VETA WAHASWA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU WAO….

WAZIRI wa Kazi na Ajira , Gaudensia Kabaka wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao.

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wametakiwa kuhakikisha wanasikiliza maoni ya wadau ili kujua mahitaji yao sambamba na kubadili mitaala ya elimu ya mafunzo yanayotolewa kwenye vyuo hivyo ili kuendana na soko la ajira.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Waziri wa kazi na ajira, Gaudensia Kabaka  wakati alipokuwa akizindua kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto sanjari na kuzindua kitabu kinachoainisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana.

Aidha  aliwataka vijana  kutumia fursa za kujiunga na VETA ili waweze kujiajiri na kuzalisha vitu vyenye ubora.

kutoka kushoto ni mwakilishi wa Bg Tanzania Ms Kate Sullam anaemfatia ni Mr Jean Van Wetter ni Mkurugenzi wa VSO Tanzania.

Waziri  Kabaka (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Profesa Idrissa Mshoro wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na  Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi (hayupo pichani) kuhusiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia.

Mwenyekiti wa bodi ya VETA Idrissa Mshoro (kulia), Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi (katikati) wakimsikiliza Waziri hayupo pichani.

Washiriki wakiendelea kufuatilia kwa umakini zaidi.

Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi Zebadiah Moshi akizungumza katika kongamano hilo.

Wadau kutoka sekta ya gesi na petroli nao walishiriki.

Katibu mkuu wa  VET Pro.Sifuni Mchome akiwasilisha mada.

IMG_0186

Waandishi  wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuhoji Mwenyekiti wa bodi ambaye alisema ni vyema sasa Vyuo vya VETA vikaweka mkazo katika sekta ya madini na gesi ili waweze kuangalia mahitaji ya wataalam ni yapi na kutoa elimu hiyo ambayo itawezesha vijana wengi kupata ajira na kukuza uchumi wananchi.

IMG_0160

Waziri wa ajira na kazi, Mh. Gaudensia Kabaka akiwa katika picha ya pamoja wadau waliohudhuria katika kongamano hilo.

IMG_0164

Picha ya pamoja ya washiriki wa kongamono hilo wakiwa pamoja na waziri wa ajira na kazi nje ya ukumbi wa hoteli ya Naura Springs iliyopo ndani ya jiji la Arusha.

 

 

 

Advertisements

WARIOBA ATILIA SHAKA MAAMUZI YA BUNGE JUU YA ESCROW

Makamu wa kwanza wa rais na waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na kutoa maazimio manane kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi huo kwa kuwa nazo zinahusika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.
Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa, mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na wizara hizo kuachwa.
“Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga urais mwaka 2015.”
Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6 milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni, nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani wakati ilikuwa Sh20 milioni.
“Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, waliweka saini tu,” alisema.
Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na ile ya Viwanda.
“Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya kamati imesema Kampuni ya PAP kwa kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA walidanganya. Hivi suala la kudanganya linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa juu hawahusiki?”
Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo, hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo… “Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika. Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje wengine waachwe wakati imeonekana wazi kuwa Serikali imepata hasara?”

Waliopata mgawo

Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa, lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo katika magunia hawakutajwa.

“Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata ukichukua fedha katika gunia lazima benki itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua. Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni dalili za kulindana.

Msingi wa uamuzi

“Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo walisema fedha za escrow ni za umma na wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma. Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda haki,” alisema.
Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo utakapomalizika… “IPTL imeendelea kutoa huduma na umma umepata umeme kutoka katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo. Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote katika kipindi kile ambacho walikuwa hawajakubaliana.
“Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.
“Kama fedha hizo zingekuwa za umma zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi zilikuwa kiasi gani.”
Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni kodi ambayo haikuwekwa wazi.“Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji. Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara wanayoisema na haihusiani na escrow kwa sababu hata kama escrow isingekuwa na matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu wa kawaida,” alisema.

Source:- Gazeti la Mwananchi

BBC SASA KUNGURUMA KUTOKEA DAR ES SALAAM

19Idhaa ya kiswahili ya BBC imezindua rasmi studio zake za jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ni matokeo ya mkakati na uwekezaji wa miaka mingi wa shirika la BBC duniani kuhakikisha kuwa matangazo yake yanawafikia wasikilizaji katika hali ya ubora wa hali ya juu na ya kisasa zaidi.

