WORLD SOCIAL FORUM TUNIS

Wanaharakati na wapigania ukombozi wa kijamii na kisiasa wanajumuika Tunis kuanzia 26-30 March 2013 kama njia ya kuonyesha umoja wao na kupaaza sauti dhidi ya udhalimu na unyonyaji.Nawaletea habari kwa picha ikiwemo mwanaharakati wa jinsia na mwanabadiliko Jovitha Mlay akijiachia kwenye maandamano ya ufunguzi wa Tamasha.

WSF(6)

wsf4

wsf2

wsf1

wsf(9)

Advertisements

WAZIRI MKUU, PINDA ALIPOTEMBELEA VATICAN


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakifanya mahojiano na mtangazaji wa Radio Vatican, Padri Richard Mjigwa (katikati) kweye moja kati ya studio za Raido hiyo Mjini Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Diuniani, Papa Francis 1 Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakiongozwa na Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa Benedikti, Roma kutoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma walikohudhuria sherehe za kumsimikwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 kwenye viwanja vya Kanisa hiloMachi 19,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakipata maelezo kuhusu historia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma kutoka kwa Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa wa Benedikti, Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Machi 202013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Chakula (FAO), Jose Graziano da Silva wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva kabla ya kusaini kitabu cha wageni baadae walifanya mazungumzo yao katika makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva baada ya mazungumzo yao wakati alipotembelea makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AFRICAN BARRICK GOLD KUTENGA DOLA MILIONI 10 KILA MWAKA KWA AJILI YA UWEKEZAJI

Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG Greg Hawkins akizungumzia Mfuko wa Maendeleo wa ABG amesema mpaka sasa mfuko huo umewekeza dola za Marekani milioni 2.2 (zaidi ya shilingi bilioni 3.6) kusaidia kuboresha afya ya umma kwenye jamii zinazo zunguka migodi yake.

Amesema kwa upande wa elimu, Mfuko umetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 1.9 (takriban shilingi bilioni 3) kuwekeza kwenye sekta muhimu na kuwa uwekezaji wa mfuko huo umesaidia kujenga shule mpya na kuongeza idadi ya madarasa kwenye shule nyingine ili kuwapa watoto wengi zaidi fursa ya kupata elimu bora.

Vice President Corporate Affairs Deo Mwanyika (kulia) amesema lengo kubwa la kuwepo kwa mfuko huo ni kutaka kuhakikisha jamii iliyozunguka migodi hiyo inafaidika na kuwa lmtazamo bado uko katika masuala muhimu kama elimu, masuala ya maji, masuala ya afya na kwa kiasi Fulani masuala ya miundo mbinu.

Akizungumzia mgodi wa North Mara uliopo wilaya ya Tarime, amesema Mfuko umewekeza dola za Marekani 800,000 (sawa na shilingi bilioni 1.3) kwa ajili ya kuchimba visima vya maji ili kuwasaidia wananchi wapate maji safi na salama ya kunywa.

Corporate Manager – community Relations Steve Kisakye (wa pili kulia) akifafanua jinsi Mfuko huo unavyoweza kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali, ambapo ili kuboresha maisha ya jamii zinazozunguka migodi hiyo minne, Mfuko wa Maendeleo wa ABG umeweka dola za Marekani milioni 1.4 (zaidi ya shilingi bilioni 2) kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.

Mfuko wa Maendeleo wa African Barrick Golg ulioanzishwa mnamo Septemba 2011 umeweza kusimamia uwekezaji wa kampuni ya ABG kwenye jamii katika kipindi cha miezi 18 iliyopita na kufanikiwa kutekeleza zaidi ya miradi 50 yenye thamani ya dola za marekani milioni 7.5 (takriban shilingi bilioni 12) katika kipindi cha mwaka 2011/2012.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam  leo Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG Greg Hawkins amesema wanafurahi kuona mafanikio makubwa ambayo Mfuko wa maendeleo wa ABG umeyapata kwenye kipindi cha miezi 18 mpaka sasa.

Ameongeza kuwa walianzisha Mfuko huo kama sehemu ya jitihada zao za kuchangia kwenye maendeleo endelevu nchini Tanzania na tayari mafanikio makubwa yameonekana kwenye zaidi ya miradi 50.

Mfuko wa Maendeleo wa AGB unashirikiana na jamii husika kubaishinisha vipau mbele vyao ili wanajamii wenyewe wawe mstari wa mbele kwenye utekelezaji wa miradi.

