganda. He gave them a home.
If there was one man in these myriad of liberation movements whom Kikwete could relate to because they shared the same experience of intelligence chiefs who’ve had to bury their bitterness for the “picture bigger” as their political leaders cut political deals, it was Jacob Zuma.
Zuma was deputy Chief Representative of the ANC in Mozambique until the Mkomati Accords. When Umkhonto shipped out to Uganda, Zuma was forced to leave Mozambique and move to Lusaka. There he became Head of its Underground Structures, and then ANC’s Chief of Intelligence.

But Kikwete’s and Zuma’s moments hadn’t arrived yet. Mandela related to the RPF struggle and was outraged by the Rwanda genocide. He liked Kagame and Museveni. As someone put it, he “treated Kagame and Museveni like they were his sons”. His successor Thabo Mbeki didn’t get along with Museveni, but was a buddy Presidents Kikwete and Zuma do a jig: They have brought the sharp end of southern African liberation politics into Great Lakes geopolitics.

of Kagame’s. No one would have guessed that things would change dramatically in South Africa in 2008. Zuma orchestrated a party coup against Mbeki and became president. In Tanzania Kikwete had become president in 2005. For the first time in Tanzania and South Africa, two men who had been at their sharp end reunited the liberation movements of past decades. The securitariat in South Africa and Tanzania, could finally claim their prizes.

How would the Zuma-Kikwete pairing of former intelligence chiefs imprint itself on the wider region? With Mandela ailing, and Mbeki out of the way, Kagame was no longer getting birthday cards from Pretoria. The breaking point came in February 2010 when Lieutenant General Kayumba Nyamwasa, Rwanda’s former Chief of Staff and also ambassador to India fled to South Africa after Kigali accused him of being involved in terrorist activities.

The Kigali government accused Kayumba of working with Col. Patrick Karegeya, Rwanda’s former intelligence chief who had fallen out the powers back home and was living in exile in South Africa. In June 2010 Nyamwasa survived an assassination in Johannesburg. His wife, and later himself, accused the Kagame government of being behind the attack. Again, Rwanda denied the accusation, but the situation between Kigali and Pretoria degenerated badly months later when South African officials claimed that their investigations had established the Rwandese suspected to have been part of the hit squad were operative of Rwandan intelligence. The Rwanda government at that point basically asked South Africa to make a choice between it and the exiles. By the looks of it, Zuma chose his security friends (Kayumba and Karegeya).

Thousands of displaced Congolese walk along a road heading north of Goma in 2008: This is not the past, it is likely to be the future for the people in Eastern DR Congo in 2008: This is not just the past, it looks likely to be eastern DR Congo’s future too (AP hhoto)

While the likeable, generally charismatic, but according to his critics undisciplined, Karegeya was intelligence top dog in Rwanda, his closest friend was Kikwete who was Foreign minister then. Without being gossipy, the two men shared an active interest in the “good things of life”. With his friend president in Dar es Salaam, Karegeya soon was able to sojourn between Tanzania and South Africa, and found comfort and succor from the leaders of the two countries.

And so we are where we are today. Kikwete shares both the same intelligence and southern African liberation fellowship with Zuma. History has placed both men on different sides of the fence from Kagame’s Rwanda. But South Africa is far away from Rwanda, so Kigali needn’t have worried that it could do it harm.

That was not to be. Besides the personal relationships explored here, South Africa too changed. Mandela and Mbeki’s South Africa’s were always shy about their relations with the rest of Africa. Though by far the richest nation on the continent, Mandela and Mbeki didn’t want to be seen to be lording it over other African nations because then their South Africa would look like the one from the apartheid era. Also, because many countries had supported them during the anti-apartheid struggle, they were paralysed by gratitude.
Zuma started to change that. And in Tanzania, Kikwete started to shift from Tanzania’s post-1982-Uganda-campaign disdain for military intervention (its short stint in Comoros peacekeeping notwithstanding).
Even when Rwanda dipped its toes in peacekeeping in Darfur, and Uganda and Burundi – and eventually Kenya – plunged into the Somalia madness, Tanzania was the only EAC nation that stayed out on dry land. Yet today it has its troops in the bitter conflict of the DRC.
And that presents us with the first issue fuelling Rwanda and Tanzania tensions: the fact that Rwanda considers Tanzania a Trojan horse for South Africa’s designs against the Kagame government. And, secondly, that the two have chosen a battlefield close to Rwanda, DRC, to fight this proxy war.