2

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika ofisi hizo hizo mpya zilizoko eneo la Mikocheni, mkuu wa kitengo cha uandishi wa habari katika BBC, Nicki Clarke, ameshukuru serikali ya Tanzania, kwa kuwaruhusu kujenga studio hizo za kisasa zitakazoinua tasnia ya habari nchini humo na uhuru wa habari kwa ujumla.

7

Naye mkuu wa ofisi ya Dar es Salaam, Hassan Mhelela mbali na kuwataka wafanyakazi wa BBC Tanzania, kuzidi kuonyesha ushirikiano pamoja na utendaji kazi wa pamoja, pia ametangaza kuanishwa rasmi kwa ushirikiano kati ya BBC na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari.

11

Ushirikiano huo amesema kuwa unalenga kusaidia kutoa mafunzo kwa wandishi wa habari chipukizi walioko mafunzoni katika chuo hicho, ambao kwa nyakati tofauti, watakuwa wakijiunga na BBC ili kupata mafunzo katika uandaaji vipindi vya redio na televisheni pamoja na utangazaji.

22

Kwa upande wa BBC, kuanzishwa kwa ofisi hii, yenye studio za kisasa kabisa za redio na televisheni mbali na kuongeza ubora wa vipindi lakini pia kutawezesha matangazo ya redio na televisheni kufanyika moja kwa moja kutokea Dar es Salaam.

Na kuanzia sasa matangazo ya Amka na BBC yatakuwa yakiandaliwa Dar es Salaam.

Itakumbukwa kuwa Tanzania mbali na kuwa na wasikilizaji wengi wa idhaa ya kiswahili ya BBC, lakini pia ndiko kunakozungumzwa zaidi lugha ya kiswahili.

Tanzania pia ina rekodi ambapo mtangazaji wa kwanza au sauti ya kwanza iliyosikika mwaka 1957, ilikuwa ya mtanzania Oscar Kambona ambapo alikuwa mwanafunzi mjini London.

26

12

13

14

16

17

18

22

25
Chanzo: BBC Swahili

SERENGETI FIESTA 2014 MOTO WA KIVU MWANZA.

Wasanii mbalimbali jana August 9, 2014. waliwaburudisha mashabiki wa muziki wao katika tamasha la Serengeti Fiesta jijini Mwanza.

Diamond na Linah
Diamond na Linah

Miongoni mwa wasanii waliotoa burudani ni pamoja na Stamina,Madee,Dogo Janja,Jokate, Nay wa Mitego,Nyandu Tozi, Mr Blue, Diamond, Chege na Temba na wengine wengi. Hizi ni picha za show hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Aslay
Aslay

Barakah De Prince
Barakah Da Prince

Chege na Temba
Chege na Temba

Diamond
Diamond

DJ Fetty na Adam Mchovu
DJ Fetty na Adam Mchovu

Dj Fetty
Dj Fetty

Edo Boy super nyota 2013.
Edo Boy Super nyota 2013.