Kampuni ya ABG inalipa gharama zote za uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo wa ABG ili kuhakikisha kuwa asilimia kuwa asilimia 100 ya fedha za Mfuko huo zinaenda moja kwa moja kwenye miradi ya jamii.

LWAKATARE KAACHIWA KWA DHAMANA NA KUKAMATWA TENA

Wilfred Muganyizi Lwakatare, akionesha alama ya vidole viwili

Wilfred Muganyizi Lwakatare, akionesha alama ya vidole viwili wakati akitokea Maakamani leo.

Alfred Muganyizi Lwakatare pamoja na Ludovick Joseph Rwezaura walifikishwa Mahakamani hapo Jumatatu iliyopita na kusomewa mashtaka manne: moja la kula njama na matatu ya ugaidi.Walisomewa mashtaka hayo kwa Sheria mbili tofauti. Ya kwanza ilikuwa ni Kanuni ya Adhabu,Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania ambayo ilitumika kwa shtaka la kul ya kula njama.Sheria ya pili ni Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002 iliyotumika kwa makosa matatu ya ugaidi.

Baada ya kusomewa makosa manne(matatu kwa wote na moja kwa Lwakatare pekee),Mawakili wanaomtetea Lwakatare: Profesa Abdallah Jumbe Safari,Peter Kibaatala na Tundu Antipas Mughwai Lissu walitoa hoja za kumwombea dhamana mteja wao,Alfred Lwakatare. Wakili Mkuu wa Serikali Kanda ya Dar es Salaam,Rweyongeza alipinga vikali. Baada ya mabishano ya kisheria,leo ilipangwa kuwa siku ya Mahakama kutoa uamuzii juu ya hasa ombi la dhamana.Leo,Wakili wa Serikali aliomba ridhaa ya kuondoa makosa matatu ya ugaidi dhidi ya washtakiwa na kubaki na moja la kula njama. Hakimu akaridhia.Hati ya Mashtaka ikabaki na kosa moja la kula njama ambalo lina dhamana. Hakimu akatoa dhamana kwa washtakiwa wote kiurahisi kabisa. Kosa la kwanza! Leo haikuwa siku ya kuzungumziwa kesi. Iweje Wakili wa Serikali awasilishe maombi hayo na uamuzi mwingine nao ufanyike?

Alichotakiwa kukifanya,kwa ufinyu wangu wa kuelewa,ni kuwasilisha ombi lake la kurekebisha hati ya mashtaka na kuomba ahirisho hata fupi tu.Hajafanya hivyo. Wakili wa Serikali amefanya kosa kisheria na kiuhalisia.

Tena,Lwakatare alikamatwa tena kwa makosa ya ugaidi ili eti akashtakiwe mahakama stahiki ambayo ni Mahakama Kuu. Kwani Mahakama ya Hakimu Mkazi kama Kisutu ni mara ya kwanza kuanza kushughulikia kesi ambazo haziruhusiwi kusikilizwa hapo? Mbona hata ya Papaa Msofe,tena ya mauaji,inashughulikiwa Mahakamani hapo hapo?

Hii ni danganya toto na ni mbinu za Ofisi ya DPP kupoteza muda na kujipanga. Kuachiwa kwa dhamana halafu kukamatwa tena si suala jipya.Wapo hata walioachiwa huru kabisa na kukamatwa tena.Lina ruhusa kisheria. Lakini,si kama ilivyofanyika leo.

Kosa la kwanza la DPP ni kuchanganya makosa ya kutoka sheria mbili tofauti na kuyapeleka Mahakama moja huku akijua fika kuwa atayagawanya makosa hayo na Mahakama zake. Kosa la pili ni kuwasilisha maombi siku ya uamuzi. Ni vyema makosa kama haya ili haki itendeke na ionekane inatendeka.