What changed? Why did Zuma abandon the Mandela-Thabo Mbeki era reticence? Is it really true that Kikwete has thrown his geopolitical lot with SADC, and if so why? How come Kenya, a country that has strived to calm the resentment from the break up of the EAC in 1977 by remaining neutral in East African feuds, is in Kagame’s and Museveni’s corner? The questions are endless, and we examine them in the continuation of the series.

MICHELLE OBAMA ALIPOTEMBELEA WAMA FOUNDATION YA SALMA KIKWETE JANA JIONI JULY MOSI 2013

1 bf2ba

Mke wa Rais wa Marekani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA wakati alipotembelea katika ofisi hizo kwa mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa  WAMA Salma Kikwete.

2 6e533

Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.

3 0ba29

Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake  Salma Kikwete

4 5a944

Baadhi ya wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Michelle Obama

5 33e8e

Anna Mkapa ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama katika ofisi za WAMA. {Picha zote kwa hisani ya  http://www.fullshangweblog.com/ }

JUDITH MOSHI ALIYE FARIKI KWENYE TUKIO LA BOMU TAREHE 15 KUZIKWA JUNI 20 SOKONI ONE ARUSHA.

Hawa ndiyo waanga wa tukio la bomu la tarehe 15 Juni 2013 katika viwanja vya Soweto jijini Arusha.

Hawa ndiyo waanga wa tukio la bomu la tarehe 15 Juni 2013 katika viwanja vya Soweto jijini Arusha.

Wananchi wote wenye mapenzi mema, wakiwemo wapenzi na wanachama wa CHADEMA leo Juni 20 katika Hospitali ya Mount Meru Mortuary asubuhi saa 3. ndiyo utakuwa muda wa watu wote kutoa heshima za za mwisho kwa marehemu judith Moshi aliyefariki kwenye tukio la bomu tarehe 15/2013 kwenye viwanja vya Soweto.

shuguli hii itaongozwa na Kamanda Mbowe na Lema.

Quote By mayenga View Post
Judith,
Nina imani usingizi uliolala huwezi tena kuamka. Nilipoangalia video ya tukio lililoondoa uhai wako leo na juhudi za wenzio kukuamsha japo uuone mwanga wa ulimwengu huu kwa mara ya mwisho, hukufanya hivyo. Nimeshuhudia tu kufumba kwa macho yako meno kushikana na kinywa kufumba. Kwangu mimi nina imani kubwa na matendo haya mawili.

Kinywa kinafumba kwa sababu yale uliyopaswa kuyasema uliyasema lakini hawakusikia, na macho yamefumba kwa sababu uliyoyasema na kuyapigania hukuona mabadiliko, ni matokeo hayohayo ya uovu, ufisadi na uzandiki ambayo yamekulaza chini.

Ninayo imani, umeshakutana na Mungu wa kweli mwenye kuumba, pengine huko uliko unayaona yanayotendeka katika nchi hii kwa uwazi zaidi. Mwambie Mungu ya kuwa ni wengi tunatamani kuja kwake lakini kwa matakwa yake, mweleze bila kificho ya kuwa kama atatuchukua kwake kwa njia uliyoenda pengine tutakuwa tunastahili hukumu isiyo yetu. Tuombee japo atupe miaka michache ili ukombozi wa taifa hili uonekane. Mwisho umwambie tunakushukuru kwa zawadi aliyotupa kwa muda ambayo ni WEWE. Mwambie kamwe kuzaliwa na kuondoka kwako kurudi kwake siyo kwa bahati mbaya.

Mwambie kabisa ya kuwa, dalili za ukombozi zinaonekana dhahiri, toa hesabu ya matendo yako na ueleze upepo unavyovyuma kutoka Mtwara mpaka Arusha ni dalili za kitu kamili. Mwambie kusini na Kaskazini watu wako hawaangamii tena kwa kukosa maarifa.

Mwambie kabisa, wanakushukuru na kuzipigania kwa nguvu raslimali na tunu za taifa hili.

Mwisho msihi sana Bwana Mungu wa majeshi ya kwamba, asisimame tena mbali na sisi, joka linataka kutumeza, msaada wake kwa wakati huu ni wa muhimu sana.

Kwaheri Kamanda dada Judith, ulale usingizi wa amani!

Miss Lou Acquiring Lore

Gallery of Life...

MAISHAZONE

ITS ALL ABOUT LIFE......For over 75 years, Jubilee Insurance has built a rich heritage of enriching lives by offering insurance solutions that make life carefree and rewarding.

this is... The Neighborhood

the Story within the Story

JAMIIBLOG

PAMELA MOLLEL

MEDIA 2 SOLUTION

- TRUTH SEEKERS -

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.