Linah
Linah

Makomando wakifanya yao
Makomando wakifanya yao

Mo Muciz
Mo Music

Mr Blue
Mr Blue

Mshindi wa serengeti super Nyota mkoa wake
Mshindi wa Serengeti super Nyota

Shangwe za mashabiki wa Mwanza
Shangwe za mashabiki wa Mwanza

Vanessa Mdee
Vanessa Mdee

Vannesa Mdee

Wadau wakishangia
Mashabiki wakishangilia

Watu wakipata burudani
Watu wakipata burudani

Yamoto Band
Yamoto Band

Young Dee
Young Dee

Young Killer Msodoki akiwa kwenye hisia
Young Killer Msodoki akiwa kwenye hisia

IMG_3635

IMG_3638

IMG_3656

IMG_3667

IMG_3669

IMG_3675

IMG_3678

IMG_3685

IMG_3690

IMG_3693

IMG_3695

IMG_3733

IMG_3761

IMG_3769

IMG_3770

IMG_3772

IMG_3776

IMG_3784

IMG_3791

IMG_3797

IMG_3804

IMG_3826

IMG_3841

IMG_3844

IMG_3846

IMG_3865

IMG_3866

IMG_3874

IMG_3897

IMG_3900

IMG_3901

IMG_3903

IMG_3904

IMG_3905

IMG_3907

IMG_3910

IMG_3912

IMG_3913

IMG_3917

IMG_3939

Picha zote kwa hisani ya bongo 5
//

“WAHENGA WALINENA UTAVUNA ULICHOPANDA, MAPENZI TELE KWA KILA MTU”, LADY JAYDEE

Lady Jaydee

Lady Jaydee  July 27 alitangazwa kuwa washindi katika tuzo za AFRIMMA 2014 nchini Marekani alipo shinda kipengele cha mwanamuziki bora wa kike Afrika mashariki. Tuzo hizo ziliwashindanisha wanamuziki mbalimbali wakubwa wa Afrika.

Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa Facebook aliwashukuru mashabiki wake, aliandika:

“Nashukuru wote mnaokubali kazi zangu, wote mnaosimama na kutetea JayDee bila kusita, nashukuru kwa Tuzo nyingine tena toka AFRIMMA . Wahenga walinena kuwa utavuna ulichopanda, mapenzi tele kwa kila mtu”

jide afrimma

Katika post nyingine Jide amepost picha ya tuzo yake na kuandika:

“Tuzo yangu ya 30. Asanteni kwa ushirikiano, nimeipokea na ninarudi nayo nyumbani. Shhhhhh! !!! Kimya Kimya”.

MOVIE REVEW;- KITU CHA COVERT AFFAIRS SEASONAL 1

Covert-Affairs-USA-Network-poster-season-1-2010

Kitu cha Covert Affairs mpaka sasa kinaendelea kuonyeshwa kwenye TV network za marekani ambapo imefikia Seasonal 5. Kwa maana hiyo unaweza kujipatia mpaka Seasonal 4.

Seasonal 1 ina jumla ya Episodes 11, Story hii inaanza pale mwanadada mwenye umri wa miaka 28 Annie Walker, anapoitwa ghafla kutoka mafunzoni ya upelelezi na shirika la kijasusi la CIA nchini Marekani ili kufanya kazi maalum. Ofisi ya CIA ilieleza kuwa walimchagua kutoka miongoni mwa wanafunzi wenzake kutokana na umakini katika mafunzo maalum, Sifa nyingine ya ziada ni uwezo wake wa kuzungumza kwa ufasaha lugha za Kirusi, kitaliano, Kihispania, Kijerumani, Kifaransa, Kiajemi, Kireno na lugha nyingine kadhaa.

Alipo wasili CIA alikabidhiwa kwa Jasusi Agosti Anderson, jina la utani “Auggie” ambaye amepoteza uwezo wake wa kuona alipokuwa kwenye operation nchini Iraq, Idara hiyo ikiongozwa na jasusi Joan Campbell, ambapo yeye alikuwa na wajibu wa kumpa msaada wa kiufundi.

Original Title: Covert Affairs
Country, Channel: USA, USA Network
Release Date: June 13, 2010
Genres: Action, Crime, Drama, Mystery, Thriller
Creators: Chris Ord, Matt Corman
Cast: Piper Perabo as Anne Catherine “Annie” Walker, Christopher Gorham as August “Auggie” Anderson, Kari Matchett as Joan Campbell, Anne Dudek as Danielle Brooks, Sendhil Ramamurthy as Jai Wilcox, Peter Gallagher as Arthur Campbell, Emmanuelle Vaugier as Liza Hearn, Gregory Itzin as Henry Wilcox, Eion Bailey as Ben Mercer, Noam Jenkins as Vincent Rossabi, Oded Fehr as Eyal Lavin

Runtime: 60 min
Language: English

Kama unaitaji movie hii au nyingine zozote wasiliana nasi kwa simu +255 732 981 189

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA.

Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana.