ISHARA ZA MAUAJI YA KIMBARI ZI WAZI TANZANIA; KIJO-BISIMBA

Dr-Helen-Kijo-BisimbaTanzania imekuwa ikijulikana kama kisiwa cha amani na hivyo kuwa kimbilio la wakimbizi kutoka nchi jirani. Hata hivyo kwa takribani miaka mitatu tumeshuhudia amani hiyo ikitoweka kwa kuwepo matukio mbalimbali yanayohusiana na itikadi za kidini yanayojenga mazingira ya kutokea kwa mauaji ya halaiki (mass killings) au ya kimbari (genocide). Kwa muda mrefu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekuwa kikifuatilia hali ya kuendelea kupungua kwa uvumilivu (tolerance) baina ya vikundi vyenye misimamo tofauti ya kisiasa au vile vinavyotofautiana kwa imani za dini. Kupungua kwa uvumilivu wa kisiasa kulianza mwishoni mwa miaka ya 1990 na kwa wakati huo hali ilikuwa tete zaidi kwa upande wa Tanzania Zanzibar. Kwa upande wa Tanzania bara hali hiyo ilikuwa ikijitokeza zaidi wakati wa chaguzi ndogo. Kwa ujumla uvumilivu wa kidini haukutetereka sana kama ulivyokuwa uvumilivu wa kisiasa. Hata hivyo, hali ya kupungua kwa uvumilivu wa kidini ilianza kujitokeza kwa kasi zaidi kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010 wakati ambapo baadhi ya wanasiasa walitumia dini kama kiungo cha kupata madaraka na kuweka mambo mbalimbali yanayohusiana na dini kwenye ilani za uchaguzi. Aidha wakati huohuo viongozi tofauti wa kidini walitoa matamko kadha wa kadha kuhusiana na mustakabali wa taifa.

Mara baada ya uchaguzi huo, tulishuhudia baadhi ya taasisi za dini zikiitisha makongamano kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa. Mengine yakiendelea kuonesha kutoridhishwa na muelekeo wa maendeleo ya taifa na mengine yakikejeli au kujaribu kutoa majibu kwa makongamano menza ya dini kwa kuutetea mfumo uliopo. Aidha yapo makongamano mengine yaliyokwenda mbali zaidi na kuanza kushutumu kuwa nchi ya Tanzania inaendeshwa kwa ‘mfumo kristo’. Kwa sababu hiyo kumekuwa na vipeperushi, kanda, makongamano kuzunguka mikoa yote ya Tanzania, vipindi vya radio na magazeti yakitoa kauli zinazojenga chuki za kidini miongoni mwa wananchi wa Tanzania. Pamoja na harakati zote hizo, Kituo kilishtushwa kwa kuona kuwa hakukuwa na hatua madhubuti zilizochukuliwa na serikali ili kuzuia kuendelea kujenga chuki za kidini. Matokeo yake Tanzania ilishuhudia kuchomwa kwa Makanisa, kuharibiwa kwa mali mbalimbali, kuumizwa kwa watu mbalimbali na hata kuuwawa kwa viongozi wa dini. Kwa muhtasari – tangu mwaka 2010 Kituo kimeweka kumbukumbu ya matukio kumi na tisa (19) yanayohusiana na vurugu za kidini na hakuna hatua yoyote makini inayochukuliwa na vyombo husika kuzuia hali hii.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinahofu kuwa, ikiwa hali hii ikiachwa bila udhibiti inaweza kabisa kulifikisha taifa katika mauwaji ya halaiki, vita ya wenyewe kwa wenyewe au hata mauaji ya kimbari. Kitaalam mauaji ya kimbari huweza kupitia katika hatua nane, na ya kwanza ni Ubaguzi (classification) ambao watu hujiita sisi dhidi ya wao na kuanza kuwatenga wale walio tofauti. Kwa mfano kabila dhidi ya kabila na dini dhidi ya dini (ukristo dhidi ya uislam. Pili ni kutoa majina au alama (symblolization) ambazo huonyesha chuki dhahiri na kuwaita majina mabaya waliotofauti. Ukifuatilia kwa kina vipeperushi, jumbe katika mikutano na kanda utaona majina mbalimbali wanayopewa waumini wa dini ya kikristo dhidi ya waislam [kwa mfano Makafiri]. Hatua ya tatu ni udhalilishaji (dehumanization) ambapo mhusika huwaondolea heshma ya utu wale wote wanaotofautina naye na kuwaweka kwenye daraja la chini kama vile ni viumbe duni wasio na hadhi ya ubinadamu. Katika hatua hii, kundi fulani huhesabu kuwa dini/imani/dhehebu/itikadi yao fulani ni bora kuliko nyingine hivyo kuanza kuwadhalilisha wote wasiokuwa wa dini/imani/dhehebu/itikadi yao. Hatua ya nne ni kujiunga pamoja au kujiratibu (mobilization) kwa kuanza kuandaa mipango, kutoa mafunzo ya chuki na kubuniwa mbinu na hatua mbalimbali za kuchukuwa dhidi ya watu waliotofauti. Tano ni mgawanyiko/kambi mbili (polarization) ambapo kauli za kuchochea chuki na propaganda kusambazwa. Hatua ya sita maandalizi (preparation) kuwatambua rasmi watu tofauti na kuwatendea kama adui na kuwajengea mazingira ya kuwashambulia. Hapa watu wanatayarisha silaha, wapiganaji wa kichinichini kama tunavyosikia huko ukerewe na sehemu zingine ambazo hatujazijua bado. Hatua ya saba maangamizi (extermination) ambayo ni mauaji yaliyoratibiwa na kufanyika mfululizo kwa utaratibu maalum dhidi ya kundi moja. Ikiwa katika hatua hii mauaji hayo yatafanikiwa ndiyo huitwa mauaji ya kimbari(genocide) na ikiwa walengwa wataamua kupambana ndipo hutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe (civil war). Hatua ya mwisho ni kukanusha (denial). Katika hatua hii, mara zote wauaji na vizazi vyao vilivyopo na vitakavyokuja mara zote hujitahidi kukanuasha kuwa hayo hayakuwa mauaji ya kimbari ila ilikuwa ni kulipiza kisasi, kusafisha jamii dhidi ya uchafu, kuadhibu waasi, au kuwaondoa vibaraka.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, baada ya kufanya ufuatiliaji wa karibu na kuweka kumbukumbu ya matukio mbalimbali ya nayohusiana na kukosekana kwa uvumilivu wa kidini, kinatoa wito ufuatao kwa Seikali, taasisi za kidini na wananchi:

Serikali:
i) Serikali ichukue hatua za haki na za dhati katika kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wale wote wanaohusika na harakati za kuondoa uvumilivu wa kidini katika nchi yetu
ii) Serikali ihusike katika kupiga marufuku vyombo vya habari, mikutano na matangazo yote yanayoeneza chuki, ikiwa ni pamoja na kuondoa vipeperushi, kanda na nyaraka zozote yanayochochea chuki na zinazohatarisha taifa kutumbukia katika mauaji ya kimbari
iii) Serikali isimamie sheria na katiba ya nchi kuhakikisha kuwa uhuru wa kuabudu pamoja na uhuru wa maoni hautumiwi vibaya na kuhatarisha usalama wa taifa na watu wake.
iv) Serikali ishughulikie kero za watanzania waliowengi ambao huweza kusadiki propaganda yoyote kutokana na wingi wa mahitaji yao ya kila siku kama elimu, afya, maji, chakula, ajira na malazi.

Taasisi za Dini:
i) Kila taasisi ya kidini iheshimu ibara ya 19 ya Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa kuabudu dini tunayoitaka na kuheshimu imani za wengine.
ii) Viongozi wa dini waweke mkazo na kuwahimiza waumini wao kuhusu umuhimu wa uvumilivu wa imani tofauti kama moja wapo ya nguzo kuu za amani ya taifa.
iii) Viongozi wakuu wa dini, wakaripie na kuwachukulia hatua wenzao wanaotoa kauli zinazoashiria chuki na uvunjifu wa amani

Wananchi:
i) Wananchi wa Tanzania tukatae kutumiwa na wanasiasa au viongozi wa dini wanaotuhamasisha kugombana baina yetu kwa misingi ya dini
ii) Wananchi tuendeleze amani ya taifa letu kwa kuheshimu imani ya kila mmoja ili kuliepusha taifa na mauaji ya kimbari au vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vitatuongezea zaidi shida kuliko kutatua matatizo tuliyonayo
iii) Wananchi tuchukue hatua ya kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama pale watu wanapotoa kauli na propaganda zinazochochea chuki miongoni mwa jamii

Imetolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Dr.Helen Kijo-Bisimba,
Mkurugenzi Mtendaji.

A CONCERT IS CUT SHORT AFTER RAPPER TONE LOC COLLAPSES ON STAGE.

TONE

Rapper Tone Loc has collapsed on stage during a performance in Iowa.

 Loc, whose real name is Anthony T Smith, collapsed after finishing a song during a night concert on a bridge in central Des Moines.