PRINCE AKISHINO NA MKEWE WAFURAHI WIKENDI YAO SERENGETI NA NGORONGORO

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MP) inamkaribisha Prince Akishino na mke wake Princess Kito kutoka Japan kwenye kiwanja kidogo cha ndege cha Manyara tayari kwa ziara yao ya Ngorongoro Crater na Serengeti National Park mwishoni mwa wiki.

 

 

Princess Kito wa Japan akipokea shada la maua kutoka kwa Bi. Lilian Sukhe wa Bodi ya Utalii Tanzania wakati wa mapokezi yao kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Manyara tayari kwa ziara yao ya Ngorongoro Crater na Serengeti National Park mwishoni mwa wiki.

 

 

Kikundi cha utamaduni cha kabila ya Wamasai wakimburudisha Prince Akishino na mke wake Princess Kito walipofika Loduare Gate, Ngorongorto Conservation Area.

 

 

Prince Akishino na mke wake Princess Kito waliamua kufanya matembezi ya miguu kwa muda mfupi ndani ya mbuga za Serengeti National Park.

 
Kaimu Mkuu wa Mkoa Mara Bi. Angelina Mabula akimkabidhi zawadi ya kinyago cha tembo Prince Akishino mara baada ya kumaliza dhihara yao Serengeti National Park.

WAKAZI MTO WA MBU NA WAFANYAKAZI WA HIFADHI YA ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA

DSC_0281

DSC_0285

DSC_0286

DSC_0290

DSC_0292

DSC_0296

DSC_0301
Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani

WAKAZI HAO WA KATA YA MTO WA MBU waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko

Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbal;i wanaokuja kutembelea mbuga hizo

Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu.

SOURCE:- MAHMOUD AHMAD

PRINCE AKISHIO NA MKEWE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Mwana wa Mfalme wa Japan Prince Akishino na mkewe Princess Kiko leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuona jinsi inavyotoa huduma zake kwa Watanzania.

Akitoa salamu za pongezi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa amesema Hospitali imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA katika maeneo mbalimbali ya huduma ikiwemo ujenzi wa maabara maalumu ya watoto, ujenzi wa Kituo cha Maelezo ya Afya Muhimbili pamoja na kuongeza uwezo wa Hospitali katika kuboresha huduma zake kupitia mpango wa uboreshaji huduma (quality improvement program).

Katika ziara yao, wametembelea Jengo la watoto kitengo cha watoto walioungua moto, wodi ambazo zimekidhi viwango vya ubora wa huduma, na jengo la wazazi ili kuona namna ambavyo akina mama wanapata huduma za afya ya mama na mtoto.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa akisalimiana na Prince Akishino wakati alipowasili Hospitalini hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Dkt. Mahadhi Juma Maalim.

Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko wakifurahia jambo katika mojawapo ya wodi za watoto ambazo zimekidhi viwango vya program ya uboreshaji wa huduma.

Mkuu wa Idara ya Afya ya Akina Mama Dkt. Mathew Kallanga akitoa ufafanuzi kwa Prince Akishino kuhusu idara yake inavyowahudumia akina mama.

Princess Kiko akifurahia na akina mama baada ya kuona mtoto aliyekuja kliniki.

TACAIDS WAONGEA NA WANAHABARI KWENYE VIWANJA VYA SABASABA JIJINI DAR

Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa

 

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Genofeva Matemu)

SAFARI YA MWISHO YA MWANAHABARI NGULI NCHINI, MZEE NKWABI NG’WANAKILALA

Mwanahabari wa Reuters nchini Bw. Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Mzee Nkwabi Ng’wanakilala enzi za uhai wake.

Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.

Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO BW. Raphael Hokororo (kati) akiwa na wadau wa habari waliokuwepo mazishini

Miss Lou Acquiring Lore

Gallery of Life...

MAISHAZONE

ITS ALL ABOUT LIFE......For over 75 years, Jubilee Insurance has built a rich heritage of enriching lives by offering insurance solutions that make life carefree and rewarding.

this is... The Neighborhood

the Story within the Story

JAMIIBLOG

PAMELA MOLLEL

MEDIA 2 SOLUTION

- TRUTH SEEKERS -

The WordPress.com Blog

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.