 According to the Des Moines Register newspaper, the concert ended abruptly and fans were asked to leave while the 47-year-old was treated.

 Police sergeant Steve Woody said paramedics responded after Loc collapsed, but the singer refused to be taken to hospital.

 The rapper’s condition was not immediately clear. He was not listed publicly as a patient at any Des Moines hospital.

 Loc’s representative did not immediately respond to phone and email messages.

In 2009, Tone Loc collapsed on stage after apparently overheating

 It is not the first time the rapper has collapsed on stage.

 Loc, who is best known for his 1980s hits Funky Cold Medina and Wild Thing, collapsed and had a seizure during a 2009 concert in Pensacola, Florida, after authorities said he had apparently overheated.

 He also collapsed in 1995 while attending a Los Angeles Lakers game with no reason provided.

 Loc has also appeared in a number of television shows and movies, including Ace Ventura: Pet Detective with Jim Carrey and Heat with Al Pacino.

 He has also been the voice of several animated characters.

ZIMBABWE WANANCHI WAUNGA MKONO KATIBA MPYA

???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

Wapiga kura nchini Zimbabwe wameunga mkono mabadiliko ya katiba.

Katika kura ya maoni iliyopigwa mwishoni mwa wiki ililopita, asilimia 95 ya wapiga kura hao wamepiga kura ya ndio.

Kura hiyo imetayarisha mchakato wa uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu, ambao utamaliza kipindi cha utawala wa mpito wenye mivutano, unaoshirikisha rais Robert Mugabe na mpinzani wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.

Mabadiliko hayo ya katiba yanaweka kikomo cha mihula miwili ya miaka mitano kwa rais, na yanalipa bunge madaraka makubwa.

Mabadiliko hayo hali kadhalika yanaondoa wadhifa wa Waziri Mkuu.-DW.

NINAVYOMFAHAMU LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA. (KILIO CHA USALITI)

Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:

USALITI;

Usaliti ni neno pana sana…,

Lina madhara mengi sana…,

Hujuma hukwamisha mambo mengi sana…,

Tamaa huzaa usaliti…,

Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini…!

Baada ya Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukio ya kigaidi.

Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION “BAED”) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.

Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na Chadema na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga chadema.(LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history&political science).

Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa Chadema kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama. Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya Chadema, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na “mwanzilishi pekee” wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa Chadema mimi Nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo.

Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling’atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang’ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.

Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya Chadema kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii (ikiwemo JF kwa ID ya MPEPO)

Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha , ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.

Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-

 1. LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.

 2. Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya Chadema na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa Chadema.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)

 3. Credit nyingine aliyoipata kwa Dr Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A sabasaba.

 4. Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.

Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.

Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chadema kwa kupanga ba kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka Chadema, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa jamiiforums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.

PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU……….,INAHUZUNISHA..!

Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.

Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na Chadema ambao idadi yao ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa Chadema wamekana kumtambua LUDOVICK.,ni USALITI KIASI GANI HUU..?

Mawakili wote watano ambao ni:-

 1. MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA

 2. ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA

 3. NYARONYO KICHERE

 4. TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI

 5. PETER KIBATALA

Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? ama kama si hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea Chadema, pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama hicho.

ANGALIZO:

Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.

Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.

Chanzo: www.jamiiforums.com Na Mtela Mwampamba

MKANDA WA VIDEO UNAOITWA VIDEO YA LWAKATARE HUU HAPA

 

Wahandishi wamegawanyika katika sakata hili la kutekwa, kuteswa na kunyofolewa kuchwa kwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya New Habari, Absolom KIbanda na unaoitwa mkanda wa video wa Willifred Lwakatare ila lililo wazi ni kuwa kwa sehemu moja  TISS inahusika, lakini si bado akuna uakika kama ndiyo waanzilishi wa mkati huu uliopewa jina la operation funga kazi.

TUTASIKIA MENGI NA KUONA PIA

KIKWETE ZIARANI AFRIKA YA KUSINI, AMTEMBELE KIBANDA

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini jana jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).

Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Freeedom Park mjini Pretoria Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyioshiriki katika harakati za ukombozi Kusini Mwa Afrika.

Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini(Katikati) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa vyama vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika leo mchana.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa FreedomPark,Jijini Pretoria Afrika ya Kusini. Kushoto ni Rais Jakaya Kikwete mbaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni kiongozi wa ZANU PF.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini ambaye pia ni kiongozi wa ANC(Watatu kushoto), Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika ya Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC.(picha na Freddy Maro).

ZAIDI YA WATU 2000 WAJITOKEZA KUMZIKA BENSON MOLLEL

Clip 61

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 62

Mama na Baba Mzazi pamoja na wadogo wa Marehemu aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 4

Wachungaji walioendesha Misa ya kumuombea Marehemu aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha, Misa hiyo ilifanyika nyumbani kwao kata ya Elerai jijini Arusha.

Clip 5

Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mazishi aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 10

Msafara wa vijana wa CCM walio beba na kuusindikiza Mwili aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha. kwenda kwenye nyumba yake ya milele.

Clip 11

Msafara wa vijana wa CCM walio beba na kuusindikiza Mwili aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha. kwenda kwenye nyumba yake ya milele.

Clip 12

Msafara wa vijana wa CCM walio beba na kuusindikiza Mwili aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha. kwenda kwenye nyumba yake ya milele.

Clip 16

Msafara wa vijana wa CCM walio beba na kuusindikiza Mwili aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha. kwenda kwenye nyumba yake ya milele.

Clip 22

Mama mzazi wa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha. alishindwa kujizuia baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wake.

Clip 23

Mama mzazi wa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha. alishindwa kujizuia baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wake.

Clip 25

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akitoa heshima zake za mwisho mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 26

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Limo Mwenye suti nyeusi akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 31

Mmoja wa waombolezaji walio fika kwenye msiba wa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 34

Naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele katikati mwenye nguo za kijani na kofia akifwatilia kwa makini shuguli za mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26) aliyefariki siku ya Jumapili ya Tarehe 3 March 2013 katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 35

Clip 38

Mfanya Biashara maharufu wa Madini Jijini Arusha Bw. Mathias Manga pamoja na mkewe ambaye pia alikuwa mwajiri wa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha, akiweka shada la maua kwenye kaburi.

Clip 40

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli Mh.Edward Lowassa akipeleka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 44

Naibu waziri wa ardhi nyumba na makazi Godluck Ole medeye akipeleka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 45

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akipeleka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 50

Baadhi ya viongozi wa UVCCM kitaifa na Mkoa wa Arusha waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 51

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 52

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 53

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 55

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 56

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 57

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

Clip 60

Baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Mjumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel (26)aliyefariki siku ya Jumapili ya tarehe 3 March 2013 dunia katika hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji la Arusha.

MAELFU WAFURIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU BENSON AKIWEMO LOWASSA

0022222_b8f52

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ametoa pole nyumbani mwa mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa Vijana CCM Benson Mollel aliyefariki katika mazingira ya kutatanisha jana hotelini jijini Arusha. Mh Lowassa akiwapa pole baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu Benson Mollel

002222222_2c582

Mh Lowassa akiwa na mwenyekiti wa CCM Monduli(kulia) Ruben Kunei na mjumbe wa halmashauri kuu taifa NEC (kushoto) Mathias Manga

0022222222_cb1eb

Mh Lowassa akitoa pole kwa mama mzazi wa Mollel nyumbani kwao Daraja Mbili Arusha

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000429

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000431

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000443

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000447

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000532

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000536

KIFO CHA KIONGOZI WA UVCCM_20130306000539

 

 

 

KAZI IMEANZA KENYA… SAFARICOM LAWAMANI KWA UCHAKACHUAJI

KENYA

Kumezuka sintofaham nchini Kenya huku duru za kisiasa za mlengo wa kushoto zikitilia shaka kuhusu utitiri wa matokeo kutoka mashinani na kutoa shutuma kuwa yamechakachuliwa na Injinia wa kampuni ya Simu Safaricom kabla ya kukabidhi matokeo hayo kwa tume ya uchaguzi na vyombo vya habari nchini humo.

Safaricom ni kampuni ya simu iliojitolea kusaidia tume ya uchaguzi kutoka mashinani na kutarajiwa kuzikabidhi kwa wahusika bila ya kuvurugwa kwa namna yoyote ile lakini uhalisia wa mambo haukua hivo.

Hali hiyo ilionekana kumkera sana meneja mkuu wa kampuni hiyo ya simu mara baada ya kubaini kwamba hadi hivi sasa sehemu kubwa ya matokeo yanayorushwa hewani kamwe hayafanani na yale yaliopokelewa na kampuni yake tangu awali kiasi cha kumfanya kuchapisha katika rundo la makaratasi ‘matokeo halisi’ anayodai kuwa ni tofauti kabisa na yale yanayoendelea kuzungushwa kote katika vyombo vya habari nchini humo.

Kwa msingi wa hali hiyo ya sintofahamu katika uchaguzi wa Kenya kuna madai kwamba kuna misururu ya mikutano inayoendelea hadi hivi sasa nyuma ya pazia kutafuta namna gani ya kudhibiti taarifa hizi zisiwafikie wananchi wa nchi hiyo kwa ujumla wao na pengine kusababisha hasira na michafuko.

CORD KENYA CAMPAIGN TEAM RAISES CREDIBILITY CONCERNS OF RESULTS BEING RELEASED

m2s breaking news

CORD Campaign team has raised concerns on the credibility of the results streamed on live TV from the IEBC national tallying centre at Bomas of Kenya.
The CORD national steering committee chairman Franklin Bett accompanied by ODM Secretary General Anyang’ Nyong’o and Lands Minister James Orengo raised several key concerns that puts credibility of results into question. Here are the concerns raised:

 • Collapse of IEBC server for more than six hours puts to doubt the results being released; arguing that if the server has been down for more than six hours, from where are the results are being streamed on live TV coming from?

 • Credibility of the BVR system and ability of IEBC to verify voters. It was reported that BVR kits failed in the better part of the morning at which time IEBC officials resorted to manual register, later in the afternoon the BVR kits started working and IEBC put them into use.

 • IEBC staff caught issuing multiple ballot papers in some regions where the competition has strongperson on the ground.

 • Voting reportedily going on at 2:30am 5th March in Jubilee strongholds of Kimilili, Kitale, Ongata Rongai while in CORD strongholds voting closed on time as per IEBC guidelines.

 • CORD agents denied access into some areas

 • Others was the live streaming of voter results on TV, radio and mobile devices while voting was underway terming it a psychological manipulation of voters who waiting to vote in polling centres.

Bett’s concerns sets the stage for contesting of the results if the CORD concerns are not resolved.

By the time of going to press IEBC, Safaricom and Political Party ICT officials were reported to be in a crisis meeting to discuss the crash of the server and possible remedy.

IEBC is yet to respond to the concerns raised.

UNGANA NASI KUFWATILIA UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI WA KENYA, LIVE KAMA TUNAVYO PATA TAHARIFA BILA CHENGA

m2s breaking news

16:27 :Sehemu nyingi za starehe na ulevi mjini Nyeri Mkoa wa Kati zimefungwa na zitafunguliwa Jumanne ili kuwaruhusu wapiga kura kupiga kura. Eneo la Mkoa wa Kati lina tatizo la uraibu wa pombe

16:24: Ng’endo Angela ambaye yuko Mooa wa Kati ansema kuwa kuwa sababu ya hitilafi za kimitambo, tume imelazimika kutumia mfumo wa kawaida kwa kutumia daftari za wapiga kura. Ni Nyeri peke yake ambako shughuli hiyo ilifanikiwa kwa njia ya Elktroniki

15:54 Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema kuwa foleni mjini Nakuru zimeanza kupungua na huenda wapiga kura wakamaliza shughuli hiyo itimiapo saa kumi na moja jioni muda wa mwisho wa kupiga kura


15:16 Mmoja wa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta ameelezea maskitiko yake kuhusu yaliyojiri Mombasa ambako washukiwa wa kundi la MRC waliwaua polisi na raia katika mashambulizi usiku wa kuamkia leo. Lengo lao lilikuwa kuvuruga shughuli ya uchaguzi

14:57 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu Ann Mawathe anasema milolongo ya watu imepungua sana katika sehemu nyingi za mji huo ikizingatiwa kuwa asubuhi watu walikuwa wamejaa pomoni


14:51 Kuna taarifa kuwa magari ya Abiria yameanza kuongeza nauli ya magari kwa sababu ya upungufu wa magari hayo wakati wakenya wakiwa wamejitokeza kupiga kura

Mpigaji kura mjini Mombasa

13:33 Tume ya uchaguzi imeagiza uachaguzi kurejelewa katika wodi tano kati ya zote 1’450 ambako mitambo ya tume hiyo ilikumbwa na hitilafu pamoja na makosa kwenye karatasi za kupigia kura

13:31 Katika baadhi ya vituo vya kupigia kura, ambako foleni ndefu zimeshuhudiwa, taarifa zinasema kuwa watu wanaonekana kukata tamaa na wameamua kurejea nyumbani kwani foleni hazisongi


13:24 Mwandishi wa BBC Wanyama wa Chebusire anaripoti kuwa gari la mbunge mmoja wa zamani limeteketezwa moto maeneo ya Kakamega na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa mpinzani wake. hakuna taharifa za mahafa yoyote.

11:25 Mkuu wa Polisi David Kimaiyo asema kuwa takriban wanachama 200 wa kundi la MRC au Mombasa Republican Council walivamia kituo cha polisi wa doria wakiwa wanaelekea kusambaratisha shughuli za kupiga kura. Inaarifiwa polisi wanne waliuawa katika makabiliano kati yao na wanachama hao.

11:14 Mgombea wa urais Uhuru Kenyatta anapiga kura yake katika eneo bunge lake la Gatundu , mkoa wa Kati


Milolongo mirefu ilishuhudiwa kote nchini

10:39 Mwandishi wa BBC aliye mjini Nyeri Ng’endo Angela anasema kila baada ya nyumba kumi kuna kituo cha kupigia kura, wapiga kura wamejitokeza kwa wingi, baadhi ya mashine za tume ya uchaguzi zilishindwa kufanya kazi lakini baada ya kushughulikiwa mambo yakarejea kuwa sawa.

10:31 Mwandishi wa BBC mjini Eldoret Wanyama wa Chebusire amesema vituo vilifunguliwa mapema, na mambo yameenda shwari kwa ujumla wake, lakini katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mushkil kidogo, mashine ziligoma katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya UG, zaidi ya wapiga kura elfu tatu , hadi sasa ni chini ya watu hamsini wamepiga


10:27 Mkuu wa tume huru ya uchaguzi Isaac Hassan anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto inazokabiliwa nazo tume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua kuchelewa, vitahakikisha wapiga kura wote wamepiga kura


10:22: Ingawaje tume ya uchaguzi IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura, wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo. Mjini Kisumu katika kituo cha upigaji kura cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wa BBC Ann Mawathe ameshuudia dada mmoja alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu na akubaliwe kwenda hadi mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na wapiga kura wenzake.

Katika kituo hicho hicho, baba fulani aliyekuwa amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto mgongoni, naye alirudishwa hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume mwingine aliyejitwika ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na kutaka kuruka foleni, alikatazwa kufanya hivyo.


Karani katika kituo cha kupigia kura

09:04 Waziri mkuu Raila Odinga ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera. Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa shwari

08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa


08:30 Solomon Mugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12

08:25 Hassan Majid mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa na panga katika eneo la Mishomoroni, taharifa hii aijajulikana kama inausiana na uchaguzi unao endelea hadi sasa.


08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa, Karen Allen ametupa taharifa za kusikitisha pale alipotujuzakuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana taarifa zaidi kwa sasa

Mama mwenye mtoto alijitokeza mapema na hapa anaonekana amefanikiwa kupiga kura.

08:16: Frawaso Kimutai  yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru. kura ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda polepole mwendo wa kobe


08:15: Fatma Sanbur yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina. hadi mida ya saa moja asubuhii, shughuli ya upigaji kura ilikuwa haijaanza


07:24 Kips Oscar: Kupitia Facebook yuko Marsabit anasema upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi

Kwa upande wa usalama, polisi na wanajeshi wanaonekana kudhibiti shehemu kubwa ya nchi ya Kenya. Magari ya Kijeshi yakiwemo madelaya ya kivita yalionekana yakishika dolia toka mapema asubuhi ya leo wakati upigaji kura ulipoanza

07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret


07:32: William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.

07:43 Upiga kura bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya kupiga kura zao


07:47 Eco Seyar Papa akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo la Dagoreti. Watu walianza kupanga Foleni kuanzia saa tisa usiku, hii ni mara ya kwanza kwa wakenya kujitokeza kwa wingi kama hilivyo shuhudiwa leo hii.

07:50 Mwandishi wa BBC Ann Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu wakiwa na hamasa ya kupiga kura. Wamepanga foleni tangu saa nane usiku.


07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao